Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachodaiwa nyakati za sasa kuwa “wazazi” wa Petro? Yamekuwa kama tu mwili na damu ya mwanadamu. Je, hatima, mategemeo ya baadaye ya mwili yatakuwa ni kumwona Mungu wakati ukiwa hai, au kwa roho kukutana na Mungu baada ya kifo? Je, mwili kesho utaishia katika tanuu kubwa kama katika taabu, au utakuwa katika kuteketezwa kwa moto? Je, maswali kama haya yanayohusu iwapo mwili wa mwanadamu utahimili taabu au mateso ni habari kubwa sana ambayo kila mtu sasa katika mkondo huu ambaye ana ubongo na akili yake iko sawa anahangaika zaidi nayo? (Hapa, kuhimili mateso hurejelea kupokea baraka; kuteseka humaanisha kwamba majaribu ya siku zijazo ni yenye manufaa kwa hatima ya mwanadamu. Taabu hurejelea kushindwa kusimama imara, au kudanganywa; au, humaanisha kwamba mtu atakumbana na hali za bahati mbaya na kupoteza maisha ya mtu katikati ya majanga, na kwamba hakuna hatima nzuri kwa roho.) Watu wanajitayarisha na mantiki timamu lakini pengine kile wanachofikiri hakifanani kabisa na kile ambacho mantiki yao inapaswa kutayarishwa nayo. Hii ni kwa sababu ni waliochanganyikiwa kiasi na wanafuata vitu bila kufikiri. Wote wanapaswa kuwa na uelewe wa kina wa kile ambacho wanapaswa kuingia kwacho, na kwa mahususi wanapaswa kutatua kile wanachopaswa kuingia kwacho wakati wa mateso (yaani, wakati wa utakasaji wa tanuu), na kile wanachopaswa kutayarishwa nacho katika jaribu la moto. Usiwatumikie wazazi wako siku zote (kumaanisha mwili) ambao ni sawa na nguruwe na mbwa, na ni wabaya zaidi kuliko chungu na wadudu. Kuna haja gani ya kuteseka juu ya hilo, kufikiri sana, kuutesa ubongo wako? Mwili si wako, bali upo katika mikono ya Mungu ambaye Hakudhibiti wewe pekee bali pia Anamwamuru Shetani. (Kwa asili ilimaanisha kuwa ulikuwa wa Shetani. Kwa kuwa Shetani pia yupo mikononi mwa Mungu, ingeweza kuwekwa hivyo tu. Maana inashawishi zaidi kusema namna hiyo—inamaanisha kuwa wanadamu hawapo chini ya miliki ya Shetani kabisa, bali wapo mikononi mwa Mungu.) Unaishi chini ya mateso ya mwili, lakini je, mwili ni wako? Upo chini ya udhibiti wako? Kwa nini usumbuke kufikiri sana juu ya hilo? Kwa nini usumbuke sana kumsihi Mungu kwa ajili ya mwili wako uliooza ambao umeshahukumiwa zamani sana na kulaaniwa, vilevile kutiwa najisi na roho wachafu? Kwa nini usumbuke siku zote kwa kushikilia washirika wa Shetani karibu na moyo wako? Huna wasiwasi kwamba mwili unaweza kuharibu mategemeo yako halisi ya baadaye, matumaini mazuri, na hatima ya kweli ya maisha yako?

Njia ya leo si rahisi kuitembea. Mtu anaweza kusema kwamba ni vigumu kuipitia na ni adimu sana katika enzi zote. Hata hivyo, nani angeweza kufikiria kuwa mwili wa mwanadamu pekee ungetosha kumwangamiza? Kazi leo hakika ni ya thamani kama vile mvua wakati wa majira ya kuchipua na ni ya thamani kama wema wa Mungu kwa mwanadamu. Hata hivyo, ikiwa mwanadamu hajui kusudi la kazi Yake leo au kuelewa kiini cha mwanadamu, inawezekanaje tunu na thamani yake vizungumziwe? Mwili si wa wanadamu wenyewe, hivyo kwa kweli hakuna mtu anayeweza kuona waziwazi hatima yake itakuwa wapi. Hata hivyo, unapaswa kujua vizuri kwamba Mungu wa uumbaji Atawarudisha binadamu, ambao waliumbwa, katika nafasi yao ya asili, na kurejesha sura yao ya asili kutoka wakati wa kuumbwa kwao. Atachukua tena kikamilifu pumzi Aliyompuliza ndani ya binadamu, na kuchukua tena mifupa na mwili wake na kurudisha vyote kwa Bwana wa viumbe. Atabadilisha na kufanya upya binadamu kikamilifu, na kuchukua tena kutoka binadamu urithi wote ambao kwa asili haukuwa wa binadamu, bali ulikuwa wa Mungu. Hatamkabidhi tena binadamu urithi huo. Maana hakuna hata kitu kimoja kati ya hivyo vilikuwa vya binadamu kwa asili. Atavichukua vyote tena—huu si uporaji usio wa haki, bali unakusudiwa kuirejesha mbingu na dunia katika hali yake ya asili, na kubadilisha na kumfanya upya binadamu. Hii ni hatima inayofaa kwa mwanadamu, ingawa pengine si kuichukua tena baada ya kuuadibu mwili kama watu wanavyofikiri. Mungu hataki mifupa ya mwili baada ya maangamizi yake, bali vitu vya asili katika mwanadamu ambavyo mwanzo vilikuwa vya Mungu. Hivyo, hatawaangamiza binadamu au kuuondoa kabisa mwili wa binadamu, maana mwili wa binadamu si mali binafsi ya mwanadamu. Badala yake, ni kiungo cha Mungu, ambaye anasimamia binadamu. Angewezaje kuuangamiza mwili wa binadamu ili Yeye “afurahi”? Je, wakati huu, kwa kweli umeachana na kila kitu cha huo mwili wako ambao hauna thamani hata ya senti moja? Kama ungeweza kuelewa asilimia thelathini ya kazi ya siku za mwisho (asilimia thelathini tu, yaani, kuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu leo, vilevile kazi ya neno Mungu hufanya katika siku za mwisho), basi usingeweza kuendelea “kuutumikia” au “kuwa” na upendo kwa mwili wako kama unavyofanya leo, ambao umepotoka kwa miaka mingi. Unapaswa kuelewa kwa kina kwamba binadamu sasa wameendelea kwa hali ambayo haijawahi kutokea na hawataendelea tena kusonga mbele kama magurudumu ya historia. Mwili wako wa udongo umeshafunikwa na nzi tangu zamani, hivyo unawezaje kuwa na nguvu ya kurudisha nyuma magurudumu ya historia ambayo Mungu ameyawezesha kuendelea hadi siku hii ya leo? Unawezaje kufanya saa ya siku za mwisho ambayo ni kama bubu ipige tena na kuendelea kusogeza mikono yake kwa upande wa kulia? Unawezaje kuubadilisha upya ulimwengu ambao unaonekana kama umefunikwa na ukungu mzito? Je, mwili wako unaweza kufufua milima na mito? Je, mwili wako, ambao una kazi ndogo tu, unaweza kweli kurejesha ulimwengu wa binadamu ambao umekuwa ukiutamani? Unaweza kweli kuwaelimisha wadhuria wako kuwa “binadamu”? Unaelewa sasa? Mwili wako unamilikiwa na nini hasa? Makusudi halisi ya Mungu ya kumfinyanga mwanadamu, ya kumkamilisha mwanadamu, na ya kumbadilisha mwanadamu hayakuwa kukupatia nchi nzuri ya asili au kuleta pumziko la amani kwa mwili wa mwanadamu. Badala yake, ilikuwa ni kwa ajili ya utukufu Wake na ushuhuda Wake, kwa furaha bora ya binadamu hapo baadaye, na ili kwamba hivi karibuni waweze kufurahia pumziko. Bado, si kwa ajili ya mwili wako, maana mwanadamu ni mtaji wa usimamizi wa Mungu na mwili wa mwanadamu ni kiungo tu. (Mwanadamu ni kitu chenye roho na mwili, wakati mwili ni chombo kiozacho tu. Hii humaanisha kwamba mwili ni chombo kwa ajili ya mpango wa usimamizi.) Unapaswa kujua kwamba Mungu kuwakamilisha wanadamu, kuwatimiza wanadamu, na kuwapata wanadamu hakujaleta kitu chochote zaidi ya mapanga na maangamizi kwa mwili wao, na kumeleta mateso yasiyokoma, kuungua kwa moto, hukumu zisizokuwa na huruma, kuadibu, na laana, na vilevile majaribu yasiyokuwa na mipaka. Hicho ni kisa cha ndani na ukweli wa kazi ya kumsimamia binadamu. Hata hivyo, vitu hivi vyote vimelengwa dhidi ya mwili wa binadamu, na mikuki yote ya uhasama bila huruma inaelekezwa kwenye mwili wa binadamu (maana kwa asili binadamu hakuwa na hatia). Hayo yote ni kwa ajili ya utukufu na ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake. Hii ni kwa sababu kazi Yake si tu kwa ajili ya binadamu, bali ni kwa ajili ya mpango wote na kutimiza mapenzi Yake ya asili Alipomuumba binadamu. Kwa hiyo, pengine asilimia tisini ya kile ambacho watu wanapitia ni mateso na majaribu ya moto, lakini kuna siku chache sana tamu na za furaha au hata hakuna kabisa ambazo mwili wa mwanadamu umekuwa ukitamani, na hata hawawezi kufurahia nyakati za furaha katika mwili wakishinda nyakati nzuri pamoja na Mungu. Mwili ni mchafu, hivyo kile ambacho mwili wa mwanadamu unakiona au unakifurahia si chochote bali ni adabu ya Mungu ambayo haipendwi na mwanadamu, na ni kana kwamba ulikuwa unakosa mantiki ya kawaida. Hii ni kwa sababu Atadhihirisha tabia Yake ya haki ambayo haipendwi na mwanadamu, haivumilii makosa ya mwanadamu, na huchukia kabisa maadui. Mungu hufichua waziwazi tabia Yake yote kupitia njia yoyote iwezekanayo, na hivyo Akihitimisha kazi ya vita Vyake na Shetani vya miaka elfu sita—kazi ya wokovu wa binadamu wote na maangamizi ya Shetani wa zamani!

Iliyotangulia: Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

Inayofuata: Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki