Sura ya 12

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambao pia ni wakati hasa Naanza kutamka maneno Yangu—umeme unapotoka, mbingu yote inaangazwa, na mabadiliko yanatokea kwenye nyota zote. Wanadamu wote wanakuwa kana kwamba wamepangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya asili, macho yao yaking’aa, wakikosa uhakika wa kile wanachopsawa kufanya, na sembuse jinsi ya kuficha sifa zao mbaya. Wao pia ni kama wanyama wanaoitoroka kutoka kwa mwangaza Wangu amabao wanakimbilia usalama katika mapango ya milimani—ilhali, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kufutiliwa mbali kutoka katika mwanga Wangu. Wanadamu wote wako na hofu na wasiwasi, wote wanangoja, wote wanatazama; na ujio wa mwanga Wangu, wote wanasherehekea katika siku waliozaliwa, na vilevile wote wanailaani siku waliyozaliwa. Hisia zinazopingana haziwezi kuelezeka; machozi ya kujiadhibu huunda mito, na yanabebwa mbali juu ya mvo unaofagia, kwenda mara moja yasionekane tena. Kwa mara nyingine, siku Yangu inakaribia jamii ya binadamu, mara nyingine ikiamsha jamii ya binadamu, ikiwapa binadamu hatua ya kutengeneza mwanzo mpya. Moyo Wangu unapiga na, kufuatia mdundo wa mpigo wa moyo Wangu, milima inaruka kwa furaha, maji yanacheza kwa furaha, na mawimbi, kwa wakati ufaao, yanagonga juu ya mawe ya mwamba. Ni vigumu kuonyesha kile kilicho ndani ya moyo Wangu. Nataka vitu vyote visivyo safi vichomeke na kuwa majivu Nikitazama, Nataka wana wote wa kutotii wapotee kutoka mbele ya macho Yangu, wasikawie tena katika uwepo. Sijatengeneza mwanzo mpya katika makao ya joka kubwa jekundu pekee, Nimeanza pia kazi mpya katika ulimwengu. Hivi karibuni falme za dunia zitakuwa ufalme Wangu; hivi karibuni falme za dunia zitakoma kuwepo milele kwa sababu ya ufalme Wangu, kwa sababu Nimetimiza ushindi tayari, kwa sababu Nimerejea kwa ushindi. Joka kubwa jekundu limetumia njia zote za kuweza kufikiriwa ili kuvuruga mpango Wangu, likitumaini kufuta kazi Yangu duniani, lakini Naweza kukata tamaa kwa sababu ya mbinu zake za udanganyifu? Naweza kutishwa hadi kukosa kujiamini na vitisho vyake? Hakujawahi kuwa na kiumbe hata mmoja mbinguni ama duniani ambaye Simshiki katika kiganja cha mkono Wangu; ni kiwango gani zaidi ambacho huu ni ukweli kuhusu joka kuu jekundu, chombo hiki kinachotumika kama foili[a] Kwangu? Je, pia si kitu cha kutawaliwa na mikono Yangu?

Wakati wa kupata mwili Kwangu katika dunia ya binadamu, binadamu alifika pasipo kujua katika siku hii na usaidizi wa uongozi wa mkono Wangu, pasipo kujua akaja kunifahamu. Lakini, kuhusu jinsi ya kutembea katika njia iliyo mbele, hakuna aliye na fununu, hakuna anayejua, na bado hakuna aliye na kidokezo juu ya mwelekeo ambao hiyo njia itampeleka. Mwenyezi pekee akimwangalia ndipo yeyote ataweza kutembea njia hiyo hadi mwisho; akiongozwa tu na umeme kutoka Mashariki ndipo yeyote ataweza kuvuka kizingiti kinachoelekea katika ufalme Wangu. Miongoni mwa wanadamu, hakujawahi kuwa na yeyote ambaye ameuona uso Wangu, ambaye ameona umeme katika Mashariki; sembuse yule ambaye amesikia sauti inayotoka kwa kiti Changu cha enzi? Kwa kweli, kutoka siku za zamani, hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye amewasiliana na nafsi Yangu moja kwa moja; leo tu, wakati Nimekuja duniani, ndipo wanadamu wana nafasi ya kuniona. Lakini hata sasa, wanadamu bado hawanifahamu, jinsi wanavyouangalia uso Wangu na kuisikia tu sauti Yangu, lakini bila kuelewa Ninachomaanisha. Wanadamu wote wako hivi. Ukiwa mmoja wa watu Wangu, je huhisi fahari ya kina unapoona uso Wangu? Na, je, huhisi aibu kwa sababu hunifahamu? Natembea kati ya wanadamu, na Naishi kati ya wanadamu, kwa kuwa Nimekuwa mwili na Nimekuja katika ulimwengu wa binadamu. Lengo Langu sio tu kuwawezesha binadamu kuutazamia mwili Wangu; cha muhimu zaidi, ni kuwawezesha binadamu kunifahamu Mimi. Zaidi, kupitia mwili Wangu, Nitamhukumu binadamu kwa dhambi zao; kupitia mwili Wangu, Nitashinda joka kuu jekundu na kuangamiza pango lake.

Ingawa wanadamu ambao wanajaza dunia ni wengi kama nyota, Nawajua wote wazi kama Ninavyotazama kiganja cha mkono Wangu mwenyewe. Na, ingawa wanadamu ambao “wananipenda” ni wengi pia kama mchanga wa bahari, ni wachache tu ndio waliochaguliwa na Mimi: wale tu wanaotafuta mwanga unaong’aa, walio kando na wale “wanaonipenda.” Sithamini mno mwanadamu, wala Sikadiri upungufu wake; ila, Namwekea mwanadamu mahitaji kulingana na sifa zake za kiasili, na hivyo kile Ninachohitaji ni aina ya mwanadamu anayenitafuta kwa dhati—hii ni kwa ajili ya kufikia lengo Langu katika kuwachagua wanadamu. Kuna wanyama wa porini wasiohesabika milimani, lakini wote ni wapole kama kondoo mbele Zangu; mafumbo yasiyoeleweka yako chini ya bahari, lakini yanajiwakilisha Kwangu wazi kama vitu vyote vilivyo katika uso wa dunia; katika mbingu juu kuna ulimwengu ambao mwanadamu hawezi kufikia kamwe, ilhali Natembea kwa uhuru katika malimwengu hayo yasiofikika. Mwanadamu hajawahi kunifahamu katika mwanga, lakini ameniona tu katika ulimwengu wa giza. Huko katika hali sawa kabisa na hiyo leo? Ilikuwa katika kilele cha ghasia ya joka kuu jekundu ndipo Nilivaa kirasmi mwili ili kufanya kazi Yangu. Ulikuwa wakati ambapo joka kuu jekundu lilifichuliwa maumbile yake ya kweli kwa mara ya kwanza ndipo Nilipokuwa na ushuhuda kwa jina Langu. Nilipotembea katika barabara za binadamu, hakuna kiumbe hata mmoja, hata mtu mmoja, aliyebumburushwa hadi kuamka, kwa hivyo Nilipokuwa mwili katika ulimwengu wa mwanadamu, hakuna aliyejua. Lakini wakati, Nikiwa katika mwili Wangu, Nilianza kufanya kazi Yangu, halafu binadamu wakaamka, walibumburushwa kutoka kwa ndoto zake na sauti Yangu ya radi, na kutoka wakati huu wakaanza maisha chini ya uongozi Wangu. Kati ya watu Wangu, Nimeanza tena kwa mara nyingine kazi mpya. Baada ya kusema kazi Yangu duniani haijaisha, hii ni toshelezi kuonyesha kuwa watu Wangu niliowazumgumzia sio wale Ninaohitaji moyoni Mwangu, lakini hata hivyo, bado Nachagua baadhi kati yao. Ni Dhahiri kutoka kwa hili kwamba Siwawezeshi watu Wangu kumjua Mungu mwenye mwili tu, bali pia kuwatakasa. Kwa sababu ya ukali wa amri Zangu za utawala, watu wengi bado wako katika hatari ya kuondolewa na Mimi. Isipokuwa ukifanya juhudi zote kujishughulikia, kuushinda mwili wako mwenyewe—isipokuwa ukifanya haya, utakuwa bila shaka kitu Ninachodharau na kukataa, cha kutupwa chini kuzimu, kama jinsi Paulo alivyopokea adabu moja kwa moja kutoka kwa mikono Yangu, ambapo hakukuwa na kutoroka kutoka hapo. Je, pengine umegundua kitu kutoka kwa maneno Yangu? Kama hapo awali, bado ni nia Yangu kulitakasa kanisa, kuendelea kuwatakasa watu Ninaohitaji, kwani Mimi ni Mungu Mwenyewe, ambaye ni mtakatifu na safi kikamilifu. Nitafanya hekalu Langu lisiwe tu lenye rangi aina tofauti na rangi za upinde wa mvua, lakini pia liwe na usafi usiokuwa na doa, na ndani kufanane na nje yake. Katika uwepo Wangu, lazima nyote mfikirie nyuma kuhusu kile ambacho mmefanya hapo awali, na kuamua kama leo, mnaweza kuamua kunipa utoshelezo kamili katika moyo Wangu.

Mwanadamu hanifahamu Mimi tu katika mwili Wangu; zaidi ya haya, ameshindwa kuielewa nafsi yake mwenyewe inayoishi katika mwili. Kwa miaka mingi wanadamu wamekuwa wakinidanganya, wakinichukua kama mgeni kutoka nje. Mara nyingi sana, wamenifungia nje “ya milango ya nyumba zao”; mara nyingi sana, wakiwa wamesimama mbele Yangu hawajanisikiliza; mara nyingi sana wamenikana miongoni mwa wanadamu wengine; mara nyingi sana wamenikana mbele za ibilisi; na mara nyingi sana, wamenishambulia kwa midomo yao ya kugombanagombana. Ilhali siweki rekodi ya unyonge wa mwanadamu, wala kwa sababu ya kutotii kwake Sijataka kulipiza kisasi. Yote ambayo Nimefanya ni kuweka dawa kwa magonjwa yake, ili kutibu magonjwa yake yasiyotibika, hivyo kumrudisha kwa afya, ili mwishowe aje kunifahamu Mimi. Yote ambayo Nimefanya si kwa ajili ya kuishi kwa binadamu, kwa ajili ya kuupa binadamu fursa ya maisha? Mara nyingi Nilikuja katika ulimwengu wa wanadamu, lakini wanadamu, kwa sababu Nilikuja Mimi Mwenyewe katika dunia, hawakujishughulisha nami; badala yake, kila mmoja alitenda kama alivyopenda, na alijitafutia suluhisho. Ila hawajui kuwa kila moja ya barabara chini ya mbingu inatoka kwa mikono Yangu! Ila hawajui kuwa kila kitu kilichoko chini ya mbingu kinakabiliwa na uratibu Wangu! Yupi kati yenu anathubutu kuhifadhi chuki katika moyo wake? Yupi kati yenu anathubutu kwa urahisi kufikia makubaliano? Nimekuwa Nikiendelea na kazi Yangu kwa kimya miongoni mwa binadamu, ni hayo tu. Kama, katika wakati wa kupata mwili Kwangu, Singekuwa mwenye huruma kwa udhaifu wa mwanadamu, basi binadamu wote, kwa sababu ya kupata Kwangu mwili, wangetishwa kabisa, na kwa sababu hiyo, ungeingia kuzimu. Ni kwa sababu tu Nilijinyenyekeza na kujificha mbali ndiyo binadamu wameepuka janga, wakapata ukombozi kutoka kwa kuadibu Kwangu, na kwa namna hii ukafika leo. Ukizingatia ilivyokuwa vigumu kufika leo, je, si ni heri uihifadhi kwa upendo mkubwa sana kesho ambayo haijafika bado?

Machi 8, 1992

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Sura ya 11

Inayofuata: Sura ya 13

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp