Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 67

Wana Wangu wanaonekana wazi, na wanaonekana mbele ya watu wote. Nitawaadhibu vikali wale wanaothubutu kuwakataa wao kwa wazi; hiyo ni hakika. Leo, wale wote wanaoweza kusimama na kuchunga kanisa sasa wamepata cheo cha mzaliwa wa kwanza na sasa wako pamoja katika utukufu Na Mimi—yale yote yaliyo Yangu ni yenu pia. Ninawakabidhi wale wanaonitii Mimi kwa dhati neema tele, ili uweze kuwa wenye nguvu, zaidi ya nguvu ya wanadamu wengine. Mapenzi Yangu yako juu yenu kwa ukamilifu wana wazaliwa wa kwanza na Nawatakia tu mkomae haraka iwezekanavyo na mkamilishe yale ambayo Nimewapa. Jua hili! Yale ambayo Nimewapa ni mradi wa mwisho wa mpango Wangu wa usimamizi. Ninatarajia tu muweze kunipa Mimi nafsi yako yote kwa moyo wako wote, akili yako yote na nguvu yako yote, na utumie rasilmali kwa ajili Yangu. Muda kweli haumngoji mtu yeyote, na hakuna yeyote, au suala, na hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kuzuia kazi Yangu. Jua hili! Kazi Yangu inaendelea taratibu bila kizuizi katika kila hatua.

Nyayo Zangu zinatembea kote katika miisho ya ulimwengu, macho Yangu daima yanachunguza kila mtu, na hata zaidi Natazama picha yote ya ulimwengu. Maneno Yangu ya utendaji yanafika katika kila pembe ya ulimwengu. Yeyote anayethubutu kutotoa huduma yake Kwangu, yeyote anayethubutu kutokuwa mwaminifu Kwangu, yeyote anayethubutu kulihukumu jina Langu, na yeyote anayethubutu kuwatukana na kuwapaka tope wana Wangu—wale wote ambao kwa kweli wanafanya vitu hivi lazima wapitie hukumu kali. Hukumu Yangu inaanguka kikamilifu. Hivi ni kusema, sasa ni enzi ya hukumu, na kwa uchunguzi wa makini utapata kuwa hukumu Yangu inaendelea kote katika ulimwengu dunia. Bila shaka, familia Yangu haijaachwa; wale ambao fikira zao, maneno, na vitendo havipatani na mapenzi Yangu watahukumiwa. Lazima uelewe, hukumu Yangu inaelekezwa kwa ulimwengu dunia wote, sio tu kikundi kimoja cha watu ama vitu—je, umegundua hili? Kama kwa muda umekuwa na wazo lililopotoka, basi mara moja utapata hukumu ndani yako.

Hukumu Yangu huja kwa maumbo na aina zote. Jua hili! Mimi ni Mungu wa kipekee na wa busara wa ulimwengu dunia! Hakuna kitu kinachozidi nguvu Yangu. Hukumu Zangu zote zimefichuliwa kwenu: Kama una mawazo yoyote yasiyo sahihi basi Nitakupa ufunuo. Yaani, Nitakuonya. Kama hutasikia, basi Nitakuacha mara moja (hili halihusu kushuku jina Langu, lakini kwa tabia za nje—zile zinazohusu raha za kimwili). Kama mawazo yako ni ya kunikataa, unanilalamikia, unakubali tena na tena mawazo ya Shetani na hufuati hisia za maisha, basi roho yako itakuwa gizani na mwili wako utapitia uchungu. Lazima uwe karibu na Mimi. Hutaweza kabisa kurejesha hali yako ya kawaida kwa siku moja au mbili tu, na maisha yako yataonekana kubaki nyuma zaidi. Wale ambao hotuba yao haifai Nitaadhibu midomo yako na ndimi na kufanya ndimi zako kupitia ushughulikaji. Wale ambao bila kupinga ni wapotovu kwa matendo Nitakuonya kwa roho zenu, na Nitaadhibu vikali wale ambao hawasikii. Wale ambao wananihukumu na kunikana kwa wazi, yaani wale ambao wanaonyesha kutotii kwa neno ama kwa tendo, Nitawaondoa kabisa na kuwaacha, Nitawafanya kuangamia na kupoteza baraka za juu; hao ni wale ambao wanaondolewa baada ya kuchaguliwa. Wale ambao ni wajinga, yaani wale ambao maono yao sio wazi, bado Nitawapa nuru na kuwaokoa. Lakini wale ambao wanaelewa ukweli lakini hawauweki katika vitendo watapewa adhabu kulingana na sheria ambazo zimetajwa hapo juu, iwe hawajui au la. Kwa wale watu ambao nia zao hazijakuwa sahihi tangu mwanzo, Nitawafanya wasiweze milele kuelewa uhalisi na mwishowe wataondolewa hatua kwa hatua, mmoja kwa mmoja—hakuna hata mmoja atakayebaki—lakini wanabaki sasa kwa mpango Wangu (kwani Sifanyi vitu kwa haraka, ila kwa mtindo wa utaratibu).

Hukumu Yangu imefichuliwa kabisa, imelengwa kwa watu tofauti, na wote lazima wachukue nafasi zao zinazostahili. Ikitegemea ni sheria gani iliyovunjwa, Nitawaadhibu na kuwahukumu kulingana na sheria hiyo. Na kwa wale ambao hawako katika jina hili na hawamkubali Kristo wa siku za Mwisho, kuna sheria moja tu: Nitachukua roho mara moja, roho na mwili wa yeyote anayenikataa na kuwatupa Kuzimu; wowote ambao hawanikatai Mimi, Nitangoja mkomae kabla ya kufanya hukumu ya pili. Maneno Yangu yanaeleza yote kwa uwazi kamili na hakuna kilichofichwa. Ninatarajia tu kuwa mtaweza kuyaweka akilini kila wakati!

Iliyotangulia:Sura ya 66

Inayofuata:Sura ya 68

Maudhui Yanayohusiana

 • Sura ya 38

  Kufuatana na sifa za asili za wanadamu, yaani, uso halisi wa wanadamu, kuweza kuendelea hadi sasa hakujakuwa jambo rahisi kweli, na ni kwa njia hii t…

 • Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

  Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza k…

 • Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

  Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria…

 • Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

  Je, unaweza kuonyesha tabia ya Mungu ya nyakati kwa lugha inayofaa iliyo na umuhimu wa nyakati? Kupitia uzoefu wako wa kazi ya Mungu, unaweza kueleza…