Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Furahini, Ninyi Watu Wote!

Katika nuru Yangu, watu wanaona nuru tena. Katika neno Langu, watu wanapata vitu vya raha. Nimekuja kutoka Mashariki nami Natoka huko. Wakati ambapo utukufu Wangu unang’aa, mataifa yote yanaangaziwa, vitu vyote vinaletwa katika nuru, hakuna kitu kinachobaki katika giza. Katika ufalme, maisha ya watu wa Mungu pamoja na Mungu ni ya furaha isiyolinganishwa. Maji yanacheza kwa ajili ya maisha ya watu yaliyobarikiwa, milima inafurahia utele Wangu pamoja na watu. Wanadamu wote wanajitahidi, wakifanya kazi kwa bidii, wakionyesha uaminifu wao katika ufalme Wangu. Katika ufalme, hakuna uasi tena, hakuna upinzani tena; mbingu na dunia vinategemeana, Mimi na mwanadamu tuko karibu nasi tunahisi kwa kina, kupitia furaha kuu za maisha, tukiegemeana…. Wakati huu, Naanza rasmi maisha ya mbinguni. Kuingilia kwa Shetani hakuko tena, na watu wanaingia katika pumziko. Kotekote katika ulimwengu, wateule Wangu wanaishi katika utukufu Wangu, wamebarikiwa kwa kiwango kisichonganishika, si kama watu wanaoishi kati ya watu, bali kama watu wanaoishi na Mungu. Kila mtu amepitia upotovu wa Shetani, ameonja uchungu na utamu wa maisha. Sasa akiishi katika nuru Yangu, mtu anawezaje kukosa kushangilia? Mtu anawezaje kuuacha tu wakati huu mzuri na kuuacha upite? Watu! Sasa imbeni nyimbo zilizo ndani ya mioyo yenu na mnichezee! Sasa inueni mioyo yenu ya kweli na kuipeana Kwangu! Sasa pigeni ngoma zenu na kunichezea! Naangaza furaha juu ya ulimwengu wote! Nawaonyesha watu uso Wangu wa utukufu! Nitanguruma! Nitaupita sana ulimwengu! Tayari Natawala kati ya watu! Nainuliwa na watu! Nachukuliwa katika mbingu za samawati na watu wanaenda na Mimi. Natembea kati ya watu na watu Wangu wananizunguka! Mioyo ya watu ni yenye furaha, nyimbo zao zatetemesha ulimwengu, Nikifanya upenyu katika mbingu! Ulimwengu haujafunikwa kwa ukungu tena; hakuna matope tena, hakuna mkusanyiko wa maji taka tena. Watu watakatifu wa ulimwengu! Chini ya ukaguzi Wangu uso wenu halisi unafichuliwa. Ninyi sio watu waliofunikwa na uchafu, bali watakatifu safi kama jiwe la thamani, wapendwa Wangu wote, wote wanaonifurahisha! Vitu vyote vinafufuka! Watakatifu wote wamerudi mbinguni wakinihudumia, wakiingia katika kumbatio Langu la joto, hawalii tena, hawana wasiwasi tena, wakijitoa Kwangu, wakirudi nyumbani Kwangu, na katika nchi yao watanipenda milele! Hawabadiliki! Huzuni uko wapi! Machozi yako wapi! Mwili uko wapi! Dunia haipo tena; mbingu ni za milele. Ninaonekana kwa watu wote, na watu wote wananisifu. Uzima huu, uzuri huu, tangu wakati wa zamani na hata milele, havitabadilika. Huu ndio uzima katika ufalme.

Iliyotangulia:Sura ya 25

Inayofuata:Sura ya 26

Maudhui Yanayohusiana

 • Sisitiza Uhalisi Zaidi

  Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu inayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu we…

 • Jinsi ya Kuingia Katika Hali Halisi

  Kadiri watu wanavyokubali maneno ya Mungu zaidi, ndivyo wanavyopata nuru zaidi, na ndivyo wanavyokuwa na njaa na kiu zaidi katika kufuatilia kwao ku…

 • Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

  Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo kwa njia inayo…

 • Kuhusu Desturi ya Sala

  Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Hapo awali sala zilikuwa za uzembe, huku mwanadamu akifanya …