Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 50

Makanisa yote na watakatifu wote wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita na kutumainia siku za usoni: Ni mangapi kati ya matendo yenu ya zamani ndiyo yanayostahili, na ni mangapi kati yao yalishiriki katika ujenzi wa ufalme? Usiwe mtu mwenye kujifanya kujua kila kitu! Unapaswa kuona wazi dosari zako na unafaa kuelewa hali zako mwenyewe. Najua kwamba hakuna yeyote kati yenu yuko tayari kuweka jitihada yoyote na kugharimika muda wowote kuhusu hili, kwa hivyo hamuwezi kupata ujuzi wowote. Mnaharibu muda wenu wote katika kula, kunywa na kustarehe. Wakati wachache wenu wanakuja pamoja mnafanya mchezo, bila kuwa makini kushiriki mambo ya kiroho maishani au kutoa maisha nyinyi kwa nyinyi. Siwezi kustahimili kuwaona mkicheka na kufanya mzaha mnapozungumza, ilhali nyinyi ni wapumbavu sana. Nimesema mara nyingi, lakini hamjui tu maana ya kile Ninachosema—je, hili si jambo ambalo liko wazi kabisa kwamba liko dhahiri kabisa kwenu? Nimesema mambo kama haya awali lakini bado hamjaridhishwa na hamkubali kile Ninachosema, mkifikiri kwamba Siwaelewi, mkifikiri kwamba kile Ninachosema sio halisi. Huo ni ukweli, sio?

Ukishughulika na Mimi kwa uzembe basi nitakuweka upande mmoja. Wewe thubutu tu kuwa mzembe tena! Wewe thubutu tu kuwa mzembe na mvivu tena! Maneno Yangu ni kisu kinachochonga; chochote kisichopatana na mapenzi Yangu kitakatwa na kisu hiki, na hufai kuwa na nadhari sana kuhusu kujiheshimu. Ninakuchonga ili uweze kupata umbo na kufuata mapenzi Yangu. Usikose kuuelewa moyo Wangu; njia ya pekee inayokubalika ni kwa wewe kuwa mwenye kuujali moyo Wangu kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo. Ukionyesha kujali hata chembe, Sitakuacha. Daima usilidharau kwa porojo; njia ya pekee inayokubalika ni kwa wewe kukubali mapenzi Yangu siku zote yafanyike kwako.

Majeshi ya watakatifu yote yako katika nafasi tofauti, kwa hivyo bila shaka nyote mko na kazi tofauti. Lakini mnapaswa kufanya kila kitu katika uwezo wenu kugharimika kwa kweli kwa ajili Yangu, na wajibu wenu ni kufanya kila mnaloweza. Mnapaswa kuwa waaminifu katika hili, muwe na hiari kwa furaha, na kwa kweli ni sharti msiwe shingo upande. Vinginevyo, hukumu Yangu daima itakuwa juu yenu, miili yenu, roho na nafsi havitaweza kuistahimili, na kutakuwa na kulia na kusaga meno.

Iliyotangulia:Sura ya 49

Inayofuata:Sura ya 51

Maudhui Yanayohusiana

 • Sura ya 32

  Maneno ya Mungu huwaacha watu wakikuna vichwa vyao; ni kana kwamba, Anapozungumza, Mungu anaepukana na mwanadamu na kuzungumza na hewa, kana kwamba H…

 • Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

  Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mun…

 • Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

  Kwanza, hebu tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Unashuka Duniani. Kiambata: Watu wanamshangilia Mungu, watu wanamsifu Mungu; …

 • Njia … (5)

  Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu m…