Sura ya 44

Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu! Nitafichua mara moja aliye wa kweli na aliye wa uongo. Hakuna haja ya kuwa na hofu, vitu vyote hufanya kazi kwa wakati Wangu. Ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati, ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati—Nitawaambia. Kuleni tu vizuri, kunyweni vizuri, njoo mbele Yangu na Nikaribieni nami Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe. Msiwe na hamu sana ya matokeo ya haraka, kazi Yangu si kitu ambacho kinaweza kufanywa mara moja. Ndani yake kuna hatua Zangu na hekima Yangu, hivyo hekima Yangu inaweza kufichuliwa. Nitawawezesha kuona ni nini kinachofanywa kwa mikono Yangu—kuadhibu uovu na kuzawadia mema. Mimi hakika Simpendelei mtu yeyote. Ninakupenda kwa dhati wewe unayenipenda kwa dhati, na ghadhabu Yangu daima itakuwa pamoja na wale wasionipenda kwa dhati, ili kwamba waweze kukumbuka daima kwamba Mimi ni Mungu wa kweli, Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu. Usitende kwa njia moja mbele ya wengine na utende kwa namna nyingine bila wao kufahamu; Ninaona wazi kila kitu unachofanya na ingawa unaweza kuwadanganya wengine huwezi kunidanganya Mimi. Ninaona yote waziwazi. Haiwezekani kwako kuficha chochote; vyote vimo mikononi Mwangu. Usifikiri kuwa wewe ni mjanja sana, kwa kufanya hesabu zako ndogondogo zikufaidi. Nakwambia: Haijalishi mwanadamu anaweza kubuni mipango kiasi kipi, iwe elfu kadhaa ama elfu nyingi, mwishowe hawezi kuepuka kutoka kwenye kiganja cha mkono Wangu. Vitu na matukio yote huendeshwa katika mikono Yangu, sembuse mtu mmoja! Usijaribu kuepuka au kujificha, usijidanganye au kuficha. Je, huwezi kuona kwamba uso Wangu mtukufu, hasira Yangu na hukumu Yangu imefichuliwa hadharani? Nitahukumu mara moja na bila huruma wale wote ambao hawanitaki Mimi kwa dhati. Huruma Yangu imefika mwisho na hakuna tena iliyobaki. Usiwe mnafiki tena na acha njia zako za kishenzi.

Mwanangu, tahadhari; tumia muda zaidi mbele Zangu nami Nitakuwa msaada wako. Usiogope, toa upanga Wangu mkali ukatao kuwili, na—kulingana na mapenzi Yangu nami—pigana na Shetani mpaka mwishoni, Nitakulinda; usiwe na wasiwasi. Mambo yote yaliyofichwa yatafunguliwa na kufichuliwa. Mimi ni Jua ambalo linatoa nuru, likimulika giza lote bila huruma. Hukumu Yangu imeshuka kabisa na kanisa ni uwanja wa vita. Nyote mnapaswa kuwa tayari na mnapaswa kutoa nafsi zenu zote kwa vita vya mwisho vya uamuzi; Mimi hakika Nitakulinda ili uweze kunipigania vita vizuri, vya ushindi.

Kuwa makini, mioyo ya watu leo ​​ni yenye udanganyifu na haitabiriki na hawapaswi kuaminiwa. Ni Mimi tu Niliye upande wako kabisa. Hakuna udanganyifu ndani Yangu; Niegemee Mimi tu! Hakika wana Wangu watashinda katika vita vya mwisho vya uamuzi na bila shaka Shetani atajitokeza na kushambulia katika uchungu wake wa kifo. Usiogope! Mimi ni nguvu yako, Mimi ni kila kitu chako. Usifikiri juu ya mambo mara kwa mara, huwezi kushughulikia mawazo mengi sana. Nimesema hapo awali, Sitawavuta tena katika njia kwa kuwa hakuna muda wa kupoteza hata kidogo. Sina wakati wa kuwahitaji msikilize kwa makini tena na kuwakumbusha—haiwezekani! Malizeni tu maandalizi yenu kwa ajili ya vita. Mimi nakuwajibikia kikamilifu; vitu vyote viko mikononi Mwangu. Hivi ni vita vya kufa na kupona na yatakuwa mapambano ya kufa na kupona. Lakini unapaswa kutambua kwamba Mimi ni mshindi milele na Asiyeshindwa, na kwamba Shetani bila shaka ataangamia. Hii ni mbinu Yangu, kazi Yangu, mapenzi Yangu na mpango Wangu!

Imekamilika! Yote yamekamilika! Usiwe mwoga au mwenye hofu. Mimi pamoja na wewe na wewe pamoja na Mimi tutakuwa wafalme milele na milele! Maneno ambayo Nimesema hayatabadilika milele na matukio yatawafika hivi karibuni. Kesheni! Mnapaswa kutafakari vizuri kila neno; msiwe na mashaka kuyahusu tena. Lazima muwe wazi kuyahusu! Kumbuka—tumia muda zaidi mbele Zangu!

Iliyotangulia: Sura ya 43

Inayofuata: Sura ya 45

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp