Sura ya 118

Yeyote atakayeinuka kumshuhudia Mwana Wangu, Nitampa neema; yeyote ambaye hatainuka kumshuhudia Mwana Wangu, ila badala yake apinge na kutumia dhana za mwanadamu ili Amtathmini, Nitamwangamiza. Lazima wote waone waziwazi! Kumshuhudia Mwana Wangu ni kitendo cha kunicha nako kunayaridhisha mapenzi Yangu. Usimheshimu tu Baba lakini umdhulumu na kumkandamiza Mwana. Wale wanaofanya hivyo ni wa dhuria ya joka kuu jekundu na Sihitaji watu duni kama hawa kumshuhudia Mwanangu; Nitawaangamiza katika shimo lisilo na mwisho. Nawataka watendaji huduma waaminifu na wa kweli kutoa huduma kwa Mwanangu, na Simhitaji yeyote kati ya wengine wote. Hii ni tabia Yangu ya haki na inatumika kuonyesha kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe mtakatifu na Asiye na dosari. Sitamsamehe yeyote anayezikosea amri Zangu za utawala. Yeyote aliyekuasi au kukutesa zamani, iwe katika familia au dunia, Nitamwadibu mmoja mmoja na hakuna atakayehurumiwa, kwani hakuna sehemu Yangu ambayo ni ya mwili na damu. Kutoa ushuhuda ka ajili Yako leo kunaonyesha kwamba wale watendaji huduma wamemaliza kutoa huduma kwa ajili Yangu, hivyo usiwe na haya yoyote na usiwe na mashaka. Wao ni watendaji huduma Wako hata hivyo na hatimaye Wewe ni wa mbinguni, na Utarudi kwa mwili Wangu mwishowe, kwani mwili Wangu hauwezi kuwa bila Wewe. Wale waliokuasi na ambao hawakulingana na Wewe zamani (hili ni jambo ambalo wengine hawawezi kuliona, ila Wewe pekee Unalijua moyoni mwako) sasa wamefichua maumbo yao ya asili na wameanguka, kwani Wewe ni Mungu Mwenyewe na Hutavumilia yeyote kukuasi au kukukosea. Ingawa haiwezi kuonekana hata kidogo kutoka nje, Roho Wangu yuko ndani Yako na hili ni dhahiri. Lazima watu wote waliamini, fimbo Yangu ya chuma isije ikawaua wale wote wanaoniasi! Kwa sababu Ninakushuhudia, hakika Unabeba mamlaka, na kila kitu Unachosema ni maonyesho Yangu, kila kitu Unachokifanya ni dhihirisho Langu, kwani Wewe ni mpendwa Wangu na Wewe ni sehemu ambayo nafsi Yangu haiwezi kuwa bila. Hivyo kila kitendo Chako, kile Unachovaa, kile Unachotumia, na mahali Unapoishi—hakika pia ni matendo Yangu. Hakuna anayepaswa kujaribu kutafuta kitu dhidi Yako, na hakuna anayepaswa kukutia makosani. Iwapo yeyote atafanya hili, Sitamsamehe!

Nitawatoa watumishi wote waovu kutoka kwa nyumba Yangu, na ndani ya nyumba Yangu Nitawafanya watumishi wote waaminifu wawashuhudie wazaliwa Wangu wa kwanza; huu ndio mpango Wangu na ni jinsi ambayo Ninafanya kazi. Wakati watumishi waovu wanapomshuhudia Mwana Wangu inanuka kama wafu nami Ninaichukia. Wakati watumishi Wangu waaminifu wanapomshuhudia Mwana Wangu ni kwa ari na uaminifu, na inakubalika Kwangu. Hivyo, yeyote asiye tayari kumshuhudia Mwana Wangu, ondoka hapa sasa hivi! Sitakulazimisha. Nikikuambia uondoke basi lazima uondoke! Angalia matokeo kwako ni yapi na kile kinachokusubiri, na wale wanaotoa huduma wanaelewa hili zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Hukumu Yangu, hasira Yangu, laana Zangu, kuchoma Kwangu na ghadhabu Yangu kali na yenye hasira vitawafika wowote wanaoniasi wakati wowote. Mkono Wangu haumwonyeshi yeyote huruma; bila kujali jinsi yule anayehudumia alivyokuwa mwaminifu awali, akimwasi Mwana Wangu leo basi Nitamwangamiza mara moja na Sitamweka mbele Yangu. Kutokana na hili mtu anaweza kuuona mkono Wangu usio na huruma. Kwa sababu watu hawanijui na asili zao zinaniasi, hata wale walio waaminifu Kwangu ni kwa ajili ya raha yao wenyewe. Iwapo jambo litatokea la kuwaathiri vibaya, mioyo yao inabadilika mara moja na wanataka kukimbia kutoka upande Wangu. Hii ndiyo asili ya Shetani. Hampaswi kuwa wanaoshikilia maoni yenu, mkijiamini kuwa waaminifu! Kama hakuna manufaa kwao, kundi hili la wanyama hawawezi kuwa waaminifu Kwangu kabisa. Nisingetangaza amri Zangu za utawala, mngekuwa mlikimbia zamani. Nyote sasa mko matatani, msitake kunihudumia lakini msitake kuangushwa kwa mkono Wangu. Nisingetangaza kwamba maafa makuu yatawafika wowote wanaoniasi wakati wowote, mngekuwa mngekimbia kitambo. Je, Sijui ujanja ambao watu wanaweza kuugeukia? Watu wengi zaidi sasa wanahodhi matumaini haba, lakini matumaini hayo yanapogeuka na kuwa masikitiko hawataki kuendelea zaidi na wanaomba kurudi. Nimekwisha kusema awali kwamba Simweki yeyote hapa kinyume cha mapenzi yake, lakini tahadhari kufikiria matokeo yatakavyokuwa kwako, ni huu ni ukweli, si Mimi kukutisha wewe. Hakuna awezaye kuielewa asili ya mwanadamu isipokuwa Mimi, na wote wanafikiria kwamba wao ni watiifu Kwangu, pasipo kujua kwamba utiifu wao ni mchafu. Uchafu huu utawaangamiza watu kwa kuwa wao ni njama ya joka kubwa jekundu. Hilo lilidhihirishwa na Mimi zamani sana; Mimi ni mwenyezi Mungu, na je, Mimi singeweza kufahamu jambo rahisi kama hili? Mimi ninaweza kupenyeza damu yako na mwili wako ili kuziona nia zako. Si vigumu Kwangu kuielewa asili ya mwanadamu, lakini watu hujaribu kuwa wajuaji, wakifikiria kwamba hakuna mtu ajuaye nia zao isipokuwa wao wenyewe. Je, hawajui kwamba, mwenyezi Mungu anaishi ndani ya mbingu na dunia na vitu vyote?

Nitampenda Mwana Wangu hadi mwisho kabisa na Nitalichukia joka kuu jekundu pamoja na Shetani milele hata milele. Kuadibu Kwangu kutawajia wale wote wanaoniasi na hakuna adui hata mmoja atakayehurumiwa. Nimesema awali, “Naweka jiwe kubwa Sayuni. Kwa waumini, jiwe hili ni msingi wa ujenzi wao. Kwa wale wasioamini, hili ni jabali linalowakwaza. Kwa wana wa ibilisi, hili ni jiwe linalowaponda hadi wafe.” Sijasema maneno haya awali tu, ila yametabiriwa na watu wengi na watu wengi wameyasoma katika enzi hii. Aidha, watu wengine wamejaribu kueleza maneno haya, lakini hakuna mtu amewahi kufumbua siri hii awali, kwa sababu kazi hii inafanywa tu wakati uliopo wa siku za mwisho. Hivyo, ingawa watu wengine wamejaribu kuyaeleza maneno haya maelezo yao yote ni uongo. Leo, Nafichua maana nzima kwenu ili mweze kujua uzito wa Mimi kuwashuhudia wazaliwa Wangu wa kwanza, na kusudi Langu katika kufanya hivyo. Naweka jiwe kubwa Sayuni na jiwe hili linarejelea wazaliwa Wangu wa kwanza wakishuhudiwa. Neno “kubwa” halimaanishi kwamba kushuhudia huku kunafanywa kwa kiwango fulani kikubwa kabisa, ila badala yake kwamba katika kuwashuhudia wazaliwa Wangu wa kwanza, watendaji huduma wengi zaidi watakimbia. Hapa, “wale wasioamini” wanarejelea wale wanaokimbia kwa sababu Mwana Wangu anashuhudiwa, kwa hiyo jiwe ni kipingamizi kwa mtu wa ina hii. Nasema ni jabali kwa sababu mtu wa aina hii atauawa kwa mkono Wangu, kwa hiyo jabali linalowasababisha watu kujikwaa halisemwi kuhusiana na kuanguka au kuwa dhaifu, ila linasemwa kuhusiana na kuuawa kwa mkono Wangu. “Waumini” katika “Kwa waumini, jiwe hili ni msingi wa ujenzi wao” wanarejelea wale watendaji huduma ambao ni waaminifu, na “msingi wa ujenzi wao” unarejelea neema na baraka ambazo watapokea baada ya wao kunihudumia kwa uaminifu. Kwamba wazaliwa wa kwanza wameshuhudiwa inaonyesha kwamba enzi hii yote nzee itapita punde, na inaashiria uharibifu wa ufalme wa Shetani; kwa hiyo, kwa mataifa ni jabali linalowaponda hadi wafe. Hivyo kuyavunjavunja mataifa yote na kuwa vipande vipande inarejelea dunia nzima kufanywa upya kabisa; mambo ya zamani yatapita na mapya yataanzishwa—hii ndiyo maana ya kweli ya “kuvunjavunja.” Je, mnaelewa? Kazi Ninayoifanya katika hatua hii ya mwisho inaweza kufupishwa kwa maneno haya machache tu. Hili ni tendo Langu la ajabu na unapaswa kuyaelewa mapenzi Yangu ndani ya maneno Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 117

Inayofuata: Sura ya 119

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp