Sura ya 119
Ni lazima nyote muelewe nia Zangu, nyote mnapaswa kuelewa hali Yangu ya moyo. Sasa ni wakati wa kujiandaa kurudi Sayuni, sina mawazo ya lolote isipokuwa hili. Mimi Ninatumaini tu kwamba Ninaweza kukutana nanyi siku moja hivi karibuni, na kutumia kila dakika na kila sekunde pamoja nanyi katika Sayuni. Mimi Naichukia kabisa dunia, Nauchukia kabisa mwili, na Mimi Namchukia kabisa hata zaidi kila binadamu duniani; Sina nia ya kuwaona, kwa sababu wote ni kama mapepo, bila hata chembe ya asili ya binadamu; Sina nia ya kuishi duniani, Mimi Nawachukia kabisa viumbe wote, Mimi Nawachukia kabisa wote ambao ni wa mwili na damu. Nchi yote inavunda maiti; Mimi Nataka kurudi Sayuni mara moja, ili kuiondoa harufu yote mbaya ya maiti kutoka dunia, na kufanya dunia yote ijae sifa kwa ajili Yangu. Mimi Nitarejea Sayuni, Mimi Nitajiondoa kutoka kwa mwili na ulimwengu, hakuna yeyote anayepaswa kuweka kizuizi mbele Yangu; Mkono wangu ambao huua mwanadamu hauna hata chembe ya hisia! Kuanzia sasa na kuendelea, hakuna yeyote anayepaswa kunena juu ya ujenzi wa kanisa, vinginevyo Mimi sitamsamehe. (Hii ni kwa sababu sasa ni wakati wa kushuhudia wana Wangu wazaliwa wa kwanza, wakati wa kujenga ufalme; yeyote anayezungumza kuhusu ujenzi wa kanisa anaubomoa ujenzi wa ufalme na kuukatiza usimamizi Wangu.) Yote yako tayari, yote yametayarishwa, kilichobaki ni kwa wana wazaliwa wa kwanza kuinuliwa, kushuhudiwa, na hilo likitukia, bila kukawia kwa muda na bila kufikiria umbo, mara moja Nitarudi Sayuni—mahali mnapashikilia akilini mwenu usiku na mchana. Msiangalie tu jinsi dunia ilivyo laini na thabiti sasa; lakini kazi hii yote ni kuhusu hali ya kurudi Sayuni; msijali kuhusu mambo hayo sasa, na wakati siku ya kurudi Sayuni inapowadia yote yatakuwa kamili. Ni nani ambaye hataki kurejea Sayuni hivi karibuni? Ni nani asiyetamani Baba na wana wapatane tena hivi karibuni? Haijalishi jinsi starehe za kidunia zinavyofurahisha, haziwezi kushikilia miili yetu; tutavuka mipaka ya miili yetu ya sasa na kwa pamoja tutarudi Sayuni. Ni nani huthubutu kuzuia? Ni nani huthubutu kuweka vikwazo? Mimi bila ya shaka Sitamsamehe! Mimi Nitaviondoa vikwazo vyote. (Sababu kwa nini Ninasema Siwezi kurudi Sayuni moja kwa moja ni kwa sababu ya hili. Ninatekeleza kazi hii ya utakaso wakati huo huo Ninaposhuhudia wana Wangu wazaliwa wa kwanza; kazi hizi mbili zinaendelea kwa wakati mmoja. Wakati kazi ya utakaso imekamilika, utakuwa wakati wa Mimi kuwafichua wana wazaliwa wa kwanza. Vikwazo ambavyo Nimezungumzia vinarejelea idadi kubwa ya watenda huduma, hivyo Ninasema kwamba kazi hizi mbili zinafanyika sawia.) Nitawafanya wanangu wazaliwa wa kwanza wazunguke pamoja na Mimi kote ulimwenguni na kufika miisho ya dunia, kuvuka milima na mito na vitu vyote; ni nani huthubutu kukwamisha? Ni nani huthubutu kuzuia? Mkono Wangu haumuachilii kwa urahisi mtu yeyote; mbali na wanangu wazaliwa wa kwanza, Mimi hughadhibika dhidi ya na kuwalaani wote. Kote katika nchi zote hakuna mwenye kufa hata mmoja anayepokea baraka Zangu; wote hukumbana na laana Yangu. Tangu mwanzo wa uumbaji wa dunia, Mimi Sijambariki yeyote; hata wakati Mimi Nimepeana baraka imekuwa maneno tu, haijawahi kamwe kuwa uhalisi, kwa sababu Mimi Ninamchukia Shetani kwa hali ya juu, na Mimi Sitawahi kamwe kumbariki, ila kumwadhibu tu. Ni mwishowe tu, baada ya Mimi kumshinda Shetani kikamilifu, baada ya ushindi kamili kuwa Wangu, Nitakapowapa baraka za kimwili wahudumu wote waaminifu, Niwaache wanisifu Mimi kama starehe, kwa sababu kazi Yangu itakuwa imekamilika.
Kwa kweli muda Wangu hautakuwa mrefu zaidi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita unafikia ukamilisho mbele ya macho yako. (Hakika ni mbele ya macho yako; siyo kuonyesha kabla, unaweza kuona kutoka kwa hali Yangu ya moyo.) Mimi Nitawachukua wanangu wazaliwa wa kwanza mara moja hadi nyumbani Sayuni. Baadhi ya watu watasema, “Kwa kuwa ni kwa ajili ya wazaliwa wa kwanza tu, kwa nini Utumie miaka elfu sita yenye thamani ya wakati? Na kwa nini Ufanye watu wengi?” Nimesema kabla kuwa kila kitu Changu ni cha thamani. Ni jinsi gani wanangu wazaliwa wa kwanza wasiwe hivyo hata zaidi? Mimi Nitawahamasisha wote kunitumikia Mimi, na zaidi ya hayo, Mimi Nitafichua nguvu Yangu, ili kila mtu aweze kuona kwamba katika ulimwengu dunia wote hakuna kitu hata kimoja ambacho hakimo mikononi mwetu, hakuna mtu hata mmoja ambaye hayuko katika huduma Yetu, na hakuna ufanikishaji hata mmoja ambao haujatekelezwa kwa ajili yetu. Mimi nitafanikisha kila kitu. Kwangu Mimi hakuna wazo la muda; ingawa Mimi nadhamiria kuukamilisha mpango na kuikamilisha kazi Yangu kwa miaka elfu sita, kwangu Mimi yote yamekombolewa na huru. Hata kama ni chini ya miaka elfu sita, mradi kwa maoni Yangu wakati umefika, ni nani angethubutu kutamka neno la upinzani? Ni nani angethubutu kusimama na kuhukumu apendavyo? Kazi Yangu, Mimi hufanya Mwenyewe; Muda wangu, Mimi hupanga Mwenyewe. Hakuna mtu, hakuna jambo, hakuna kitu huthubutu kutenda kimakusudi; Mimi nitavifanya vyote vinifuate. Kwangu Mimi hakuna jema au bovu; Mimi Nikisema ni jema, ni jema kabisa; Mimi Nikisema ni bovu, hilo ni kweli pia. Hupaswi daima kutumia dhana za binadamu kunipima Mimi! Mimi Ninasema wana wazaliwa wa kwanza pamoja na Mimi tumebarikiwa—ni nani huthubutu kukataa kunyenyekea? Mimi Nitakuangamiza papo hapo! Wakataa kunyenyekea! Wewe ni muasi! Mimi sina huruma kabisa kwa wanadamu wote, Mimi nimewachukia kwa kiasi fulani; Mimi siwezi kabisa kuwa mvumilivu zaidi. Kulingana na Mimi, ulimwengu mzima ni lazima uangamizwe mara moja, ni hapo tu ndipo kazi Yangu kubwa itakapokamilishwa, ni hapo tu ndipo usimamizi wa mpango Wangu wa usimamizi utakapokamilishwa, ni hapo tu ndipo chuki iliyo moyoni Mwangu itakapoondoka. Sasa Mimi Ninajali tu kuhusu kushuhudia wanangu wazaliwa wa kwanza, masuala mengine yote Mimi Nitayaweka kando na kutojali kwa sasa; kwanza fanya jambo lililo kuu, kisha fanya jambo la kufuata. Hizi ndizo hatua za kazi Yangu, hakuna yeyote anayepaswa kuenda kinyume na hili, wote lazima wafuate Ninayosema Mimi, ili wasiwe malengo ya laana Yangu.
Sasa kazi Yangu imekamilika, Naweza kupumzika. Kuanzia sasa na kuendelea, Sitafanya kazi tena, Nitawaamuru wana Wangu wazaliwa wa kwanza kunifanyia yote Ninayotaka kufanyiwa, kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza ni Mimi, wana Wangu wazaliwa wa kwanza ni nafsi Yangu; hili si kosa hata kidogo, msifuate dhana na kuhukumu. Kuwaona wana wazaliwa wa kwanza ni kuniona Mimi, kwa sababu sisi ni kitu kimoja; yeyote anayetutenganisha hivyo ananipinga Mimi, na Sitasamehe. Katika maneno Yangu, kuna mafumbo yasiyoeleweka kwa mwanadamu. Ni wale tu Ninaowapenda wanaoweza kunieleza Mimi, na hakuna wengine wanaoweza kufanya hivyo; hili limeamuliwa na Mimi, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Maneno Yangu ni thamani, Maneno Yangu ni ya kina na hayawezi kueleweka. Wote ni lazima watumie juhudi kubwa kwa maneno Yangu, jaribuni kuyatafakari maneno Yangu mara kwa mara, msikose neno hata moja au sentensi, vinginevyo watachukua maana yenye makosa, na kutoyaelewa maneno Yangu. Mimi Nimesema tabia Yangu haivumilii kosa, ikimaanisha kuwa wanangu wazaliwa wa kwanza walioshuhudiwa hawawezi kupingwa. Wanangu wazaliwa wa kwanza huwakilisha kila kipengele cha tabia Yangu, kwa hivyo tarumbeta takatifu inapopigwa, hapo ndipo Mimi Ninapoanza kuwashuhudia wana wazaliwa wa kwanza; na hivyo baadaye tarumbeta takatifu itakuja baadaye kuwa tangazo taratibu la tabia Yangu kwa halaiki. Kwa maneno mengine, wakati wana wazaliwa wa kwanza wanapofichuliwa, huo ndio utakuwa wakati ampapo tabia Yangu inafichuliwa. Ni nani anayeweza kulielewa hili? Mimi nasema hayo hata katika mafumbo niliyoyafichua Mimi, hapo yanabaki mafumbo ambayo watu hawawezi kufumbua. Ni nani kati yenu ambaye kwa kweli amejaribu kuelewa maana ya kweli ya maneno haya? Tabia Yangu ni nafsi ya mtu kama vile ambavyo mmefikiria? Ni kosa la kijinga lililoje! Leo yeyote ambaye huona wanangu wazaliwa wa kwanza ni kitu cha baraka na huona tabia Yangu, hili ni kweli kabisa. Wanangu wazaliwa wa kwanza huniwakilisha Mimi mzima, bila shaka yoyote ni nafsi Yangu. Hakuna yeyote anayepaswa kutilia hili shaka! Walio watiifu wanabarikiwa na neema, na waasi wanalaaniwa. Hili ndilo Ninaloamrisha Mimi, na hakuna yeyote anayeweza kulibadilisha!