Sura ya 19

Ni wajibu wa mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kujiletea maangamizo na kujiletea dharau. Ubinadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha. Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda michango ya mwanadamu, lakini Nachukia madai yake. Wanadamu wote wana mioyo iliyojaa ulafi; ni kama moyo wa binadamu unadhibitiwa na Shetani, na mwanadamu hawezi kuponyoka na kutoa moyo wake Kwangu. Ninapozungumza, watu husikiliza sauti Yangu kwa makini sana; Ninaponyamaza kimya, hata hivyo, wao huanza “shughuli” zao wenyewe na kuacha kabisa kusikiliza maneno Yangu, kana kwamba maneno Yangu yalikuwa tu kijalizo cha “shughuli” zao. Sijawahi kuwa mzembe kwa binadamu, na bado Nimekuwa pia mwenye subira na mvumilivu kwa binadamu. Na hivyo, kwa sababu ya huruma Yangu, binadamu wote hujiinua na wanakosa maarifa na kujitafakari; wanatumia vibaya uvumilivu Wangu ili kunidanganya. Hakuna mmoja kati yao anayenijali kwa dhati, na hakuna mmoja kweli ananithamini kama kitu apendacho moyoni mwake; ni wakati tu walipo na wakati wa ziada ndipo wanaponitambua kwa kiwango duni. Juhudi ambazo Nimetumia kwa mwanadamu tayari ni zaidi ya kipimo. Ninamfanyia mwanadamu aina ya pekee ya kazi, na mbali na haya, Nimempa mzigo wa ziada, ili, ndani ya kile Ninacho na kile Nilicho, mwanadamu anaweza kupata maarifa na kupitia mabadiliko. Siwataki watu wawe ‘watumiaji’ tu; pia Nawataka wawe “wazalishaji” wanaomshinda Shetani. Ingawa Sidai chochote kutoka kwa mwanadamu, hata hivyo Nina viwango vya matakwa Ninayoyatoa, kwani kuna madhumuni kwa yale Ninayoyafanya, na vile vile msingi wa matendo Yangu: Sichezi kiholela, anavyodhani mwanadamu, wala Siundi mbingu na dunia na mambo mengi ya uumbaji kwa ghafla na bila mpango. Katika kazi Zangu, mwanadamu anapaswa kuwa na uwezo wa kuona kitu, kupata kitu. Wasipoteze wakati wa machipuko ya ujana wao, au wasiyafanye maisha yao kama mavazi ambayo juu yake vumbi limeruhusiwa kukusanyika kwa uzembe; badala yake, wanapaswa kujilinda vikali, wakichukua kutoka kwa fadhila Yangu ili kujipatia starehe zao wenyewe, mpaka, kwa ajili Yangu, hawawezi kumrudia Shetani, na, kwa ajili Yangu, wanafanya mashambulizi dhidi ya Shetani. Je, madai Yangu kwa ubinadamu si rahisi sana?

Mwangaza hafifu wa nuru unapoanza kuonekana katika Mashariki, watu wote katika ulimwengu huupa uangalifu zaidi. Wakiwa hawajalala, wanadamu wanajitokeza kutazama chanzo cha nuru hii ya mashariki. Kwa sababu ya uwezo wao mdogo, bado hakuna mtu ambaye ameweza kuona mahali ambapo nuru inatokea. Wakati yote yaliyo ulimwenguni yameangaziwa kabisa, binadamu watazinduka kutoka usingizini na ndotoni, na ni hapo tu ndipo wanapotambua pole pole kwamba siku Yangu imewajia. Binadamu wote wanasherehekea kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu ya haya hawalali tena, na si wapumbavu tena. Chini ya mng’aro wa mwangaza Wangu, binadamu wote wanakuwa na uwazi wa akili na mtazamo, na ghafla wanakuwa na furaha ya maisha. Chini ya kifuniko cha ukungu, Naulinda ulimwengu. Wanyama wote wako katika mapumziko; kwa sababu ya ujio wa mwangaza hafifu, kila kitu katika uumbaji kinafahamu kwamba maisha mapya yanakaribia. Kwa sababu hii, wanyama pia wanatoka nje ya mapango yao, kutafuta chakula. Mimea, bila shaka, si tofauti, na kwa mng’aro wa mwangaza majani yao ya kijani yanang’aa, yakingoja kutekeleza sehemu yao wenyewe kwa ajili Yangu Nikiwa duniani. Wanadamu wote wanatamani ujio wa nuru, na bado wanaogopa ujio wake, wakiwa na wasiwasi mwingi kwamba ubaya wao wenyewe hautafichwa tena. Hii ni kwa sababu wanadamu wako uchi kabisa, na wanakosa chochote cha kuwafunika. Kwa hivyo, watu wengi wameingiwa na hofu kutokana na kuja kwa nuru, na wako katika hali ya mshtuko kwa sababu ya kuonekana kwake? Watu wengi sana, wanapoona nuru, wamejawa na majuto yasiyo na kikomo, wakichukia uchafu wao wenyewe, ilhali, bila uwezo wa kubadilisha ukweli, hawawezi kufanya lolote ila kungoja Mimi Nitoe hukumu. Watu wengi sana, waliosafishwa na mateso gizani, wanapoiona nuru, ghafla huguswa na maana yake ya kina, na tangu hapo huikumbatia nuru hiyo karibu na vifua vyao, wakiogopa sana kuipoteza tena. Watu wengi, badala ya kutupwa nje ya uzingo na mwonekano wa ghafla wa nuru, wanaendelea tu na kazi ya kila siku mikononi mwao kwa sababu wamekuwa vipofu kwa miaka mingi na kwa hivyo sio tu kwamba hawaoni kuwa nuru imekuja, lakini pia hawaridhishwi nayo. Katika mioyo ya wanadamu, Mimi si wa juu, wala duni. Kwa kadiri wanavyohusika, haileti tofauti ikiwa Nipo au la; ni kana kwamba maisha ya watu hayangepata upweke zaidi kama Singekuwapo, na kama Ningekuwepo, maisha yao yasingekuwa ya furaha zaidi. Kwa sababu wanadamu hawanithamini, raha Ninayowapa ni chache. Lakini punde tu ubinadamu unaponiabudu kidogo, basi pia Nitafanya mabadiliko kwa mtazamo Wangu kwa binadamu. Kwa sababu hii, wakati tu ubinadamu unapofahamu sheria hii, ndipo tu wanadamu watakapokuwa na bahati ya kujitolea Kwangu na kudai vitu vilivyo mikononi Mwangu. Hakika pendo la mwanadamu Kwangu halifungwi tu na maslahi yake mwenyewe? Hakika imani yake Kwangu haifungwi tu kwa mambo Ninayompa? Inaweza kuwa kwamba, isipokuwa tu yeye kuona mwangaza Wangu, mwanadamu hawezi kunipenda kwa dhati kwa njia ya imani yake? Hakika nguvu za mwanadamu na afya hazizuiliwi na hali ya leo? Inaweza kuwa kwamba mwanadamu anahitaji ujasiri ili anipende?

Kutegemea kuwepo Kwangu, mambo mengi ya uumbaji yanakubali kwa utiifu mahali yanamoishi, na katu, bila ya nidhamu Yangu, hayajihusishi na uasherati bila kujali. Kwa hiyo, milima inakuwa mipaka kati ya mataifa ulimwenguni, maji yanakuwa vikwazo vya kuwatenga watu wa nchi tofauti mbali mbali, na hewa inapuliza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika nafasi zilizo juu ya dunia. Binadamu tu ndio hawawezi kweli kutii matakwa ya mapenzi Yangu; hii ndiyo maana Nasema kwamba, kwa viumbe vyote, mwanadamu pekee ni ndiye wa kundi la wasiotii. Mwanadamu hajawahi kweli kunitii, na kwa sababu hii wakati wote Nimemweka chini ya nidhamu kali. Iwapo katikati ya ubinadamu, itakuja kuwa kwamba utukufu Wangu umetandaa ulimwengu nzima, basi hakika Nitachukua utukufu Wangu wote na kuufanya uwe wazi mbele ya mwanadamu. Kwa sababu katika uchafu wake mwanadamu hafai kutazama utukufu Wangu, kwa maelfu ya miaka Sijawahi kujitokeza hadharani, lakini Nimebakia mafichoni; kwa sababu hii utukufu Wangu hujawahi kuwa wazi mbele ya mwanadamu, na mwanadamu daima amezama kwa shimo la kina la dhambi. Nimeusamehe udhalimu wa binadamu, lakini wanadamu hawajui jinsi ya kujihifadhi, na badala yake daima wanajiweka wazi kwa dhambi, kuruhusu dhambi kuwajeruhi. Huu si ukosefu wa mwanadamu wa kujiheshimu na kujipenda? Katikati ya ubinadamu, kuna kweli yeyote anayeweza kupenda? Je, ibada ya binadamu inaweza kupima wakia ngapi? Je, hakuna bidhaa mbovu zilizochanganywa katika kile kinachoitwa uhalisi wa watu? Si ibada yake imeungana kabisa na mkanganyiko? Ninachohitaji ni upendo wa mwanadamu usiogawanyika. Wanadamu hawanijui, na ingawa wanaweza kutafuta kunijua, hawatanipa Mimi mioyo yao ya kweli na ya dhati. Kutoka kwa wanadamu sidai kile ambacho hawako tayari kutoa. Iwapo watanipa Mimi ibada yao, Nitaikubali bila pingamizi. Iwapo hawataniamini Mimi, na kukataa kutoa hata chembe moja yao Kwangu, basi, badala ya kukasirika zaidi kwa sababu hiyo, Nitawaondoa kwa njia nyingine na kuwapangia hatima inayowafaa. Radi, inayovuma angani, itawapiga wanadamu; milima mirefu, itakapoanguka, itawazika; wanyama wakali katika njaa yao watawala; na bahari, zikifurika, zitawagubika juu ya vichwa vyao. Ubinadamu unapojihusisha na migogoro ya jamii, wanadamu wote watatafuta maangamizi yao wenyewe katika majanga yatokayo katikati yao.

Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; ubinadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtasimama imara na thabiti katika nchi ya Sinimu. Kupitia katika mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.

Machi 19, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 18

Inayofuata: Sura ya 20

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp