Sura ya 116
Kati ya maneno Yangu, kunayo mengi ambayo huwafanya watu waogope. Maneno Yangu mengi huwafanya watu watetemeke kwa hofu, namaneno Yangu mengi huwafanya watu wateseke na kukata tamaa, na hata zaidi husababisha maangamizo ya watu. Hakuna anayeweza kuelewa wingi wa maneno Yangu au kuelewa wingi huo vizuri. Ni wakati Ninapowaambia maneno Yangu, sentensi kwa sentensi, na kuyafichua kwenu ndipo mnaweza kufahamu hali ya jumla ya mambo, huku mkisalia msiojua kuhusu sura kamili ya mambo mahsusi. Hivyo, Nitatumia ukweli kufichua maneno Yangu yote, na hapo kuwaruhusu mpate ufahamu wa juu zaidi. Tukizingatia mbinu ya usemi Wangu, sineni tu kwa maneno Yangu, lakini hata zaidi, Mimi natenda kwa maneno Yangu; hii ndiyo maana ya kweli ya “maneno na ufanikishaji kutendeka sawia.” Kwani na Mimi kila kitu ni bure, na kila kitu kinaachiliwa, na kwa msingi huu, yote Ninayoyafanya yamejazwa na hekima. Sineni kiholela, wala Sitendi kiholela. (Iwe ni katika ubinadamu au uungu, Nanena na kutenda kwa hekima, kwa sababu ubinadamu Wangu ni sehemu isiyotenganika ya Mimi Mwenyewe.) Ilhali Ninaponena, hakuna anayezingatia sauti ya usemi Wangu; Ninapotenda, hakuna anayezingatia mbinu ya kazi Yangu. Huu ni upungufu wa mwanadamu. Nitafichua nguvu Yangu juu ya wanadamu wote, siyo tu juu ya wana wazaliwa Wangu wa kwanza, ila hata zaidi Nitafichua nguvu Yangu ndani ya mataifa yote na miongoni mwa watu wote; ni kufanya hivyo tu ndio ushuhuda wa nguvu unaomwaibisha Shetani. Sitendi kwa upumbavu. Watu wengi hufikiri kwamba ushuhuda Wangu kwa wana wazaliwa wa kwanza ni makosa; wanasema kwamba kuna Miungu wengine kando na Mimi, kwamba Natenda bila akili, kwamba Najishusha hadhi; na katika hili, upotovu wa mwanadamu unafunuliwa hata zaidi. Je, Naweza kuwa nimekosea katika kuwashuhudia wazaliwa wa kwanza? Mnasema kwamba Mimi nimekosea, basi, mnaweza kushuhudia? Isingelikuwa kwa sababu uinuaji Wangu, ushuhuda Wangu, bado mngemponda Mwana Wangu chini yenu, bado mngemtendea kwa kutojali kwa dharau, na bado mngemtendea kama mtumishi wenu. Ninyi kundi la nguruwe! Nitamtupa kila mmoja wenu kwa wakati wake! Hakuna atakayesamehewa! Niambieni, ni mambo ya aina gani ndiyo ambayo hayalingani na mtu aliye na ubinadamu wa kawaida? Bila shaka, wao ni nguruwe! Siwezi kuvumilia kabisa kuwaona. Ningesubiri ushuhuda wenu, kazi Yangu tayari ingekuwa imecheleweshwa! Ninyi kundi la nguruwe! Ninyi hamna ubinadamu kabisa hata kidogo! Sikuhitaji wewe unitumikie! Ondoka hapa wakati huu huu! Umemdhulumu na kumnyanyasa Mwanangu kwa muda mrefu sana; Nitakukanyaga hadi upondekepondeke! Utaona kitakachofanyika ukithubutu kuwa mshenzi tena; utaona kitakachofanyika ukithubutu kuniaibisha tena! Tayari Nimekamilisha kazi Yangu kuu; Napaswa kugeuka na kuliangamiza kundi hili la wanyama!
Vyote vinakamilishwa mikononi Mwangu (Inavyohusiana na wale Ninaowapenda), na vyote pia vinaangamizwa mikononi Mwangu (kuhusiana na wale wanyama ambao Ninachukia, na wale watu, masuala na mambo Ninayodharau). Ninawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza kuona yote Nitakayofanya, Ninawaruhusu waelewe kikamilifu na humo kuona yote ambayo Nimefanya tangu kutoka Sayuni. Baadaye, tutaingia pamoja katika Mlima Sayuni, kuingia mahali tulipokuwa kabla ya enzi, na kuishi maisha yetu upya. Kuanzia hapo kuendelea, hakutakuwa na mawasiliano zaidi na dunia na kundi hili la nguruwe, ila uhuru kamili; yote hayatazuiliwa na hayatakuwa na kizuizi. Ni nani anayethubutu kumkataa yeyote kati ya wazaliwa Wangu wa kwanza? Ni nani anayethubutu kuendelea kuwapinga wazaliwa Wangu wa kwanza? Sitamsamehe kwa urahisi! Bila kujali ulivyonicha hapo zamani, hivyo ndivyo lazima uwache wazaliwa Wangu wa kwanza leo. Usiwe namna moja mbele Yangu na nyingine nyuma Yangu; Mimi huona jinsi kila mtu alivyo kwa uwazi dhahiri. Kutokuwa mwaminifu kwa Mwana Wangu ni kutokuwa na upendo wa mtoto kwa mzazi Kwangu, ambao ni ukweli dhahiri, kwani Sisi ni wa mwili mmoja. Ikiwa mtu ni mzuri Kwangu lakini ashikilie mtazamo tofauti kuelekea kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, basi bila shaka ni uzao wa kawaida wa joka kuu jekundu, kwa sababu anauvunja mwili wa Kristo; dhambi hii haiwezi kusameheka kamwe! Kila mmoja wenu lazima aone hili. Ni wajibu wenu kunishuhudia, na zaidi ya hayo, ni wajibu wenu kuwashuhudia wazaliwa wa kwanza. Hakuna yeyote kati yenu atakayekwepa jukumu lake; Nitamtupa yeyote atakayevuruga mara moja! Usifikiri kwamba wewe ni kitu bora. Nakwambia sasa: Yeyote aliye hivyo sana, atakuwa mlengwa wa adhabu Yangu kali! Yeyote aliye hivyo ndiye aliye na tumaini la chini zaidi, na ndiye mwana wa kuangamia zaidi. Nitakuadibu milele!
Kazi Yangu yote inafanywa binafsi na Roho Wangu, na Siruhusu yeyote wa namna ya Shetani kuingilia. Hii ni ili kuepuka kuvuruga mipango Yangu. Mwishowe, Nitawaacha watu wazima na watoto wote wainuke na kunisifu na wazaliwa Wangu wa kwanza, wayasifu matendo Yangu ya ajabu, na kusifu udhihirisho wa nafsi Yangu. Nitaacha sauti ya sifa ingurume katika ulimwengu mzima na hadi miisho ya dunia, ikitikisa milima, mito, na vitu vyote, na Nitamwaibisha Shetani kikamilifu. Nitatumia ushuhuda Wangu kuharibu dunia nzima nzee chafu na ovu, na kutengeneza dunia mpya takatifu na safi. (Katika kusema jua, mwezi, nyota, na sayari za juu hazitabadilika baadaye, Simaanishi kwamba dunia nzee bado iko, ila kwamba dunia nzima itaharibiwa na dunia nzee itabadilishwa. Sinuii kuubadilisha ulimwengu.) Ni hapo tu ndipo itakuwa dunia inayolingana na mapenzi Yangu; ndani yake, hakutakuwa na aina hii ya uonevu iliyoko leo, wala hakutakuwa na hali ya sasa ya watu kunyanyasana. Badala yake, kutakuwa na usawa na busara kamili ndani ya mwili. (Ingawa Nasema kutakuwa na usawa na busara, itakuwa ndani ya mwili; itakuwa tofauti sana na ufalme Wangu—tofauti kama mbingu na dunia; hakuna njia ya kulinganisha hivyo viwili kabisa—hata hivyo, dunia ya binadamu ni dunia ya binadamu, na dunia ya roho ni dunia ya roho.) Wakati huo, wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tutatumia mamlaka juu ya dunia kama hiyo (katika dunia hii hakutakuwa na vurugu kutoka kwa Shetani, kwa sababu Shetani atakuwa ametupwa nje kabisa na Mimi), lakini maisha yetu bado yatakuwa maisha ya ufalme, jambo ambalo hakuna mtu anayeweza kukana. Katika enzi zote, hakujawahi kuwa na binadamu yeyote (bila kujali jinsi alivyo mwaminifu) ambaye amepitia maisha ya aina hii, kwa sababu katika enzi zote, hakujawahi kuwa na mtu yeyote wa kuchukua wajibu wa mzaliwa Wangu wa kwanza, na bado atanitolea huduma baadaye. Ingawa hawa watendaji huduma ni waaminifu, wao hata hivyo ni uzao wa Shetani ambao wameshindwa na Mimi, hivyo baada ya kifo cha mwili bado wanazaliwa ndani ya dunia ya binadamu kufanya huduma kwa ajili Yangu; hii ndiyo maana ya kweli ya “wana hata hivyo ni wana, na watendaji huduma hata hivyo ni uzao wa Shetani.” Katika enzi zote haijulikani ni watu wangapi waliopo wa kufanya huduma kwa ajili ya wazaliwa wa kwanza wa leo; kati ya watendaji huduma wote, hakuna anayeweza kutoroka, na Nitawafanya wanitumikie milele. Kuhusiana na asili zao, wao wote ni wana wa Shetani, na wote hunipinga Mimi, na ingawa wananifanyia huduma, wao hulazimishwa, na hakuna yeyote kati yao aliye na mbadala. Hii ni kwa sababu kila kitu kinadhibitiwa na mkono Wangu, na watendaji huduma Ninaowatumia lazima wanitumikie hadi mwisho. Hivyo, bado kuna watu wengi leo ambao wana asili sawa na manabii na mitume wa enzi zote, kwa sababu wao ni wa roho moja. Hivyo, bado kuna watendaji huduma wengi waaminifu ambao hukimbia huku na kule kwa ajili Yangu, lakini mwishowe (kwa miaka elfu sita, wamekuwa wakinifanyia huduma siku zote, kwa hivyo watu hawa ni miongoni mwa watendaji huduma), hakuna mtu anayeweza kupata kile ambacho wote katika enzi zote wamekitumainia, kwa sababu kile ambacho Nimetayarisha si kwa ajili yao.
Kila kitu Changu tayari kimekamilishwa mbele ya macho; Nitawafanya wazaliwa Wangu wa kwanza warudi nyumbani Kwangu na warudi upande Wangu, ili tuunganishwe. Kwa sababu Nimerudi kwa shangwe na ushindi na Nimepata utukufu kikamilifu, Naja kuwarudisha. Zamani, watu wengine walibashiri “mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu”. Ingawa utabiri huo si sahihi, lakini pia si wenye makosa kabisa—hivyo, Naweza kuwapa ninyi maelezo fulani. “Mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu” kwa pamoja hawawakilishi idadi ya watu wala aina ya mtu. “Mabikira watano wenye busara” inaashiria idadi ya watu, na “mabikira watano wapumbavu” inaashiria aina moja ya watu, lakini hakuna kati ya hivi viwili inayorejelea wana wazaliwa wa kwanza. Badala yake, vinawakilisha uumbaji. Hii ndiyo maana wameulizwa waandae mafuta katika siku za mwisho. (Viumbe hawana sifa Yangu; kama wanataka kuwa wale wenye busara, wanahitaji kuandaa mafuta, na hivyo wanahitaji kujitayarisha na maneno Yangu.) “Mabikira watano wenye busara” wanawakilisha wana Wangu na watu Wangu kati ya wanadamu Niliowaumba. Wanaitwa “mabikira” kwa sababu wanapatwa na Mimi, licha ya wao kuzaliwa duniani; mtu anaweza kuwaita watakatifu, kwa hivyo wanaitwa “mabikira.” “Watano” liliotajwa awali linawakilisha idadi ya wana Wangu na watu Wangu ambao Nimewajaalia. “Mabikira watano wapumbavu” linarejelea watendaji huduma, kwa kuwa wananifanyia huduma bila kushikilia hata umuhimu mdogo kwa maisha, wakifuatilia tu mambo ya nje (kwa sababu hawana sifa Yangu, bila kujali kile wanachokifanya, hicho ni kitu cha nje), na hawawezi kuwa wasaidizi Wangu wenye uwezo, kwa hiyo wanaitwa “mabikira wapumbavu.” “Watano” lililotajwa awali linamwakilisha Shetani, na ukweli kwamba wanaitwa “mabikira” kunamaanisha wameshindwa na Mimi na wanaweza kunifanyia Mimi huduma—lakini watu kama hao sio watakatifu, kwa hivyo wanaitwa watendaji huduma.