Jinsi ya Kuingia Katika Hali ya Kawaida

Kadiri watu wanavyokubali maneno ya Mungu zaidi, ndivyo wanavyopata nuru zaidi, na ndivyo wanavyokuwa na njaa na kiu zaidi katika kufuatilia kwao kumjua Mungu. Ni wale tu wanaoyakubali maneno ya Mungu ndio wanaoweza kuwa na uzoefu mkuu na wa kina zaidi, na wao pekee ndio ambao maisha yao yanaweza kuendelea kukua kama maua ya ufuta. Wote wanaofuatilia maisha wanapaswa kuchukulia hili kama kazi yao ya wakati wote; wanapaswa kuhisi kwamba “bila Mungu, siwezi kuishi; bila Mungu, siwezi kutimiza chochote; bila Mungu, kila kitu ni tupu.” Vile vile pia, wanapaswa kuwa na azimio kwamba “bila uwepo wa Roho Mtakatifu, sitafanya chochote, na ikiwa kuyasoma maneno ya Mungu hakuna matokeo basi sijali kufanya chochote.” Msijifurahishe. Uzoefu wa maisha hutoka kwa nuru na mwongozo wa Mungu, na ndilo dhihirisho la juhudi zenu za nafsi. Mnachopaswa kuhitaji kutoka wenyewe kufanya ni: “Inapokuja kwa suala la uzoefu wa maisha, siwezi kujipa uhuru wa kufanya nipendavyo.”

Wakati mwingine, unapokuwa katika hali zisizo zakawaida, unapoteza uwepo wa Mungu, na unashindwa kumhisi Mungu unapoomba. Ni kawaida kuhisi hofu nyakati kama hizo. Unapaswa kuanza kutafuta mara moja. Usipofanya hivyo, Mungu atakuwa mbali zaidi na wewe, na utakuwa bila uwepo wa Roho Mtakatifu—na zaidi ya hayo, utakuwa bila kazi ya Roho Mtakatifu kwa siku moja, siku mbili, hata mwezi mmoja au miezi miwili. Katika hali hizi, unakuwa mtu asiye na hisia hata kidogo na kwa mara nyingine unachukuliwa mateka na Shetani, hadi kwa kiwango ambapo unaweza kufanya vitendo vya kila aina. Unatamani utajiri, unawadanganya ndugu zako, unatazama filamu na video, unacheza mahjong, na hata kuvuta sigara na kunywa pombe bila nidhamu. Moyo wako umepotoka mbali kutoka kwa Mungu, umeenda katika njia yako mwenyewe kwa siri, na umeihukumu kazi ya Mungu kiholela. Katika visa vingine, watu hupotoka sana kiasi kwamba hawahisi haya au aibu katika kufanya dhambi za kingono. Mtu wa aina hii ametelekezwa na Roho Mtakatifu; kwa kweli, kazi ya Roho Mtakatifu haijakuwa kwa mtu kama huyo kwa muda mrefu. Mtu anaweza tu kumwona akizama zaidi katika upotovu huku mikono ya uovu ikizidi kunyooka. Mwishowe, anakana uwepo wa njia hii, na anachukuliwa mateka na Shetani anapotenda dhambi. Ukigundua kuwa una uwepo wa Roho Mtakatifu tu, lakini huna kazi ya Roho Mtakatifu, tayari hiyo ni hali hatari kuwa ndani. Wakati huwezi hata kuhisi uwepo wa Roho Mtakatifu, basi uko karibu kufa. Usipotubu, basi utakuwa umemrudia Shetani kabisa, na utakuwa miongoni mwa wale wanaoondolewa. Kwa hivyo, unapogundua kuwa uko katika hali ambayo kuna uwepo wa Roho Mtakatifu tu (hutendi dhambi, unajizuia, na hufanyi chochote kinachompinga Mungu waziwazi) lakini unakosa kazi ya Roho Mtakatifu (huhisi kuguswa unapoomba, hupati nuru au mwangaza wa wazi unapokula na kunywa maneno ya Mungu, hujali kuhusu kula na kunywa maneno ya Mungu, hakuna ukuaji wowote katika maisha yako kamwe, na umeondolewa mwanga mkuu kwa muda mrefu sasa)—katika nyakati kama hizi, lazima uwe mwangalifu zaidi. Lazima usijifurahishe, lazima usiipe tabia yako uhuru zaidi. Uwepo wa Roho Mtakatifu unaweza kutoweka wakati wowote. Hii ndiyo maana hali kama hii ni hatari sana. Ukijipata katika hali ya aina hii, jaribu kuyabadilisha mambo haraka iwezekanavyo. Kwanza, unapaswa kusema sala ya toba na uombe kwamba Mungu akupe huruma Yake kwa mara nyingine tena. Omba kwa bidii zaidi na uutulize moyo wako ili ule na kunywa maneno zaidi ya Mungu. Ukiwa na msingi huu, lazima utumie wakati zaidi katika maombi; uongeze bidii yako mara dufu katika kuimba, kusali, kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutekeleza wajibu wako. Unapokuwa dhaifu kabisa, moyo wako unamilikiwa na Shetani kwa urahisi kabisa. Hilo linapofanyika, moyo wako unachukuliwa kutoka kwa Mungu na kurudishwa kwa Shetani, na punde baada ya hapo unakuwa bila uwepo wa Roho Mtakatifu. Katika nyakati kama hizi, inakuwa vigumu mara dufu kupata tena kazi ya Roho Mtakatifu. Ni bora kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu wakati bado Yeye yuko pamoja nawe, jambo ambalo litamruhusu Mungu kukupa nuru Yake zaidi na kutomfanya Akuache. Kuomba, kuimba nyimbo, kufanya shughuli yako, na kula na kunywa maneno ya Mungu—yote haya yanafanywa ili Shetani asiwe na fursa ya kufanya kazi yake, na ili kwamba Roho Mtakatifu aweze kufanya kazi ndani yako. Usipoipata tena kazi ya Roho Mtakatifu kwa njia hii, ukingojea tu, basi kuipata tena kazi ya Roho Mtakatifu haitakuwa rahisi wakati ambapo umepoteza uwepo wa Roho Mtakatifu, isipokuwa kama Roho Mtakatifu amekugusa wewe hasa, au Amekupa nuru na kukuangazia hasa. Hata hivyo, haichukui siku moja au mbili tu kwa hali yako kurejea; wakati mwingine hata miezi sita inaweza kupita bila urejesho wowote. Hii yote ni kwa sababu watu huwa wazembe sana, hawawezi kupitia vitu kwa njia ya kawaida na hivyo wanaachwa na Roho Mtakatifu. Hata ukipata tena kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya sasa ya Mungu bado inaweza kukosa kuwa wazi kabisa kwako, kwa kuwa umesalia nyuma sana katika uzoefu wako wa maisha, kana kwamba umeachwa maili elfu kumi nyuma. Je, hili si jambo baya sana? Hata hivyo, nawaambia watu kama hao kwamba hawajachelewa sana kutubu sasa, lakini kwamba kuna sharti moja: Lazima ufanye kazi kwa bidii zaidi, na usijiingize katika uvivu. Ikiwa watu wengine wanaomba mara tano kwa siku moja, wewe lazima uombe mara kumi; ikiwa watu wengine wanakula na kunywa maneno ya Mungu kwa saa mbili kwa siku, wewe lazima ufanye hivyo kwa saa nne au sita; na ikiwa watu wengine wanasikiliza nyimbo kwa saa mbili, lazima wewe usikilize kwa angalau siku nusu. Kuwa na amani mara kwa mara mbele za Mungu na ufikirie kuhusu upendo wa Mungu hadi uguswe, moyo wako umrudie Mungu, na usithubutu kupotoka kutoka kwa Mungu—ni hapo tu ndipo matendo yako yatazaa matunda; ni hapo tu ndipo utaweza kurejesha hali yako ya kawaida ya zamani.

Watu wengine huweka shauku nyingi katika ufuatiliaji wao na bado hushindwa kuingia kwenye njia sahihi. Hii ni kwa sababu wao ni wazembe sana na hawatilii maanani mambo ya kiroho. Hawajui jinsi ya kupitia maneno ya Mungu, na hawajui kazi na uwepo wa Roho Mtakatifu ni nini. Watu kama hawa ni wenye shauku lakini ni wapumbavu; hawafuatilii uzima. Hiyo ni kwa sababu huna maarifa hata kidogo ya Roho, hujui chochote kuhusu ukuaji katika kazi inayoendelea ya Roho Mtakatifu, na hujui kuhusu hali iliyo ndani ya roho yako mwenyewe. Je, imani ya watu kama hao siyo aina ya imani iliyo pumbavu? Ufuatiliaji wa watu kama hao hatimaye hauzai chochote. Jambo la muhimu katika kufikia ukuaji wa maisha katika imani ya mtu kwa Mungu ni kujua ni kazi gani ambayo Mungu hufanya katika uzoefu wako, kuona uzuri wa Mungu, na kuelewa mapenzi ya Mungu, kiasi kwamba unastahi mipango yote ya Mungu, maneno ya Mungu yanakita mizizi ndani yako ili yawe uzima wako, na hivyo kumridhisha Mungu. Ikiwa imani yako ni imani ya kipumbavu, ikiwa hutilii maanani mambo ya kiroho na mabadiliko katika tabia yako ya maisha, ikiwa huweki jitihada yoyote kwa ukweli, je, utaweza kuyaelewa mapenzi ya Mungu? Ikiwa huelewi kile ambacho Mungu anataka, basi hutaweza kupata uzoefu, na hivyo hutakuwa na njia ya kutenda. Kile ambacho lazima uzingatie unapopitia maneno ya Mungu ni matokeo ambayo maneno hayo yanatoa ndani yako, ili uweze kumjua Mungu kutoka katika maneno Yake. Ikiwa wewe unajua tu jinsi ya kusoma maneno ya Mungu, lakini hujui jinsi ya kuyapitia, je, hili halionyeshi kuwa wewe hujui kuhusu mambo ya kiroho? Hivi sasa, watu wengi hawawezi kuyapitia maneno ya Mungu, na hivyo hawaijui kazi ya Mungu. Je, huku si kushindwa katika kutenda kwao? Wakiendelea kwa namna hii, ni lini wataweza kupitia mambo kwa uzuri wake mkamilifu na kufanikisha ukuaji katika maisha yao? Je, haya si mazungumzo matupu tu? Kuna wengi kati yenu wanaozingatia nadharia, ambao hawajui chochote kuhusu masuala ya kiroho, na bado wanatamani kutumiwa sana na Mungu na kubarikiwa na Mungu. Hili ni jambo lisilowezekana kabisa! Kwa hivyo, lazima mkomeshe kushindwa huku, ili nyote muweze kuingia kwenye njia sahihi katika maisha yenu ya kiroho, muwe na uzoefu halisi, na muingie katika uhalisi wa maneno ya Mungu kwa kweli.

Iliyotangulia: Waovu Hakika Wataadhibiwa

Inayofuata: Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp