Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?
Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushirikiane kuhusu mada ya kumfuata Mungu. Lakini, lazima Niwakumbushe wote wanaoyasoma maneno haya kwamba neno la Mungu huelekezwa kwa wale wanaomtambua na wale wanaomfuata Mungu, na sio kwa watu wote wa ulimwengu, wakiwemo wale wasiomtambua Mungu. Ikiwa unaamini kuwa Mungu Anazungumza na halaiki, ya kuwa Anaongelesha watu wote duniani, basi neno la Mungu halitakuwa la mabadiliko kwako. Kwa hivyo, unafaa uyaweke maneno yote karibu na moyo wako, na usijiweke nje ya wigo la maneno haya. Kwa lolote lile, tuzungumze juu ya mambo yanayofanyika katika nyumba yetu.
Mnafaa nyote kufahamu sasa maana kamili ya kumwamini Mungu. Maana ya imani katika Mungu Niliyozungumzia awali inahusiana na kuingia kwenu kwa hali dhahiri. Lakini leo hii si juu ya hayo. Leo hii Ningependa kuchambua umuhimu wa imani yako katika Mungu. Bila shaka, lengo la jambo hili ni kuwaelekeza kutoka kwenye mabaya; Nisipofanya hivyo, basi hamtawahi kuifahamu sura yako kamili na utakuwa ukijisifu kila mara kuhusu kujitolea kwako na uaminifu wako. Kwa maneno mengine, Nisipoangazia uovu uliomo ndani ya mioyo yenu, basi kila mmoja wenu atajitwika taji kichwani na kujipa utukufu wote. Asili zenu za majivuno na kiburi huwaelekeza kusaliti dhamiri zenu wenyewe, kuasi na kumpinga Kristo, na kufichua uovu wenu, hivyo basi kuleta kwenye mwangaza fikra zenu, mawazo, tamaa nyingi na macho yaliyojaa ulafi. Ilhali mnaendelea kukiri kwamba mtajitolea maisha yenu kwa ajili ya kazi ya Kristo, na mnakariri tena na tena mambo ya kweli yaliyosemwa na Kristo zamani zile. Hii ndiyo “imani” yenu. Hii ndiyo “imani yenu isiyokuwa na doa”. Kwa muda huu wote, Nimemweka mwanadamu katika nidhamu ya hali ya juu. Iwapo uaminifu wako unakuja na nia na masharti, basi ni heri Nisijihusishe na huo mnaoita uaminifu wenu hata kidogo, kwa maana Ninachukia wale hunidanganya kupitia kwa nia zao na kunanihadaa na masharti. Natamani tu mwanadamu awe mwaminifu kabisa Kwangu, na afanye mambo yote kwa ajili ya, na kudhibitisha neno hilo moja: imani. Ninachukizwa na matumizi yenu ya maneno matamu ili Unifurahishe Mimi. Kwa maana daima Mimi napenda mtende pia kwa ukweli mtupu na uwazi na hivyo Ningependa pia mfanye matendo yenu Kwangu kwa imani ya kweli. Inapofika katika swala la imani, watu wengi hufikiri kwamba wanamfuata Mungu kwa sababu wako na imani, la sivyo hawangevumilia mateso hayo. Basi Nakuuliza hivi: Ni kwa nini humheshimu Mungu ilhali unaamini kuwepo Kwake? Ni kwa nini, basi, haumchi Mungu moyoni mwako iwapo unaamini kuwa Mungu Yupo? Unakubali kuwa Kristo ni kupata mwili kwa Mungu, basi ni kwa nini uwe na dharau Kwake? Kwa nini unatenda bila heshima Kwake? Ni kwa nini unamhukumu wazi wazi? Ni kwa nini siku zote unachunguza Yeye anakoenda? Mbona usijisalimishe katika mipango Yake? Ni kwa nini hutendi kulingana na neno Lake? Ni kwa nini unamhadaa na kumpokonya matoleo Yake? Ni kwa nini unazungumza katika nafasi ya Kristo? Ni kwa nini unatoa hukumu ya kubaini iwapo kazi Yake na neno Lake ni ya kweli? Mbona unathubutu kumkufuru Yeye kisiri? Ni mambo haya na mengine ndiyo yanayounda imani yenu?
Kila sehemu ya usemi na tabia zenu hufichua dalili za kutoamini katika Kristo ulizobeba ndani yako. Nia na malengo yenu kwa yale mnayoyafanya yamejaa kutoamini; hata hiyo hisi itokayo kwa macho yenu imetiwa doa na dalili hizi. Kwa maneno mengine, kila mmoja wenu, katika kila dakika ya kila siku, amebeba vipengele vyenu vya kutoamini. Hii ina maana kuwa kila wakati mko katika hatari ya kumsaliti Kristo, kwa maana damu iliyo ndani ya mishipa yenu imechanganyika na kutomwamini Mungu Aliyepata mwili. Kwa hivyo, Ninasema kwamba nyayo mnazoziwacha katika njia ya imani katika Mungu si nyingi. Safari yenu katika njia ya kumwamini Mungu haina msingi mzuri, na badala yake mnafanya kazi bila ya kujali matokeo yake. Nyinyi huwa na shaka na neno la Kristo na huwezi kulitia katika matendo mara moja. Hii ndio sababu ya nyinyi kutokuwa na imani katika Kristo, na daima kuwa na fikira kumhusu Kristo ndio sababu nyingine ya nyinyi kutoamini Kristo. Kuwa na shaka kila mara kuhusu kazi ya Kristo, kuacha neno Lake kuangukia sikio lisilosikia, kuwa na maoni kwa kila kazi inayofanywa na Kristo na kutoifahamu vizuri kazi hiyo, kuwa na ugumu wa kutupilia mbali fikira zako hata baada ya nyinyi kupewa sababu za kufanya vile, na kadhalika; hizi zote ni dalili za kutoamini zilizochanganyika ndani ya mioyo yenu. Ingawa mnafuata kazi ya Kristo na kamwe hubaki nyuma, kuna uasi mwingi uliochanganyika ndani ya mioyo yenu. Uasi huu ni doa la uchafu katika imani yenu kwa Mungu. Pengine hamkubaliani na haya, lakini iwapo huwezi kutambua nia yako kutoka kwayo, basi wewe ndiwe utakayeangamia. Kwa maana Mungu hustawisha wale wanaomwamini kwa kweli pekee, wala sio wale walio na shaka na hasa wale wanaomfuata shingo upande licha ya kutowahi kuamini kuwa Yeye ni Mungu.
Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa wanaitwa wanaotafuta mamlaka. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.
Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa hukuwa na chaguo jingine. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.
Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo. Umeweza sasa kutambua kiasi cha kutoamini kilicho ndani yako? Na kiasi gani cha usaliti kwa Kristo? Kwa hivyo Nakuhimiza hivi; Kwa maana umeichagua njia ya ukweli, basi huna budi ila kujitolea na moyo wote; usiwe na kuchanganyikiwa au wa kusitasita. Unafaa kufahamu kuwa Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu, na wote wale waliojitolea na wanaoamini katika Mungu.
Kwa wakati huu, kuna kutoamini kwingi sana ndani yenu. Jaribu kuangalia kwa makini ndani yako na kwa hakika mtajionea jibu mwenyewe. Unapopata jibu halisi, basi utakubali kuwa wewe kweli si muumini wa Mungu, bali ni mdanganyifu, unayekufuru, unayemsaliti, na usiye mwaminifu kwa Mungu. Kisha utagundua kuwa Kristo si mwanadamu, ila ni Mungu. Siku hiyo itakapowadia, basi utamheshimu, utamcha na utampenda kwa dhati Kristo. Kwa sasa, imani yenu ni asilimia thelathini tu ya moyo wenu, ilhali asilimia sabini zimekumbwa na shaka. Tendo lolote likifanywa na sentensi yoyote ikitamkwa na Kristo vyaweza kusababisha muwe na fikira na maoni kumhusu Yeye. Fikira na maoni haya hutokana na kutokuwa na imani kabisa ndani Yake. Mnamtamani na kumcha tu Mungu msiyemwona aliye mbinguni lakini hauna haja na Kristo Anayeishi duniani. Hii pia si ni ukosefu wa imani? Mnamtamani tu Mungu Aliyefanya kazi kitambo kile lakini hutaki kukumbana na Kristo wa leo. Hizi ndizo huwa “imani” zilizochanganyika katika mioyo yenu isiyomwamini Kristo wa leo. Sikuchukulii kwa hali ya chini kwa maana ndani yako mna kutoamini kwingi, ndani yenu mna uchafu mwingi sana ambao lazima uchunguzwe kwa kina. Madoa na uchafu huu ni ishara kuwa huna imani hata kidogo; ni alama za ninyi kumkana Kristo na huonyesha kuwa nyinyi ni msaliti wa Kristo. Hiyo ni kama kitambaa kinachofunika ufahamu wenu wa Kristo, kizuizi cha nyinyi kupatwa na Kristo, kitu kinachowakinga kulingana na Kristo, na dhihirisho kuwa Kristo Hawatambui. Huu ndio wakati wa kuchunguza kila sehemu ya maisha yenu! Kufanya hivyo kutakufaidi kwa njia zote ambazo mnaweza kufikiria!