Sura ya 15

Tofauti kubwa zaidi kati ya Mungu na mwanadamu ni kwamba kila mara maneno ya Mungu hugonga ndipo, na hakuna kilichofichwa. Kwa hiyo hali hii ya tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika maneno ya kwanza ya leo. Kipengele kimoja ni kuwa yanaonyesha tabia halisi ya mwanadamu, na kipengele kingine ni kuwa yanafichua wazi tabia ya Mungu. Hizi ni asili kadhaa za jinsi maneno ya Mungu yanaweza kutimiza matokeo. Hata hivyo, watu hawalielewi hili, kila mara wao huja kujijua tu katika maneno ya Mungu lakini “hawajamchangua” Mungu. Ni kana kwamba wanaogopa sana kumkosea, kwamba Mungu atawaua kwa “umakini” wao. Kwa kweli, watu wengi zaidi wanapokula na kunywa neno la Mungu, ni kutokana na hali hasi, sio hali ya kujenga. Ingeweza kusemwa kwamba watu wameanza sasa “kulenga unyenyekevu na utii” chini ya uongozi wa maneno Yake. Inaweza kuonekana kutoka kwa jambo hili kwamba watu wameanza kuvuka mipaka, kutoka kwa kutozingatia maneno Yake na kuelekea kwa kuyazingatia maneno Yake kupita kiasi. Lakini kamwe hakujakuwa na mtu ambaye ameingia ndani kutokana na hali ya kujenga, na kamwe hakujakuwa na mtu ambaye ameelewa kweli lengo la Mungu katika kumtaka mwanadamu azingatie maneno Yake. Inajulikana kutokana na kile asemacho Mungu kwamba Hahitaji kupitia mwenyewe maisha ya kanisa ili kuweza kuelewa hali halisi za watu wote kanisani, sawasawa na bila kosa. Kwa kuwa mbinu mpya imeingiwa hivi karibuni, watu wote bado hawajaacha misingi yao hasi; harufu ya maiti bado inapeperuka kotekote kanisani. Ni kana kwamba watu wamekunywa dawa hivi karibuni na bado wametunduwaa, na bado hawajapata fahamu kwa ukamilifu. Ni kana kwamba bado wanatishwa na kifo, kiasi kwamba bado wako katikati ya hofu yao kuu na hawawezi kujifanyia miujiza. “Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu”: Kauli hii bado inasemwa kwa kutegemea mbinu ya ujenzi wa kanisa. Kanisani, ingawa kila mtu huzingatia maneno ya Mungu, bado asili zao zimetopea sana na hawawezi kujinasua. Hii ndio maana Mungu hutumia mbinu ya kunena kutoka kwa awamu ya mwisho kuwahukumu watu ili wakubali kugonga kwa maneno ya Mungu huku wakiwa wanajipenda sana. Hata ingawa watu walipitia miezi mitano ya usafishaji katika kuzimu, hali yao halisi bado ni ile ya kutomjua Mungu. Bado wao ni wapotovu—wameongeza tu kwa kiasi fulani tahadhari yao kumwelekea Mungu. Ni katika hatua hii tu ndiyo watu huanza kuingia katika njia ya kuyajua maneno ya Mungu, kwa hiyo wakati wanafanya uwiano na kiini cha maneno ya Mungu, si vigumu kuona kwamba hatua ya awali ya kazi iliandaa njia kwa ajili ya leo, na ni leo tu ndio kila kitu kinafanywa kuwa kawaida. Udhaifu mkuu wa watu ni kupenda kutenganisha Roho wa Mungu kutoka kwa nafsi Yake ya mwili ili waweze kupata uhuru wao wenyewe, ili waepuke kuzuiwa kila mara. Hii ndiyo maana Mungu humfafanua mwanadamu kama ndege wadogo wanaorukaruka kwa furaha mahali pote. Hii ndiyo hali halisi ya wanadamu wote. Hili ndilo hufanya kuwapindua watu wote kuwa rahisi sana, linalofanya kupotea kwao kuwa rahisi sana. Inaweza kuonekana kutoka kwa hili kwamba kazi ambayo Shetani hufanya ndani ya wanadamu ni hii tu. Kadri Shetani anavyofanya hili ndani ya watu, ndivyo masharti ya Mungu kwao huzidi kuwa makali. Anawahitaji watu kuzingatia maneno Yake na Shetani hufanya kila juhudi kuliharibu. Mungu, hata hivyo, Amewakumbusha watu kila mara wazingatie maneno Yake; hiki ni kilele cha vita vya ulimwengu wa kiroho. Inaweza kusemwa hivi: Kile ambacho Mungu anataka kufanya ndani ya mwanadamu ndicho hasa Shetani anataka kuharibu, na kile ambacho Shetani anataka kuharibu kinaonyeshwa kupitia kwa mwanadamu bila kufichwa kabisa. Kile ambacho Mungu hufanya ndani ya watu kina madhihirisho wazi—hali zao zinazidi kuwa bora. Uharibifu wa Shetani ndani ya wanadamu unawakilishwa pia kwa dhahiri—wanapotoshwa zaidi na zaidi na hali zao zinazama zaidi na zaidi. Kama ni kubaya vya kutosha, wangeweza kutekwa na Shetani. Hii ndiyo hali halisi ya kanisa ambalo limewasilishwa katika maneno ya Mungu, na pia ni hali halisi ya ulimwengu wa kiroho. Ni akisi ya nguvu za ulimwengu wa kiroho. Kama watu hawana imani ya kushirikiana na Mungu, wako katika hatari ya kutekwa na Shetani. Huu ni ukweli. Kama mtu anaweza kweli kuutoa moyo wake kwa Mungu kwa ukamilifu ili Aumiliki, hiyo ni kama vile tu Mungu amesema: “mbele Yangu, anaonekana kuwa amekaa katika kumbatio Langu, akionja joto la kumbatio Langu.” Hili linaonyesha kwamba matakwa ya Mungu kwa wanadamu si ya juu—Anawataka tu wainuke na kushirikiana Naye. Je, hili si jambo rahisi na la furaha? Na kitu hiki kimoja tu kimewatatiza mashujaa wote? Ni kama kwamba majenerali wa vita wanalazimishwa kuketi kila mahali katika xiu lou[a] wakishona tarizi—“mashujaa” hawa wamesimamishwa kabisa na tatizo hilo na hawajui wanachopaswa kufanya.

Katika hali yoyote ile matakwa ya Mungu kwa wanadamu ni makuu zaidi, ina maana kwamba mashambulio ya Shetani yatakuwa makubwa zaidi katika hali hiyo, na hali za watu wote hufichuliwa kupitia hili. “…nani kati yenu, mlio mbele Yangu, angekuwa mweupe kama theluji inayoendeshwa, bila doa kama jiwe safi la thamani?” Watu wote bado wanamdanganya na kumficha Mungu kitu fulani; bado wanatekeleza biashara yao wenyewe ya hila. Hawajamkabidhi Mungu mioyo yao ili kumridhisha, lakini wanataka kupata thawabu Zake kupitia kwa shauku yao wenyewe. Watu wanapokula chakula kitamu, wanamtaka Mungu asimame kando, Asiwe na uwezo wa kujilinda dhidi yao. Watu wanapokuwa na nguo nzuri, wao husimama tu mbele ya kioo wakifurahia uzuri wao, na hawamridhishi Mungu kutoka kwa kina cha mioyo yao. Wanapokuwa na cheo, wanapokuwa na raha za anasa, wao huketi tu katika hali yao na kuanza kufurahia, lakini hawajinyenyekezi kwa sababu ya kupandishwa cheo na Mungu. Badala yake, wanasimama katika vyeo vyao vya juu wakitumia maneno ya kifahari na kutozingatia kuwepo kwa Mungu, wala hawafuatilii kuijua thamani ya Mungu. Wakati ambapo watu wana sanamu ndani ya mioyo yao au wakati ambapo mioyo yao imetekwa na mtu mwingine, basi tayari walikuwa wamekana kuwepo kwa Mungu, na ni kana kwamba Mungu ni mdukizi katika mioyo yao. Wao huogopa sana kwamba Mungu atauiba upendo wa watu wengine kwao na watahisi upweke. Kulingana na kusudi la Mungu, hakungekuwa na kitu chochote duniani ambacho kingewasababisha watu kumpuuza Mungu; hata upendo kati ya watu haungeweza kumwondoa Mungu kutoka kwa “upendo” huo. Vitu vyote vya dunia ni vitupu, hata hisia kati ya watu zisizoweza kuonekana wala kugusika. Bila kuweko kwa Mungu, viumbe wote wangekuwa bure. Duniani, watu wote wana vitu vyao wavipendavyo, lakini hakujawahi kuwa na mtu ambaye amefanya maneno ya Mungu kuwa kile kitu akipendacho. Hili huamua kiwango cha ufahamu wa watu kuhusu maneno ya Mungu. Ingawa maneno Yake ni makali, watu hawaumii kwa sababu hawayazingatii maneno Yake kwa kweli, badala yake wanayatazama kama maua. Hawayachukulii kuwa matunda ya wao kuonja, kwa hiyo hawajui kiini cha maneno ya Mungu. “Kama binadamu wangeweza kufahamu kwa kweli ukali wa upanga wangu, wangetoroka kwa uoga kama vile panya wanavyokimbilia mashimo yao.” Nikizungumza kwa kutegemea hali ya mtu wa kawaida, baada ya kuyasoma maneno ya Mungu wangetiwa bumbuazi, wajawe na aibu, na wasiweze kuwatazama wengine. Lakini sasa watu ni kinyume tu—wao hutumia maneno ya Mungu kama silaha ya kuwapiga wengine kumbo. Kweli hawana aibu!

Tumeletwa katika hali hii pamoja na maneno ya Mungu: “Ndani ya ufalme, matamshi hayatoki tu kwenye kinywa Changu, lakini miguu Yangu inakanyaga kila mahali juu ya ardhi kwa utaratibu.” Katika vita kati ya Mungu na Shetani, Mungu anashinda kila hatua ya njia. Anaipanua kazi Yake kwa kiwango kikubwa kotekote katika ulimwengu mzima, na ingeweza kusemwa kwamba nyayo Zake ziko kila mahali, na dalili za ushindi Wake zinaweza kuonekana kila mahali. Katika hila za Shetani, anataka kuharibu usimamizi wa Mungu kwa kuyatenganisha mataifa, lakini Mungu ametumia hili kuupanga tena ulimwengu mzima, wala sio kuuangamiza. Mungu hufanya kitu kipya kila siku lakini watu hawajakifahamu. Watu hawazingatii nguvu za ulimwengu wa kiroho, kwa hiyo hawawezi kuiona kazi mpya ya Mungu. “Ndani ya ulimwengu, kila kitu kinakuwa kipya katika mng’ao wa utukufu Wangu, kikiwasilisha kipengele chenye upendo kinachochangamsha akili na kuinua roho, kana kwamba sasa kiko katika mbingu zaidi ya mbingu, kama inavyoonekana katika mawazo ya binadamu, ambayo hayajachafuliwa na Shetani, ambayo hayajapata mashambulizi ya adui kutoka nje.” Hili linatabiri mandhari ya furaha ya ufalme wa Kristo duniani, na pia linatanguliza hali ya mbingu ya tatu kwa wanadamu: Kuna uwepo tu wa vitu vitakatifu ambavyo ni vya Mungu bila uvamizi wowote wa nguvu za Shetani. Lakini kilicho muhimu zaidi ni kuwaruhusu watu kuona hali za kazi iliyo duniani ya Mungu Mwenyewe. Mbingu ni mbingu mpya, na kwa ajili ya hilo dunia pia imefanywa upya tena. Kwa kuwa ni maisha chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, watu wote wana furaha kupita kiasi. Katika ufahamu wa watu, Shetani ni “mfungwa” wa wanadamu na hawana haya wala woga kwa ajili ya kuweko kwake. Kwa sababu ya maagizo na uongozi wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu, hila zote za Shetani zimeambulia patupu, ambalo hata linathibitisha kwamba yeye hayuko tena, kwamba ameondolewa kabisa na kazi ya Mungu. Hiyo ndiyo maana husemwa “... anaishi katika mbingu iliyo juu zaidi ya mbingu.” Kile ambacho Mungu alisema: “Hakuna usumbufu ambao umewahi kutokea, wala umoja wa ulimwengu haujapata kuvunjwa,” kilikuwa kinahusu hali ya ulimwengu wa kiroho. Ni thibitisho ambalo kwalo Mungu hutangaza ushindi kwa Shetani, nayo ni ishara ya ushindi wa mwisho wa Mungu. Hakuna mwanadamu anayeweza kubadili mawazo ya Mungu, na hakuna anayeweza kuyajua. Ingawa watu wameyasoma maneno ya Mungu na wameyachunguza kwa makini, lolote litokealo, hawawezi kusema kiini chake ni nini. Kwa mfano, Mungu alisema: “Mimi Naruka juu ya nyota, na wakati jua linachomoza mionzi yake, Ninalizuia joto la miale hiyo, Nikituma mabonge ya chembe za theluji kama manyoya ya bata yakianguka chini kutoka katika mikono Yangu. Lakini Nikibadili mawazo Yangu, theluji yote inayeyuka na kuwa mto. Kwa muda mfupi, majira ya kuchipua yameibuka kila mahali chini ya anga, na zamaradi ya kijani inageuza mazingira yote juu ya nchi.” Ingawa watu wanaweza kuwaza maneno haya ndani ya akili zao, kusudi la Mungu si rahisi hivyo. Wakati ambapo kila mtu chini ya mbingu ametunduwaa, Mungu hutamka sauti ya wokovu, Akizindua mioyo ya watu. Lakini kwa kuwa kila aina ya maafa yanatokea, wanahisi ukiwa wa ulimwengu kwa hiyo wote wanatafuta kifo na wako katika mapango baridi, yenye barafu. Wanagandishwa na baridi ya dhoruba kubwa za theluji kiasi kwamba hawawezi kuendelea kuishi kwa sababu hakuna joto duniani. Ni kwa sababu ya upotovu wa watu ndio sababu watu wanauana kwa kikatili zaidi na zaidi. Na kanisani, wengi wa watu watamezwa na joka kubwa jekundu kwa bwia moja. Hata hivyo, majaribio yote yakishapita, vurugu za Shetani zitaondolewa. Ulimwengu wote, katikati ya mgeuzo, utapenyezwa na majira ya kuchipua na joto litaufunika ulimwengu. Ulimwengu utajaa nguvu. Hizi zote ni hatua za mpango wote wa usimamizi. Umuhimu wa “usiku” ambao Mungu alizungumzia unahusu wakati ambapo wazimu wa Shetani unafikia kilele chake, ambao utakuwa wakati wa usiku. Je, hiyo si hali ya sasa? Ingawa watu wote wanaendelea kuishi chini ya uongozi wa nuru ya Mungu, wanapitia kuteseka kwa giza la usiku. Wataishi milele katikati ya usiku wa giza iwapo hawawezi kuponyoka kutoka kwa minyororo ya Shetani. Kisha tazama nchi za dunia: Kwa sababu ya hatua za kazi ya Mungu, nchi za dunia “zinakimbia huku na huko,” na zote zinatafuta hatima yao wenyewe ya kufaa. Kwa kuwa siku ya Mungu haijawadia, duniani yote bado yako katika hali ya ghasia ya giza. Wakati ambapo Mungu ataonekana wazi kwa ulimwengu mzima, utukufu Wake utajaa juu ya Mlima Zayuni na vitu vyote vitakuwa vizuri na nadhifu chini ya mpango wa mikono Yake. Maneno ya Mungu hayazungumzii tu leo bali pia hutabiri kesho. Leo ni msingi wa kesho, kwa hiyo watu walio katika hali hii ya leo hawawezi kufahamu kabisa maneno ya Mungu. Ni baada tu ya maneno Yake kutimizwa kwa ukamilifu ndio wataweza kuyafahamu kwa ukamilifu.

Roho wa Mungu huijaza kabisa nafasi yote katika ulimwengu lakini Yeye pia hufanya kazi ndani ya watu wote. Hivi, katika mioyo ya watu ni kana kwamba umbo la Mungu liko kila mahali, na kila mahali pana kazi ya Roho Wake. Kwa kweli, kuonekana kwa Mungu katika mwili ni kuishinda mifano hii ya Shetani na mwishowe kuwapata. Lakini huku Akifanya kazi katika mwili, Roho pia anashirikiana na mwili ili kuwageuza watu hawa. Inaweza kusemwa kwamba matendo ya Mungu hufikia kotekote katika ulimwengu wote na kwamba Roho Wake huujaza ulimwengu wote, lakini kwa ajili ya hatua za kazi Yake, wale ambao hufanya maovu hawajaadhibiwa, huku wale ambao hufanya mema hawajapewa thawabu. Kwa hiyo, matendo Yake hayajathaminiwa na watu wote walio duniani. Mungu yuko juu na ndani ya vitu vyote, na hata zaidi, Yuko miongoni mwa watu wote. Hili linatosha kuonyesha kuweko halisi kwa Mungu. Kwa kuwa Hajaonekana wazi kwa wanadamu, watu wamekuza uongo kama vile: “Kulingana na binadamu, Naonekana kuwa na maisha halisi, na hata hivyo Naonekana pia kutokuwa na nafsi.” Mpaka sasa, kati ya wale wote wanaomwamini Mungu, hakuna walio na hakika kabisa, asilimia mia moja kwamba Mungu anaishi kweli. Wote ni sehemu tatu shaka na sehemu mbili imani. Hii ndiyo hali halisi kwa wanadamu. Watu wote sasa wako katika hali ifuatayo: Wanaamini kwamba kuna Mungu, lakini hawajamwona. Au, hawaamini kwamba kuna Mungu, lakini kuna matatizo mengi ambayo hayawezi kutatuliwa na wanadamu. Inaonekana kila mara huwa kuna kitu fulani kinachowatega wasichoweza kukitoroka. Ingawa wanamwamini Mungu, inaonekana kwamba kila mara wao huhisi kutokuwa dhahiri kwa kiasi fulani. Lakini wasipoamini, wangeogopa kutofanikiwa kama ni kweli. Hii ni hisia yao kinzani.

“Kwa ajili ya jina Langu, kwa ajili ya Roho Wangu, kwa ajili ya mpango Wangu mzima wa usimamizi—nani ambaye anaweza kutoa nguvu zake zote katika mwili wake?” Na Akasema pia: “Leo, wakati ufalme uko katika ulimwengu wa watu, ndio wakati ambao Nimekuja binafsi katika ulimwengu wa wanadamu. Yupo ambaye angeweza, kwa ujasiri, kwenda katika uwanja wa vita kwa niaba Yangu?” Lengo la maneno ya Mungu ni hili: Isingekuwa Mungu katika mwili kufanya kazi Yake takatifu moja kwa moja, au isingekuwa Mungu mwenye mwili Aliyefanya kazi kupitia kwa wahubiri, basi Mungu hangeweza kamwe kulishinda joka kubwa jekundu, na Hangeweza kutawala kama Mfalme miongoni mwa wanadamu. Wanadamu hawangeweza kumjua Mungu Mwenyewe kwa uhalisi, kwa hiyo Shetani ndiye angekuwa bado anatawala. Hivyo, hii hatua ya kazi lazima ifanywe binafsi kupitia kwa mwili wa Mungu. Kama mwili ungebadilishwa basi hatua hii ya mpango haingeweza kumalizika kamwe kwa sababu umuhimu na kiini cha mwili si sawa. Watu wanaweza tu kuelewa maana halisi ya maneno haya kwa kuwa Mungu huelewa kiini. Mungu alisema: “Lakini, hatimaye, hakuna yeyote ambaye anaelewa kama hii ni kazi ya Roho, au ni kutokana na mwili. Hili jambo moja pekee linatosha kumfanya mwanadamu kupitia mwendo wa maisha kwa undani.” Watu wamepotoshwa na Shetani siku zote kwa miaka mingi, na walipoteza utambuzi wa masuala ya kiroho zamani sana. Kwa sababu hii sentensi moja tu ya maneno ya Mungu yanawapendeza watu. Kwa sababu ya umbali ulioko kati ya Roho na pepo, wale wote ambao wanamwamini Mungu wana hali ya kumtamani, na wote wako radhi kuwa karibu zaidi na kumweleza mambo yanayowahangaisha, lakini hawathubutu kuwasiliana na Yeye, na wao hubaki tu wakiwa na hofu. Hii ndiyo nguvu ya mvuto wa Roho. Kwa kuwa Mungu ni Mungu wa kupendwa na watu, na ndani Yake kuna vitu vingi sana vya wao kupenda, watu wote wanampenda na wote wanataka kuwa na imani Kwake. Kwa kweli, kila mtu ana moyo wa kumpenda Mungu, ni vurugu ya Shetani tu ndiyo imewafanya watu wasiosikia, wajinga, wa kusikitisha wasiweze kumjua Mungu. Hii ndiyo maana Mungu alieleza maono yake kuhusu hisia halisi za wanadamu kumwelekea Mungu: “Mwanadamu hajawahi kunichukia katika undani wa moyo wake kabisa; badala yake, yeye huambatana na Mimi katika kina cha roho yake. … Ukweli Wangu humfanya mwanadamu asijue la kusema, aduwae na kushtuka, na bado yeye yuko tayari kukubali hayo yote.” Hii ni hali halisi iliyo ndani kabisa mwa mioyo ya wale wanaomwamini Mungu. Watu wanapomjua Mungu kweli kwa kawaida watakuwa na mtazamo tofauti kumwelekea, na wataweza kutamka sifa kutoka ndani ya mioyo yao kwa sababu ya wajibu wa roho. Mungu yuko ndani kabisa mwa roho za watu wote, lakini kwa sababu ya upotovu wa Shetani wamedhani Mungu ni Shetani. Leo Mungu Anafanya kazi kutokana na hii hali hasa, na hili limekuwa lengo la vita vya ulimwengu wa kiroho kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Tanbihi:

a. Xiu lou palikuwa mahali ambapo palitumiwa na wanawake hasa kushona tarizi katika Uchina ya kale.

Iliyotangulia: Sura ya 14

Inayofuata: Sura ya 16

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Njia … (1)

Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi atakavyoenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa...

Fumbo la Kupata Mwili (2)

Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini...

Sura ya 35

Ngurumo saba zinatoka katika kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinazipindua mbingu na dunia, na zinaenea kote angani! Sauti hiyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki