Sura ya 105

Kwa sababu ya kanuni za maneno Yangu, kwa sababu ya mbinu ya kazi Yangu, watu wananikana; hili ndilo kusudi la kuzungumza Kwangu kwa muda mrefu sana (lililozungumzwa kuhusiana na wazao wote wa joka kuu jekundu). Ni mbinu ya hekima ya kazi Yangu; ni hukumu Yangu kwa joka kuu jekundu; huu ni mkakati Wangu, hakuna hata mtu mmoja anayeweza kuuelewa kikamilifu. Katika kila kipindi muhimu, yaani, katika kila awamu ya mpito ya mpango Wangu wa usimamizi, baadhi ya watu lazima waondolewe; wanaondolewa kulingana na utaratibu wa kazi Yangu. Hii pekee ndiyo mbinu ya kufanya kazi ya mpango Wangu mzima wa usimamizi. Baada ya kuwatupa nje, mmoja baada ya mwingine, watu Ninaotaka kuwaondoa, kisha Ninaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu. Hata hivyo, wakati huu wa kuondosha ni wakati wa mwisho (ndani ya makanisa ya China), na pia ni wakati ambapo idadi kubwa ya watu itaondolewa katika awamu ya mpito tangu uumbaji wa ulimwengu. Katika historia yote, kila wakati ambapo watu wameondolewa kumekuwa na sehemu iliyoachwa ili kutoa huduma kwa kazi ya baadaye, lakini wakati huu sio sawa na hapo awali; ni nyumbufu na safi, ni muhimu zaidi na kamilifu zaidi kuliko nyakati zote. Hata ingawa baada ya kusoma maneno Yangu, watu wengi hujaribu kuyalazimishia shaka kutoka akilini mwao, lakini mwishoni wao hawawezi kuyashinda, na hatimaye wanaanguka katika mapambano yao. Hili sio juu ya mwanadamu kuamua, kwa sababu wale ambao Nimewajaalia hawawezi kutoroka, na wale ambao Sijawajaalia Ninaweza kuwadharau tu. Ni wale ambao Ninawaangalia kwa fadhila pekee ndio ambao Ninawapenda, vinginevyo, hakuna hata mtu mmoja anayeweza kuondoka na kuingia kwa hiari katika ufalme Wangu; huu ndio utawala Wangu mkali, na huu pekee ndio ushahidi wenye nguvu na udhihirisho kamili wa kutekeleza amri Zangu za utawala. Hakika hili si suala la kuwa na moyo wenye ari tu. Kwa nini Nimesema Shetani ni dhaifu na aliyeanguka? Mara ya kwanza alikuwa na nguvu, lakini yuko katika mikono Yangu; Nikimwambia alale chini, ni lazima alale; Nikimwambia ainuke ili kunitolea huduma, ni lazima ainuke na kutoa huduma Kwangu vizuri. Siyo kwamba Shetani yuko radhi kufanya haya, ni kwamba fimbo Yangu ya chuma humtawala Shetani, na ni wakati huo pekee ndipo anashawishika moyoni na kwa neno. Amri Zangu za utawala humwongoza, Nina uwezo Wangu, na hivyo hana budi ila kushawishika kabisa, lazima apondwe chini ya kiti Changu cha miguu, bila dalili ya upinzani. Hapo zamani wakati ambapo alikuwa akiwahudumia wana Wangu, alikuwa fidhuli kupita kiasi na aliwadhulumu wana Wangu kwa hiari, akitumai kwa njia hiyo kuniaibisha Mimi, akisema kuwa Sina uwezo. Kipofu kweli! Nitakukanyaga hadi ufe! Wewe thubutu tu kuwa nduli tena! Wewe thubutu tu kuwatendea wana Wangu kwa kutojali kwa baridi tena! Kadiri watu wanavyokuwa waaminifu zaidi, na kadiri wanavyozidi kusikiliza maneno Yangu na kunitii, ndivyo unavyozidi kuwadhalimu, na ndivyo unavyozidi kuwatenga (hii ina maana kuwasajili watu, kuwaunganisha pamoja). Sasa siku zako za ukatili ziko mwishoni, kidogo kidogo Ninalipiza kisasi kwako, na Sitakuachilia kwa urahisi hata kidogo. Sasa sio wewe—Shetani—ambaye umechukua mamlaka; badala yake Nimechukua mamlaka hayo tena, na wakati wa kuwaita wana Wangu kukushughulikia umewadia. Ni lazima utii, na usiwe na upinzani hata kidogo. Bila kujali jinsi ulivyokuwa na mwenendo mzuri mbele Yangu hapo zamani, hilo halitakusaidia leo. Kama wewe si mmoja wa wale Ninaowapenda, basi Sikutaki. Mmoja zaidi ya idadi hiyo haikubaliki, lazima iwe nambari Niliyoamua kabla; mmoja chini ya hiyo ni mbaya zaidi. Shetani, usiwe mdakizi! Je, inaweza kuwa kwamba Sina hakika katika moyo Wangu kuhusu yule ambaye Ninampenda na ambaye Ninamchukia? Je, Ninahitaji kukumbushwa nawe? Shetani anaweza kuzaa wana Wangu? Wote ni wa upuuzi! Wote ni duni! Nitawatupa kabisa na kikamilifu, hakuna hata mmoja anayetakiwa, wote lazima waondoke! Mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita umefika mwisho, Kazi Yangu imekamilika na ni lazima Niliondoe kundi hili la wanyama na wenye tabia mbaya na wakatili!

Wale wanaoamini maneno Yangu na kutekeleza maneno Yangu lazima wawe wale Ninaowapenda, Sitamwacha hata mmoja, hakuna hata mmoja atakayeachwa, kwa hivyo wale ambao ni wana wazaliwa wa kwanza hawahitaji kuwa na wasiwasi. Kwa kuwa imetolewa na Mimi, hakuna mtu anayeweza kuichukua, na Sina budi kuwakirimu wale Ninaowabariki. Wale ambao Ninawakubali (kabla ya uumbaji wa ulimwengu), Ninawabariki (leo). Hivi ndivyo Ninavyofanya kazi, pia ndiyo kanuni kuu ya kila kifungu cha amri Zangu za utawala, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha hili; neno moja zaidi haliwezi kuongezwa, wala sentensi moja zaidi, na hata zaidi neno moja haliwezi kuachwa, wala sentensi moja. Hapo zamani mara nyingi Nilisema kuwa nafsi Yangu inaonekana kwenu; hivyo basi nafsi Yangu ni nini, na huonekana vipi? Je, ina maana Mimi Mwenyewe tu? Je, ina maana ya kila sentensi ambayo Ninasema tu? Vipengele hivi viwili, huku vikiwa vya msingi, vinachukua tu sehemu ndogo, yaani, hivyo sio maelezo kamili ya nafsi Yangu. Nafsi Yangu inanijumuisha Mimi Mwenyewe, maneno Yangu, na pia matendo Yangu, lakini maelezo kamili zaidi ni kwamba wana Wangu wazaliwa wa kwanza na Mimi ni nafsi Yangu. Yaani, kikundi cha wanadamu wa shirika la Ukristo, ambao hutawala na wana mamlaka, ni nafsi Yangu. Kwa hivyo, kila mmoja wa wana wa kwanza ni muhimu, ni sehemu ya nafsi Yangu, na kwa hivyo Ninasisitiza kwamba idadi ya watu haiwezi kuwa moja zaidi (kufedhehesha jina Langu), wala, muhimu zaidi, moja pungufu (hawawezi kuwa udhihirisho Wangu kamili), na Nasisitiza tena na tena kwamba wana wa kwanza ni wapendwa Wangu, tunu Yangu, udhihirisho wa mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita; ni wazaliwa wa kwanza pekee wanaoweza kuwa dhihirisho Langu timilifu na kamili, Mimi Mwenyewe pekee ndiye ninayeweza kuwa onyesho kamili la nafsi Yangu; pamoja tu na wana wa kwanza ndipo Mimi mwenyewe naweza kusemekana kuwa ni onyesho timilifu na kamili. Hivyo, Ninaweka madai makali kwa wana Wangu wa kwanza, bila kusamehe chochote, na kukata na kuua wale wote walio tofauti na wana Wangu wa kwanza tena na tena; hiki ndicho kiini cha yote ambayo Nimeyasema, ndilo lengo kuu la yote ambayo Nimeyasema. Zaidi ya hayo, mara nyingi Mimi husisitiza kuwa lazima wawe wale walioidhinishwa na Mimi, wale ambao Nimewachagua binafsi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Hivyo, sasa ni ipi namna ya kueleza “kuonekana”? Je, ni wakati wa kuingia katika ulimwengu wa kiroho? Watu wengi wanaamini kwamba ni wakati ambapo Mimi Mwenyewe Nilitiwa mafuta, au wakati ambapo waliniona Mimi Mwenyewe; yote haya ni uongo, hata hayakaribii ukweli. “Kuonekana” kwa mujibu wa maana yake ya asili si vigumu kuelewa kabisa, lakini kuelewa kulingana na nia Yangu ni vigumu sana. Inaweza kusemwa hivi: Wakati ambapo niliwaumba binadamu, Nilikuwa nikiweka ubora Wangu katika kundi hili la watu Niliowapenda, na kundi hili la watu lilikuwa nafsi Yangu. Ili kuieleza kwa njia nyingine, nafsi Yangu ilikuwa tayari imeonekana wakati huo. Siyo kwamba nafsi Yangu ilionekana baada ya jina hili kupokewa, bali badala yake ilionekana baada ya kuliamua kabla kundi hili la watu, kwa sababu lina ubora Wangu (asili yao haibadiliki, wao bado ni sehemu ya nafsi Yangu). Kwa hivyo, nafsi Yangu, tangu uumbaji wa ulimwengu mpaka siku ya sasa, imeonekana daima. Katika dhana za watu, wengi wanaamini kwamba Mimi Mwenyewe ndimi nafsi Yangu, ambayo sivyo kabisa; hayo yote ni mawazo ya watu, fikra za watu. Kama nafsi Yangu ya mwili pekee ingekuwa nafsi Yangu, basi hiyo haingeweza kutosha kumtia aibu Shetani. Isingeweza kulitukuza jina Langu, na kwa kweli ingekuwa na athari za kinyume, na hivyo kuliaibisha jina Langu, na kuwa alama ya Shetani kuliletea aibu jina Langu katika enzi zote. Mimi ni Mungu mwenye hekima Mwenyewe, na siwezi kamwe kufanya jambo la upumbavu kama hilo.

Kazi yangu lazima iwe na matokeo, hata zaidi lazima Nizungumze maneno kwa mbinu; maneno na matamshi Yangu yote yananenwa kwa kufuata Roho Wangu, na Ninazungumza kulingana na yote ambayo Roho Wangu hufanya. Kwa hivyo wote wanapaswa, kwa njia ya maneno Yangu, kuhisi Roho Wangu, kuona ni nini hasa ambacho Roho Wangu anafanya, kuona ni nini hasa Ninachotaka kufanya, kuona njia Yangu ya kufanya kazi kulingana na maneno Yangu, na kuona kanuni za mpango Wangu mzima wa usimamizi ni zipi. Mimi hutazama taswira nzima ya ulimwengu: Kila mtu, kila tukio, na kila mahali, vyote viko chini ya utawala Wangu. Hakuna mtu anayeweza kukiuka mpango Wangu; wote husonga mbele hatua kwa hatua kwa utaratibu ambao Nimeagiza. Huu ni uwezo Wangu, ni pale ambapo hekima ya kusimamia mpango Wangu wote upo. Hakuna anayeweza kuelewa kikamilifu, hakuna anayeweza kusema waziwazi. Yote hufanywa na Mimi binafsi, na kudhibitiwa na Mimi pekee.

Iliyotangulia: Sura ya 104

Inayofuata: Sura ya 106

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp