Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa

Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati ya hawa wafuasi wote, kuna wale wanaohudumu kama makuhani, wale wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Nawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina zao, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu. Moja baada ya mwingine, Nayaita makundi ya wale Ningependa kuwaokoa kurejea katika nyumba Yangu, kisha Nawaruhusu watu hawa wote wakubali kazi Yangu katika siku za mwisho. Wakati uo huo, Nawaainisha wanadamu kulingana na aina, kisha Namtunuku au kumwadhibu kila mmoja kulingana na matendo yake. Hizi ndizo hatua zinazojumuisha kazi Yangu.

Sasa Naishi duniani na Naishi miongoni mwa wanadamu. Wanadamu wote wanashuhudia kazi Yangu na kutazama matamko Yangu, na pamoja na hili Natoa ukweli kwa kila mfuasi Wangu ili waweze kupokea uzima kutoka Kwangu na hivyo apate njia anayoweza kufuata. Kwa maana Mimi ni Mungu, mpaji wa uhai. Katika miaka mingi ya kazi Yangu, mwanadamu amepokea vitu vingi na kujinyima vitu vingi, lakini bado Nasema kuwa mwanadamu haniamini kikamilifu. Kwa maana mwanadamu anakubali kijuujuu tu kuwa Mimi ni Mungu lakini hakubaliani na ukweli Ninaounena, sembuse kuuweka ukweli katika matendo Ninavyohitaji kwake. Hiyo ni kusema, mwanadamu anakubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio ule wa ukweli; mwanadamu hukubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio wa uzima; mwanadamu anakubali tu jina la Mungu, lakini sio kiini Chake. Kutokana na ari yake, mwanadamu amekuwa chukizo mbele Zangu. Kwa kuwa mwanadamu anatumia tu maneno yanayofurahisha masikio kunihadaa, na hakuna anayeniabudu kwa moyo wa kweli. Maneno yenu yanabeba majaribu ya ibilisi. Na maneno yenu ni yenye kiburi kupindukia, ni vile tu kama yamesemwa na malaika mkuu. Zaidi ya hayo, matendo yenu yamechakaa; tamaa zenu zisizo na kiasi na nia zenu zenye tamaa ni za kukera zikisikizwa. Nyote mmegeuka nondo katika nyumba Yangu, vyombo vya kukataliwa na chukizo. Kwa maana hapana kati yenu ambao ni wapenda ukweli, bali ni wanadamu wanaopenda baraka tu, walio na matamanio ya kupaa mbinguni, na ya kumwona Kristo anapoonyesha nguvu Zake duniani. Lakini mmewahi kuwaza jinsi mwanadamu kama ninyi, aliyepotoka sana, na asiyejua kabisa Mungu ni nini, angestahili kumfuata Mungu? Mnawezaje kupaa mbinguni? Mnawezaje kustahili kuuona uzuri wa ukuu usio na kifani? Vinywa vyenu vimejaa maneno ya uongo na uchafu, usaliti na kiburi. Kamwe hamjawahi kunena maneno ya ukweli Kwangu, wala maneno matakatifu, wala maneno ya kunitii baada ya kulipitia neno Langu. Hatimaye, hii imani yenu ni ya aina gani? Nyoyo zenu zimejaa tamaa na mali, mawazo yenu yamejaa mali ya kilimwengu. Kila siku, mnafanya hesabu jinsi mtakavyofaidika kutoka Kwangu, mkihesabu kiasi cha mali na vitu vya kidunia mlivyopata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangoja baraka zaidi ziwashukie ili muweze kufurahia, hata zaidi na vyema zaidi, vitu zaidi vya raha. Vile vilivyo katika mawazo yenu kila wakati si Mimi, wala ukweli utokao Kwangu, bali ni mume (mke), mwanao, bintiyo au mlacho na kuvaa, na vile mtakavyoburudika na starehe nzuri zaidi. Hata mlishindilie tumbo lenu kwa vyakula hadi pomoni, je, si nyinyi bado ni zaidi ya maiti tu? Hata wakati ambapo, kwa nje, mnavalia mavazi ya kupendeza sana, si nyinyi bado ni maiti inayotembea isiyo na uhai? Mnafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya tumbo lenu mpaka mnapotokwa na mvi, ilhali hakuna aliye tayari kuutoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnasafiri kila mara, mnafanya kazi na kupiga bongo kwa ajili ya miili yenu, na kwa sababu ya watoto wenu, ilhali hakuna yeyote anayeshughulika wala kufikiria kuhusu mapenzi Yangu. Ni nini ambacho bado mnatarajia kufaidi kutoka Kwangu?

Katika kufanya kazi Yangu, kamwe Siharakishwi. Hata mwanadamu anifuate vipi, Mimi hufanya kazi Yangu kulingana na kila hatua, kulingana na mpango Wangu. Kwa hivyo, hata ingawa mnaweza kuasi dhidi Yangu sana, bado Sisimamishi kazi Yangu na Ninaendelea kunena maneno Ninayotaka kunena. Nawaita katika nyumba Yangu wale Niliowajaalia kulisikiliza neno Langu, kisha Nawaweka wote wanaotii na kulitarajia neno Langu mbele ya kiti Changu cha enzi. Wale wanaolisaliti neno Langu, wale wasiotii na kujisalimisha Kwangu, na wale wanaonipinga kwa wazi, watatupwa kando wakingoja adhabu ya mwisho. Wanadamu wote wanaishi katika upotovu na chini ya mkono wa yule mwovu, kwa hivyo sio wengi wanaonifuata wako na hamu ya ukweli kwa hakika. Hiyo ni kusema, wengi wao hawaniabudu kwa moyo wa kweli au kwa ukweli, lakini wanajaribu kupata uaminifu Wangu kupitia ufisadi, uasi na njia nyinginezo danganyifu. Ni kwa sababu hii ndiyo Nasema: Wengi wameitwa, lakini ni wachache wamechaguliwa. Wote walioitwa wametoka kupindukia na wanaishi katika enzi sawa, lakini wale waliochaguliwa ni lile kundi tu la wanaoamini na kuukubali ukweli na kuutia ukweli katika matendo. Wanadamu hawa ni sehemu ndogo tu ya wanadamu wote, na kutoka miongoni mwa wanadamu hawa Nitapata utukufu zaidi. Ukijipima kulingana na maneno haya, je, mnajua kama nyinyi mumo kati ya waliochaguliwa? Je, hatima yenu itakuwa namna gani?

Tayari Nimeshasema kuwa wale wanaonifuata ni wengi lakini wanaonipenda kwa moyo wa kweli ni wachache. Huenda ikawa wengine wanasema, “Ningeweza kulipa gharama kubwa kiasi hicho kama ningekuwa sikupendi Wewe? Ningefuata mpaka hatua hii kama singekuwa nakupenda?” Kwa hakika, unazo sababu nyingi, kwa hakika, upendo wako ni mkubwa sana, lakini umuhimu wa mapenzi yako Kwangu ni nini? “Upendo,” kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi, na kuwa na mawazo. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi na hakuna kutenga. Katika upendo hakuna shaka, hakuna uongo na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna mabadilishano na hakuna kitu kisicho safi. Ukipenda, basi hutadanganya, hutalalamika, hutalalamika, hutaasi kulazimisha au kutafuta kupata kitu au kupata kiwango fulani. Ukipenda, basi utajinyima bila kusononeka na kuvumilia hali ngumu, na utaambatana na Mimi. Utaacha kila kitu chako kwa sababu Yangu, utaacha familia yako, siku zako za baadaye, ujana wako, na ndoa yako. La sivyo, basi upendo wako haungekuwa upendo hata kidogo, bali ungekuwa uongo na usaliti! Upendo wako ni upendo wa aina gani? Je, ni upendo wa kweli? Je, ni wa uongo? Umejinyima kiasi gani? Umejitolea kiasi gani? Je, Nimepata upendo kiasi gani kutoka kwako? Je, unajua? Mioyo yenu imejaa maovu, usaliti na uongo na hivyo kuna kiwango kipi cha uchafu katika upendo wenu? Mnafikiri kuwa mmeacha ya kutosha kwa ajili Yangu; mnafikiri kuwa upendo wenu Kwangu tayari umetosha. Ila ni kwa nini basi maneno yenu na matendo yenu huambatana na uasi na uongo daima? Mnanifuata, ilhali hamkubali neno Langu. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, kisha mnanitenga na kunitupa kando. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, na bado mko na shaka na Mimi. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, ilhali hamkubali kuwepo Kwangu. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali hamnitendei vile Ninavyopaswa kutendewa na mnafanya mambo yawe magumu Kwangu katika kila hatua. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, na bado mnanichukua kama mjinga na kunidanganya Mimi katika kila jambo. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanihudumia, na bado hamnichi. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanipinga katika kila hali na kila jambo. Je, yote haya yanachukuliwa kama upendo? Mmejinyima mengi, huu ni ukweli, lakini bado hamjawahi kutenda Ninayowaagiza mfanye. Je, huu unaweza kuchukuliwa kama upendo? Uchunguzi wa makini unaashiria kuwa hamna upendo Kwangu ndani yenu. Baada ya miaka mingi sana ya kazi na maneno yote mengi Niliyosambaza, ni kiasi kipi mlichopokea kwa hakika? Je, hili halistahili kuangaliwa tena kwa makini? Nawaonya: Wale Niwaitao Kwangu sio wale ambao hawajawahi kupotoshwa, bali wale Ninaowachagua ni wale wanaonipenda kwa ukweli. Kwa hivyo, mnapaswa kuwa makini na maneno na matendo yenu, na mchunguze maazimio na mawazo yenu ili vitu hivi visije vikavuka mipaka. Wakati huu wa siku za mwisho, fanyeni jitihada ili muonyeshe mapenzi yenu Kwangu, isije ghadhabu yangu ikabaki kwenu milele!

Iliyotangulia: Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Inayofuata: Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp