Sura ya 24 na 25

Bila kusoma kwa makini, haiwezekani kugundua kitu chochote katika matamko ya siku hizi mbili; kwa kweli, yangepaswa kunenwa kwa siku moja, lakini Mungu aliyagawanya kwa siku mbili. Hiyo ni kusema, matamko ya siku hizi mbili yanaunda moja kamili, lakini ili iwe rahisi kwa watu kuyakubali, Mungu aliyagawanya kwa siku mbili ili kuwapa watu nafasi ya kupumua. Hiyo ndiyo fikira ya Mungu kwa mwanadamu. Katika kazi yote ya Mungu, watu wote hutekeleza kazi zao na wajibu wao mahali pao wenyewe. Sio tu watu wenye roho ya malaika ambao hushirikiana; wale walio na roho ya pepo mbaya pia “hushirikiana,” kama vile roho zote za Shetani. Katika matamko ya Mungu huonekana mapenzi ya Mungu na matakwa Yake kwa mwanadamu. Maneno “Kuadibu kwangu kunawajia watu wote, lakini pia kunakaa mbali na watu wote. Maisha yote ya kila mtu yamejaa upendo na pia chuki Kwangu” yanaonyesha kwamba Mungu hutumia kuadibu ili kuwatisha watu wote, Akiwasababisha wapate ufahamu kumhusu Yeye. Kwa sababu ya upotovu wa Shetani na udhaifu wa malaika, Mungu hutumia maneno tu, na sio amri za utawala, kuwaadibu watu. Tangu wakati wa uumbaji hadi leo, hii imekuwa kanuni ya kazi ya Mungu kuhusu malaika na watu wote. Kwa sababu malaika ni wa Mungu, bila shaka siku moja watakuwa watu wa ufalme wa Mungu, nao watatunzwa na kulindwa na Mungu. Wengine wote, wakati huo, pia wataainishwa kulingana na aina, aina zote mbalimbali za pepo wabaya wa Shetani wataadibiwa, na wote ambao hawana mapepo wataongozwa na wana na watu wa Mungu. Huo ndio mpango wa Mungu. Hivyo, Mungu Alisema wakati mmoja “Je, wakati wa kufika kwa siku Yangu ni wakati wa kufa kwa mwanadamu kweli? Je, hakika Ningeweza kumwangamiza mwanadamu wakati ufalme Wangu utatengenezwa?” Ingawa haya ni maswali mawili rahisi, ni mipango ya Mungu kwa ajili ya hatima ya wanadamu wote. Mungu atakapofika ndio wakati ambao “watu katika ulimwengu wote watasulubiwa msalabani vichwa vikiangalia chini.” Hili ndilo lengo ambalo Mungu anaonekana kwa watu wote, Akitumia kuadibu ili kuwajulisha kuwepo kwa Mungu. Kwa kuwa wakati ambao Mungu anashuka duniani ni hatua ya mwisho, na wakati ambao nchi zilizo duniani ziko katika ghasia kubwa mno, hivyo Mungu anasema “Nikija chini duniani, giza limetanda na mwanadamu ‘amelala fofofo.’” Kwa hivyo, leo kuna watu wachache tu ambao wana uwezo wa kumjua Mungu mwenye mwili, takriban hakuna hata mmoja. Kwa kuwa sasa ni enzi ya mwisho, hakuna yeyote aliyewahi kumjua Mungu wa vitendo kwa kweli, na watu wana ufahamu wa juujuu tu kuhusu Mungu. Na ni kwa sababu ya hii ndio watu wanaishi kati ya usafishaji mchungu. Watu wanapoacha usafishaji ndipo pia wanapoanza kuadibiwa, ndio wakati ambapo Mungu anaonekana kwa watu wote ili waweze kumwona wenyewe. Kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, watu huingia katika maafa, nao hawawezi kujinasua—ambayo ni adhabu ya Mungu kwa joka kubwa jekundu, na amri Yake ya utawala. Wakati joto la majira ya kuchipua limekuja na maua kuchanua, wakati vyote chini ya mbingu ni kijani kibichi na vitu vyote duniani viko mahali pake, watu na vitu vyote vitaingia hatua kwa hatua katika kuadibu kwa Mungu, na wakati huo kazi yote ya Mungu duniani itaisha. Mungu hatafanya kazi tena au kuishi duniani, kwa maana kazi kubwa ya Mungu itakuwaimetimizwa. Je, watu hawawezi kuweka kando miili yao kwa muda huu mfupi? Mambo gani yanaweza kuunganisha upendo kati ya mwanadamu na Mungu? Ni nani anayeweza kutenganisha upendo kati ya mwanadamu na Mungu? Je, ni wazazi, waume, dada, wake, au usafishaji mchungu? Je, hisia za dhamiri zinaweza kufuta sura ya Mungu ndani ya mwanadamu? Je, kuwa na deni kwa watu na vitendo vyao baina yao kumesababishwa na wao wenyewe? Je, wanaweza kuponywa na mwanadamu? Ni nani anayeweza kujilinda? Watu wanaweza kujikimu? Ni nani wenye nguvu maishani? Ni nani anayeweza kuniacha na kuishi peke yake? Mara kwa mara, kwa nini Mungu anawataka watu wote watekeleze kazi ya kutafakari? Kwa nini Mungu anasema, “Ugumu wa nani umepangwa kwa mikono yao wenyewe?”

Kwa sasa, kuna usiku wa giza kotekote ulimwenguni, na watu hawajali nao ni wapumbavu, lakini akrabu za saa daima hupiga kuendelea mbele, dakika na sekunde hazisimami, na mizunguko ya dunia, jua, na mwezi huendelea kwa kasi zaidi. Katika hisia zao, watu wanaamini kwamba siku hiyo haiko mbali sana, kama kwamba siku yao ya mwisho ipo mbele ya macho yao. Watu hutayarisha kila kitu bila kukoma kwa ajili ya wakati wao wa kifo, ili kutimiza kusudi wakati wa kufa kwao; la sivyo, wangekuwa wameishi bure, na je, hilo sio la kujutia? Wakati Mungu anaangamiza ulimwengu, Anaanza na mabadiliko katika masuala ya ndani ya nchi, ambapo hutokea mapinduzi; hivyo, Mungu huhamasisha huduma ya watu kotekote ulimwenguni. Nchi ambamo joka kubwa jekundu hulala likiwa limejiviringisha ni eneo la maonyesho. Kwa sababu, ndani, imepasuka, mambo yake ya ndani yameingia katika machafuko, kila mtu anafanya kazi ya kujitetea, akijitayarisha kukimbilia mwezini—lakini ni jinsi gani wanaweza kuepuka utawala wa mkono wa Mungu? Kama Mungu alivyosema tu kwamba watu “watakunywa kutoka kwenye kikombe chao kichungu.” Wakati wa ugomvi wa ndani ndio hasa wakati Mungu anaondoka duniani; Mungu hataendelea kukaa katika nchi ya joka kubwa jekundu, na Atamaliza kazi Yake duniani mara moja. Inaweza kusemwa kuwa wakati hukimbia, na hakuna muda mwingi uliobaki. Kutokana na sauti ya maneno ya Mungu inaweza kuonekana kwamba tayari Mungu amenena kuhusu hatima ya wote kotekote ulimwenguni, kwamba Hana lolote la kusema kwa wakati uliosalia. Hilo ndilo Mungu anamfichulia mwanadamu. Ni kwa sababu ya lengo la Mungu kumuumba mwanadamu ndio Anasema “Machoni Pangu, mwanadamu ndiye mtawala wa vitu vyote. Nimempa mamlaka si haba, Nikimwezesha kusimamia vitu vyote duniani—nyasi iliyo juu ya milima, wanyama katika misitu, na samaki majini.” Mungu alipomuumba mwanadamu, Aliamua mbeleni kuwa mwanadamu angekuwa bwana wa vitu vyote—lakini mwanadamu alipotoshwa na Shetani, na hivyo hawezi kuishi jinsi ambavyo angependa. Hili limesababisha ulimwengu wa leo, ambamo watu hawatofautiani na wanyama, na milima imechanganyika na mito, na matokeo ni kwamba “Maisha yake yote ni yale ya maumivu makali, na kukimbia hapa na pale, na raha kuongezwa kwa utupu.” Kwa sababu hakuna maana kwa maisha ya mwanadamu, na kwa sababu hili halikuwa lengo la Mungu katika kumuumba mwanadamu, ulimwengu wote umevurugika. Wakati Mungu ataweka ulimwengu wote kwa utaratibu, watu wote wataanza rasmi kupitia maisha ya mwanadamu, na wakati huo tu ndipo maisha yao yataanza kuwa na maana. Watu wataanza kutumia mamlaka waliyopewa na Mungu, wataonekana rasmi mbele ya vitu vyote kama bwana wao, na watakubali uongozi wa Mungu duniani, na hawatamuasi Mungu tena bali watamtii Mungu. Watu wa leo, hata hivyo, wako mbali sana na hilo. Yote wafanyayo tu ni “kupata pesa kwa njia ya udanganyifu” kupitia kwa Mungu, na kwa hiyo Mungu anauliza msururu wa maswali kama vile “Je, kazi Ninayofanya kwa mwanadamu haina faida yoyote kwake?” Kama Mungu hakuuliza maswali haya, hakuna kile ambacho kingefanyika; lakini wakati Anauliza mambo kama hayo, watu wengine hawawezi kusimama imara, kwa sababu kuna kuwiwa katika dhamiri zao, na sio kwa ajili ya Mungu kabisa, bali kwao wenyewe. Mambo yote ni matupu: hivyo, watu hawa na “watu wa kila dini, nyanja ya jamii, taifa, na dhehebu wote wanajua utupu ulio duniani, na wote wananitafuta na kungoja kurejea Kwangu.” Watu wote wanatamani sana kurudi kwa Mungu ili Aweze kukomesha enzi ya kale ya utupu, lakini pia wanaogopa kuingia katika maafa. Ulimwengu mzima wa dini utabaki ukiwa mara moja, na kutotunzwa na wote; hawana ukweli, na watatambua kwamba imani yao kwa Mungu sio dhahiri nayo ni dhahania. Watu wa kila eneo la jamii pia watatawanyika, na kila taifa na dhehebu litaanza kuangukia msukosuko. Kwa kifupi, ukawaida wa mambo yote utatenganishwa, yote yatapoteza ukawaida wake, na kwa hiyo, pia, watu watafichua nyuso zao za kweli. Hivyo Mungu anasema, “Wakati mwingi sana Nimepaza sauti Nikimwita mwanadamu, lakini je, kuna yule ambaye amehisi huruma? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuishi katika ubinadamu? Mwanadamu anaweza kuishi katika mwili, lakini hana ubinadamu. Je, alizaliwa katika ufalme wa wanyama?” Mabadiliko pia yanatokea miongoni mwa wanadamu, na kwa sababu ya mabadiliko haya kila mmoja anaainishwa kulingana na aina. Hii ni kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na athari ambayo inapaswa kutimizwa kwa kazi ya siku za mwisho. Mungu anavyozidi kuzungumzia waziwazi kiini cha mwanadamu, hivyo inathibitishwa kuwa mwisho wa kazi Yake unakaribia, na zaidi ya hayo kuwa Mungu amejificha zaidi kutoka kwa watu, ambalo huwafanya wahisi kubabaika zaidi. Kadri watu wanavyozingatia mapenzi ya Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyozingatia kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa kiasi kidogo; hili huwazuia kutoingilia, na hivyo Mungu hufanya kazi ambayo Ananuia kuifanya wakati hakuna mtu anayezingatia. Hii ni kanuni moja ya kazi ya Mungu kotekote katika enzi. Kadri anavyozingatia udhaifu wa watu kwa kiasi kidogo, hivyo inaonyeshwa kuwa uungu wa Mungu ni wazi zaidi, na hivyo siku ya Mungu inakaribia.

Iliyotangulia: Sura ya 22 na 23

Inayofuata: Sura ya 26

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp