Sura ya 21

Kazi ya Roho Mtakatifu sasa imewaleta katika mbingu mpya na dunia mpya. Kila kitu kinaendelea kufanywa upya, kila kitu ki mikononi Mwangu, kinarudi ulingoni! Kwa dhana zao, watu wanashindwa kulifikiria kwa makini, na kwao haina maana, lakini ni Mimi ambaye niko kazini, na hekima Yangu iko ndani yake. Kwa hiyo mnaweza kukomesha dhana zenu zote na maoni yenu. Mnaweza kujishughulisha na kula na kunywa neno la Mungu katika utii, bila wasiwasi wowote kamwe. Kwa kuwa Nafanya kazi kwa njia hii, Nitachukua jukumu takatifu. Kwa kweli, watu hawana haja ya kuwa namna fulani. Badala yake, ni Mungu anayefanya mambo ya kimiujiza, na kudhihirisha kudura Yake. Watu wasijivune isipokuwa kama wanajivuna kuhusu Mungu. Vinginevyo mtapata hasara. Mungu huwainua masikini kutoka mavumbini, ambako wanyenyekevu wanainuliwa. Mimi nitatumia hekima Yangu katika hali zake zote kulitawala kanisa la watu wote, kutawala mataifa yote na watu wa makabila yote, ili wao wote wawe ndani Yangu, na ili nyote katika kanisa muweze kunitii. Wale ambao hawakutii kabla lazima sasa wawe watiifu mbele Yangu, ni lazima watiiane, wapokeane wao kwa wao, wawe na maisha yanayohusiana, na wapendane, wote wakifaidi kwa weledi wa wenzao katika sehemu ambazo kila mmoja ana udhaifu, wakihudumu kwa uratibu. Kwa njia hii kanisa litajengwa, na Shetani hatakuwa na nafasi ya kuwatumia watu. Ni hapo tu ambapo mpango Wangu wa usimamizi hautakuwa umeshindwa. Acha Niwape kumbusho jingine hapa. Usiruhusu kutoelewana kuzuke ndani yako kwa sababu mtu fulani ni wa namna fulani, au alitenda mambo kwa njia fulani, likikuacha uwe mtu wa kufifia katika roho. Mimi ninavyoona, hili halifai, na ni kitu bure. Je, Yule unayemwamini si Mungu? Siyo mtu fulani. Shughuli si za aina moja. Kuna mwili mmoja. Kila mmoja hufanya kazi yake, kila mmoja kwa nafasi yake na kufanya kadiri ya uwezo wake—kila cheche ya shauku mwako wa mwanga—kutafuta ukomavu katika maisha. Ni hivyo ndivyo nitakavyoridhika.

Ni lazima mjishughulishe tu na kuwa na amani mbele Yangu. Kuweni katika ushirika wa karibu na Mimi, tafuteni pale ambapo hamuelewi, fanyeni maombi, na muusubiri wakati Wangu. Angalia kila kitu kwa dhahiri kutoka kwa roho. Usifanye mambo bila hadhari, ili kuzuia kupotoka. Ni kwa njia hii tu ambapo kula kwako na kunywa kwa maneno yangu kwa kweli kutazaa matunda. Kula na unywe maneno Yangu mara kwa mara, yatafakari niliyoyasema Mimi, zingatia kutenda maneno Yangu, na uishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno Yangu; hili ndilo suala muhimu. Maendeleo ya kujenga kanisa ndiyo pia maendeleo ya ukuaji wa maisha. Maisha yako yakiacha kukua, huwezi kujengwa. Kutegemea uasilia tu, kwa mwili, kwa raghba, kwa michango, kwa sifa, bila kujali jinsi ulivyo mzuri, hutajengwa. Lazima uishi katika maneno ya maisha, ishi ndani ya unurishwaji na kuwa katika hali ya kuangazwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, jua hali yako halisi, na uwe mtu aliyebadilika. Lazima uwe na ufahamu huo huo ndani ya roho yako, upate nuru mpya, na uwe na uwezo wa kuendelea sawa na mwanga mpya. Lazima uwe na uwezo wa kupata mawasiliano ya karibu na Mimi bila kukoma, uwe na uwezo wa kutegemeza matendo yako katika maisha ya kila siku kwa maneno Yangu, uwe na uwezo wa kuwashughulikia vizuri watu wa kila aina, matukio, na mambo kwa kutegemeza maneno Yangu, shughuli zote katika maisha ukiwa na maneno Yangu kama kiwango chako na ukiishi kwa kudhihirisha tabia Yangu.

Ikiwa unatamani kuelewa na kuyatunza mapenzi Yangu, lazima uyazingatie maneno Yangu. Usifanye mambo kwa pupa. Yale yote ambayo Mimi sikubaliani nayo yataishia vibaya. Baraka huja tu kwa kile ambacho Mimi nimekikubali. Kama Mimi nikisema, litakuwa. Kama Mimi nikiamuru, litasimama imara. Kabisa lazima ninyi msifanye kile ambacho sijaruhusu Mimi, kuepuka kunikasirisha Mimi. Wakati huo hakutakuwa na wakati wa kujuta.

Iliyotangulia: Sura ya 20

Inayofuata: Sura ya 22

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp