Sura ya 78
Nimesema kabla ya kuwa kazi inafanywa na Mimi, sio na mwanadamu yeyote. Kwangu, kila kitu kimetulia na kufurahi, lakini na ninyi mambo ni tofauti sana na chochote mnachofanya ni kigumu sana. Kitu chochote Ninachokubali hakika kitatimizwa na Mimi, wakati mtu yeyote Ninayemkubali atakamilishwa na Mimi. Wanadamu—msiingilie katika kazi Yangu! Chote tu mnachohitaji kujishughulisha nacho ni kufuata uongozi Wangu, kufanya kile Ninachopenda, kukataa yote ambayo Ninayachukia, mjivute kutoka kwa dhambi, na mjitupe ndani ya kumbatio Langu lenye upendo. Mimi sijisifu kwenu, wala Mimi sitii chumvi. Huo ndio ukweli hakika. Nikisema nitauangamiza ulimwengu, basi kufumba na kufumbua, ulimwengu utageuka kuwa majivu. Nyinyi mara kwa mara huwa na wasiwasi sana na kuongezea mzigo wenu wenyewe, mkiogopa sana kwamba maneno Yangu ni matupu, kwa hivyo nyinyi mnakimbia huku na kule mkijaribu “kutafuta njia ya kutokea” kwa ajili Yangu. Kipofu! Mjinga! Hujui hata thamani yako mwenyewe na unajaribu kuwa mshauri Wangu. Je, unastahili? Jiangalie vizuri kwenye kioo!
Hebu Nikwambie! Waoga lazima waadibiwe kwa ajili ya uoga wao, wakati walio waaminifu zaidi watapata baraka kwa ajili ya imani yao. Ili kuwa wazi, jambo muhimu zaidi sasa ni “imani.” Wakati baraka ambazo zitawafikia hazijafichuliwa bado, nyinyi mnahitaji kufanya jitihada zenu zote kujitumia kwa ajili Yangu kwa wakati huu. Wale wanaodaiwa kuwa “kubarikiwa” na “kuteseka na janga” hurejelea kipengele hiki. Wana Wangu! Je, maneno Yangu bado yamewekwa katika mioyo yenu? “Kwa wale wanaojitumia kwa dhati kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki sana.” Leo, unaelewa kweli maana inayokaa ndani? Sisemi maneno matupu; kuanzia sasa hakuna kitakachofichwa. Hiyo ni kusema kwamba mambo ambayo yalifichwa katika maneno Yangu hapo awali sasa yataambiwa ninyi moja baada ya nyingine, bila kufichwa kabisa. Zaidi ya hayo, kila neno litakuwa maana Yangu ya kweli, bila kutaja kuwa kufichua watu, matukio na mambo yote yaliyofichwa mbele Yangu kutakuwa rahisi kufanywa na hakutakuwa kugumu Kwangu. Kila kitu ninachokifanya Mimi kina kipengele cha ubinadamu Wangu wa kawaida, na pia kipengele cha uungu Wangu kamili. Je, nyinyi kweli mna ufahamu wazi wa maneno haya? Hiyo ndiyo maana Ninaendelea kurudia: Usiwe na haraka nyingi sana. Kumfichua mtu au kitu si vigumu Kwangu, na daima kuna wakati kwa ajili ya hilo. Je, sivyo? Watu wengi sana wamefunuliwa maumbo yao ya kweli mbele Yangu. Iwe ni roho wa mbweha, mbwa, au mbwa mwitu, wote hufichua maumbo yao ya kweli katika wakati maalum ambao Ninaamua, kwa sababu kila kitu Ninachofanya ni sehemu ya mpango Wangu. Kuhusu hoja hii lazima uelewe vizuri kabisa!
Je! Wewe kweli unafahamu ni nini “Wakati hauko mbali sana” unalenga? Katika siku zilizopita, daima ulifikiria kuwa ilirejelea siku Yangu, lakini ninyi nyote mmekuwa mkifasiri maneno Yangu kwa msingi wa dhana zenu. Hebu nikwambie! Mtu yeyote ambaye anafasiri vibaya maneno Yangu kuanzia sasa kuendelea bila shaka ni mpuuzi! Maneno “Wakati hauko mbali sana” ambayo nilinena yanarejelea siku zenu za kufurahia baraka, yaani, siku ambapo roho zote zenye uovu zitaangamizwa na kuondolewa kanisani Mwangu, njia zote za binadamu za kufanya mambo zitakataliwa, na zaidi ya hayo yanarejelea siku zile wakati majanga yote makubwa yatashuka. Kumbuka hili! Ni “majanga yote makubwa,” na hili usilielewe vibaya tena. Majanga Yangu makubwa yatashuka juu ya ulimwengu wote kutoka mikono Yangu kwa wakati mmoja. Wale ambao wamepata jina Langu watabarikiwa na hakika hawatavumilia mateso haya. Je! Bado unakumbuka? Je, unaelewa wazi juu ya kile Nilichosema? Wakati Ninapozungumza ndio wakati Ninaanza kufanya kazi (majanga yale makubwa huja wakati huu). Nyinyi kwa kweli hamfahamu malengo Yangu. Je, mnajua kwa nini Mimi huwawekea matakwa makali namna hiyo, bila kukuonyesha huruma yoyote hata kidogo? Pindi wakati hali ya kimataifa ni ya wasiwasi, na huku wale (wanaoidaiwa kuwa) walio mamlakani ndani ya China wanafanya maandalizi yote, ndio wakati ambapo bomu la wakati linakaribia kulipuka. Wale wanaotafuta njia ya kweli kutoka kwa mataifa yale saba watafurika nchini China kama maji kupitia njia za mafuriko, bila kujali gharama. Wengine huchaguliwa na Mimi, wengine ni wa kunitumikia Mimi, lakini hakuna mwana mzaliwa wa kwanza kati yao. Hili ni tendo Langu! Hili lilikuwa limefanyika wakati Niliumba ulimwengu. Ondoa dhana zako za kibinadamu. Usifikiri Mimi nazungumza maneno yasiyo na maana! Yale Ninafikiri ndiyo yale Nimeyatenda. Mpango Wangu pia ni kitu ambacho Nimekwisha kutimiza. Je! Unaelewa wazi jambo hili?
Mambo yote ya kila kitu yanatulia pamoja na mawazo Yangu na kwa mpango Wangu. Mwanangu! Nilikuchagua kwa ajili yako binafsi na zaidi ya hayo kwa sababu Ninakupenda. Yeyote anayethubutu kuasi katika mawazo, au kukuza moyo wenye wivu, atakufa kwa laana Yangu na kuchomeka. Hii inahusisha amri za utawala za ufalme Wangu kwa sababu ufalme leo tayari umeundwa. Lakini mwana Wangu, wewe inabidi uwe mwangalifu na haupaswi kuichukulia hii kama aina ya mtaji. Unapaswa kuzingatia moyo wa Baba na, kwa njia hii, kutambua juhudi za Baba zenye uangalifu. Kutokana na hili, mwana Wangu lazima aelewe ni aina gani ya mtu Ninayempenda zaidi, ni aina gani ya mtu Ninayempenda pili, ni aina gani ya mtu Ninayemchukia zaidi, na ni aina gani ya mtu Ninayemchukia. Usiendelee kuongeza shinikizo kwako mwenyewe. Tabia yoyote uliyo nayo yote ilikuwa imepangwa kabla na Mimi na ni ufunuo wa kipengele kimoja cha tabia Yangu ya uungu. Ondoa mashaka yako! Sifichi chuki kuelekea wewe. Napaswa kulisema hili jinsi gani? Je, wewe bado haufahamu? Je! Bado unazuiliwa na hofu yako? Ni nani mwaminifu, ni nani mwenye shauku, ni nani ambaye ni mwaminifu, ni nani mdanganyifu—Najua yote, kwa vile kama Nilivyosema hapo awali, Najua hali ya watakatifu kama vile kiganja cha mkono Wangu.
Katika macho Yangu, kila kitu kimekwisha kutimizwa kitambo na kufichuliwa (Mimi ni Mungu anayechunguza mioyo ya ndani ya watu. Ni kwa ajili tu ya kuwaonyesha kipengele cha ubinadamu Wangu wa kawaida, ni hayo tu), lakini kwenu nyinyi imefichwa na haijatimizwa. Hii yote ni kwa sababu nyinyi hamnijui Mimi. Yote yako katika mikono Yangu, yote yako chini ya miguu Yangu, na macho Yangu yanachunguza vitu vyote; ni nani anayeweza kuepuka hukumu Yangu? Wote walio wachafu, wale walio na vitu vya kuficha, wale wanaohukumu nyuma ya mgongo Wangu, wale ambao wana upinzani katika mioyo yao, na kadhalika—watu wote ambao hawaonekani kuwa na thamani katika macho Yangu lazima wapige magoti mbele Yangu na wajitue mzigo wao wenyewe. Labda baada ya kusikia hili, watu wengine watahamasishwa kidogo, wakati wengine hawataamini ni jambo lenye uzito kiasi hiki. Hebu niwaonye! Hebu wenye hekima waharakishe kutubu! Ikiwa wewe ni mpumbavu basi subiri tu! Angalia ni nani atakabiliwa na janga wakati ufikapo!
Mbingu bado ni mbingu ya awali na dunia bado ni dunia ya awali, lakini kwa mtazamo Wangu mbingu na dunia tayari zimebadilika na si mbingu na dunia zilivyokuwa hapo awali. Mbingu inarejelea nini? Unajua? Na mbingu ya leo inarejelea nini? Mbingu ya zamani inarejelea nini? Hebu Niwajulishe hili: Mbingu ya zamani ilirejelea Mungu uliyemwamini lakini ambaye hakuna mtu aliyemwona, na ni Mungu ambaye watu walimwamini kwa unyoofu wa kweli (kwa sababu hawakuweza kumwona), lakini mbingu ya leo inarejelea ubinadamu Wangu wa kawaida pamoja na uungu Wangu kamili, yaani, Mungu huyu wa vitendo Mwenyewe. Ni Mungu yuleyule, basi kwa nini nasema mimi ni mbingu mpya? Haya yote yanaelekezwa kwenye dhana za mwanadamu. Dunia ya leo inarejelea mahali mlipo. Dunia ya zamani haikuwa na sehemu moja ambayo ilikuwa takatifu, ambapo maeneo unayoenda leo yametengwa kuwa patakatifu, ndiyo maana nasema ni dunia mpya. Neno “mpya” hapa linamaanisha “takatifu.” Mbingu mpya na dunia sasa zimetimizwa kabisa. Je, mko wazi juu ya hili? Nitawafunulia siri zote, ukurasa kwa ukurasa. Msiwe na haraka, na siri kubwa zaidi zitafunuliwa kwenu!