Sura ya 7
Matawi yote ya magharibi yanapaswa kuisikiliza sauti Yangu:
Je, mmekuwa waaminifu Kwangu hapo awali? Je, mmeyatii maneno Yangu mazuri ya ushauri? Je, mna matumaini ambayo ni halisi na yasiyo na mashaka? Utiifu wa mwanadamu, upendo wake, imani yake—hamna kipatikanacho ila kutoka Kwangu, hamna hata kimoja ila kilichotolewa na Mimi. Enyi watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je, mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Hapo zamani, mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwaokoa? Ni mara ngapi mmeanguka katika mitego ya Shetani? Ni mara ngapi mmejiingiza katika mitego ya wanadamu? Na tena, ni mara ngapi mmejikuta katika ugomvi usio na kikomo kati yenu kwa kukosa kuziachilia nafsi zenu? Ni mara ngapi miili yenu imekuwa katika nyumba Yangu ila roho zenu zikiwa kusikojulikana? Licha ya hayo, ni mara ngapi Nimewanyooshea mkono Wangu kuwainua; ni mara ngapi Nimewaonea huruma; ni mara ngapi Nimekosa uvumilivu wa kuziona hali zenu za kuhuzunisha za mateso? Ni mara ngapi … je, mnamfahamu?
Lakini leo kwa ulinzi Wangu, hatimaye mmezishinda shida zote na Nafurahia pamoja nanyi; hili ndilo dhihirisho la busara Yangu. Hata hivyo, likumbuke hili vyema! Ni nani kati yenu amewahi kuanguka na akaendelea kuwa thabiti? Ni nani kati yenu amewahi kuwa thabiti bila kuwa na nyakati za unyonge? Miongoni mwa wanadamu, ni nani amewahi kupokea baraka ambazo hazikutoka Kwangu? Ni nani amepitia misukosuko isiyotoka Kwangu? Inawezekana kuwa wale wote wanaonipenda hupokea baraka peke yake? Inawezekana kwamba misukosuko ilimpata Ayubu kwa sababu alikosa kunipenda ila alinikana Mimi? Inawezekana kwamba Paulo aliweza kunihudumia kwa utiifu mbele Yangu kwa sababu aliweza kunipenda kwa dhati? Ijapokuwa mnaweza kushikilia kwa uthabiti ushuhuda Wangu, lakini je, kuna mtu kati yenu aliye na ushuhuda safi kama dhahabu ambayo haijatiwa najisi? Je, mwanadamu anaweza kuwa na uaminifu halisi? Kwamba ushuhuda wenu huniletea furaha hakukinzani na “uaminifu” wenu kwa sababu Sijawahi kumtarajia mtu yeyote kutoa zaidi. Kwa kufuata dhamira asilia ya mpango Wangu, nyinyi nyote mngekuwa “bidhaa zenye kasoro”—zisizokidhi kiwango. Je, huu sio ni mfano wa kile Nilichowaambia kuhusu “kuwaonea huruma”? Je, mnachoona ni wokovu Wangu?
Nyinyi nyote mnafaa kuvuta kumbukumbu zenu: Tangu mrejee katika nyumba Yangu, kuna yeyote kati yenu, bila kutafakari faida na hasara, amenifahamu sawa na Petro alivyonifahamu? Mmekariri Biblia kikamilifu, lakini je, mlijifunza chochote kuhusu kiini chake? Japo hivyo, bado mmeshikilia “mtaji” wenu, mkikataa kuziachilia nafsi zenu. Ninapotoa tamko, Nikiwazungumzia ana kwa ana, Ni nani kati yenu amewahi kuweka chini “nyaraka” zilizofunikwa kupokea maneno ya uzima ambayo Nimeyaweka wazi? Hamyajali maneno Yangu na wala hamyathamini. Badala yake, mnatumia maneno Yangu kama bombomu dhidi ya maadui wenu ili kudumisha nafasi zenu; hamjaribu hata kidogo kuyakubali maoni Yangu ili mnifahamu. Kila mmoja wenu anamwangazia sana mtu mwingine, nyinyi nyote ni “wasio bahili,” nyote “mnawajali wengine” katika kila hali; je, haya siyo hasa mliyokuwa mnafanya jana? Na leo je? “Utiifu” wenu umepanda juu kwa alama kidogo, na nyinyi wote mmekuwa wazoefu kiasi na mmekomaa kidogo; kwa sababu ya haya, “heshima” yenu Kwangu imeongezeka kwa kiasi fulani, na hamna hata mmoja “anatenda bila kujali.” Kwa nini mnaishi katika hali ya ubaridi wa kudumu? Ni kwa nini sifa nzuri hazipatikani kabisa ndani yenu? Enyi watu Wangu! Ya zamani yalipita kitambo; msiendelee kuyashikilia zaidi. Zamani mlishikilia msimamo wenu, leo mnapaswa kunipa utiifu wenu wa dhati, na hata zaidi mnafaa kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu siku za usoni, na mtarithi baraka Zangu hapo baadaye. Hili ndilo mnapaswa kufahamu.
Ingawa Siko nanyi, Roho Wangu hakika ataleta neema juu yenu. Kwa kutegemea hili, Natumaini mtaienzi baraka Yangu na mtaweza kujitambua. Msichukulie hili kuwa mtaji wenu; badala yake, mnatakiwa kujaza kinachokosekana ndani yenu kutoka katika maneno Yangu, na kutoka humu mpate mambo mazuri mnayovihitaji. Huu ndio ujumbe Ninaowaachia.
Februari 28, 1992