Fumbo la Kupata Mwili (3)

Wakati ambapo Mungu huitekeleza kazi Yake, Yeye haji kujishughulisha katika ujenzi wowote au mabadiliko; Yeye huja kutimiza huduma Yake. Kila wakati Anapopata mwili, ni kwa ajili tu ya kufanikisha hatua ya kazi na kuifungua enzi mpya. Sasa Enzi ya Ufalme imefika, na mafundisho ya ufalme. Hatua hii ya kazi si kazi ya mwanadamu, si ya kumfanyia kazi mwanadamu kwa kiwango fulani; ni kuimaliza sehemu ya kazi ya Mungu tu. Kazi Yake si kazi ya mwanadamu, si kufikia matokeo fulani katika kumfanyia kazi mwanadamu kabla ya kuondoka duniani; ni kutimiza huduma Yake kwa ukamilifu na kuimaliza kazi ambayo Anapaswa kuifanya, ambayo ni kutengeneza mipango ya kufaa ya kazi Yake duniani, na hivyo kupata kutukuka. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni tofauti na ile ya wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Mungu anapofanya kazi Yake duniani, Yeye anajali kutimilika kwa huduma Yake pekee Yake. Na kwa mambo mengine yasiyohusiana na huduma Yake, Yeye kimatendo hajishughulishi hata kidogo, hata kwa kiwango cha kuzipa mgongo shughuli hizo. Yeye hufanya tu kazi Anayopaswa kufanya, na hajishughulishi na kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya. Kazi Anayofanya ni ile tu inahusiana na enzi Aliyomo na huduma Anayopaswa kukamilisha, kana kwamba mambo mengine yote si jukumu Lake. Yeye hajijazi na maarifa ya kawaida kuhusu jinsi ya kuishi kama mwanadamu, na Hajifunzi mahusiano ya jamii au mambo yoyote ambayo mwanadamu anaelewa. Hajishughulishi kamwe na mambo ambayo mwanadamu anapaswa kujua na Anafanya tu kitu ambacho ni jukumu Lake. Kwa hivyo, mwanadamu anavyoona, Mungu mwenye mwili ni mwenye upungufu katika mambo mengi mno, hata kwa kiasi kwamba Anavipa mgongo vingi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, na kwamba hana ufahamu wa mambo kama hayo. Mambo kama ufahamu wa maisha ya kawaida, na vile vile kanuni za tabia na kuhusiana na wengine, huonekana kuwa hazina uhusiano Kwake. Hata hivyo, huwezi kuona kutoka kwa Mungu mwenye mwili tabia zozote zisizo za kawaida. Hiyo ni kusema, ubinadamu Wake unadumisha maisha Yake kama mwanadamu wa kawaida na fikira za kawaida za ubongo Wake, na kumpa uwezo wa kutofautisha kati ya mazuri na mabaya. Hata hivyo, Hajajazwa na kingine chochote, yote ambayo ni ya wanadamu (walioumbwa) pekee. Mungu anapata mwili ili kukamilisha huduma Yake pekee. Kazi Yake inaelekezwa kwa enzi nzima na sio kwa mtu binafsi au mahali fulani. Kazi Yake inaelekezwa kwa ulimwengu mzima. Huu ndio mwelekeo wa kazi Yake na kanuni Anayofuata katika kazi Yake. Hii haiwezi kubadilishwa na yeyote, na mwanadamu hawezi kuhusika kwa sehemu yoyote. Kila wakati ambapo Mungu hupata mwili, Yeye huja pamoja na kazi ya enzi hiyo, na sio dhamira ya kuishi ubavuni mwa mwanadamu kwa miaka ishirini, thelathini, arobaini, au hata miaka sabini, themanini ili waweze kuelewa bora zaidi na kupata utambuzi Kwake. Hakuna haja ya hilo! Kufanya hivyo hakungeweza katu kuzidisha ufahamu ambao mwanadamu anao wa tabia ya asili ya Mungu; badala yake, kungeongeza tu kwa fikira zao na kufanya fikira na mawazo ya mwanadamu yawe kuukuu. Na kwa hiyo nyote mnapaswa kuelewa hasa ni nini kazi ya Mungu aliyepata mwili. Yawezekana kwamba hamyaelewi maneno Yangu: “Siji kuyapitia maisha ya mwanadamu wa kawaida”? Je, mmesahau maneno: “Mungu haji duniani kuishi maisha ya mwanadamu wa kawaida”? Hamlielewi kusudi la Mungu kupata mwili, wala hamjui maana ya “Mungu angekujaje duniani na dhamira ya kuyapitia maisha ya kiumbe aliyeumbwa?” Mungu anakuja tu duniani kukamilisha kazi Yake, na kwa hivyo Kazi Yake duniani ni ya muda mfupi. Haji duniani na nia ya Roho wa Mungu kukuza mwili Wake kuwa mkuu wa kipekee wa kanisa. Mungu anapokuja duniani, ni Neno ambalo kugeuka kuwa mwili; mwanadamu, hata hivyo, hajui kuhusu kazi Yake na kwa nguvu anaona Yeye kuwa sababu ya mambo. Lakini nyote mnapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Neno lililogeuka kuwa mwili, na sio mwili uliokuzwa na Roho wa Mungu ili kusimamia nafasi ya Mungu kwa ufupi. Mungu Mwenyewe hakuzwi, ila ni Neno kugeuka mwili, na leo hii Anatekeleza kazi Yake kirasmi miongoni mwenu. Nyote mwajua na kukubali kwamba kupata mwili kwa Mungu ni ukweli, lakini mnajidai kuwa na ufahamu ambao kwa kweli hamna. Ninyi hamthamini kabisa kazi ya Mungu aliyepata mwili au umuhimu na kiini cha Yeye kupata mwili, na husimulia kwa urahisi tu maneno ambayo hunenwa na wengine. Je, unaamini kwamba Mungu aliyepata mwili ni kama unavyodhani.

Mungu hugeuka mwili ili tu Aiongoze enzi na Aanzishe kazi mpya. Lazima muelewe hoja hii. Hii ni tofauti kabisa na kazi ya mwanadamu, na mawili haya hayawezi kuzungumzwa kwa pamoja. Mwanadamu anahitaji muda mrefu wa kukuzwa na kufanywa mkamilifu kabla mwanadamu aweze kutumiwa kutekeleza kazi, na ubinadamu wa hali ya juu unahitajika. Mwanadamu hapaswi kudumisha hali yake ya ubinadamu wa kawaida tu, bali pia mwanadamu zaidi ya hapo lazima aelewe kanuni nyingi na sheria za tabia kabla ya mengine, na zaidi ya hayo lazima ajifunze zaidi kuhusu hekima na maadili ya mwanadamu. Haya ndiyo mwanadamu lazima kujengwa nayo. Hata hivyo, hivi sivyo ilivyo na Mungu mwenye mwili, kwa maana kazi Yake haimwakilishi mwanadamu na wala si ya binadamu; bali ni dhihirisho la moja kwa moja la hali Yake na utekelezaji wa moja kwa moja wa kazi Anayopaswa kufanya. (Kwa kawaida, kazi Yake hufanyika wakati inapaswa kufanyika, na sio tu wakati wowote kiholela. Badala Yake, kazi Yake hufanyika wakati ambapo ni wakati wa kukamilisha huduma Yake). Yeye hajihusishi katika maisha ya mwanadamu wala katika kazi ya mwanadamu, hiyo inamaanisha, ubinadamu Wake haujengwi na yoyote kati ya haya (lakini hili haliathiri kazi Yake). Anatimiza huduma Yake tu ikiwa wakati umewadia wa kufanya hivyo; haijalishi hali Aliyomo, Yeye huendelea mbele na kazi Anayopaswa kufanya. Haijalishi mwanadamu anajua nini kumhusu, au maoni ya mwanadamu kumhusu, kazi Yake haiathiriki. Hii ni kama tu vile Yesu Alivyofanya kazi Yake; hakuna aliyejua Yeye ni nani, lakini Aliendelea tu mbele na kazi Yake. Mambo haya hayakumuathiri katika utendaji wa kazi Yake Aliyopaswa kufanya. Kwa hivyo, Hakukiri au kutangaza kuwa Yeye ni nani, na Yeye alimfanya mwanadamu Amfuate tu. Kwa kawaida, huu haukuwa tu uvumilivu wa Mungu; ilikuwa ni njia ambayo Yesu anafanya kazi katika mwili. Angeweza tu kufanya kazi kwa namna hii, kwani mwanadamu hangeweza kumtambua Yesu kwa jicho la kawaida. Na hata kama mwanadamu angeweza, mwanadamu hangeweza kusaidia katika kazi Yake. Zaidi ya hayo, hakugeuka mwili ili mwanadamu apate kujua mwili huu Wake; ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi Yake na kukamilisha huduma Yake. Kwa sababu hii, hakutilia maanani hali ya kufanya Ajulikane. Alipokamilisha kazi Aliyopaswa kufanya, utambulisho Wake na hadhi Yake vilijulikana wazi kwa mwanadamu. Mungu mwenye mwili hukaa kimya na hafanyi matangazo yoyote. Yeye hajishughulishi na mwanadamu au vile mwanadamu anaendelea katika kumfuata, na yeye husonga tu mbele katika kutimiza huduma Yake na kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Hakuna Anayeweza kusimama mbele ya njia ya kazi Yake. Wakati muda unawadia wa kazi Yake kukamilika, ni muhimu kazi hiyo ikamilike na kufikishwa kikomo. Hakuna anayeweza kusema vinginevyo. Baada tu ya Yeye kuondoka kutoka kwa mwanadamu baada ya kukamilisha kazi Yake ndipo mwanadamu ataelewa kazi Anayofanya, ingawa hataifahamu kikamilifu. Na itachukua muda mrefu ndipo mwanadamu aelewe nia Yake Alipofanya kazi hiyo mara ya kwanza. Kwa maneno mengine, kazi ya enzi ambapo Mungu anageuka mwili imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu moja ni kupitia katika kazi na maneno ya Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Pindi tu huduma ya mwili Wake imetimika kikamilifu, sehemu nyingine ya kazi inatakiwa kutekelezwa na Roho Mtakatifu; basi utakuwa wakati wa mwanadamu kutimiza wajibu wake, kwa maana Mungu ameshafungua njia tayari, na lazima itembelewe na mwanadamu mwenyewe. Hiyo ni kusema, Mungu anageuka kuwa mwili ili kutekeleza sehemu moja ya kazi Yake, na inaendelezwa kwa urithi na Roho Mtakatifu na vile vile wale watu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu. Kwa hivyo mwanadamu anapaswa kujua kazi ya msingi inayopaswa kutekelezwa na Mungu mwenye mwili katika hatua hii ya kazi. Mwanadamu lazima aelewe hasa umuhimu wa Mungu kugeuka kuwa mwili na kazi Anayopaswa kufanya, badala ya kumuuliza Mungu ni nini kinachotakiwa kwa mwanadamu. Haya ni makosa ya mwanadamu, na vile vile fikira, na zaidi ya hayo, ni kutotii kwake.

Mungu anakuwa mwili bila nia ya kumfanya mwanadamu apate kuujua mwili Wake, ama kukubali mwanadamu kutofautisha tofauti kati ya mwili wa Mungu mwenye mwili na ule wa mwanadamu; Mungu hapati mwili ili kufunza mwanadamu uwezo wa utambuzi, na zaidi nia ya mwanadamu kumwabudu Mungu mwenye mwili, ambayo kupitia kwayo atapata utukufu mkuu. Hakuna kati ya haya yaliyo mapenzi ya Mungu ya awali ya Mungu kuwa mwili. Mungu hawi mwili ili kulaani mwanadamu, kufichua mwanadamu akipenda, ama kufanya vitu kuwa vigumu kwa mwanadamu. Hakuna kati ya hayo lililo penzi la awali la Mungu. Kila wakati ambapo Mungu anakuwa mwili, ni kazi isiyo na budi. Ni kwa ajili ya kazi Yake kuu na usimamizi Wake mkuu ndio maana Anafanya hivyo, na si kwa sababu ambazo mwanadamu anafikiria. Mungu anakuja tu duniani Anavyohitajika na kazi Yake, na kila wakati ikiwa lazima. Haji duniani Akiwa na nia ya kuzurura, ila kutekeleza kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mbona basi Ajipatie kazi hii ngumu na kujiweka katika hatari kubwa kufanya kazi hii? Mungu anakuwa mwili tu inapobidi, na kila wakati ikiwa na umuhimu wa kipekee. Kama ingekuwa tu kwa sababu ya kumfanya mwanadamu amuangalie na kufungua macho yao, basi kwa uhakika kabisa, hangekuja kati ya wanadamu kwa kubembeleza. Anakuja duniani kwa usimamizi Wake na kazi Yake kuu, na kuwa na uwezo wa kutwaa wanadamu zaidi. Anakuja kuwakilisha enzi na kumshinda Shetani, na ni katika mwili ndimo Anakuja kumshinda Shetani. Zaidi, Anakuja kuwaongoza binadamu wote katika maisha yao. Haya yote yanahusu uongozi Wake, na yanahusu kazi ya ulimwengu wote. Mungu angekuwa mwili ili tu kumruhusu mwanadamu kuja kuujua mwili Wake na kuyafungua macho ya mwanadamu, basi mbona Hangesafiri kwa kila taifa? Je hili sio jambo la wepesi zaidi? Lakini hakufanya hivyo, badala yake, Akachagua mahali palipofaa pa kuishi na kuanza kazi Aliyopaswa kufanya. Mwili huu pekee ni wa umuhimu mkuu. Anawakilisha enzi nzima, na Anatekeleza kazi ya enzi nzima; Analeta enzi ya zamani kufika tamati na kuikaribisha mpya. Haya yote ni mambo muhimu yanayohusu usimamizi wa Mungu, na ni umuhimu wa hatua ya kazi iliyotekelezwa na Mungu kuja duniani. Wakati ambapo Yesu alikuja duniani, Alizungumza tu maneno kiasi na kutekeleza kazi kiasi; Hakujishughulisha na maisha ya mwanadamu, na Aliondoka baada ya kumaliza kazi Yake. Baada ya Mimi kumaliza kuzungumza na kuyapokeza maneno Yangu kwenu siku hii, nanyi nyote mkishayaelewa, basi hatua hii ya kazi itakuwa imemalizika, haijalishi maisha yenu yatakuwa vipi. Katika siku za usoni, lazima kuwe na wale wa kuendeleza hatua hii ya kazi na kufanya kazi kwa mujibu wa maneno haya duniani; kisha kazi ya mwanadamu na ujenzi wa mwanadamu utaanza. Lakini sasa, ni kazi ya Mungu tu kutimiza huduma Yake na kumaliza hatua ya kazi. Mungu hufanya kazi kwa njia isiyo sawa na ya mwanadamu. Mwanadamu hupenda mikusanyiko na mabaraza, na huthamini sana utaratibu. Mungu huchukia sana mikusanyiko na mikutano ya mwanadamu. Mungu huzungumza na kunena na mwanadamu visivyo rasmi; hii ni kazi ya Mungu, ambayo ni iliyokombolewa isivyo kawaida na pia hukuweka wewe huru. Hata hivyo, Nachukia zaidi kukusanyika nanyi, na Mimi siwezi kuzoea maisha yaliyoshurutishwa sana kama yenu. Mimi huziona sheria kuwa za kuchukiza sana; hizo humzuia mwanadamu kiasi cha kumfanya mwanadamu aogope kuanza kutenda, aogope kuzungumza, na aogope kuimba, na macho yake hukodolewa kwako moja kwa moja. Nachukia zaidi namna yenu ya mkusanyiko na mikusanyiko mikubwa. Sitamani kabisa kukusanyika nanyi kwa njia hii, kwani njia hii ya kuishi humfanya mtu ahisi amewekewa mipaka na mnafuata utaratibu mwingi sana na sheria nyingi sana. Mngeruhusiwa kuwaongoza wanadamu mngewaongoza wote ndani ya miliki ya sheria na wanadamu hawangekuwa na njia ya kuziacha sheria chini ya uongozi wenu, na badala yake maana ya udini ingekuwa kali sana milele, na desturi za mwanadamu kuongezeka kwa idadi kubwa zaidi. Wanadamu wengine huendelea kuzungumza na kunena wakati ambapo wanakusanyika na hawahisi uchovu kamwe, ilhali wengine wanaweza kuendelea kunena kwa siku nyingi. Hii yote inafikiriwa kuwa mikusanyiko mikubwa na mikutano ya mwanadamu; haina uhusiano wowote na maisha ya kula na kunywa, ya kufurahia, au ya maisha roho huwekwa huru. Hii yote ni mikutano! Mikutano yenu ya mfanyakazi mshiriki, na vilevile mikusanyiko mikubwa na midogo, yote inanichukiza Mimi, na Sijawahi kuwa na hamu nayo. Hii ni kanuni ambayo Nafanyia kazi; Siko radhi kuhubiri wakati wa mikusanyiko, wala Siko radhi kutangaza chochote kwa watu wote, sembuse kuitisha mkutano wa ninyi nyote kwa siku chache za mkutano maalumu. Sioni likiwa la kupendeza kwenu nyote kukusanyika pamoja kwa kufaa; Nachukia kabisa kuwaona ninyi mkiishi ndani ya mipaka ya utaratibu wowote, aidha, Siko radhi kushiriki katika utaratibu wenu wowote kama huo. Kadri mnavyofanya hivyo, ndivyo Ninavyoiona kuwa ya kuchukiza zaidi. Sina hamu hata kidogo na utaratibu na sheria zenu; haijalishi mnavifanya kwa jinsi nzuri iliyoje, Nayaona yote kuwa ya kuchukiza. Sio kwamba mipango yenu ni isiyofaa au kwamba ninyi ni duni sana; ni kwamba Nachukia sana mwenendo wenu wa kuishi, na zaidi ya hayo, Mimi siwezi kuuzoea. Ninyi hamwelewi kabisa kazi Ninayotaka kufanya. Kipindi hicho, wakati ambapo Yesu alitekeleza kazi Yake mahali fulani na kisha Akamaliza kuhubiri mahubiri, Angewaongoza wanafunzi Wake na kuondoka katika mji huo; Akiondoka kati ya wanadamu, na kuwaongoza wanafunzi wake wachache wapendwa na kuzungumza nao kuhusu njia walizopaswa kuelewa. Alifanya kazi kila mara kwa njia hiyo. Kazi Yake kati ya umma ya jumla ilikuwa nadra. Kulingana na kile mnachotaka kutoka Kwake, Mungu aliyepata mwili hapaswi kuwa na maisha ya mwanadamu wa kawaida; lazima Aitekeleze kazi Yake, na lazima Azungumze, kama Anaketi, Anasimama, au kutembea. Lazima Afanya kazi nyakati zote na Hawezi kukoma “kukimbia”, la sivyo Anazembea katika majukumu Yake. Je, mahitaji haya ya mwanadamu ni kwa mujibu wa akili ya mwanadamu? Uadilifu wenu uko wapi? Je, hamtaki mengi kupita kiasi? Kazi Yangu inahitaji kuchunguzwa na wewe? Je, Nakuhitaji wewe kuangalia Ninapotimiza huduma Yangu? Najua vizuri kazi Ninayopaswa kufanya na wakati ambapo Napaswa kuifanya; Sihitaji kuingilia kutoka kwa wengine. Labda inaweza kuonekana kwako kana kwamba Sijafanya mengi, lakini kufikia wakati huo kazi Yangu tayari imefika mwisho. Chukueni mfano wa maneno ya Yesu katika Injili Nne. Hayo vilevile hayakuwa na mipaka? Wakati huo, Yesu aliingia katika sinagogi na kuhubiri mahubiri; Alikuwa ameimaliza katika muda usio zaidi ya dakika kadhaa. Baada ya Yeye kumaliza kunena, Aliwaongoza wanafunzi Wake ndani ya mashua na Akaondoka bila maelezo yoyote. Sanasana, wale waliokuwa ndani ya sinagogi walijadiliana miongoni mwao wenyewe, na jambo hilo halikumhusu Yesu tena. Mungu alitekeleza tu kazi ambayo Alipaswa kuifanya, na sio zaidi. Siku hizi, wengi huniomba Ninene na kuzungumza mengi zaidi, angalau kwa masaa kadhaa kwa siku. Kama mwonavyo, Mungu huacha kuwa Mungu isipokuwa Azungumze, na ni Yule anayezungumza tu ni Mungu. Ninyi nyote ni vipofu! Nyote ni katili! Nyote ni vitu visivyojua visivyo na hisi! Mna fikira nyingi sana! Madai yenu hupita mipaka! Ninyi ni wasio na utu! Hamwelewi kabisa Mungu ni nini! Ninyi huamini kwamba wazungumzaji na wasemi wote ni Mungu, kwamba yeyote ambaye yuko radhi kuwapa ninyi maneno ni baba yenu. Niambieni, je, ninyi nyote mlio na maumbo “yaliyoumbwa vizuri” na sura “ya ajabu” bado mna hata sehemu kidogo ya hisi? Je, mnajua sasa jua la mbinguni! Kila mmoja wenu ni kama maofisa wapotovu na wenye uchoyo, kwa hiyo mwawezaje kuona maana? Mwawezaje kutambua kati ya mema na mabaya? Nimewapa ninyi mengi sana, lakini ni wangapi miongoni mwenu wamezingatia? Nani anaweza kulipata kwa ukamilifu? Ninyi hamjui ni nani alifungua njia ambayo kwayo mnatembea siku hii, kwa hiyo ninyi huendelea kunidai Mimi, mkifanya madai yasiyo na maana kutoka Kwangu. Je, nyuso zenu hazijabadilika kwa sababu ya aibu? Sijazungumza mengi? Je, Sijafanya mengi? Ni nani miongoni mwenu anaweza kweli kuyatunza maneno Yangu kama hazina? Ninyi hunisifu mno katika kuwepo Kwangu, lakini hudanganya na kulaghai bila Mimi kujua! Matendo yenu ni yenye kustahili dharau sana na ya kuchukiza! Najua kwamba ninyi huniambia Mimi nizungumze na kufanya kazi ili muweze kushibisha macho yenu na kupanua uzoefu wenu tu, sio kuyageuza maisha yenu. Ni mangapi ambayo Nimenena kwenu tayari? Maisha yenu yangekuwa yamebadilika kitambo sana, kwa hiyo mbona mnaendelea kurudia hali mbaya leo? Yaweza kuwa kwamba maneno Yangu yameibwa kutoka kwenu kwa hivyo hamkuyapokea? Kusema kweli, Sitamani kusema zaidi kwa walioharibika tabia namna hivyo kama ninyi. Haileti manufaa! Siko radhi kufanya kazi isiyoleta manufaa hivyo! Ninye mnataka tu kupanua uzoefu wenu au kuyashibisha macho yenu, sio kupata uzima! Nyote mnajidanganya wenyewe! Nawauliza, ni mangapi kati ya yale Niliyowazungumzia ana kwa ana yametiwa katika vitendo na ninyi? Yote mfanyayo ni ulaghai wa kudanganya! Nachukia sana wale miongoni mwenu wanaofurahia kutazama, na Nauona udadisi wenu kuwa wa kuchukiza kabisa. Kama hamko hapa kuitafuta njia ya kweli au kuwa na kiu ya ukweli, basi ninyi ni wale Ninaowachukia sana! Najua kwamba ninyi hunisikiliza tu ili kuridhisha udadisi wenu au kutimiza mojawapo ya shauku yenu. Hamna wazo la kutafuta kuweko kwa ukweli au kuchunguza kuingia katika njia sahihi ya uzima; matakwa haya hayako miongoni mwenu kabisa. Ninyi humchukulia tu Mungu kuwa mtu anayechezewa wa kuchunguza na kustahi. Moyo wenu unaotafuta uzima ni mdogo sana, ilhali shauku yenu ya udadisi sio! Kuzungumza kwa watu kama hao kuhusu njia ya uzima ni kimsingi kuzungumza na kitu kisichokuwepo; ingekuwa heri kutozungumza! Hebu Niwaambie: Kama mnatazamia tu kuijaza tupu iliyo ndani ya moyo wenu, basi heri msije Kwangu! Mnapaswa kuyalenga maisha yenu! Msijidanganye! Heri msichukulie udadisi wenu kama msingi wa ufuatiliaji wenu wa maisha, au kuutumia kama kisingizio cha kuniomba Mimi kuzungumza na ninyi. Huu wote ni ulaghai, ambao kwao ninyi ni mabingwa! Nakuuliza tena: Ni kiasi gani cha yale ambayo Nimekwambia uingie ndani umefanya kwa kweli? Je, wajua yote ambayo Nimenena kwako? Umetia katika vitendo yote ambayo Nimenena kwako.

Kazi ya kila enzi huanzishwa na Mungu Mwenyewe, lakini unapaswa kujua kwamba licha ya kazi yoyote ya Mungu, Yeye haji kuanzisha muungano au kufanya mikutano yoyote halisi au kuanzisha makundi ya aina yoyote kwa ajili yenu. Yeye huja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Kazi Yake haizuiliwi na mwanadamu yeyote. Yeye hufanya kazi Yake vile Anavyopenda; haijalishi kile mwanadamu anajua au kufikiri, Yeye hutilia maanani katika kutekeleza kazi Yake. Tangu kuumbwa kwa dunia, kumekuwa na hatua tatu za kazi; kutoka kwa Yehova mpaka kwa Yesu, na kutoka kwa Enzi ya Sheria mpaka kwa Enzi ya Neema, Mungu hajawahi kuitisha mkutano halisi kwa mwanadamu, wala hajawahi kuwakusanya wanadamu wote pamoja kufanya mkutano halisi wa ulimwengu ili kupanua kazi Yake. Yeye hufanya tu kazi ya mwanzo wa enzi nzima wakati muda na wakati na mahali uko sawa, na kupitia kwa hili Anaikaribisha enzi ili kuwaongoza wanadamu katika maisha yao. Mikutano halisi ni mikutano ya wanadamu; kuwakusanya watu pamoja kusherehekea siku kuu katika kazi za mwanadamu. Mungu hasherehekei siku kuu na, zaidi ya hayo, Anachukizwa nazo; Yeye haitishi mikutano halisi na zaidi ya hayo Anachukizwa nayo. Sasa lazima uelewe ni nini hasa kazi ya Mungu mwenye mwili.

Iliyotangulia: Fumbo la Kupata Mwili (2)

Inayofuata: Fumbo la Kupata Mwili (4)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp