Sura ya 32

Watu wanapokusanyika pamoja na Mimi, moyo Wangu unajawa na furaha. Mara moja, Ninatoa baraka zilizo mkononi Mwangu miongoni mwa binadamu, ili watu waweze kukutanika na Mimi, na kutokuwa maadui wanaoniasi lakini marafiki wanaotangamana na Mimi. Hivyo, Mimi pia ni wa dhati kwa mwanadamu. Katika kazi Yangu, mwanadamu anaonekana kama mwanachama wa shirika la ngazi ya juu, hivyo Ninamzingatia zaidi, kwa maana daima amekuwa kusudi la kazi Yangu. Nimeweka imara mahali Pangu katika mioyo ya watu, ili mioyo yao iweze kuniheshimu—ilhali wanabaki wasiojua kabisa kwa nini Ninafanya hili, na hawafanyi lolote ila kusubiri. Ingawa kuna mahali ambapo Nimeweka imara katika mioyo ya watu, hawahitaji kwamba Niishi hapo. Badala yake, wanamsubiri “Mtakatifu” katika mioyo yao kuwasili ghafla. Kwa sababu utambulisho Wangu ni duni sana, Sifikii mahitaji ya watu na hivyo Naondolewa na wao. Kwa sababu wanachotaka ni “Mimi” ambaye ni mkuu na mwenye nguvu—lakini Nilipokuja, Sikuonekana kwa njia hii kwa mwanadamu, kwa hivyo waliendelea kutazama kwa mbali, wakimngoja yule aliye mioyoni mwao. Nilipokuja mbele ya watu, walinikataa mbele ya umati. Ningeweza tu kusimama upande mmoja, Nikingoja “kushughulikiwa” na binadamu, Nikitazama kuona kile ambacho watu wangeishia kufanya na Mimi, hii “bidhaa” yenye upungufu. Siyaangalii makovu ya watu, lakini katika sehemu yao ambayo haina makovu, na kutokana na hili Napata uridhisho. Katika macho ya watu, Mimi ni “nyota ndogo” tu ambayo imeshuka kutoka kwenye anga, Mimi ni mdogo zaidi tu mbinguni, na ujaji Wangu duniani leo uliagizwa na Mungu. Kwa hiyo, watu wamebuni fasiri zaidi za maneno “Mimi” na “Mungu,” wakiogopa sana kumzingatia Mungu pamoja na Mimi kuwa kitu kimoja. Kwa sababu taswira Yangu haina sura ya Mungu hata kidogo, watu wote wanaamini kwamba Mimi ni mtumishi ambaye si wa jamii ya Mungu, na kusema kwamba hii si taswira ya Mungu. Pengine kuna watu ambao wamemwona Mungu—lakini kwa sababu ya ukosefu Wangu wa utambuzi ulimwenguni, Mungu hajawahi “kuonekana” Kwangu. Pengine nina “imani” ndogo sana na hivyo watu wananiona kama aliye duni. Watu wanadhani kwamba iwapo mtu kweli ni Mungu, basi hakika atakuwa stadi katika lugha ya mwanadamu, kwani Mungu ndiye Muumba. Lakini ukweli ni kinyume kabisa: Sio tu kwamba mimi si bingwa katika lugha ya mwanadamu, lakini kuna nyakati ambapo siwezi hata “kukimu” “upungufu” wake. Kwa hivyo, Ninahisi “hatia” kidogo, kwa kuwa sifanyi kama watu “wanataka,” lakini Ninatayarisha tu nyenzo na kufanya kazi kulingana na kile “wanachokosa.” Madai Ninayotoa kwa mwanadamu si makubwa kwa vyovyote, ilhali watu wanaamini vinginevyo. Hivyo, “unyenyekevu” wao unafichuliwa katika kila hatua yao. Daima wanawajibika kutembea mbele Yangu, wakiniongoza njia, wakiogopa sana kwamba Nitapotea, wakiwa na hofu kwamba Nitatangatanga kwenye misitu ya kale ndani kabisa ya milima. Matokeo yake, watu daima wameniongoza mbele, wakiwa na hofu kubwa kwamba Nitaingia kwenye shimo. Nina “hisia nzuri” kwa imani ya watu, kwani “wametaabika” kwa ajili Yangu bila kufikiria chakula au kulala, kiasi kwamba kazi yao kwa ajili Yangu imewaacha bila usingizi mchana na usiku na hata kuwa na nywele nyeupe—ambayo ni kutosha kuonyesha kwamba imani yao “imevuka” ulimwengu mzima, na “kuwapita” mitume na manabii katika enzi zote.

Sipigi makofi kwa shangwe kwa sababu ya ustadi mkubwa wa watu, wala Siwaangalii kwa ubaridi kwa sababu ya mapungufu yao. Mimi hufanya tu kile ambacho kiko mikononi Mwangu, Simpi mtu yeyote upendeleo maalum, lakini Ninafanya kazi tu kulingana na mpango Wangu. Lakini watu hawajui mapenzi Yangu na wanaendelea kuombea vitu kutoka Kwangu, kana kwamba utajiri Niliowapa hauwezi kukidhi mahitaji yao, kana kwamba mahitaji yanashinda ugavi. Lakini katika enzi ya leo, watu wote wanahisi kuna “kupanda kwa gharama za maisha”—na hivyo, wanashughulika sana na kile Nilichowapa wafurahie. Ni kwa sababu ya hili ndio wanachoshwa na Mimi, na hivyo maisha yao yanajaa vurugu, na hawajui kile wanachopaswa na wasichopaswa kula. Wengine hata hushika vitu ambavyo Nimewapa kufurahia, wakivitazama kwa makini. Kwa sababu watu walikuwa wanateseka kutokana na njaa, na si jambo rahisi kwao kupata furaha za leo, wote ni “wenye shukrani zisizokuwa na mwisho,” na kumekuwa na mabadiliko fulani katika mtazamo wao Kwangu. Wanaendelea kulia mbele Yangu; kwa sababu Nimewapa mengi sana, mbele Yangu wanaendelea kuushika mkono Wangu na kutoa “sauti za shukrani.” Natembea juu ya ulimwengu, na Ninapotembea Ninawaangalia kwa makini watu wa ulimwengu mzima. Kati ya umati wa watu duniani, hakujawahi kuwa na wowote ambao wanafaa kwa kazi Yangu ama ambao wananipenda kwa kweli. Hivyo, kwa wakati huu Nahema kwa kuvunjika moyo, na watu wanatawanyika mara moja, wasikusanyike tena, wakiogopa sana kwamba “Nitawakamata wote katika wavu mmoja.” Ninatumia fursa hii kuja miongoni mwa wanadamu, kufanya kazi Yangu—kazi inayofaa—miongoni mwa watu hawa waliotawanyika, Nikiwachagua wale ambao wanafaa kufanyia kazi ndani yao. Sitaki “kuwazuia” watu katikati ya kuadibu Kwangu, wasitoroke kamwe. Nafanya tu kazi ambayo lazima Niifanye. Nimekuja kuomba “msaada” kutoka kwa mwanadamu; kwa sababu usimamizi Wangu unakosa matendo ya mwanadamu, haiwezekani kuimaliza kazi Yangu kwa ufanisi, jambo ambalo linaizuia kazi Yangu kuendelea mbele kwa ufanisi. Natumaini tu kwamba watu wana azimio la kushirikiana na Mimi. Siombi kwamba wanipikie chakula kizuri, au wanipangie mahali pa kufaa ili Nilaze kichwa Changu, au wanitengenezee nguo za kupendeza—Siheshimu vitu hivi hata kidogo. Watu wanapoweza kuelewa mapenzi Yangu na kuendelea mbele na Mimi, bega kwa bega, Nitaridhika moyoni Mwangu.

Ni nani duniani amewahi kunipokea kwa moyo wake? Nani amewahi kunipenda kwa moyo wake? Upendo wa watu daima umefifia, hata Mimi “sijui” kwanini upendo wao umenyauka na usioweza kuzimuliwa. Hivyo, kuna “mafumbo” mengi yaliyo ndani ya mwanadamu pia. Miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, mwanadamu anaonekana waajabu na “asiyeeleweka,” na hivyo amekuwa na “sifa” mbele Yangu, kana kwamba yeye ni wa hadhi sawa na Mimi—lakini haoni chochote kigeni kuhusu hii “hadhi” yake. Katika hili, si kwamba Siwaruhusu watu kuwa katika nafasi hii na kuifurahia, lakini kwamba Nataka wao wawe na hisia ya adabu, kwa wao kutojitukuza sana; kuna umbali kati ya mbingu na dunia, sembuse kati ya Mungu na mwanadamu. Je, huo si umbali mkubwa hata zaidi kati yao? Duniani, mwanadamu na Mimi tuko “katika hali ileile,” na sisi “huvumilia hali mbaya pamoja.” Utambulisho Wangu haunisamehi kutopitia taabu ya dunia ya mwanadamu, na ni kwa sababu ya hili ndio maana leo Nimetumbukia katika hali hii. Sijawahi kuwa na mahali pa kuishi kwa amani duniani, ndiyo sababu watu husema, “Mwana wa Adamu hajawahi kuwa na mahali pa kulaza kichwa Chake.” Kwa hiyo, watu pia wamelia machozi ya huruma kwa ajili Yangu na kuweka kando yuan kumi kadhaa kwa ajili ya “mfuko wa msaada” kwa ajili Yangu. Ni kwa sababu ya hili tu ndio Nina mahali pa kupumzika; kama haingekuwa kwa “msaada” wa watu, nani ajuaye Ningeishia wapi!

Kazi Yangu itakapomalizika, Sitatafuta tena “msaada wa kifedha” kutoka kwa mwanadamu; badala yake, Nitatekeleza kazi Yangu ya asili, na Nitashusha “vitu vyote vya nyumba Yangu” kwa watu ili wavifurahie. Leo, kila mtu anajaribiwa katikati ya majaribu Yangu. Wakati mkono Wangu utakapomjia mwanadamu kirasmi, watu hawatanitazama tena kwa macho ya kustaajabisha, lakini watanitendea na chuki, na wakati huu Nitaitoa mioyo yao mara moja ili wawe kielelezo. Ninauchunguza moyo wa mwanadamu chini ya “hadubini”—hakuna upendo wa kweli Kwangu hapo. Kwa miaka, watu wamekuwa wakinidanganya na kunipumbaza—inaonekana kuwa upande wa kushoto wa juu wa moyo na upande wa chini wa kushoto wa moyo zote zina sumu ya chuki Kwangu, na haishangazi, basi, kwamba Nina mtazamo kama huo kwao. Na bado wanabaki wasiojua kabisa kuhusu hili, wala hawalikiri. Niwaonyeshapo matokeo ya uchunguzi Wangu, bado hawaamki; ni kana kwamba, katika akili zao, haya yote ni mambo ya kale, na hayapaswi kutajwa tena leo. Hivyo, watu wanatazama tu “matokeo ya maabara” kwa kutojali. Wanarudisha karatasi na kutoweka kwa haraka. Zaidi ya hayo, wanasema mambo kama, “Haya si muhimu, hayana athari yoyote kwa afya yangu.” Wanatoa tabasamu ndogo ya dharau, na kisha kuna mtazamo unaotisha kidogo katika macho yao, kana kwamba wakidokeza kwamba Sifai kamwe kuwa mwadilifu sana, kwamba lazima Niwe mzembe zaidi. Ni kana kwamba ufunuo Wangu wa siri zao za ndani umevunja “sheria” za mwanadamu, na hivyo wanakuwa na chuki zaidi Kwangu. Hapo ndipo Ninapoona chanzo cha chuki za watu. Hii ni kwa sababu Ninapotazama, damu yao inatiririka, na baada ya kupita kwenye mishipa katika miili yao inaingia moyoni, na ni wakati huu tu ndipo Ninapopata “ugunduzi” mpya. Walakini watu hawafikirii chochote juu ya hii. Wao ni wazembe kabisa, hawafikiri kile wanachopata au kupoteza, ambalo linatosha kuonyesha roho yao ya ibada “isiyo na ubinafsi.” Hawafikirii hali ya afya yao wenyewe, na “kurupuka hapa na pale” kwa ajili Yangu. Huu pia ni “uaminifu” wao na kile “kinachostahili kusifiwa” kuwahusu, kwa hivyo kwa mara nyingine Ninatuma barua ya “sifa” kwao, kwamba waweze kufurahishwa na hili. Lakini wanaposoma “barua” hii, mara moja wanahisi kukerwa kidogo, kwa maana yote wanayofanya yamekataliwa na barua Yangu ya kimya. Daima Nimewaelekeza watu watendavyo, ilhali inaonekana wanachukia sana maneno Yangu; hivyo, punde tu Ninapofungua mdomo Wangu, wanafumba na kubana macho yao na kufunika masikio yao kwa mikono yao. Hawanitazami kwa heshima kwa sababu ya upendo Wangu, lakini daima wamenichukia, kwa maana Nilionyesha upungufu wao, Nikifunua bidhaa zote wanazomiliki, na hivyo basi wamegubikwa na hasara katika biashara yao, na riziki yao imetoweka. Hivyo, chuki yao Kwangu inaongezeka kutokana na hiyo.

Aprili 14, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 31

Inayofuata: Sura ya 33

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp