Sura ya 10
Katika wakati wa ujenzi wa kanisa, Mungu alitaja ujenzi wa kanisa kwa nadra. Hata Alipotaja, Alifanya hivyo katika lugha ya wakati wa ujenzi wa kanisa. Mara tu Enzi ya Ufalme ilipokuja, Mungu alifuta mbinu na wasiwasi nyingine za wakati wa ujenzi wa kanisa mara mmoja na Hakuwahi tena kusema hata neno moja kuuhusu. Hii hasa ni maana ya msingi ya “Mungu Mwenyewe” ambaye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hata kama vitu vilifanywa vizuri katika siku za zamani, kwa kadri vilivyo sehemu ya enzi iliyopita, Mungu anaviweka vitu kama hivyo katika kundi la vitu vinavyotokea katika wakati kabla ya Kristo, huku wakati wa sasa ukijulikana kama wakati wa “baada ya Kristo[a].” Kuhusu suala hili, ujenzi wa kanisa unaweza kuchukuliwa kama kitangulizi cha lazima cha ujenzi wa ufalme. Uliweka msingi kwa Mungu kutumia nguvu Zake kuu katika ufalme. Leo, kazi ya ujenzi wa kanisa ni kinda la ndege la ujenzi wa ufalme tu, ambalo ni lengo la msingi la kazi ya Mungu duniani. Mungu alitayarisha utondoti wote wa kazi Yake kabla ya kumalizika kwa kazi ya ujenzi wa kanisa, na wakati ulipokuwa sawa, Alianza kazi Yake moja kwa moja. Hasa, Mungu alinena hivi, “Enzi ya Ufalme ni, hata hivyo, tofauti na nyakati za kale. Haihusu jinsi ambavyo binadamu hutenda; badala yake, Nimeshuka duniani ili Nitekeleze kazi Yangu binafsi, jambo ambalo wanadamu hawawezi kuelewa wala kufanikisha.” Kwa kweli, kazi hii lazima itekelezwe na Mungu binafsi—hakuna mwanadamu anayeweza kazi kama hii, yeye hana uwezo unaohitajika. Mbali na Mungu, ni nani angetekeleza kazi kubwa kama hii miongoni mwa wanadamu? Ni nani mwingine anaweza “kuwatesa” wanadamu wote hadi kukaribia kufa? Je, wanadamu wangeweza kuipanga kazi kama hii iwezekanavyo? Ni kwa nini Anasema, “Mimi binafsi Natekeleza kazi Yangu baada ya kushuka duniani”? Je, Roho wa Mungu angeweza kutoweka kweli kutoka kwa anga yote? “Mimi binafsi Natekeleza kazi Yangu baada ya kushuka duniani,” inahusu ukweli kwamba Roho wa Mungu anakuwa mwili ili kutenda kazi, na ukweli kwamba Roho wa Mungu anafanya kazi kwa dhahiri kupitia kwa wanadamu. Kwa kuitekeleza kazi Yake binafsi, Mungu anawaruhusu watu wengi kumwona Mungu Mwenyewe kwa macho yao, ili wasihitaji kutafuta kwa makini ndani ya roho zao. Zaidi ya hayo, linawaruhusu wanadamu wote kuona matendo ya Roho kwa macho yao wenyewe na kuwaonyesha kwamba kuna tofauti muhimu kati ya mwili wa mwanadamu na ule wa Mungu. Sawia, kotekote katika anga yote na ulimwengu dunia wote, Roho wa Mungu bado Anafanya kazi. Wale watu wote ambao wamepata nuru, kwa vile wamekubali jina la Mungu, wanaona jinsi Roho wa Mungu hufanya kazi na, hivyo, hufahamiana hata zaidi na kupata mwili kwa Mungu. Hivyo, kama tu uungu wa Mungu utafanya kazi moja kwa moja, yaani Roho wa Mungu aweze kufanya kazi bila kizuizi hata kidogo, ndio mwanadamu anaweza kufahamiana zaidi na Mungu Mwenyewe wa vitendo. Hiki ni kiini cha ujenzi wa ufalme.
Mungu amekuwa mwili mara ngapi? Yaweza kuwa mara kadhaa? Ni kwa nini Mungu amesema mara nyingi, “Wakati mmoja Nilishuka kwenye ulimwengu wa binadamu Nikapitia na Nikaangalia kwa makini mateso yao lakini nilifanya hivyo bila ya kutimiza lengo la kupata mwili Kwangu”? Je, ni kweli kwamba Mungu amekuwa mwili mara kadhaa, lakini hajawahi kamwe kujulikana na mwanadamu hata mara moja? Kauli hii haimaanishi hivi. Mara ya kwanza Mungu alipokuwa mwili, lengo Lake kwa kweli halikuwa mwanadamu amjue. Badala yake, Alitekeleza kazi Yake na kisha akaondoka bila mtu yeyote kutambua au hata kuwa na nafasi ya kumjua. Hakumruhusu mwanadamu kumjua kwa ukamilifu na pia hakumiliki kabisa umuhimu wa kupata mwili, kwa hiyo Hangeweza kusemekana kuwa mwili kwa ukamilifu. Katika kupata mwili kwa mara ya kwanza, Alitumia tu umbo la mwili ambao haukuwa na asili ya dhambi kutekeleza kazi hiyo—kazi ilipokuwa imekamilika, hakukuwa na haja ya kutaja zaidi. Kuhusu wale watu ambao wametumiwa na Mungu kotekote katika enzi, mifano kama hiyo haistahili hata kidogo kuitwa kupata mwili. Leo, Yule ambaye ni Mungu Mwenyewe wa vitendo pekee, Aliye na sura ya nje ya ubinadamu wa kawaida inayoficha uungu kamili ndani, na ambaye lengo Lake ni kumruhusu mwanadamu kumjua ndiye Anaweza kuitwa kwa ukamilifu kupata mwili. Maana ya ziara ya Mungu ya kwanza kwa ulimwengu huu ina hali moja tu yenye umuhimu wa kile kinachoitwa leo kupata mwili—ziara hii katu haikuwa na maana kamili ya kile kinachoitwa sasa kupata mwili. Hii ndiyo sababu Mungu alisema, “bila kutimiza umuhimu wa kupata mwili.” “Kupitia na kuchunguza mateso ya mwanadamu” kunahusu Roho wa Mungu na aina mbili za kupata mwili, hivyo Mungu alisema, “Punde ujenzi wa ufalme ulipoanza, Mimi nikiwa mwili nilianza rasmi kutekeleza huduma Yangu; yaani, Mfalme wa ufalme rasmi Alichukua ukuu wa mamlaka Yake makuu.” Ingawa ujenzi wa kanisa ulikuwa ushuhuda kwa jina la Mungu, kazi haikuwa imeanza rasmi—ni leo tu ndiyo inaweza kusemekana kuwa ujenzi wa ufalme. Yote yaliyofanywa awali yalikuwa limbuko tu, halikuwa jambo halisi. Ingawa ilisemekana kwamba ufalme ulikuwa umeingiwa, bado hakukuwa na kazi iliyokuwa ikifanywa ndani yake. Leo tu, vile sasa kazi inafanywa ndani ya uungu wa Mungu na Mungu ameanza rasmi kazi Yake ndipo mwanadamu hatimaye ameingia katika ufalme. Hivyo, “mshuko wa ufalme katika ulimwengu wa binadamu—mbali na kuwa tu suala la maonyesho ya moja kwa moja—ni wa ukweli halisi; hiki ni kipengele mojawapo cha maana ya ‘uhalisi wa kutenda.’” Dondoo hili ni muhtasari wa kufaa wa ufafanuzi wa hapo awali. Baada ya kutoa ufafanuzi huu, Mungu anaendelea mbele kueleza sifa za hali ya jumla ya wanadamu, Akimwacha mwanadamu katika hali ya kujishughulisha kwa siku zote. “Kotekote katika ulimwengu, binadamu wote hukaa chini ya upendo Wangu, huruma Yangu, lakini pia binadamu wote hukaa chini ya hukumu Yangu, na vivyo hivyo chini ya majaribio Yangu.” Maisha ya mwanadamu huongozwa kufuatana na kanuni na sheria fulani, ambazo Mungu ameweka. Kanuni na sheria hizi ni zifuatazo: Kutakuwa na nyakati za furaha, nyakati za kuvunjika moyo na zaidi, nyakati za usafishaji wa dhiki za kustahimili. Hivyo, hakuna mwanadamu atakayeishi maisha ya furaha tupu au mateso tupu. Kila maisha yatakuwa na milima na mabonde yake. Kwa wanadamu wote, sio tu kwamba upendo na huruma wa Mungu pekee ni dhahiri, ila pia hukumu Yake na tabia Yake kamili. Inaweza kusemekana hivi: Inaweza kusemekana hivi: Wanadamu wote huishi kupitia kwa majaribio ya Mungu, sivyo? Kote ulimwengu huu mkubwa, wanadamu wote hufanya kazi kwa kujishughulisha katika kazi ya kutafuta njia yao wenyewe. Hawana hakika wajibu wao ni gani na wengine hata huharibu au hupoteza maisha yao kwa ajili ya majaliwa yao. Hata Ayubu hakuwa tofauti na wengine: Akishinda majaribio mengi ya Mungu, yeye hata hivyo aliendelea kutafuta njia yake mwenyewe. Hakuna mwanadamu anayeweza kubaki palepale kupitia kwa majaribio ya Mungu. Kwa sababu ya ulafi wake au asili yake ya binadamu, hakuna mwanadamu anayeridhishwa kabisa na hali yake ya sasa, na hakuna mwanadamu anayeweza kubaki palepale kupitia kwa majaribio: Kila mwanadamu huvunjika chini ya hukumu ya Mungu. Kama Mungu angeendelea kuwa makini sana na mwanadamu, kama Angeendelea kushikilia madai ya kushurutisha kama hayo kwa mwanadamu, ingekuwa tu kama alivyosema Mungu: “jamii nzima ya binadamu ingeporomoka chini ya macho Yangu ya kuchoma.”
Licha ya ukweli kwamba ujenzi wa ufalme umeanza rasmi, maamkuzi kwa ufalme bado hayajatangazwa rasmi—sasa ni unabii tu wa kile kitakachokuja. Wakati ambapo watu wote watakuwa wamefanywa kamili na mataifa yote ya dunia kugeuka kuwa ufalme wa Kristo, basi huo utakuwa wakati ambapo radi saba zitanguruma. Siku ya sasa ni hatua ndefu ya kwenda mbele katika mwelekeo wa hatua hiyo, shambulio limeachiliwa huru kwa muda ujao. Huu ni mpango wa Mungu—hivi karibuni utafanikishwa. Hata hivyo, Mungu tayari amefanikisha yote ambayo Amesema. Hivyo, ni dhahiri kwamba mataifa ya dunia ni makasri tu yaliyo mchangani yanayotetemeka bamvua linapokaribia: Siku ya mwisho iko karibu sana na joka kubwa jekundu litaanguka chini ya neno la Mungu. Ili kuhakikisha kwamba mpango wa Mungu unatekelezwa kwa ufanisi, malaika wa mbinguni wameshuka juu ya dunia, wakifanya kila wanaloweza kumridhisha Mungu. Mungu Mwenyewe mwenye mwili Amejipanga katika uwanja wa vita kupigana na adui. Po pote ambapo Aliyepata mwili huonekana, adui anaangamiziwa mahali hapo. Uchina ni ya kwanza kuangamizwa, kuharibiwa kabisa kwa mkono wa Mungu. Mungu haipi Uchina upande wowote kabisa. Thibitisho la kuendelea kuanguka kwa joka kubwa jekundu linaweza kuonekana katika ukomavu wa watu unaoendelea. Hili linaweza kuonekana wazi na mtu yeyote. Ukomavu wa watu ni ishara ya kifo cha adui. Huu ni ufafanuzi kidogo wa kile kinachomaanishwa na “kufanya vita.” Hivyo, Mungu aliwakumbusha watu wakati mwingi watoe ushuhuda mzuri kwa Mungu kutangua hali ya fikira, ubaya wa joka kubwa jekundu ndani ya mioyo ya wanadamu. Mungu hutumia kumbusho kama hizo kuchangamsha imani ya mwanadamu na, kwa kufanya hivyo, Hutimiza ujuzi katika kazi Yake. Hili ni kwa sababu Mungu amesema, “Binadamu ana uwezo wa kufanya nini? Si ni afadhali Nifanye hivyo Mwenyewe?” Wanadamu wote wako hivyo. Si kwamba wao hawawezi tu, bali pia huvunjika moyo na husikitishwa kwa urahisi. Kwa sababu hii, hawawezi kumjua Mungu. Mungu hafufui tu imani ya mwanadamu, kwa siri Yeye humjaza mwanadamu nguvu siku zote.
Linalofuata, Mungu alianza kunena kwa ulimwengu wote. Mungu hakuanzisha tu kazi Yake mpya Uchina, Kotekote ulimwenguni Alianza kufanya kazi mpya ya leo. Katika hatua hii ya kazi, kwa vile Mungu anataka kufichua matendo Yake yote kotekote katika dunia ili wanadamu wote ambao wamemsaliti watakuja tena kuinama kwa utiifu mbele ya kiti Chake cha enzi, hivi ndani ya hukumu ya Mungu bado kuna huruma na upendo wa Mungu. Mungu hutumia matukio ya sasa kotekote ulimwenguni kutetemesha mioyo ya wanadamu, Akiiamsha kumtafuta Mungu ili waweze kumiminika kwenda Kwake. Hivyo Mungu asema, “Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo.” Mungu anafichua asili halisi ya mwanadamu kwa usahihi upenyao, usio na kifani, na usiohitaji bidii. Hili humwacha mwanadamu akiuficha uso wake kwa aibu, akiwa amefedheheshwa kabisa. Kila wakati Mungu anenapo, kwa kiasi fulani Yeye daima hutaja hali fulani ya unyonge wa mwanadamu ili, kwa raha zake, mwanadamu asisahau kujijua na asifikirie kujijua ni kazi ya kale. Nijuavyo asili ya mwanadamu, kama Mungu angekosa kutaja makosa yake kwa dakika moja tu, mwanadamu angegeuka kuwa mpotovu na mwenye kiburi. Hivyo, leo Mungu asema, “Binadamu—mbali na kuthamini vyeo ambavyo Nimeweka juu yao, wengi wao, kwa sababu ya jina ‘watendaji-huduma,’ wanaweka chuki katika nyoyo zao, na wengi sana, kwa sababu ya jina ‘watu Wangu,’ huzalisha upendo Kwangu katika nyoyo zao. Hakuna anayepaswa kujaribu kunidanganya; macho Yangu huona kila kitu!” Punde tu mwanadamu aonapo kauli hii, yeye huwa na wasiwasi mara moja. Yeye huhisi kwamba matendo yake ya zamani hayakuwa yamepevuka—aina ya udanganyifu tu unaomkosea Mungu. Ametaka kumridhisha Mungu hivi karibuni, lakini huku akiwa radhi kupita kiasi, anakosa nguvu na hajui analopaswa kufanya. Bila kukusudia, anatiwa moyo na azimio lililotiwa nguvu. Hili ndilo tokeo la kusoma maneno haya mtu anapokuwa ametulia.
Kwa upande mmoja, Mungu asema kwamba Shetani ni mwenye wazimu mno, huku kwa upande mwingine Asema pia wanadamu wengi sana hawabadilishi asili yao ya kale. Kutokana na hili, ni dhahiri kwamba matendo ya Shetani hudhihirishwa kupitia kwa mwanadamu. Hivyo, Mungu humkumbusha mwanadamu mara kwa mara asiwe mpotovu, asije akamezwa na Shetani. Huku si kutoa unabii tu kwamba watu wengine wataasi, zaidi ni kengele inayolia kuonya watu wote waachane na yaliyopita haraka na watafute yale ambayo ni ya wakati wa sasa. Hakuna mwanadamu anayetamani kupagawa na mashetani au kujawa na pepo waovu, kwa hiyo neno la Mungu hata zaidi ni onyo na kuasa kwao. Hata hivyo, watu wengi wanapoenda kinyume kupita kiasi, wakitilia maanani sana kila neno la Mungu, Mungu kwa zamu husema, “Wengi wa watu wanasubiri Nifichue mafumbo zaidi ili walishe macho yao. Ilhali, iwapo utakuja kuelewa siri zote za mbinguni, je, ni nini utakalofanya na hayo maarifa? Je, yataweza kuongeza upendo wako Kwangu? Je, yatachochea upendo wako Kwangu?” Kutokana na hili ni dhahiri kwamba mwanadamu hatumii neno la Mungu kumjua Mungu na kumpenda Mungu, lakini badala yake kuongeza maduka ya “kijighala chake.” Kwa hiyo, Mungu kutumia msemo “walishe macho yao” kueleza kutokuwa kadiri kwa mwanadamu kunadhihirisha jinsi upendo wa mwanadamu kwa Mungu bado si safi kwa ukamilifu. Kama Mungu hangetandua siri hizo, mwanadamu hangetilia maanani sana maneno Yake, lakini badala yake angeyaangalia kidogo tu, kuyatazama mara moja, kana kwamba anapendezwa na maua akienda shoti mgongoni mwa farasi. Hangechukua wakati kutafakari na kuyafikiria kweli maneno Yake. Watu wengi sana hawahifadhi kwa upendo mkubwa neno la Mungu. Hawafanyi kila linalowezekana kula na kunywa maneno Yake, lakini badala yake huyapitia juujuu upesi kwa uzembe. Kwa nini Mungu ananena sasa kwa njia tofauti kulika nyakati zilizopita? Kwa nini yote ni lugha isiyofahamika? Kwa mfano, “kuwavisha” katika “Mimi kamwe Singewahi kamwe kuwavisha watu taji na vitambulisho hivi kwa kawaida,” “dhahabu safi zaidi” katika “Yupo ambaye anaweza kupokea ndani ya nafsi yake dhahabu safi zaidi ambayo maneno Yangu yanaundwa nayo,” Kutaja kwake awali “usindikaji” katika “bila kupitia usindikaji wowote na Shetani” na misemo mingine kama hiyo. Mwanadamu haelewi ni kwa nini Mungu hunena kwa njia hii. Hafahamu ni kwa nini Yeye hunena kwa njia kama hii ya mzaha, ya ucheshi na ya kuchokoza. Hili hasa ni dhihirisho la kusudi la kunena kwa Mungu. Tangu mwanzo kabisa mpaka sasa, mwanadamu daima hajaweza kufahamu neno la Mungu na imeonekana kana kwamba neno la Mungu kweli lilikuwa la mashaka sana na kali. Kwa kuongeza mkazo mdogo sana wa ucheshi—kuongeza mzaha hapa na pale—Anaweza kufanya hali kuwa angavu na maneno Yake na kumruhusu mwanadamu kutuliza misuli yake kidogo. Kwa kufanya hivyo, Anaweza kutimiza hata matokeo makubwa zaidi, Akiwashurutisha wanadamu wote kutafakari juu ya neno la Mungu.
Tanbihi:
a. “Baada ya Kristo” ina maana ya “AD (Anno Domini).”