Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?
Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo kwa njia inayofaa? Je, wewe unayepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho unaweza kueleza tabia ya Mungu yenye haki kwa utondoti? Je, unaweza kushuhudia kuhusu tabia ya Mungu kwa uwazi na usahihi? Je, utapitisha vipi yale uliyoyaona na kuyapitia kwa wale waumini wa kidini wenye kusikitisha, maskini, na wacha Mungu ambao wana njaa na kiu ya haki na wanakungoja wewe uwachunge? Ni watu wa aina gani ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Unaweza kuwaza kweli? Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? Utahudumu vipi kama kiongozi mzuri wa wakati unaofuata? Je, unao hisia nzuri ya uongozi? Je, unaweza kuelezaje bwana wa mambo yote? Je, kweli ndiye mtawala wa viumbe vyote vilivyo hai na vitu vyote vilivyomo ulimwenguni? Je, una mipango gani kwa ajili ya maendeleo ya hatua inayofuata ya kazi? Je, jukumu lako ni nzito? Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, “Njia iko wapi?” Jinsi wanavyotamani nuru, kama nyota iangukayo kutoka angani, ishuke ghafla na kutawanya nguvu za giza ambazo zimewakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia, ya kutumia nguvu zako zote kumlipa Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?