Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Waovu Lazima Waadhibiwe

Kasi

Waovu Lazima Waadhibiwe

Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Mtaitwa wenye haki kwa sababu mnaweza kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu mnakubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa na Yeye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana na Mungu. Jinsi mnavyozidi kukubali maneno ya Mungu wakati huu, ndivyo mnavyozidi kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo mnavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu zaidi na kukidhi mahitaji Yake. Haya ndiyo maagizo ya Mungu kwenu na kile mnachopaswa kufikia. Mkitumia dhana kupima na kufafanua Mungu kwa maneno, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiobadilika, na mkiwekea Mungu mipaka katika Biblia, na kumweka katika wigo wenye mipaka wa kazi, basi hili linathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu katika mioyo yao, Wayahudi wa Agano la Kale walimtazama Mungu kama sanamu ya udongo, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yule pekee anayeitwa Masihi ndiye Mungu, na kwa sababu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—wakimhukumu Yesu asiye na hatia kufa. Mungu alikuwa hajatenda uhalifu wowote, ilhali mwanadamu hakumsamehe Mungu, na kumhukumu Yeye kifo bila kusita. Na ndivyo Yesu Akasulubishwa. Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kulingana na Biblia, kana kwamba mwanadamu amebaini usimamizi wa Mungu, kana kwamba kila kitu Atendacho Mungu kiko mikononi mwa mwanadamu. Wanadamu ni wa kufanya mzaha kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha lugha ya kushawishi ya kujivuna. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba hakuna walio wapinzani wa Mungu zaidi, na kwamba unamshutumu Mungu, kwa kuwa huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu kabisa na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili na Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi sana na kwa sababu badala ya kufuata uhalisi, maarifa yake yote ya Mungu yametolewa kwa chanzo kimoja, chenye ugumu na kisichobadilika. Hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Amesulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu. Wanadamu dhalimu, wakatili! Kufumba watu macho na kula njama, kusukumana, kung’ang’ania sifa na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Mungu Amezungumza maelfu na mamia ya maneno, ilhali hakuna hata mmoja ambaye amejirudi. Wanatenda matendo kwa ajili ya familia zao na watoto wao, kazi zao, matarajio, hadhi, majivuno na pesa, kwa sababu ya nguo, kwa sababu ya chakula na mwili—matendo ya nani kwa kweli ni kwa ajili ya Mungu? Hata miongoni mwa wale ambao matendo yao ni kwa ajili ya Mungu, ni wachache tu wanaomfahamu Mungu. Ni wangapi wanaotenda matendo yasiyo kwa ajili ya maslahi yao? Ni wangapi wasiobagua na kuonea wengine wakiwa na nia ya kudumisha hadhi yao wenyewe? Hivyo, Mungu amehukumiwa kifo mara nyingi kwa nguvu, mahakimu wakatili wasiohesabika wamemhukumu Mungu na mara nyingine wakamsulubisha msalabani. Wangapi wanaweza kuitwa wenye haki kwa sababu wanatenda mambo kwa ajili ya Mungu kwa kweli?

Mbele za Mungu, je, ni rahisi vile kufanywa kuwa mtu kamili, mtakatifu au mwenye haki? Ni kauli ya ukweli kwamba, “hakuna wenye haki katika dunia hii, wenye haki hawapo katika dunia hii.” Mnapokuja mbele za Mungu, fikirieni kile mnachovaa, tafakarini juu ya kila neno na tendo lenu, juu ya fikira zenu na mawazo na hata ndoto mnazoota kila siku—zote ni kwa manufaa yenu. Je, hivi sivyo hali halisi ilivyo? “Haki” haimaanishi kutoa sadaka wala haimaanishi kumpenda jirani yako vile unavyojipenda na hakumaanishi kutopigana, kutogombana, kutoiba ama kutonyang’anya. Haki inamaanisha kuchukua agizo la Mungu kama kazi yako na kuiheshimu mipango na utaratibu wa Mungu kama wito utokao mbinguni, bila kujali wakati ama mahali, kama tu yote ambayo Bwana Yesu Aliyafanya. Hiyo ndiyo haki iliyozungumziwa na Mungu. Kwamba Lutu aliweza kuitwa mwenye haki ni kwa sababu aliwaokoa malaika wawili waliotumwa na Mungu bila kujali alichopata ama kupoteza; alichotenda katika huo wakati kinaweza kuitwa haki, lakini hawezi kuitwa mwanadamu mwenye haki. Ilikuwa tu kwa sababu Lutu alikuwa amemwona Mungu ndipo akatoa wasichana wake wawili badala ya malaika. Lakini si tabia yake yote ya hapo awali inaashiria haki, na hivyo Nasema kwamba “hakuna wenye haki katika dunia hii.” Hata kati ya wale ambao wako katika mkondo wa urejesho, hakuna hata mmoja anayeweza kuitwa mwenye haki. Haijalishi matendo yako ni mazuri vipi, haijalishi jinsi unavyooneka kulisifu jina la Mungu, kutowapiga ama kuwalaani wengine, ama kuwaibia na kuwanyang’anya, huwezi kuitwa mwenye haki bado, kwa sababu vitu hivyo vinaweza kumilikiwa na mtu yeyote aliye wa kawaida. Siku ya leo, kilicho muhimu ni kwamba wewe humfahamu Mungu. Inaweza tu kusemekana kwamba leo una ubinadamu wa kawaida wa kiasi kidogo, ilhali umeondolewa haki iliyozungumziwa na Mungu, na hakuna utakachotenda kitakachokuwa ushuhuda wa ufahamu wako wa Mungu.

Hapo awali, Mungu Alipokuwa mbinguni, mwanadamu alijaribu kumdanganya Mungu kwa matendo yake; leo, Mungu amekuja miongoni mwa wanadamu—hakuna anayejua ni kwa muda upi—ilhali mwanadamu bado anamfanyia Mungu kazi kwa namna isiyo ya dhati, na hujaribu kumdanganya Mungu. Je, si mwanadamu yuko nyuma sana katika fikira zake? Ndivyo ilivyokuwa na Yuda: Kabla Yesu aje, Yuda angewadanganya ndugu zake, na hata Yesu alipokuja, bado hakubadilika; hakuwa na maarifa yoyote ya Yesu, na mwishowe alimsaliti Yesu. Je, ilikuwa kwa sababu hakumfahamu Mungu? Kama leo bado hammfahamu Mungu, basi mtakuwa Yuda, na msiba wa kusulubiwa kwa Yesu katika Enzi ya Neema, maelfu ya miaka iliyopita, utarudiwa tena. Je, hamyaamini hayo? Ni ukweli! Siku hizi watu wengi wako katika hali kama hiyo—Naweza kuwa Ninayasema haya mapema kiasi—na watu wa aina hii wanachukua nafasi ya Yuda. Sizungumzi bila kujali, bali ni kulingana na ukweli—na unapaswa kuamini. Ingawa watu wengi wanajifanya kuwa wanyenyekevu, katika mioyo yao hakuna kingine ila maji yaliyotuama, yanayonuka. Sasa, wengi sana katika kanisa wako hivi. Je, unafikiri Sijui lolote? Leo, Roho Wangu ananiongoza na kunishuhudia. Unafikiri kwamba Sijui lolote? Je, unafikiri Sielewi fikira zenu za ujanja katika nyoyo zenu na vitu vilivyowekwa katika nyoyo zenu? Je, Mungu hudanganywa kwa njia rahisi vile? Je unafikiri kwamba unaweza kumtendea vile unavyotaka? Hapo zamani, Nilikuwa na wasiwasi kwamba mlikuwa mmefungwa, na hivyo Nikaendelea kuwapa uhuru, lakini hakuna aliyetambua kuwa Nilikuwa mzuri kwake. Niliwapa kidogo na wakataka mengi. Ulizaneni wenyewe kwa wenyewe: Sijashughulikia na karibu kila mtu, na Sijakuwa na haraka ya kumkaripia yeyote—ilhali Sina tashwishi juu ya motisha na dhana za mwanadamu. Je, unafikiri Mungu Mwenyewe ambaye Mungu Anamshuhudia ni mjinga? Basi Ninasema kwamba wewe ni kipofu sana! Sitakulaumu, na basi acha tuone utakavyopotoka. Hebu tuone iwapo ujanja wako utakuokoa, ama iwapo kujaribu kadri uwezavyo kumpenda Mungu kutakuokoa. Leo, Sitakushutumu; hebu tungoje mpaka wakati wa Mungu tuone Atakavyokuadhibu. Sina wakati wa kupoteza kufanya maongezi yasiyo muhimu, na Sina nia ya kuchelewesha kazi Yangu kuu kwa ajili yako, buu kama wewe hufai kuchukua muda wa Mungu Akikushughulikia—kwa hivyo acha tuone kiwango utakachojifurahisha. Watu kama hao hawafuati ufahamu wa Mungu hata kidogo, na hawana upendo wowote kwa Mungu, ilhali wanataka kuitwa wenye haki na Mungu—je, huu si utani? Kwa sababu kuna idadi ndogo ya watu walio waaminifu, Mimi sijishughulishi na kingine ila kumpa mwanadamu uhai. Nitakamilisha tu kile kilichohitajika kukamilika leo, na baadaye, adhabu italetwa kwa kila mmoja kulingana na tabia yake. Nimesema kile Ninachopaswa kusema, kwa sababu hii ndiyo kazi Ninayoifanya. Ninafanya kile Ninachopaswa kukifanya, ila Sifanyi Nisichopaswa kukifanya, ilhali bado Natumai kwamba utatumia muda zaidi kutafakari: Kiwango gani hasa cha ufahamu wako wa Mungu ni wa kweli? Je wewe ni mmoja wa wale ambao wamemsulubisha Yesu tena? Mwisho, Ninasema hivi: Ole wao wamsulubishao Mungu.

Iliyotangulia:Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Inayofuata:Jinsi ya Kuingia Ndani ya Hali ya Kawaida