Sura ya 45

Mnawahukumu ndugu zenu hadharani kana kwamba si kitu. Hakika hamjui mema na maovu; hamna aibu! Je, hii si tabia mbaya ya kifidhuli, ya kutojali? Kila mmoja wenu amechanganyikiwa na ni mwenye moyo mzito; mnabeba mizigo mingi na hakuna sehemu Yangu ndani yako. Watu vipofu! Ninyi ni wakatili namna gani—hili litakoma lini?

Nazungumza nanyi kutoka moyoni Mwangu mara kwa mara na Ninawapa kila kitu Nilicho nacho, lakini ninyi ni wachoyo sana na hamna ubinadamu hata kidogo; hili kweli ni jambo lisiloeleweka. Kwa nini mnashikilia dhana zenu wenyewe? Kwa nini huwezi kuniruhusu Niwe na sehemu kidogo ndani yako? Ningewezaje kuwadhuru? Hampaswi kuendelea kutenda kwa njia hii—hakika siku Yangu haiko mbali na sasa. Msizungumze ovyo ovyo, kutenda kiholela, au kupigana na kusababisha shida; hili lina faida gani katika maisha yenu? Ninawaambieni kwa kweli, hata kama hakuna mtu hata mmoja atakayeokolewa siku Yangu itakapowadia, bado Nitaendelea kushughulikia masuala kulingana na mpango Wangu. Lazima mjue kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu! Hakuna kitu, hakuna mtu, hakuna tukio linalojaribu kuzuia hatua Zangu kwenda mbele. Hampaswi kufikiri kwamba Sina njia ya kutekeleza mapenzi Yangu bila ninyi. Naweza kukwambia kwamba ukiyachukulia maisha yako mwenyewe kwa namna hii hasi, utayaangamiza maisha yako mwenyewe tu na haitakuwa shida Yangu.

Kazi ya Roho Mtakatifu imeendelea hadi hatua fulani na ushuhuda umefikia kilele. Huu ni ukweli ulio wazi. Harakisheni, fungueni macho yenu yasiyoona vizuri, msiruhusu jitihada Zangu za bidii ndani yenu ziwe bure, na msijiingize katika raha tena. Mnafurahia kufanya matendo mema mbele Yangu, lakini wakati Sipo matendo yenu na tabia zenu vinaweza kuinuliwa mbele Zangu ili Nione? Hamjui tofauti kati ya mema na maovu! Ninyi hamnisikilizi, mnafanya jambo moja mbele Yangu na lingine wakati Siko. Bado hamjagundua kwamba Mimi ni Mungu ambaye Anaangalia kwa kina ndani ya moyo wa mwanadamu. Wajinga mlioje!

Baadaye, katika njia iliyo mbele, hampaswi kusababisha ulaghai au kushiriki katika udanganyifu na upotovu, vinginevyo matokeo yatakuwa yasiyofikirika! Bado hamwelewi udanganyifu na upotovu ni nini. Matendo yoyote au tabia ambazo hamwezi kuniruhusu Nione, ambazo hamwezi kuziweka hadharani ni udanganyifu na upotovu. Sasa mnapaswa kuelewa hili! Mkishiriki katika udanganyifu na upotovu katika siku zijazo, msijifanye kuwa hamwelewi, huko ni kufanya tu makosa kwa makusudi, kuwa na hatia hata zaidi. Hii itawasababisha tu kuteketezwa na moto, au hata mambo yakiwa mabaya zaidi, kujiangamiza. Lazima muelewe! Kile mnachokabiliwa nacho leo ni kuadibu kwa upendo; bila shaka si hukumu ya kikatili. Kama hamwezi kuona hili, basi ninyi ni wa kusikitisha sana, na ninyi hamna matumaini kabisa. Kama hamko tayari kukubali kuadibu kwa upendo, basi yanayoweza kuwapata tu ni hukumu ya kikatili. Jambo hilo litakapotokea, msilalamike kwamba Sikuwaambia. Si Mimi niliyekwepa majukumu Yangu bali ni nyinyi ambao hamjasikiliza maneno Yangu na hamjatekeleza maneno Yangu. Ninawaambia hili sasa, Nisije Nikalaumiwa baadaye.

Iliyotangulia: Sura ya 44

Inayofuata: Sura ya 46

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp