Sura ya 16
Kwa watu, Mungu ni mkuu mno, mwenye utele mno, wa ajabu mno, Asiyeeleweka mno; machoni pao, maneno ya Mungu hupaa juu, na huonekana kama kazi bora sana ya ulimwengu. Lakini kwa vile watu wana kasoro nyingi sana, na akili zao ni za kawaida sana, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa uwezo wao wa kukubali ni haba mno, bila kujali vile Mungu hunena maneno Yake kwa dhahiri, wanabaki palepale bila kutikisika, kana kwamba wana ugonjwa wa akili. Wanapokuwa na njaa, hawaelewi kwamba lazima wale, wanapokuwa na kiu, hawaelewi kwamba lazima wanywe maji; wanaendelea tu kupaaza sauti na kupiga yowe, kana kwamba kuna dhiki isiyoelezeka katika kina cha roho zao, lakini hawawezi kuzungumza kuihusu. Mungu alipowaumba wanadamu, kusudi Lake lilikuwa mwanadamu aishi katika ubinadamu wa kawaida na akubali maneno ya Mungu kulingana na silika yake. Lakini kwa kuwa, mwanzoni kabisa, mwanadamu alishindwa na majaribu ya Shetani, leo anabakia asiyeweza kujinasua, na bado hawezi kutambua hila za udanganyifu ambazo zimetekelezwa na Shetani kwa maelfu ya miaka, zaidi ya hayo anakosa akili ya kuyajua maneno ya Mungu kwa ukamilifu—haya yote yamesababisha hali ya sasa. Kama yalivyo mambo leo, watu bado wanaishi katika hatari ya majaribu ya Shetani, na hivyo wanabaki wasioweza kufahamu kabisa maneno ya Mungu. Katika tabia za watu wa kawaida hakuna uhalifu au udanganyifu, watu wana uhusiano wa kawaida kati yao, hawafanyi mambo pekee yao, na maisha yao si duni wala ya kufifia. Kwa hiyo, vilevile, Mungu huinuliwa miongoni mwa wote, maneno Yake hupenya miongoni mwa wanadamu, watu huishi katika amani kati yao na chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, dunia imejaa upatanifu, bila kuingilia kwa Shetani, na utukufu wa Mungu huwa na umuhimu mkuu sana miongoni mwa wanadamu. Watu kama hao ni kama malaika: watakatifu, wa kusisimua, wasiolalamika kamwe kuhusu Mungu, na hutoa juhudi zao zote kwa utukufu wa Mungu duniani pekee. Sasa ni wakati wa usiku wa giza, wote wanapapasa huku na huko na kutafuta, usiku wa giza kuu unawafanya wawe na woga, na hawana budi ila kutetemeka; wakisikiliza kwa makini, ngurumo za dhoruba baada ya dhoruba za upepo wa kaskazimagharibi unaonekana kuandamana na mamia ya kuomboleza ya mwanadamu. Watu huhuzunika na kulia kwa ajili ya majaliwa yao. Ni kwa nini wao husoma maneno ya Mungu lakini hawawezi kuyaelewa? Ni kana kwamba maisha yao yanakaribia kukosa tumaini, kana kwamba kifo kiko karibu kuwafika, kana kwamba siku yao ya mwisho iko mbele yao. Hali kama hizo za kusikitisha ndizo nyakati ambazo malaika dhaifu humwita Mungu, wakimwambia kuhusu dhiki zao wenyewe katika kilio kimoja chenye majonzi baada ya kingine. Ni kwa sababu hii ndio malaika wanaofanya kazi miongoni mwa wana na watu wa Mungu hawatashuka kamwe juu ya mwanadamu tena; hili ni kuwazuia kupatikana katika kutawala kwa Shetani wakati wapo katika mwili, wasiweze kujinasua, na kwa hiyo wao hufanya tu kazi katika ulimwengu wa kiroho usioonekana kwa mwanadamu. Hivyo, Mungu anaposema “wakati ambapo Nitapanda hadi kwa kiti cha enzi katika moyo wa mwanadamu utakuwa wakati ambapo wana na watu Wangu wataitawala dunia,” Ananena kuhusu wakati ambapo malaika walio duniani wanafurahia baraka ya huduma kwa Mungu mbinguni. Kwa kuwa mwanadamu ni onyesho la roho za malaika, Mungu asema kwamba kwa mwanadamu, kuwa duniani ni kama kuwa mbinguni, yeye kumhudumia Mungu duniani ni kama malaika kumhudumia Mungu mbinguni moja kwa moja—na hivyo, wakati wa siku zake duniani, mwanadamu hufurahia baraka za mbingu ya tatu. Hili ndilo hasa linasemwa katika maneno haya.
Kuna maana nyingi iliyofichwa katika maneno ya Mungu. “Siku itakapokuja, watu watanijua Mimi ndani kabisa ya nyoyo zao, na watakuja kunikumbuka Mimi kwenye mawazo yao” inaelekezwa kwa roho ya mwanadamu. Kwa sababu ya udhaifu wa malaika, wao humtegemea Mungu kila mara katika mambo yote, na kila mara wamempenda Mungu na kumsujudu. Lakini kwa sababu ya usumbufu wa Shetani, hawawezi kujisaidia, hawawezi kujidhibiti, wanataka kumpenda Mungu lakini hawawezi kumpenda kwa mioyo yao yote, na kwa hivyo wao hupatwa na maumivu. Ni wakati tu ambapo kazi ya Mungu inafika kiwango fulani ndio hamu ya malaika hawa ya kumpenda Mungu kweli inaweza kutimia, ndio maana Mungu alinena maneno hayo. Asili ya malaika ni kupenda, kuhifadhi kwa upendo mkubwa, na kumtii Mungu, lakini hawajaweza kutimiza hili duniani, na hawajakuwa na budi ila kustahimili mpaka wakati huu. Unaweza kuuangalia ulimwengu wa leo: Kuna Mungu ndani ya mioyo ya watu wote, lakini watu hawana uwezo wa kutofautisha iwapo Mungu aliye mioyoni mwao ni Mungu wa kweli au ni mungu wa uwongo, na ingawa wanampenda huyu Mungu wao, hawawezi kumpenda Mungu kweli, ambalo linamaanisha hawana uwezo wa kujidhibiti. Sura mbaya ya mwanadamu iliyofichuliwa na Mungu ni sura halisi ya Shetani katika ulimwengu wa kiroho. Mwanadamu alikuwa maasumu kwa asili, na bila dhambi, na hivyo tabia zote potovu, mbaya za mwanadamu ni matendo ya Shetani katika ulimwengu wa kiroho, na ni rekodi ya kweli ya maendeleo ya ulimwengu wa kiroho. “Leo, watu wamehitimu, na wanaamini wanaweza kutembea kwa maringo mbele Yangu, na kucheka na kufanya mzaha na Mimi bila kizuizi hata kidogo, na kunihutubia Mimi kama wenzao. Bado mwanadamu hanijui Mimi, bado anaamini kuwa kiasili sisi ni kama tuko sawa, kuwa sisi sote ni wa nyama na damu, na sote tunaishi kwenye dunia ya binadamu.” Hiki ndicho ambacho Shetani amefanya ndani ya moyo wa mwanadamu. Shetani hutumia dhana na macho ya mwanadamu kumpinga Mungu, lakini bila kupotosha watu Mungu huwaambia watu kuhusu matukio haya ili mwanadamu aweze kuepuka balaa hapa. Udhaifu wa kufisha wa watu wote ni kwamba wao huona tu “mwili wa nyama na damu, na hawamtambui Roho wa Mungu.” Huu ni msingi wa hali moja ya ushawishi wa Shetani kwa mwanadamu. Watu huamini kwamba Roho aliye katika mwili huu pekee ndiye Anaweza kuitwa Mungu. Hakuna mtu anayeamini kwamba leo, Roho amepata mwili na Ameonekana kwa kweli machoni pao; watu humwona Mungu kama sehemu mbili—“vazi na mwili”—na hakuna yeyote anayemwona Mungu kama kupata mwili kwa Roho, hakuna yeyote anayeona kwamba kiini cha mwili ni tabia ya Mungu. Katika mawazo ya watu, Mungu ni wa kawaida hasa, lakini hawajui kwamba katika ukawaida huu hali moja ya umuhimu mkuu wa Mungu imejificha ndani.
Mungu alipoanza kuufunika ulimwengu wote, uligeuka kuwa giza totoro, na watu walipolala, Mungu alichukua nafasi hii kushuka miongoni mwa wanadamu, na Akaanza rasmi kutoa Roho kwa kila pembe ya dunia, Akaanza kazi ya kuwaokoa wanadamu. Inaweza kusemwa kwamba wakati ambapo Mungu alianza kuchukua mfano wa mwili, Mungu alifanya kazi duniani Mwenyewe. Kisha kazi ya Roho ikaanza, na hapo kazi yote duniani ikaanza rasmi. Kwa miaka elfu mbili, Roho wa Mungu amefanya kazi kotekote ulimwenguni. Watu hawalijui wala kulihisi hili, lakini wakati wa siku za mwisho, wakati ambapo enzi hii inakaribia kuhitimishwa, Mungu tayari ameshuka duniani kufanya kazi Mwenyewe. Hii ni baraka ya wale waliozaliwa wakati wa siku za mwisho, ambao wanaweza kutazama wenyewe mfano wa Mungu anayeishi katika mwili “Wakati uso wote wa undani ulikuwa na kiza, miongoni mwa wanadamu Nilianza kuonja uchungu wa dunia. Roho Yangu husafiri kote duniani na kuangalia ndani ya nyoyo za watu wote, licha ya hayo, pia, Mimi hushinda mwanadamu katika nyama ya kuwa mwili Kwangu.” Ushirikiano wa upatanifu kati ya Mungu aliye mbinguni na Mungu aliye duniani ni kama huo. Hatimaye, katika fikira zao watu wataamini kwamba Mungu aliye duniani ni Mungu aliye mbinguni, kwamba mbingu na dunia na vitu vyote ndani mwao viliumbwa na Mungu aliye duniani, kwamba mwanadamu anadhibitiwa na Mungu aliye duniani, kwamba Mungu aliye duniani huifanya kazi iliyo mbinguni hapa duniani, na kwamba Mungu aliye mbinguni Ameonekana katika mwili. Hili ndilo lengo kuu la kazi ya Mungu duniani, na kwa hiyo, hatua hii ni kiwango cha juu zaidi cha kazi katika kipindi cha mwili, na inatekelezwa katika uungu, na husababisha watu wote kuridhika kwa kweli. Kadri watu wanavyomtafuta Mungu katika dhana zao, ndivyo wanavyohisi zaidi kwamba Mungu aliye duniani si halisi. Hivyo, Mungu asema kwamba watu humtafuta Mungu miongoni mwa maneno matupu na mafundisho ya dini. Kadri watu wanavyomjua Mungu katika dhana zao, ndivyo wanavyokuwa stadi zaidi katika kunena maneno haya na mafundisho ya dini, na ndivyo wanavyokuwa wa ajabu zaidi; kadri watu wanavyonena maneno na mafundisho ya dini, ndivyo wanavyopotea zaidi kutoka kwa Mungu, na ndivyo wasivyoweza kujua zaidi kiini cha mwanadamu, na ndivyo wanavyomuasi Mungu zaidi, na ndivyo wanavyoondoka zaidi kwa matakwa ya Mungu. Matakwa ya Mungu kwa mwanadamu si ya ajabu kama wanavyodhani watu, lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amewahi kuelewa kweli mapenzi ya Mungu, na hivyo Mungu asema, “watu hutafuta tu katika anga isiyokuwa na mipaka, au juu ya bahari ambayo si tulivu, au juu ya ziwa tulivu, au miongoni mwa barua na mafundisho tupu.” Kadri Mungu anavyomwekea mwanadamu matakwa mengi, ndivyo watu wanavyohisi zaidi kwamba Mungu hafikiki, na ndivyo wanavyoamini zaidi kwamba Mungu ni mkuu. Hivyo, katika fahamu yao, maneno yote yanayonenwa kutoka kinywani mwa Mungu hayafikiwi na mwanadamu, kumfanya Mungu asiwe na budi ili kutenda mwenyewe; mwanadamu, wakati ule ule, hana mwelekeo hata kidogo wa kushirikiana na Mungu, na anashikilia tu kuinamisha kichwa chake na kukiri dhambi zake, akijaribu kuwa mnyenyekevu na mtiifu. Kwa hivyo, bila kutambua, watu huingia katika dini mpya, katika utaratibu wa dini ulio ni wa juu zaidi kuliko ule ulio katika makanisa ya dini. Hili linahitaji kwamba watu warudi katika hali za kawaida kupitia ugeuzaji wa hali yao hasi kuwa ile ya kujenga; la sivyo, mwanadamu daima atakuwa aliyetegwa mno.
Kwa nini Mungu husisitiza kueleza milima na maji katika matamko Yake ya nyakati nyingi? Je, kuna maana ya ishara katika maneno haya? Mungu hamruhusu tu mwanadamu kuyaona matendo Yake katika mwili Wake, bali pia Humruhusu mwanadamu kuelewa nguvu Zake katika anga. Kwa njia hii, na wakati huo huo kuamini bila shaka kwamba huyu ni Mungu katika mwili, watu pia huja kuyajua matendo ya Mungu wa vitendo, na hivyo Mungu aliye duniani anatumwa kwenda mbinguni, na Mungu aliye mbinguni analetwa duniani, ni baada ya hapo tu ndipo watu wanaweza kuona kabisa kile Mungu alicho na kupata ufahamu mkuu zaidi wa kudura ya Mungu. Kadri Mungu anavyoweza kuwashinda wanadamu katika mwili na kuupita mwili na kusafiri juu na kila pahali katika ulimwengu mzima, ndivyo watu wanavyoweza kuyaona matendo ya Mungu zaidi kwa msingi wa kumwona Mungu wa vitendo, na hivyo kujua kweli ya kazi ya Mungu kotekote katika ulimwengu mzima, kwamba si ya uwongo bali halisi, na hivyo wanakuja kujua kwamba Mungu wa vitendo wa leo ni mfano halisi wa Roho, na sio wa aina moja ya mwili kama wa mwanadamu. Hivyo, Mungu asema, “Lakini Ninapoamua kutoa ghadhabu Yangu, milima hupasuliwa vipande mbalimbali mara moja, ardhi huanza kutetemeka mara moja, maji hukauka mara moja, na mwanadamu huzingirwa na maafa mara moja.” Watu wanaposoma neno la Mungu, wanayahusisha na mwili wa Mungu, na hivyo, kazi na maneno katika ulimwengu wa kiroho yanaelekea moja kwa moja kwa Mungu wa mwili, ambalo linazidisha kufaa. Mungu anaponena, mara nyingi huwa ni kutoka mbinguni kuelekea duniani, na tena kutoka duniani kuelekea mbinguni, watu wote wakiachwa wasiweze kuelewa motisha na asili za maneno ya Mungu. “Ninapokuwa miongoni mwa mbingu, kamwe nyota hazijawahi kutishiwa na kuwepo Kwangu. Bali, huwa zinaweka nyoyo zao kunifanyia kazi Mimi.” Hali ya mbinguni ni kama hii. Mungu hupanga kwa utaratibu kila kitu katika mbingu ya tatu, na watumishi wote wanaomhudumia Mungu wakimfanyia Mungu kazi yao wenyewe. Hawajawahi kufanya chochote kumuasi Mungu, kwa hiyo hawaingii katika wasiwasi unaozungumziwa na Mungu, lakini badala yake wanafanya kazi zao kwa dhati, kamwe hakuna mchafukoge wowote, na hivyo malaika wote huishi katika nuru ya Mungu. Wakati ule ule, kwa sababu ya uasi wao, na kwa sababu hawamjui Mungu, watu wote duniani huishi gizani, na kadri wanavyompinga Mungu, ndivyo wanavyoishi gizani zaidi. Mungu anaposema, “Kila mbingu inapong’aa zaidi, ndivyo dunia chini yake inazidi kuwa na giza,” Ananena kuhusu vile siku ya Mungu inakaribia zaidi na zaidi kwa wanadamu wote. Hivyo, shughuli ya Mungu ya miaka 6,000 katika mbingu ya tatu itahitimishwa hivi punde. Vitu vyote duniani vimeingia katika sura ya mwisho, na hivi punde kila kimoja kitaondolewa mkononi mwa Mungu. Kadri watu wanavyoenda mbali zaidi na kipindi cha siku za mwisho, ndivyo wanavyoweza kuonja zaidi upotovu katika ulimwengu wa mwanadamu; na kadri wanavyoenda mbali zaidi na siku za mwisho, ndivyo wanavyofurahisha miili yao; hata kuna wengi ambao wanataka kugeuza hali ya kusikitisha ya ulimwengu, lakini wote hukata tamaa katikati ya tanafusi zao kwa ajili ya matendo ya Mungu. Hivyo, watu wanapohisi joto la majira ya kuchipua, Mungu huyafunika macho yao, na kwa hiyo wao huelewa juu ya mawimbi yanayopanda na kushuka, hakuna hata mmoja wao anaweza kufikia mashua ya kuokoa maisha iliyo mbali. Kwa kuwa watu ni wadhaifu kwa asili, Mungu asema hakuna wowote wanaoweza kuyaboresha mambo. Watu wanapokata tamaa, Mungu huanza kunena kwa ulimwengu mzima, Anaanza kuwaokoa wanadamu wote, na ni baada ya hili tu ndipo watu wanaweza kufurahia maisha mapya yanayokuja baada ya mambo kuboreshwa. Watu wa leo wako katika hatua ya kujidanganya. Kwa kuwa njia iliyo mbele yao ni ya kuhuzunisha mno, na si dhahiri, na siku zao za baadaye ni “bila kikomo” na “bila mipaka,” watu wa enzi hii hawana mwelekeo wa kupigana, na wanaweza tu kupitisha siku zao kama ndege aitwaye Hanhao.[a] Kamwe hakujawahi kuwa na mtu yeyote ambaye ameyafuatilia maisha kwa makini, na kufuatilia ufahamu wa maisha ya mwanadamu; badala yake, wanangoja siku ambayo Mwokozi aliye mbinguni atashuka ghafula kugeuza hali ya kusikitisha ya ulimwengu, ni baada ya hapo tu ndio watakuwa wenye ari katika majaribio yao kuishi. Hivyo ndivyo ilivyo hali ya kweli ya wanadamu wote na fikira ya watu wote.
Leo, Mungu anatabiri maisha mapya ya mwanadamu ya siku za baadaye kulingana na fikira zake wakati huu, ambayo ni dalili ya nuru ambayo Mungu anazungumzia. Kile ambacho Mungu anatabiri ni kile ambacho hatimaye kitatimizwa na Mungu, na ni matokeo mazuri ya ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani. “Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee kamwe, na hakuna mtu ambaye yuko kama alivyokuwa. Ninapumzika katika kiti cha enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima….” Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu ya sasa. Wateule wote wa Mungu wanarudi kwa umbo lao la asili, kwa sababu hiyo malaika, ambao wameteseka kwa miaka mingi sana, wanaachiliwa, kama tu asemavyo Mungu, “kila mmoja akiwa na uso kama wa mtakatifu ndani ya moyo wa binadamu.” Kwa sababu malaika hufanya kazi duniani na kumhudumia Mungu duniani, na utukufu wa Mungu husambaa kila mahali ulimwenguni, mbingu inaletwa duniani, na dunia inainuliwa kwenda mbinguni. Kwa hivyo, mwanadamu ni kiungo kinachounganisha mbingu na dunia; mbingu na dunia haziko mbali tena, hazijatengana tena, lakini zimeunganishwa kama kitu kimoja. Kotekote ulimwenguni, Mungu na mwanadamu ndio pekee wanaoishi. Hakuna vumbi wala uchafu, na vitu vyote vinafanywa upya, kama mwanakondoo mdogo anayelala katika ukanda wa mbuga wa kijani kibichi chini ya anga, akifurahia neema yote ya Mungu. Na ni kwa sababu ya ujio wa kijani kibichi ndiposa pumzi ya uhai inaangaza, kwani Mungu anakuja duniani kuishi pamoja na mwanadamu milele yote, kama ilivyosemwa kutoka kinywani mwa Mungu kwamba “Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena.” Hii ni ishara ya kushindwa kwa shetani, ni siku ya pumziko la Mungu, na siku hii itatukuzwa na kutangazwa na watu wote, na itafanyiwa kumbukumbu na watu wote. Wakati ambapo Mungu ametulia juu ya kiti cha enzi pia ndio wakati ambapo Mungu anahitimisha kazi Yake duniani, na ndio wakati ule ambao siri zote za Mungu zinaonyeshwa kwa mwanadamu; Mungu na mwanadamu watakuwa katika upatanifu daima, hawatakuwa mbali tena—haya ni mandhari mazuri ya ufalme!
Katika siri zimefichwa siri, na maneno ya Mungu ni ya kina kweli na yasiyoeleweka!
Tanbihi:
a. Hadithi ya ndege wa Hanhao inafanana sana na hekaya ya Aesop ya mchwa na panzi. Ndege wa Hanhao hupenda zaidi kulala kuliko kujenga kiota wakati hali ya hewa ni ya vuguvugu, licha ya onyo la marudio kutoka kwa jirani wake, ndege wa jamii ya kunguru. Wakati majira ya baridi hufika, ndege huyo huganda hadi kifo.