Sura ya 117

Wewe Ndiwe unayefungua kitabu, Wewe Ndiwe unayefungua mihuri saba, kwa sababu siri zote hutoka Kwako na baraka zote hufichuliwa na Wewe. Mimi sina budi kukupenda Wewe milele, na Mimi sina budi kuwafanya watu wote wakuabudu Wewe, kwa sababu Wewe ni nafsi Yangu, Wewe ni sehemu ya onyesho Langu kamili lenye ukarimu, sehemu ya msingi ya mwili wangu. Kwa hiyo, ni lazima Mimi Nitoe ushuhuda maalum. Ni nani mwingine kando na Yule mmoja aliye ndani ya nafsi Yangu anayefuata Moyo Wangu? Si Wewe Mwenyewe ambaye hutoa ushahidi kwa ajili Yako, lakini Roho Wangu ambaye hutoa ushahidi kwa ajili Yako, na kwa hakika Mimi sitamsamehe yeyote ambaye huthubutu kukupinga Wewe, kwa kuwa hili huhusu amri Zangu za utawala. Yote ambayo Wewe husema kwa hakika Nitayatimiza, na yote ambayo Wewe hufikiri kwa hakika Nitayakubali. Ikiwa mtu fulani si mwaminifu kwako Wewe basi ananipinga Mimi waziwazi, na kwa hakika Mimi Sitamsamehe. Mimi Nitawaadhibu kwa ukali wote ambao humpinga Mwanangu, na Mimi Nitawabariki wale ambao wanalingana na Wewe. Haya ndiyo mamlaka ambayo Mimi Ninakutunukia Wewe. Katika yale yaliyozungumzwa hapo awali—matakwa na viwango vilivyowekwa kwa wana wazaliwa wa kwanza—Wewe ni kielelezo. Hiyo ni kusema, kama wewe ulivyo ndivyo Nitawataka wana wazaliwa wa kwanza. Hiki si kitu ambacho binadamu wanaweza kufanya, lakini ni kile ambacho Roho Wangu Mwenyewe hufanya. Iwapo mtu yeyote anaamini kwamba ni wanadamu ambao wanashuhudia kwa ajili Yako basi kiumbe huyo bila shaka ni mfano wa Shetani na adui Wangu! Kwa hiyo, ushahidi ni wenye kuondoa shaka, milele haubadiliki, na kile ambacho Roho Mtakatifu huthibitisha! Hakuna yeyote anayeruhusiwa kubadilisha hilo kwa urahisi, na yeyote atakayefanya kitendo hicho, Mimi Sitasamehe! Kwa kuwa wanadamu hawawezi kuwa na ushuhuda kwa ajili Yangu, Mimi Mwenyewe hushuhudia kwa nafsi Yangu, na watu hawapaswi kuingilia kazi Yangu! Haya ni maneno ya hukumu kali ambayo kwayo kila mtu lazima awe mzingatifu!

Mnapaswa kufikiria na kuzingatia kila kitu katika yale Ninayoyasema Mimi. Usichukulie maneno Yangu kikawaida, bali sikiliza kwa makini. Kwa nini Ninasema kwamba wana wazaliwa wa kwanza ni nafsi Yangu? Na sehemu ya lazima ya ufalme Wangu? Kabla ya enzi zote tuliishi pamoja na hatukuwahi kutengana. Kwa sababu ya mvurugo wa Shetani, baada ya Mimi kuwa mwili mara ya kwanza Mimi Nilirudi tena Sayuni. Kuendelea kutoka hapa, sisi sote tulikuja katika dunia, na baada ya Mimi kupata ushindi katika siku za mwisho—yaani, baada ya mimi kuwapata nyinyi tena kutoka kwa mwili ambao Shetani amepotosha—Mimi nitawaleta tena Sayuni ili nafsi Yangu iweze kuungana tena, kutotenganishwa tena kamwe. Baada ya hayo Mimi Sitapata mwili upya tena, na nyinyi hakika hamtatoka katika mwili Wangu. Hiyo ni kusema, baada ya hapo Sitaiumba dunia tena, bali Nitabaki milele bila kutenganishwa na wana Wangu wazaliwa wa kwanza katika Sayuni, kwa sababu kila kitu kimekamilishwa kwelikweli, na Mimi Nimekaribia kuhitimisha enzi nzee nzima. Ni katika Sayuni tu ambako kuna maisha ya mbingu na nchi mpya, kwa kuwa nafsi Yangu hupatikana Sayuni. Hakutakuwa na mbingu mpya au dunia mpya zaidi ambazo zipo bali na hii. Mimi ni mbingu mpya, na Mimi pia ni nchi mpya, kwa sababu nafsi Yangu hujaza Sayuni nzima. Inaweza pia kusemwa kwamba wana Wangu wazaliwa wa kwanza ndio mbingu mpya, wana Wangu wazaliwa wa kwanza ni dunia mpya. Wanangu wazaliwa wa kwanza na Mimi tu mwili mmoja, hatutengani. Kusema juu Yangu ni lazima kujumuisha wana wazaliwa wa kwanza, na Mimi kwa hakika Sitamsamehe yeyote anayejaribu kututenganisha. Wakati Ninayafanya mataifa yote na watu kurejea mbele ya kiti Changu cha enzi, mashetani yote yatafedhehiwa na mapepo machafu yatatoroka kwa woga mbali na Mimi. Halafu ni hakika kuwa haki itakuwepo miongoni mwa watu wote (kumaanisha miongoni mwa wana na watu wangu), na ni hakika kwamba hakutakuwa na usumbufu wowote wa Shetani kati ya mataifa yote, kwa kuwa Nitakuwa Nikitawala mataifa yote na watu wote, Nitakuwa na mamlaka juu ya ulimwengu wote mzima, na mashetani wataharibiwa kabisa, watashindwa kabisa, na kupokea adhabu ya amri Zangu za utawala.

Ninaendelea na kazi miongoni mwa watu wote, lakini wanayo tu nuru ya Roho Wangu, na hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyehitimu kufichua mafumbo Yangu, hakuna aliyehitimu kunieleza. Ni Yule tu mtu ambaye huja kutoka Kwangu tu mwenye sifa zinazostahili za kufanya kazi Yangu, jinsi ilivyo kwa wengine, Mimi huwatumia tu watu hao kwa muda. Roho Wangu hatamshukia mtu kiholela, kwa kuwa kila kitu ndani Yangu ni cha thamani. Kwa Roho Wangu kushuka juu ya mtu fulani na kwa Roho Wangu kufanya kazi kwa mtu fulani ni vitu tofauti kabisa. Roho Wangu hufanya kazi kwa watu walio nje Yangu, lakini Roho Wangu hushuka juu ya Yule mtu ambaye hutoka Kwangu. Haya ni mambo mawili yasiyohusiana kabisa. Kwa maana Yeye ajaye kutoka Kwangu ni mtakatifu, lakini wale walio nje yangu si watakatifu, hata wawe wazuri jinsi gani. Roho Wangu hatamshukia mtu kwa sababu yoyote ndogo. Watu wasiwe na wasiwasi. Sifanyi makosa yoyote, na Nina uhakika asilimia mia moja juu ya kile Ninachofanya! Kama Nlivyomshuhudia, hakika pia Nitamlinda; kwamba Mtu hakika anatoka Kwangu na ni wa lazima kwa nafsi Yangu. Kwa hiyo, Natumaini watu wanatenga dhana zao wenyewe, waache mawazo waliyopewa na Shetani, waamini kila tamko Langu kuwa ni la kweli, na hawayaruhusu mashaka kuingia katika mawazo yao. Hili ndilo Agizo Langu kwa ubinadamu, mawaidha Yangu kwa ubinadamu. Kila mtu lazima azingatie mambo haya, kila mtu lazima ayatii kwa dhati, na ni lazima ayachukue Ninayoyasema kuwa ndicho kiwango.

Mimi sipaswi tu kuanza kazi Yangu miongoni mwa mataifa na watu wote, bali pia Kuanzisha kazi Yangu kila mahali katika ulimwengu, na hii inaonyesha hata zaidi kwamba siku ya kurudi Kwangu Sayuni haiko mbali (kwa sababu ni muhimu Kwangu kurudi Sayuni kabla Nianze kazi miongoni mwa watu wote na katika ulimwengu mzima). Je, kuna mtu yeyote ambaye anaweza kuzielewa hatua za kazi Yangu na njia ambayo Mimi hufanya kazi? Sababu ya Mimi kusema Nitakutana na wageni katika roho ni kwa sababu hili kimsingi haliwezi kufanyika katika mwili, na kwa sababu Mimi sitaki kuhatarisha hatari kwa mara ya pili. Hizi ndizo sababu za kuwasiliana kwa karibu na wageni katika roho. Hii inapaswa kuwa katika ulimwengu wa kweli wa kiroho, sio ulimwengu wa kiroho usio wazi kama inavyofikiriwa na wale[a] wanaoishi katika mwili. Kile Ninachokisema wakati huo kitakuwa ni tofauti tu katika jinsi Mimi husema kwani itakuwa ni enzi tofauti. Kwa hiyo, Mimi Nawakumbusha binadamu tena na tena kuhakiki jinsi ambavyo Mimi hunena, na Mimi Nawakumbusha wanadamu pia kwamba kuna siri katika kile ambacho Mimi husema ambacho watu hawawezi kukifunua. Lakini hakuna anayeelewa kwa nini Mimi Nasema vitu hivi, na kwa sababu tu Mimi Nawaambia hili leo ndipo muweze kuelewa kidogo, lakini bado si kabisa. Baada ya enzi hii katika kazi Yangu, Mimi nitawaarifu hatua kwa hatua. (Bado Mimi Ninataka kuondoa baadhi ya watu kupitia hili, hivyo Mimi Sitasema chochote kwa sasa.) Hii ndiyo njia ya hatua ifuatayo katika kazi Yangu. Kila mtu anapaswa kuhakiki na kuona wazi kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni wa busara.

Tanbihi:

a. Maandiko ya awali hayana maneno “kama inavyowazwa na wale.”

Iliyotangulia: Sura ya 116

Inayofuata: Sura ya 118

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp