Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Jinsi Unavyopaswa Kuitembea Awamu ya Mwisho ya Njia

Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu yake muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kiasi, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na kusikiza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na ukiendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kukamilishwa. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kiasi fulani cha kazi ya Mungu, alipata umaizi kiasi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu. Wakati mwingine bado alikuwa na upinzani na uasi. Baada ya Yesu kutundikwa msalabani, hatimaye alizinduka kidogo na alihisi kuwa mwenye kustahili adhabu. Hatimaye ilifikia hatua ambapo hakuwa anakubali wazo lolote alilokuwa nalo ambalo halikuwa sahihi. Alijua hali yake mwenyewe vizuri sana, na pia alijua utakatifu wa Bwana vizuri. Matokeo yake ni kwamba, moyo wa upendo kwa Bwana ulikua ndani yake hata zaidi, na alilenga katika maisha yake zaidi. Kwa sababu ya hiyo alipitia dhiki kubwa, na ingawa wakati mwingine ilikuwa kama kwamba alikuwa na ugonjwa mkubwa na hata alionekana kuchungulia kaburi, baada ya kusafishwa kwa njia hii mara nyingi, alikuwa na ufahamu zaidi wa nafsi yake, na kwa njia hii tu ndipo alipata upendo wa kweli kwa Bwana. Inaweza kusemwa kuwa maisha yake yote yaliishiwa katika usafishaji, na hata zaidi, yaliishiwa katika kuadibiwa. Uzoefu wake ulikuwa tofauti na wa mtu mwingine yeyote, na upendo wake ulizidi ule wa mtu yeyote ambaye hajakamilishwa. Sababu yake kuchaguliwa kama mfano ni kwamba alipitia uchungu mwingi sana maishani mwake na uzoefu wake ulikuwa wenye mafanikio mengi sana. Ikiwa kweli mnaweza kutembea hatua ya mwisho ya njia kama vile Petro, basi hakuna kiumbe hata mmoja ambaye anaweza kuchukua baraka zenu.

Petro alikuwa mtu mwenye dhamiri, na akiwa na ubinadamu wa aina hiyo, wakati alipokuwa akimfuata Yesu mara ya kwanza, hakuwa na budi ila kuwa na mawazo mengi ya upinzani na uasi. Lakini alipokuwa akimfuata Yesu, hakuyachukulia mambo haya kwa uzito na aliamini kuwa watu wanapaswa kuwa hivyo. Kwa hivyo, mwanzoni hakuhisi hatia yoyote, wala hakushughulikiwa. Yesu hakuwa makini kuhusu majibu aliyokuwa nayo, wala Hakuyafikiria. Aliendelea tu na kazi Aliyopaswa kufanya. Hakuwahi kuwashutumu Petro na wale wengine. kwa makosa madogomadogo. Unaweza kusema: “Inaweza kuwa kwamba Yesu hakujua kuhusu mawazo haya waliyoyaonyesha?” La hasha! Ilikuwa kwa sababu Yeye alimfahamu Petro kweli—inaweza kusemwa kwamba Alikuwa na ufahamu mkubwa juu yake—hivi kwamba Hakuchukua hatua zozote dhidi ya Petro. Aliwachukia wanadamu lakini pia Aliwahurumia. Je, si kuna watu wengi kati yenu sasa ambao wana upinzani kama vile Paulo, na walio na mawazo mengi kama vile Petro alivyokuwa nayo kwa Bwana Yesu wakati huo? Nawaambieni, ingekuwa bora zaidi kwenu kutoamini sana katika hisia zenu za tatu. Kuhisi kwako hakuaminiki na kuliharibiwa kabisa na upotovu wa Shetani muda mrefu uliopita. Je, unadhani kuhisi kwako kuko kamili kabisa? Paulo alimpinga Bwana Yesu mara nyingi lakini Yesu hakuwa na majibu yoyote. Je, inaweza kuwa kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kutibu wagonjwa na kuwatoa pepo, lakini hakuweza kumfukuza “pepo” ndani ya Paulo? Kwa nini ilikuwa tu baada ya Yesu kufufuliwa na kupaa mbinguni, wakati huo huo Paulo akiendelea kuwakamata wanafunzi wa Yesu bila sababu, ndipo hatimaye Yesu alimtokea njiani kwenda Dameski, na kumbwaga? Inaweza kuwa kwamba Bwana Yesu alionyesha hisia polepole sana? Au je, ilikuwa kwa sababu Hakuwa na mamlaka yoyote katika mwili? Je, unafikiri kwamba unapokuwa mharibifu na mpinzani kisiri, Mimi sijui? Je, unadhani kuwa makombo ya nuru ambayo unayo kutoka kwa Roho Mtakatifu yanaweza kutumiwa kunipinga Mimi? Petro alipokuwa hajakomaa, alipata mawazo mengi kumhusu Yesu, hivyo kwa nini hakuwa apate lawama? Hivi sasa, watu wengi wanafanya mambo bila lawama, na hata wanapoambiwa wazi kwamba kufanya hivyo si sahihi, hawasikilizi. Je, si hii ni kwa sababu ya uasi wa mwanadamu kabisa? Nimesema mengi sana sasa, lakini bado unakosa hata chembe ya utambuzi wa dhamiri, kwa hivyo utawezaje kuwa na uwezo wa kutembea hatua ya mwisho ya njia hadi mwisho wake? Je, huhisi kwamba hili ni suala kubwa sana?

Baada ya watu kushindwa wanaweza kutii mpango wa Mungu; wanaweza kutegemea imani yao na mapenzi yao kumpenda Mungu kumfuata. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya njia inaweza kutembewa vipi? Katika siku zako za kupitia dhiki unapaswa kuvumilia shida zote, na lazima uwe tayari kuteseka; ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kuchukua hatua hii ya njia vizuri. Je, unafikiri kuwa ni rahisi hivyo kuchukua hatua hii ya njia? Mnapaswa kujua kazi ambayo mnafaa kutimiza, lazima muongeze ubora wenu wa tabia na kujiandaa na ukweli wa kutosha. Hii siyo kazi ya siku moja au mbili—si rahisi kama unavyofikiri! Kuitembea hatua ya mwisho ya njia inategemea aina ya imani na hiari ambayo unayo kweli. Labda huwezi kuona Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani yako, au labda huna uwezo wa kugundua kazi ya Roho Mtakatifu kanisani, kwa hivyo unakuwa bila rajua na kuvunjika moyo, na njia iliyo mbele inakukatisha tamaa sana. Hasa, hao waliokuwa wapiganaji mashuhuri wa zamani wote wameanguka—je, si haya yote ni pigo kwako? Unapaswa kuona vipi mambo haya? Je, una imani au la? Je, unaelewa kikamilifu kazi ya leo, au la? Mambo haya yanaweza kuamua kama una uwezo wa kutembea hatua ya mwisho ya njia vizuri.

Kwa nini inasemekana kwamba sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia? Ni kwa sababu mnaelewa kila kitu mnachopaswa kuelewa, na Nimewaambia kila kitu ambacho watu wanapaswa kufanikisha. Nimewaambia pia kuhusu kila kitu mlichoaminiwa nacho. Kwa hivyo, mnayotembea sasa ni sehemu ya mwisho ya njia inayoongozwa na Mimi. Nahitaji tu kuwa muwe na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, kwamba bila kujali ni lini daima mtakuwa na barabara ya kuchukua, muongeze ubora wenu wa tabia kama kawaida, muyasome maneno ya Mungu vizuri, na muwe na maisha ya kibinadamu yanayostahili. Sasa Nakuongoza uishi kwa njia hii, lakini siku zijazo wakati Sikuongozi, je, utaweza bado kuishi hivi? Je, utaweza kuendelea? Huu ndio ulikuwa uzoefu wa Petro. Yesu alipokuwa akimwongoza, hakuwa na ufahamu; alikuwa daima asiyejali kama mtoto, na hakutilia maanani mambo aliyoyafanya. Baada tu ya Yesu kuondoka ndipo alianza maisha yake ya kibinadamu yaliyofaa. Maisha yake yenye maana yalianza tu baada ya Yesu kuondoka. Ingawa yeye alikuwa na urazini kiasi wa binadamu wa kawaida na kile ambacho binadamu wa kawaida anapaswa kuwa nacho, uzoefu na ufuatiliaji wake wa kweli ulianza tu upya Yesu alipoondoka. Je, mambo yako vipi kwenu wakati huu? Sasa Nawaongoza kwa njia hii na mnafikiri kuwa ni nzuri. Hakuna mazingira na majaribio ambayo hukufikia, lakini kwa njia hii hakuna njia ya kuona aina ya kimo ulicho nacho hasa, wala hakuna njia yoyote ya kuona kama kweli wewe ni mtu anayefuatilia ukweli. Unasema kwa mdomo wako kwamba unaelewa kiini chako mwenyewe, lakini haya ni maneno matupu. Baadaye, wakati ambapo ukweli unakujia, wakati huo tu ndipo ufahamu wako utathibitishwa. Hata ingawa sasa una ufahamu wa aina hii: “Naelewa kwamba mwili wangu binafsi umepotoka sana, na asili ya mwili wa watu ni kumwasi na kumpinga Mungu. Kuwa na uwezo wa kupokea hukumu ya Mungu na kuadibiwa yote ni kuinuliwa na Yeye. Nimeelewa hayo sasa, na niko tayari kuulipiza upendo wa Mungu”, ambayo ni rahisi kusema, baadaye dhiki, majaribio, na mateso vitakapokujia, haitakuwa rahisi kuvipitia. Mnafuata njia hii kila siku, lakini bado hamwezi kuendelea na uzoefu wenu. Ingekuwa vibaya hata zaidi kama Ningewaachilia na Nisiwatilie maanani tena; watu wengi wataanguka chini na kuwa nguzo ya chumvi, ishara ya aibu. Haya yote yanawezekana sana. Je, huna mahangaiko au wasiwasi kuhusu hili? Petro alipitia aina hiyo ya mazingira na kupitia aina hiyo ya mateso, lakini bado alisimama imara. Kama mazingira hayo yangeletwa kwako, je, ungeweza kusimama imara? Mambo ambayo Yesu alisema na kazi Aliyofanya Alipokuwa duniani vilimpa Petro msingi, na ilikuwa kutoka msingi huu ndiyo alitembea njia yake ya baadaye. Je, mnaweza kufikia kiwango hicho? Njia ambazo umetembea awali na ukweli ambao umeelewa—je, zinaweza kuwa msingi wako wa kusimama imara katika siku zijazo? Je, zinaweza kuwa maono yako ya kusimama imara baadaye? Nitawaambia ukweli—mtu anaweza kusema kwamba kile watu wanachokielewa sasa yote ni mafundisho ya dini. Hii ni kwa sababu kile wanachokielewa siyo mambo yote ambayo wameyapitia. Kwamba umeweza kuendelea mpaka sasa ni kwa sababu ya uongozi wa mwanga mpya kabisa. Sio kwamba kimo chako kimefikia kiwango fulani, lakini imekuwa ni maneno Yangu ambayo yamekuongoza hadi leo; sio kwamba una imani kubwa, lakini kwa sababu ya hekima ya maneno Yangu, hukuwa na budi ila kufuata mpaka sasa. Ikiwa singezungumza sasa, Singetoa sauti Yangu, hungeweza kusonga na ungeacha kwenda mbele mara moja. Je, hiki si kimo chenu halisi? Hamjui mtaingia ndani kutoka kwa vipengele gani na ni katika vipengele gani kufidia kile mnachokosa. Hamna ufahamu wa jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kibinadamu yenye maana, jinsi ya kulipiza upendo wa Mungu, au kuwa na ushuhuda wenye nguvu na mkubwa sana. Hamwezi kufikia mambo haya kabisa! Ninyi ni wavivu na wajinga! Yote mnayoweza kufanya ni kuegemea kwa kitu kingine, na kile mnachoegemea ni mwanga mpya, na Yule aliye mbele akiwaongoza. Kwamba umeweza kuendelea mpaka leo imetegemea kabisa nuru mpya na matamko ya hivi karibuni. Ninyi sio kama Petro, ambaye alikuwa stadi wa kufuatilia njia ya kweli, au kama Ayubu, ambaye aliweza kumwabudu Yehova kwa uaminifu na kuamini kwamba Yeye alikuwa Mungu bila kujali jinsi Yehova alivyomjaribu, na kama Alimbariki au la. Je, unaweza kufanya hivyo? Mmeshindwaje? Kipengele kimoja ni hukumu, kuadibiwa, na laana, na kipengele kingine ni mafumbo ambayo yanawashinda. Ninyi nyote ni kama punda. Ikiwa Ninachokisema sicho cha kifahari vya kutosha, ikiwa hakuna mafumbo yoyote, basi hamwezi kushindwa. Ikiwa angekuwa mtu anayehubiri na daima angehubiri kuhusu vitu vile vile kwa kipindi cha muda, ingechukua chini ya miaka miwili kwa ninyi nyote kukimbia, na msingeweza kuendelea. Hamjui jinsi ya kwenda ndani zaidi, wala hamwelewi jinsi ya kufuatilia ukweli au njia ya uzima. Yote mnayoelewa ni kupokea kitu ambacho ni kigeni, kama vile kusikiliza mafumbo au maono, au kusikiliza jinsi Mungu alivyokuwa akifanya kazi, au kusikiliza uzoefu wa Petro, au historia ya kusulubiwa kwa Yesu.... Mko tayari kusikiliza mambo haya tu, na kadiri mnavyozidi kuyasikiliza ndivyo mnavyozidi kupata nguvu. Mnayasikiliza haya yote ili kuondoa huzuni zenu na uchoshi! Maisha yenu yanahimiliwa kabisa na mambo haya mageni. Je, unafikiri kwamba umefika hapa leo kwa ajili ya imani yako mwenyewe? Je, hivi si vimo vidogo, vya kusikitisha ambavyo mnavyo? Uadilifu wenu uko wapi? Ubinadamu wenu uko wapi? Je, mna uhai wa binadamu? Je, ni vipengele vingapi ambavyo mnavyo kwa ajili ya kukamilishwa? Je, Ninayosema si ukweli? Nazungumza na kufanya kazi kwa njia hii lakini bado mnatilia maanani kwa nadra sana. Wakati mnapofuata, pia mnatazama. Daima mnaendelea kuonekana kutojali, na daima mnaongozwa kwa kushurutishwa. Hivi ndivyo nyote mmeendelea. Imekuwa kuadibiwa, usafishaji, na kurudi kabisa ambavyo vimewaongoza hadi leo. Laiti mahubiri fulani kuhusu kuingia katika maisha yangehubiriwa, je, si nyote mngeteleza zamani? Kila mmoja wenu ni mwenye majivuno zaidi kuliko anayefuata; kwa kweli, mmejaa maji machafu pekee! Mmeelewa baadhi ya mafumbo, na mmeelewa baadhi ya mambo ambayo watu hawajapata kuelewa hapo awali, kwa hivyo mmefikia hata sasa kwa shida. Hamna sababu ya kutofuata, kwa hivyo mmejidhibiti kwa shida na kwenda pamoja na mtiririko. Haya ni matokeo tu ambayo yamefanikishwa kwa njia ya maneno Yangu, lakini hakika si kwa uwezo wenu wenyewe. Hamna kitu cha kujisifu kuhusu. Kwa hivyo, katika hatua hii ya kazi mmeongozwa hadi siku ya leo hasa kwa njia ya maneno. Vinginevyo, ni nani kati yenu angeweza kutii? Nani angeweza kufika hadi leo? Kuanzia mwanzoni kabisa mlitaka kuondoka katika nafasi ya kwanza iliyowezekana, lakini hamkuthubutu; hamkuwa na ujasiri. Hadi leo, mmekuwa mkifuata shingo upande.

Ilikuwa tu baada ya Yesu kutundikwa msalabani na kuondoka ndipo Petro alianza kwenda katika njia yake mwenyewe, akaanza kuitembea njia ambayo ilimpasa; alianza kujiandaa baada tu ya kuona mapungufu yake na kasoro zake. Aliona kwamba alikuwa na upendo mdogo mno kwa Mungu na radhi yake ya kuteseka haikuwa ya kutosha, kwamba hakuwa na umaizi wowote, na kwamba urazini wake haukuwepo. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ndani yake ambavyo havikukubaliana na mapenzi ya Yesu, na kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo viliasi na kupinga na vingi vilivyochanganyika na mapenzi ya kibinadamu. Ilikuwa tu baada ya hapo ndiyo alipata kuingia katika kila kipengele. Yesu alipokuwa akimwongoza, Alifunua hali yake na Petro alikubali bila kusita, lakini hakuwa na ufahamu wa kweli hadi baada ya hapo. Hiyo ilikuwa kwa sababu wakati huo, hakuwa na uzoefu wowote kabisa, na hakujua kimo chake mwenyewe kabisa. Hiyo ni kusema, sasa Natumia maneno tu ili kuwaongoza, na haiwezekani kuwakamilisha kwa muda mfupi, na mtaweza tu kuelewa na kujua ukweli. Hii ni kwa sababu kuwashinda na kuwafanya muamini mioyoni mwenu ndiyo kazi ya sasa, na baada tu ya watu kushindwa ndipo baadhi yao watakamilishwa. Sasa hivi maono hayo na ukweli huo unaoelewa vinajenga msingi wa uzoefu wako wa baadaye; katika dhiki ya baadaye nyote mtapata uzoefu wa utendaji wa maneno haya. Baadaye, wakati majaribio yanakujia na unakabiliwa na dhiki, utafikiria maneno unayosema leo: Bila kujali shida, majaribio, au maumivu makubwa ninayokumbana nayo, ni lazima nimkidhi Mungu. Fikiria kuhusu uzoefu wa Petro, na fikiria kuhusu ule wa Ayubu—utaamshwa na maneno ya leo. Ni kwa njia hii tu ndiyo imani yako itatiwa moyo. Wakati huo, Petro alisema kuwa hakustahili kupokea hukumu wala kuadibu kwa Mungu, na wakati huo pia utakuwa radhi watu wote waone tabia ya haki ya Mungu kupitia kwako. Utakuwa tayari kabisa kukubali hukumu Yake na kuadibu, na hukumu Yake, kuadibu, na laana vitakuwa faraja kwako. Hivi sasa, huwezi kabisa kujiandaa kwa ukweli. Licha ya kuwa utashindwa kusimama imara katika siku zijazo, lakini pia huenda usiwe na uwezo wa kupitia kazi ya sasa. Kwa njia hii, je, si utakuwa mlengwa wa kuondolewa na kuadibiwa? Hivi sasa hakujakuwa na ukweli wowote uliokujia, na Nimekupa katika vipengele ambavyo unakosa; Nasema kutoka kila kipengele. Hakika hamjavumilia mateso mengi; mnachukua tu kinachopatikana, hamjalipa aina yoyote ya gharama, na hata zaidi hamna uzoefu na utambuzi wenu halisi. Kwa hiyo, mnayoelewa si vimo vyenu vya kweli. Mmewekewa mipaka katika kuelewa, maarifa, na kuona, lakini hamjavuna mavuno mengi. Nisingewatilia maanani lakini Niwaruhusu muwe na uzoefu nyumbani kwenu wenyewe, mngekuwa mmetoroka tena hadi kwenye ulimwengu mkubwa zamani. Njia ambayo mtaitembea siku zijazo itakuwa njia ya mateso, na mkitembea hatua ya sasa ya njia vizuri, mtakapopatwa na dhiki kuu baadaye, mtakuwa na ushuhuda. Ikiwa unaelewa umuhimu wa maisha ya binadamu na umechukua njia sahihi ya maisha ya binadamu, na ikiwa katika siku zijazo, bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, utatii mbinu Zake bila malalamiko yoyote au chaguo, na hutakuwa na matakwa yoyote kwa Mungu, kwa njia hii utakuwa mtu wa thamani. Hivi sasa hujapitia taabu, hivyo unaweza kutii chochote. Unasema kwamba vyovyote aongozavyo Mungu ni vizuri, na kwamba utatii miundo Yake yote. Mungu akikuadibu au kukulaani, utakuwa tayari kumridhisha. Baada ya kusema hivyo, unachosema sasa hakiwakilishi kimo chako kwa lazima. Ulicho tayari kufanya sasa hakiwezi kuonyesha kwamba una uwezo wa kufuata mpaka mwisho. Dhiki kuu zitakapokujia au unapopitia mateso au kulazimishwa kiasi, au majaribio makubwa, hutaweza kuyasema maneno hayo. Ikiwa unaweza kuwa na ufahamu wa aina hiyo kisha usimame imara, hiki tu ndicho kitakuwa kimo chako. Petro alikuwa vipi wakati huo? Alisema: “Bwana, nitatoa maisha yangu kafara kwa ajili Yako. Ikiwa ungependa nife, nitakufa!” Hivyo ndivyo alivyoomba wakati huo pia, na pia alisema: “Hata kama wengine hawakupendi, lazima nikupende mpaka mwisho. Nitakufuata wakati wote.” Hivyo ndivyo alivyosema wakati huo, lakini mara tu majaribio yalipomjia, akavunjika moyo na kulia. Nyote mnajua kwamba Petro alimkana Bwana mara tatu, siyo? Kuna watu wengi ambao watalia na kuonyesha udhaifu wa wanadamu wakati ambapo majaribio yatawajia. Wewe si bwana wako mwenyewe. Katika hili, huwezi kujidhibiti. Labda leo unaendelea vizuri sana, lakini hiyo ni kwa sababu una mazingira yanayofaa. Ikiwa hilo lingebadilika kesho, ungeonyesha woga wako na kutoweza kwako, na ungeonyesha pia kustahili dharau kwako na kutothaminika kwako. “Ujasiri” wako ungekuwa umepotea bure muda mrefu uliopita, na wakati mwingine hata ungeshindwa na kuondoka. Hii inaonyesha kwamba kile ulichokielewa wakati huo si kimo chako halisi. Mtu lazima aangalie kimo halisi cha mtu ili aone kama anampenda Mungu kwa kweli, kama anaweza kutii mpango wa Mungu, na kama anaweza kutia nguvu zake zote katika kufikia kile ambacho Mungu anahitaji na bado kusalia kujitolea kwa Mungu na kutoa kile kilicho bora zaidi kwa Mungu, hata ikiwa inamaanisha kutoa maisha yake mwenyewe.

Lazima ukumbuke kwamba maneno haya yamezungumzwa sasa: Baadaye, utapitia shida kubwa zaidi na mateso makubwa zaidi! Kukamilishwa si jambo la kawaida au rahisi. Angalau kabisa lazima uwe na imani ya Ayubu au labda hata imani kubwa kuliko yake. Unapaswa kujua kwamba majaribio wakati ujao yatakuwa makubwa zaidi kuliko majaribio ya Ayubu, na kwamba bado unapaswa kupitia kuadibiwa kwa muda mrefu. Je, hili ni jambo rahisi? Ikiwa ubora wako wa tabia hauwezi kuboreshwa, uwezo wako wa kuelewa umepungukiwa, na unajua kidogo sana, basi wakati huo hutakuwa na ushuhuda wowote, lakini utakuwa mpumbavu, kitu cha kuchezewa na Shetani. Ikiwa huwezi kushikilia maono sasa, basi huna msingi wowote hata kidogo, na utaondolewa siku zijazo! Kila sehemu ya barabara si rahisi kutembea, kwa hiyo usichukulie hili kwa urahisi. Chunguza hili kwa uangalifu sasa na ufanye maandalizi ya jinsi ya kutembea hatua ya mwisho kabisa ya njia hii. Hii ndiyo njia ambayo inapaswa kuchukuliwa siku zijazo na watu wote wanapaswa kuichukua. Huwezi kuruhusu ufahamu huu wa sasa uingie katika sikio moja na kutokea kwa hilo lingine, wala usifikiri kwamba kile Ninachosema kwako yote ni kupoteza pumzi. Siku itakuja wakati ambapo utakitumia vizuri—maneno hayawezi kusemwa bure. Huu ndio wakati wa kujitayarisha; ni wakati wa kuandaa njia kwa ajili ya siku zijazo. Unapaswa kuandaa njia ambayo unapaswa kutembea baadaye; unapaswa kuwa na hangaiko na wasiwasi kuhusu jinsi utakavyoweza kusimama imara baadaye na kujiandaa vizuri kwa ajili ya njia yako ya baadaye. Usiwe mlafi na mvivu! Lazima ufanye kila kitu unachoweza kabisa kutumia vizuri muda wako ili upate kila kitu unachohitaji. Nakupa kila kitu ili uweze kuelewa. Mmeona kwa macho yenu wenyewe kwamba katika chini ya miaka mitatu, Nimesema mambo mengi na kufanya kazi nyingi. Kipengele kimoja cha kufanya kazi kwa njia hii ni kwa sababu watu wana mapungufu sana, na kipengele kingine ni kwa sababu muda ni mfupi sana na hakuwezi kuwa na kuchelewa zaidi. Kulingana na vile unavyoufikiria, watu lazima kwanza wapate udhahiri wa ndani usio na dosari kabla waweze kuwa shahidi na kutumiwa—je, hiyo si polepole sana? Kwa hiyo Nitalazimika kukuandama kwa kiasi gani cha muda? Ikiwa ungependa Niandamane nawe hadi Nitakapokuwa mzee na mwenye mvi, hilo halitawezekana! Kwa kupitia dhiki kubwa zaidi, ufahamu wa kweli ndani ya watu wote utafanikishwa. Hii ni hatua ya kazi. Mara tu unapofahamu kikamilifu maono yaliyoshirikishwa leo na ufanikishe kuwa na kimo halisi, dhiki zozote utakazopitia wakati ujao hazitakushinda—utaweza kuzihimili. Wakati Nimekamilisha hatua hii ya mwisho ya kazi na Nimemaliza kuyatamka maneno ya mwisho, baadaye watu watahitaji kutembea njia yao wenyewe. Hii itatimiza maneno yaliyosemwa awali: Roho Mtakatifu ana agizo kwa kila mmoja, na kazi ya kufanya katika kila mmoja. Katika siku zijazo, kila mtu atatembea njia ambayo anapaswa kuchukua, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Nani ataweza kuwatunza wengine wakati wa kupitia mateso? Kila mtu ana mateso yake mwenyewe, na kila mmoja ana kimo chake mwenyewe. Hakuna kimo cha mtu kilicho sawa na cha mtu mwingine. Waume hawatawachunga wake zao na wazazi hawatawachunga watoto wao; hakuna mtu atakayeweza kumchunga mtu mwingine yeyote. Sio kama sasa—utunzaji na usaidizi wa pande mbili bado unawezekana. Hiyo itakuwa wakati wa kufichua kila aina ya mtu. Yaani, wakati ambapo Mungu anampiga mchungaji, kondoo wa kundi litatawanyika, na wakati huo hamtakuwa na kiongozi yeyote wa kweli. Watu watagawanyika—haitakuwa kama sasa, ambapo mnaweza kukusanyika pamoja kama mkusanyiko wa watu. Baadaye, wale ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wataonyesha tabia zao za kweli. Wanaume watawasaliti wake zao, wake watawasaliti waume zao, watoto watawasaliti wazazi wao, wazazi watawatesa watoto wao—moyo wa binadamu hauwezi kutabiriwa! Yote ambayo yanaweza kufanywa ni kwa mtu kushikilia kile anacho, na kutembea hatua ya mwisho ya njia vizuri. Hivi sasa hamuoni haya kwa uwazi na nyote ni wasioona mbali. Kufanikiwa katika kupitia hatua hii ya kazi silo jambo rahisi.

Wakati wa dhiki hautakuwa wa muda mrefu sana—hautakuwa hata mwaka. Ikiwa ungedumu kwa mwaka mmoja ungechelewesha hatua ya pili ya kazi, na kimo cha watu hakitakuwa kimetosha. Kama ungekuwa muda mrefu sana hawangeweza kuuhimili—vimo vyao vina mipaka yake. Baada ya kazi Yangu kukamilika, hatua inayofuata itakuwa kwa watu kutembea katika njia wanayopaswa. Kila mtu lazima aelewe njia anayopaswa kutembea—hii ni njia ya mateso na mchakato wa kuteseka, na pia ni njia ya kusafisha radhi yako ya kumpenda Mungu. Unapaswa kuingia katika ukweli gani, ni ukweli gani unapaswa kuongezea, unavyopaswa kupitia, na unapaswa kuingia kutoka kwa kipengele kipi—unapaswa kuelewa mambo yote haya. Lazima ujiandae sasa. Ukisubiri mpaka dhiki ikujie, muda utakuwa umechelewa sana. Kila mtu lazima awe na mzigo kwa ajili ya maisha yake mwenyewe; daima usisubiri maonyo ya wengine au wao kuzungumza nawe kila wakati. Nimesema mengi sana lakini bado hujui unapaswa kuingia katika ukweli gani au kujiandaa mwenyewe nao. Hii inaonyesha kwamba hujatia juhudi katika kusoma maneno ya Mungu. Huubebi mzigo wowote kwa ajili ya maisha yako kabisa—je, hilo linawezaje kuwa sawa? Huna uwazi kuhusu kile unachopaswa kuingia katika, huelewi kile unachopaswa kuelewa, na wewe hujali kabisa kuhusu njia ya baadaye unayopaswa kuchukua—je, si wewe tu ni vipande vidogo sana vya mabaki ya meli yanayoelea majini? Je, wewe una maana gani? Mnachofanya sasa ni kujenga na kuandaa njia zenu wenyewe. Lazima ujue kile ambacho watu wanapaswa kufanikisha na kiwango cha mahitaji ya Mungu kwa wanadamu. Lazima uwe na ufahamu ufuatao: Bila kujali chochote, ingawa mimi ni mpotovu sana, ni lazima nifidie mapungufu haya mbele ya Mungu. Wakati ambapo Mungu hakuwa ameniambia, sikuelewa, lakini sasa kwa kuwa Ameniambia, kwa kuwa nimeelewa lazima niharakishe kufidia, kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na kuishi kwa kudhihirisha mfano ambao unaweza kuyakidhi mapenzi ya Mungu. Hata kama siwezi kufikia kile Petro alichofanya, angalau kabisa ni lazima niishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na kwa njia hii naweza kukidhi moyo wa Mungu.

Hatua ya mwisho ya njia hii inatoka sasa hadi mwisho wa dhiki ya baadaye. Hatua hii ya njia utakuwa wakati ambapo vimo halisi vya watu vitafunuliwa na kama wana imani ya kweli au la. Kwa kuwa hatua hii ya njia itakuwa ngumu zaidi kuliko yoyote ambayo ilipitiwa katika siku za nyuma, na itakuwa barabara iliyojaa mawe kuliko hapo awali, inaitwa “hatua ya mwisho ya njia.” Ukweli ni kwamba si sehemu ya mwisho ya barabara; hii ni kwa sababu baada ya kupata dhiki, utapitia kazi ya kupanua injili na kutakuwa na sehemu ya watu ambao watapitia kazi ya kutumiwa. Kwa hivyo “hatua ya mwisho ya njia” huzungumzwa tu kwa kutaja dhiki ya kusafisha watu na mazingira magumu. Katika sehemu hiyo ya barabara katika siku za nyuma, ni Mimi Mwenyewe ndiye Niliyekuwa Nikikuongoza katika safari yako ya furaha, Nikikuchukua kwa mkono kukufundisha na Kukulisha kinywa—kwa—kinywa. Ingawa umepitia kuadibu na hukumu mara nyingi, vimekuwa mapigo madogo kwako yaliyorudiwa rudiwa tu. Kwa kweli hiyo imesababisha mtazamo wako kuhusu imani katika Mungu kubadilika kabisa kidogo; imesababisha pia tabia yako kuwa imara kidogo, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mdogo kunihusu. Lakini Nasema hili, kwa kutembea katika sehemu hiyo ya njia, gharama au jitihada zilizolipwa na watu ni ndogo sana—ni Mimi niliyekuongoza hadi leo. Hii ni kwa sababu Mimi sikuhitaji kufanya chochote na mahitaji Yangu kwako si ya juu kamwe—Nakuruhusu tu wewe kuchukua kile kinachopatikana. Katika kipindi hiki Nimeyakimu mahitaji yenu bila kukoma, na Sijawahi kamwe kuwa na madai yasiyofaa. Mmepitia kuadibiwa mara kwa mara lakini bado hamjafikia mahitaji Yangu ya awali. Mnarudi nyuma na huvunjika moyo, lakini Sizingatii hili kwa sababu huu sasa ni wakati wa kazi Yangu binafsi na Sichukulii kwa uzito “kujitolea” kwako kwa ajili Yangu. Lakini katika njia kutoka hapa kuendelea, Sitafanya kazi tena au kuzungumza, na wakati huo Sitawafanya tena muendelee katika mtindo kama huu usiovutia. Nitawaruhusu kuwa na masomo maridhawa ya kujifunza, na Sitawaruhusu kuchukua kile kinachopatikana. Vimo halisi mlivyo navyo leo lazima vifunuliwe. Ikiwa jitihada zenu za miaka mingi zimekuwa za faida au la itaonekana katika jinsi mnavyotembea hatua ya mwisho ya njia. Katika siku za nyuma, mlifikiri kuwa kumwamini Mungu kulikuwa rahisi sana, na hiyo ilikuwa kwa sababu Mungu hakuwa makini na wewe. Na sasa je? Je, mnafikiri kuwa kumwamini Mungu ni rahisi? Je, bado mnahisi kuwa kuamini katika Mungu ni furaha na bila mawazo kama watoto wanaocheza mitaani? Ni kweli kwamba wewe ni kondoo, hata hivyo, lazima uwe na uwezo wa kutembea njia ambayo unapaswa kutembea ili kulipa neema ya Mungu, na kumpata kabisa Mungu unayeamini. Msijichezee wenyewe—msijipumbaze! Ikiwa unaweza kufaulu katika hatua hii ya njia, utakuwa na uwezo wa kuona hali isiyokuwa ya kawaida, ya ajabu ya kazi Yangu ya injili ikienea katika ulimwengu wote, na utakuwa na bahati nzuri ya kuwa mwandani Wangu wa karibu, na kutekeleza sehemu yako katika kupanua Kazi Yangu katika ulimwengu wote. Wakati huo, utafurahia sana kutembea kwenye njia ambayo unapaswa kutembea. Siku zijazo zitakuwa na uchangamfu usio na mwisho, lakini jambo la msingi sasa ni kutembea hatua ya mwisho ya njia vizuri. Lazima utafute, na ujiandae jinsi ya kufanya hili. Hili ndilo unalopaswa kufanya hivi sasa—hili ni suala la dharura sasa!

Iliyotangulia:Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!

Inayofuata:Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

Maudhui Yanayohusiana

 • Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

  Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo kwa njia inayo…

 • Njia … (8)

  Wakati ambapo Mungu anakuja duniani kuchanganyika na wanadamu, kuishi nao, sio tu kwa siku moja au mbili. Labda kwa wakati huu wote watu wamemjua Mung…

 • Utendaji (2)

  Katika nyakati zilizopita, watu walijifunza wenyewe kuwa na Mungu na kuishi ndani ya roho kila wakati. Ukilinganishwa na utendaji wa leo, hayo ni ma…

 • Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!

  Kwa sasa kuna watu wengi ambao huamini kwa njia ya rabsha. Udadisi wenu ni mkubwa mno, tamaa yenu ya kufuatilia baraka ni kubwa mno, na hamu yenu ya k…