Sura ya 26

Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wametoweka kabisa. Kila mtu ana hisia ya kuogofya, na ingawa wote wanajitahidi sana, na wanataka kuridhisha malengo ya Mungu, wote wakitumia kila nguvu waliyo nayo kutimiza nia ya Mungu ili mapenzi ya Mungu yaweze kuendelea sawasawa, bila kizuizi, hisia kama hiyo kila mara huchanganyika na hisia ya kuogofya. Chukua matamko ya leo: Kama yangeenezwa kwa umma, yakatangazwa kwa ulimwengu wote, basi watu wote wangeinamishwa vichwa vyao na kulia, kwani katika maneno “Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!” wote wanaoelewa mambo ya kiroho wanaona kwamba hakuna mtu anayeweza kuhepa kuadibu kwa Mungu, kwamba wote watafuata aina yao wenyewe baada ya kupitia mateso ya kuadibu. Kwa kweli, hii ni hatua ya kazi ya Mungu, na hakuna mtu anayeweza kuibadilisha. Wakati Mungu aliumba ulimwengu, Alipowaongoza wanadamu, Alionyesha hekima na ajabu Yake, na Anapoikomesha enzi hii tu ndio watu wanaona haki Yake ya kweli, uadhama, ghadhabu, na kuadibu. Zaidi ya hayo, ni kwa njia ya kuadibu tu ndio wanaweza kuona haki, uadhama, na ghadhabu Yake; hii ni njia ambayo inapaswa kufuatwa, kama vile, katika siku za mwisho, kupata mwili kwa Mungu ni muhimu, na ni ya lazima. Baada ya kutangaza mwisho wa wanadamu wote, Mungu anamwonyesha mwanadamu kazi Anayoifanya leo. Kwa mfano, Mungu anasema, “Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha kuwepo kupitia kwa watu Wangu!” “Aa, Misri yenye chuki! … Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu?” Mungu kwa makusudi Anawaonyesha watu matunda yaliyopatikana na nchi mbili zilizo kinyume kutoka kwa mikono ya Mungu, kwa hali moja Akitaja Israeli, ambayo ni yakinifu, na kwa hali nyingine Akiashiria wateule wote wa Mungu—ambalo ni kusema, jinsi wateule wa Mungu wanavyobadilika jinsi Israeli inavyobadilika. Wakati Israeli imerejelea kabisa umbo lake la asili, wateule wote watafanywa wakamilifu baadaye—ambalo ni kusema, Israeli ni ishara ya maana ya wale ambao Mungu anawapenda. Misri, wakati huo huo, ni kukutana kwa wawakilishi wa wale ambao Mungu anawachukia. Inavyozidi kuoza, ndivyo wale wanaochukiwa na Mungu wanavyozidi kuwa wapotovu—na baadaye Babeli inaanguka. Hii inafanya tofauti ya wazi. Kwa kutangaza miisho ya Israeli na Misri, Mungu anafichua hatima ya watu wote; hivyo, Anapotaja Israeli, Mungu pia Anazungumza kuhusu Misri. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba siku ya uharibifu wa Misri ni tarehe ya maangamizo ya ulimwengu, tarehe ambayo Mungu anawaadibu watu wote. Hili litatokea hivi karibuni; liko karibu kufanikishwa na Mungu, na ni kitu ambacho hakionekani kabisa na jicho la mwanadamu, lakini pia ni cha lazima, na hakiwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Mungu anasema, “wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe wanadamu kwa urahisi kwa yote ambayo wametenda.” Kwa nini Mungu anazungumza kwa masharti haya kamili? Na kwa nini Yeye mwenyewe Amepata mwili katika taifa la joka kuu jekundu? Kutoka kwa maneno ya Mungu lengo Lake linaweza kuonekana: Hakuja kuwaokoa watu, au kuwaonyesha huruma, au kuwatunza, au kuwalinda—bali kuwaadibu wale wote wanaompinga Yeye. Kwa maana Mungu anasema, “Hakuna anayeweza kuhepa kuadibu Kwangu.” Mungu anaishi katika mwili, na, zaidi ya hayo, Yeye ni mtu wa kawaida—hata hivyo Hawasamehei watu kwa udhaifu wao kwa kutoweza kumjua Yeye kwa udhahania; badala yake, kwa sababu Yeye ni wa kawaida, Anawashutumu watu kwa dhambi zao zote, Anawafanya wale wote wanaouona mwili wake kuwa wale wanaoadibiwa, na hivyo wanakuwa sadaka kwa niaba ya wale wote ambao sio watu wa taifa la joka kuu jekundu. Lakini hii siyo mojawapo ya malengo ya msingi ya kupata mwili kwa Mungu. Mungu alipata mwili kimsingi ili Apigane vita, katika mwili, na joka kuu jekundu, na kuleta aibu kwalo kupitia vita. Kwa sababu nguvu kuu ya Mungu inadhihirishwa zaidi kwa kupambana na joka kuu jekundu katika mwili kuliko katika Roho, Mungu hupigana katika mwili ili kuonyesha matendo na kudura Yake. Kwa sababu ya kupata mwili kwa Mungu, watu wengi mno wameshutumiwa “bila hatia”, watu wengi mno wametupwa jehanamu, na kutupwa katika kuadibu, wakiteseka katika mwili. Hili ni dhihirisho la tabia ya haki ya Mungu, na bila kujali jinsi wale wanaompinga Mungu wanavyobadilika leo, tabia adilifu ya Mungu haitabadilika kamwe. Kwa kushutumiwa mara moja, watu wanashutumiwa milele, na wasiweze kamwe kuinuka tena. Tabia ya mwanadamu haiwezi kuwa kama ya Mungu. Kwa wale wanaompinga Mungu, watu huwa moto na baridi kwa zamu, wanayumbayumba kushoto na kulia, wanaenda juu na chini, hawawezi kubaki vilevile wakati wote, wakati mwingine wakichukiwa kabisa, wakati mwingine wakishikiliwa kwa karibu; hali za leo zimetokea kwa sababu watu hawajui kazi ya Mungu. Kwa nini Mungu anasema maneno kama vile, “Malaika ni, hata hivyo, malaika; Mungu, hata hivyo, ni Mungu; pepo ni, hata hivyo, pepo; Wadhalimu bado ni wadhalimu; na watakatifu bado ni watakatifu”? Je, huwezi kulielewa? Je, yawezekana kwamba Mungu amekumbuka visivyo? Hivyo, Mungu anasema, “kila mtu anatengwa kulingana na aina yake, na kutafuta njia bila kujua wanajipata wakirejea katika ngome za familia zao.” Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba leo, tayari Mungu ameainisha vitu vyote katika familia zao, ili usiwe tena “ulimwengu usio na mwisho,” na watu wasile tena kutoka kwenye chungu kimoja kikubwa, bali watekeleze kazi zao wenyewe nyumbani kwao, wakitekeleza wajibu wao wenyewe. Huu ulikuwa mpango wa asili wa Mungu wakati wa uumbaji wa ulimwengu; baada ya kuainishwa kulingana na aina, watu “wangekula chakula chao wenyewe”—Mungu angeanza hukumu. Kutokana na hilo, maneno haya yalitoka kinywani mwa Mungu: “Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu.” Hilo ndilo lengo halisi la kazi yote ya Mungu, na si vigumu kulielewa. Mungu atakamilisha kazi Yake—mtu angeweza kuizuia kazi Yake? Na Mungu angeweza kuchana agano lililowekwa kati Yake na mwanadamu? Ni nani anayeweza kubadilisha kile kinachofanyika na Roho wa Mungu? Angeweza kuwa mtu yeyote miongoni mwa wanadamu?

Zamani, watu walielewa kwamba kulikuwa na sheria kwa maneno ya Mungu: Mara tu Mungu aliponena, ukweli ulifanikishwa punde. Hakuna uongo katika hili. Kwa kuwa Mungu amesema Atawaadibu watu wote, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa Ametoa amri za utawala, inaweza kuonekana kwamba kazi ya Mungu imetekelezwa kwa kiwango fulani. Katiba iliyotolewa kwa watu wote hapo zamani ililenga maisha yao na mtazamo wao kwa Mungu. Haikufikia asili; haikusema kwamba ilitegemea majaliwa ya Mungu, bali kwa tabia ya mwanadamu wakati huo. Amri za utawala za leo ni za pekee, zinazungumzia jinsi “Binadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya.” Bila kusoma kwa makini, hakuna tatizo linaloweza kupatikana katika hili. Kwa sababu ni katika enzi ya mwisho tu ndio Mungu anafanya vitu vyote vifuate aina yao wenyewe, baada ya kusoma hili watu wengi hubaki wamekanganywa na kuchanganyikiwa, bado ni vuguvugu, hawaoni umuhimu wa nyakati, na hivyo hawachukulii hili kama onyo. Kwa nini, kwa wakati huu, amri za utawala wa Mungu—ambazo zinatangazwa kwa ulimwengu wote—zinaonyeshwa kwa mwanadamu? Je, hawa watu wanawakilisha wale wote walio kotekote ulimwenguni? Yawezekana kwamba, baadaye, zaidi, Mungu anaongeza huruma kwa watu hawa? Je, watu hawa wamekuwa na vichwa viwili? Wakati Mungu anawaadibu watu wa ulimwengu wote, wakati maafa ya kila aina yanapofika, kutokana na maafa haya, mabadiliko yatatokea kwenye jua na mwezi, na wakati misiba hii itakapomalizika, jua na mwezi vitakuwa vimebadilishwa—na huu unaitwa mpito. Inatosha kusema, maafa ya siku zijazo yatakuwa ya kusikitisha. Usiku unaweza kuchukua nafasi ya mchana, jua linaweza kutoonekana kwa mwaka, kunaweza kuwa na miezi kadhaa ya joto la kuunguza, mwezi unaopotea unaweza kumkabili wanadamu daima, kunaweza kuonekana hali ya ajabu ya jua na mwezi kuchomoza pamoja, n.k. Kufuatia mabadiliko kadhaa ya mafuatano, hatimaye, baada ya kupita kwa muda, yatafanywa upya. Mungu huzingatia sana mipango ya wale ambao ni wa shetani. Hivyo, Anasema kwa makusudi, “Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa shetani wataangamizwa.” Wakati “watu” hawa bado hawajaonyesha tabia zao halisi, daima Mungu hutumia huduma zao; kutokana na hilo, Hazingatii matendo yao, Yeye hawapatii “thawabu” wanapofanya mema, wala Hapunguzi “mishahara” wanapofanya vibaya. Kwa hivyo, Yeye huwapuuza, Hawathamini. Habadiliki ghafla kwa sababu ya “wema” wao, kwani haijalishi wakati au mahali, asili ya mwanadamu haibadiliki, kama tu agano lililoanzishwa kati ya Mungu na mwanadamu, kama vile, mwanadamu asemavyo, “hakutakuwa na mabadiliko hata kama bahari zitakauka na miamba ivunjike.” Hivyo, Mungu huwaainisha tu watu hao na Hawasikilizi kwa urahisi. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, shetani hajawahi kujistahi vizuri. Kila mara, yeye amepinga, amechafua, na kutokubali. Mungu anapotenda au kunena, daima yeye hujaribu kushiriki—lakini Mungu hamtambui. Kwa kumtaja shetani, ghadhabu ya Mungu inabubujika, bila kuzuilika; kwa sababu yeye si kitu kimoja na Roho, hakuna uhusiano, bali umbali na utengano tu. Kufuatia ufichuzi wa mihuri saba, hali ya dunia inazidi kuwa matatani, vitu vyote “vinaendelea bega kwa bega na mihuri saba,” bila kubaki nyuma hata kidogo. Kotekote katika maneno ya Mungu, Mungu anawatazama watu kama walioduwazwa, lakini hawajaamka kamwe. Ili kufikia kiwango cha juu, ili kuonyesha nguvu za watu wote, na zaidi ya hayo, ili kuihitimisha kazi ya Mungu katika kilele chake, Mungu anawauliza watu msururu wa maswali, kama kwamba Anapanua matumbo yao, na hivyo Anawajaza tena watu wote. Kwa sababu watu hawa hawana kimo halisi, kulingana na mazingira halisi, wale ambao wanajazwa ni bidhaa ambazo zinazofikia kiwango, na wale ambao hawajajazwa ni takataka isiyofaa. Haya ni matakwa ya Mungu kwa mwanadamu, na lengo la njia ambayo kwayo Anaizungumzia. Hasa, wakati Mungu anasema “Je, yawezekana kwamba Mimi, Nikiwa duniani, Siko sawa na Mimi niliye mbinguni? Je, yawezekana kwamba Mimi, Ninapokuwa mbinguni, Siwezi kushuka chini duniani? Je, yawezekana kwamba Mimi, Nikiwa duniani, Sistahili kustahimili hadi mbinguni?” maswali haya huendelea kuwafanya watu wamjue Mungu hata zaidi. Kutoka kwa maneno ya Mungu, makusudi ya dharura ya Mungu inaonekana; watu hawawezi kuyafikia, na Mungu Anaongeza masharti tena na tena, hivyo Akiwakumbusha watu wote wamjue Mungu wa mbinguni Aliye duniani, na kumjua Mungu aliye mbinguni lakini Anaishi duniani.

Kutokana na maneno ya Mungu hali za mwanadamu zinaweza kuonekana: “Wanadamu wote wanaweka bidii kwa maneno Yangu, wakifanya uchunguzi wao wenyewe kuhusu sura Yangu ya nje, lakini wote wanashindwa, bila matokeo yoyote ya kuonyesha, badala yake, wanaangushwa na maneno Yangu na hawawezi kuthubutu kusimama tena.” Nani anaweza kuelewa huzuni ya Mungu? Nani anaweza kuufariji moyo wa Mungu? Ni nani anayeupendeza moyo wa Mungu katika kile ambacho Mungu anataka? Wakati watu hawatoi matokeo, wanajikana na kwa kweli wako chini ya mipango ya Mungu. Hatua kwa hatua, wanapoionyesha mioyo yao ya kweli, kila mmoja hufuata aina yake mwenyewe, na hivyo inaonekana kwamba asili ya malaika ni utii mtakatifu kwa Mungu. Na kwa hiyo, Mungu anasema, “Binadamu wanafunuliwa katika hali yao halisi.” Kazi ya Mungu inapofikia hatua hii, kazi yote ya Mungu itakuwa imekamilika. Mungu anaonekana kutosema chochote kuhusu Yeye kuwa mfano wa wanawe na watu wake, badala yake Akilenga kuwafanya watu wote kuonyesha umbo lao la asili. Je, unaelewa maana halisi ya maneno haya?

Iliyotangulia: Sura ya 24 na 25

Inayofuata: Sura ya 27

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp