Sura ya 11

Kwa macho ya mwanadamu, inaonekana hakuna badiliko katika matamshi ya Mungu wakati wa kipindi hiki, ambalo ni kwa sababu watu hawawezi kuelewa sheria ambazo kwazo Mungu hunena, na hawafahamu muktadha wa maneno Yake. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu hawaamini kwamba kuna mafumbo yoyote mapya katika maneno haya; hivyo, hawawezi kuishi maisha yaliyo mapya kiajabu, na badala yake huishi maisha yaliyokwama na yasiyokuwa na uhai. Lakini katika matamshi ya Mungu, tunaona kwamba kuna kiwango cha kina cha maana, kile kisichofahamika na pia kisichofikika na mwanadamu. Leo, kwa mwanadamu kubahatika vya kutosha kusoma maneno kama hayo ya Mungu ni baraka kuu zaidi ya zote. Kama hakuna ambaye angesoma maneno haya, mwanadamu daima angesalia mwenye kiburi, wa kujidai, asiyejijua, na asiyefahamu tu ni dosari ngapi alizo nazo. Baada ya kusoma maneno ya Mungu yenye maana sana, yasiyoeleweka, watu huyastaajabia kisiri, na kuna kusadikisha kwa kweli ndani ya mioyo yao, isiovunda na uwongo; mioyo yao huwa mfano halisi, siyo bidhaa za kughushi. Hili ndilo hufanyika kwa kweli ndani ya mioyo ya watu. Kila mtu ana hadithi yake mwenyewe moyoni mwake. Ni kana kwamba wanajiambia wenyewe: Huenda hili lilinenwa na Mungu Mwenyewe—kama si Mungu, nani mwingine angetamka maneno kama haya? Mbona siwezi kuyanena? Mbona mimi siwezi kufanya kazi kama hiyo? Inaonekana Mungu aliyepata mwili ambaye Mungu huzungumzia kweli ni halisi, naye ni Mungu Mwenyewe! Sitakuwa na shaka tena. La sivyo, huenda hata ikawa kwamba wakati ambapo mkono wa Mungu utafika, muda wa majuto utakuwa umepita mno! … Hiki ndicho watu wengi sana hufikiria ndani ya mioyo yao. Ni haki kusema kwamba, tangu wakati ambapo Mungu alianza kunena mpaka leo, watu wote wangekuwa wamepotea bila msaada wa maneno ya Mungu. Mbona husemekana kwamba kazi hii yote hufanywa na Mungu Mwenyewe, na sio na mwanadamu? Mungu asingetumia maneno kuyasaidia maisha ya kanisa, kila mtu angetoweka bila dalili. Je, hii si nguvu ya Mungu? Hii kweli ni lugha ya kushawishi ya mwanadamu? Je, hii ni vipaji vya ajabu vya mwanadamu? Bila shaka la! Bila uchunguzi, hakuna ambaye angejua ni aina gani ya damu hutiririka katika vena zake, hawangefahamu ni mioyo mingapi waliyo nayo, au bongo ngapi, na wote wangefikiri kwamba wanamjua Mungu. Hawajui kwamba bado upinzani upo ndani ya ufahamu wao? Si ajabu kwamba Mungu husema, “Kila mtu katika wanadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chake, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu.” Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba maneno ya Mungu si yasiyo na lengo maalum na kutokuwa na msingi. Mungu hajawahi kamwe kumtendea mtu yeyote bila haki; hata Ayubu, na imani yake yote, hakusamehewa—yeye pia alichunguzwa, na kuachwa bila mahali popote pa kujificha kutokana na aibu yake. Na sembuse watu wa leo. Hivyo, Mungu kisha huuliza mara moja: “Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani?” Swali la Mungu lina maana kidogo, lakini huwaacha watu wamekanganyika: “Tunahisi nini? Sisi bado hatujui wakati ambao ufalme utawasili, kwa hiyo tungezungumzaje kuhusu hisia? Zaidi ya hayo, hatuna habari. Kama Ningehisi kitu fulani, kingekuwa ‘kustaajabishwa,’ na siyo kingine zaidi.” Kwa kweli, swali hili si lengo la maneno ya Mungu. Zaidi ya yote, “Wakati Wanangu na watu Wangu wanamiminika katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi,” sentensi hii moja inatoa muhtasari wa maendeleo ya ufalme wote wa kiroho. Hakuna anayejua kile ambacho Mungu anataka kufanya katika ufalme wa kiroho wakati wa kipindi hiki, na ni baada tu ya Mungu kutamka maneno haya ndipo kuna kuzinduka kidogo ndani ya watu. Kwa sababu kuna hatua tofauti katika kazi ya Mungu, kazi ya Mungu kotekote katika ulimwengu pia hubadilika. Wakati wa kipindi hiki, Mungu hasa huwaokoa wana na watu wa Mungu, ambako ni kusema, wanapochungwa na malaika, wana na watu wa Mungu huanza kukubali kushughulikiwa na kuvunjwa, wao huanza kwa urasimu kuondoa mawazo na fikira zao, na kuagana na dalili yoyote ya dunia hii; kwa maneno mengine, “hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi” iliyozungumziwa na Mungu huanza kwa urasimu. Kwa sababu ni hukumu ya Mungu, Mungu lazima atamke sauti Yake—na ingawa maudhui ni tofauti, lengo kila mara huwa lile lile. Leo, kwa kuzingatia toni ambayo kwayo Mungu huzungumza, inaonekana kwamba maneno Yake yanaelekezwa kwa kundi fulani la watu. Kwa kweli, zaidi ya yote, maneno haya hushughulikia asili ya wanadamu wote. Maneno hayo huingia moja kwa moja hadi uti wa mgongo wa mwanadamu, hayaachi kuumiza hisia za mwanadamu, nayo hufichua asili yake yote, bila kuacha chochote, bila kuruhusu chochote kupita. Kuanzia leo, Mungu anafichua kwa urasimu sura ya kweli ya mwanadamu, na hivyo “huiachilia sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima.” Athari ambayo hutimizwa hatimaye ni “Kupitia maneno Yangu, Nitawasafisha wanadamu na mambo yote miongoni mwa yote yaliyo mbinguni na duniani, ili nchi isiwe chafu na fisadi tena, lakini uwe ufalme mtakatifu.” Maneno haya yanadhihirisha siku za baadaye za ufalme, ambayo yote ni ya ufalme wa Kristo, kama tu alivyosema Mungu, “Yote ni matunda mazuri, wote ni wakulima wenye bidii.” Kwa kawaida, hili litatokea kotekote katika ulimwengu, na halijawekewa mipaka Uchina tu.

Ni wakati tu ambapo Mungu huanza kunena na kutenda ndipo watu humfahamu Yeye kidogo katika dhana zao. Hapo mwanzo, ufahamu huu huwepo tu ndani ya dhana zao, lakini kadiri muda unavyopita, watu huanza kuhisi kwamba mawazo yao wenyewe yanaendelea kutokuwa na manufaa na hayafai; hivyo, wao huja kuamini yote ambayo Mungu husema, kiasi kwamba wao “hutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya akili zao.” Ni katika akili zao pekee ndipo watu huwa na mahali pa Mungu wa vitendo. Kwa kweli, hata hivyo, hawamjui Mungu, na hunena maneno matupu tu. Ilhali ikifananishwa na zamani, wameendelea vizuri mno—ingawa bado wako mbali sana na Mungu Mwenyewe wa vitendo. Kwa nini Mungu husema kila mara, “Kila siku Natembea miongoni mwa mtiririko usiokoma wa watu, na kila siku Nafanya kazi ndani ya kila mtu”? Kadri ambavyo Mungu husema mambo kama hayo, ndivyo watu wanavyoweza kuyafananisha zaidi na Mungu Mwenyewe wa vitendo wa leo, kwa hiyo wanaweza kumjua vizuri zaidi Mungu wa vitendo kwa kweli. Kwa sababu maneno ya Mungu yananenwa kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kutamkwa kwa kutumia lugha ya ubinadamu, watu wanaweza kutambua vyema maneno ya Mungu kwa kuyatathmini dhidi ya vitu yakinifu, na hivyo athari kuu zaidi hutimizwa. Kuongezea, mara kwa mara Mungu hunena kuhusu picha ya “Mimi” ndani ya mioyo ya watu na “Mimi” kwa kweli, ambalo huwafanya watu wawe radhi zaidi kusafisha picha ya Mungu ndani ya mioyo yao, na hivyo kuwa radhi kujua na kufungamana na Mungu Mwenyewe wa vitendo. Hii ni hekima ya maneno ya Mungu. Kadri ambavyo Mungu husema mambo kama hayo, ndivyo faida kwa ufahamu wa watu kuhusu Mungu huwa kuu zaidi, na hivyo Mungu husema, “Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi kunijua, na hata angekuja kunijua, je, si maarifa kama hayo bado yangekuwa dhana?” Kweli, kama watu wangehitajika kumjua Mungu kufuatana na dhana zao wenyewe, ingekuwa rahisi kwao, wangeburudika na kufurahi, na hivyo Mungu hangekuwa dhahiri daima, na asiye wa vitendo katika mioyo ya watu, ambalo lingethibitisha kwamba Shetani, na si Mungu, anashikilia utawala juu ya ulimwengu wote; hivyo, maneno ya Mungu kwamba “Nimerejesha mamlaka Yangu” yangesalia matupu daima.

Wakati ambapo uungu huanza kutenda moja kwa moja ni wakati ambao pia ufalme hushuka kwa urasimu kwa ulimwengu wa mwanadamu. Lakini kile ambacho husemwa hapa ni kwamba ufalme hushuka miongoni mwa binadamu, siyo kwamba ufalme huanza kuonekana polepole miongoni mwa wanadamu—na hivyo kile kinachozungumziwa leo ni ujenzi wa ufalme, na siyo jinsi unavyoanza kuonekana. Mbona Mungu husema kila mara, “Mambo yote yanakimya” Yawezekana kwamba mambo yote yanasimama kabisa? Yawezekana kwamba milima mikubwa inakimya kwa kweli? Kwa hiyo mbona watu hawana ufahamu wa hili? Yawezekana kwamba neno la Mungu lina makosa? Au Mungu anatia chumvi? Kwa sababu kila kitu ambacho Mungu hufanya hutekelezwa katika mazingira fulani, hakuna ambaye hukifahamu, au ambaye ana uwezo wa kukiona kwa macho yake mwenyewe, na yote ambayo watu wanaweza kufanya tu ni kumsikiliza Mungu akinena. Kwa sababu ya uadhama ambao Mungu hutenda, wakati ambapo Mungu hufika, ni kana kwamba kumekuwa na mabadiliko makubwa mno mbinguni na duniani; na kwa Mungu, huonekana kwamba wote wanatazama wakati huu. Leo, ukweli bado haujafika. Watu wamejifunza kidogo tu kutoka kwa sehemu ya maana halisi ya maneno ya Mungu. Maana ya kweli inangoja wakati ambao watajisafisha na dhana zao; wakati huo tu ndipo watakuwa na fahamu ya kile ambacho Mungu mwenye mwili anafanya duniani na mbinguni leo. Ndani ya watu wa Mungu Uchina hakuna tu sumu ya joka kubwa jekundu. Hiyo, pia, ndiyo asili ya joka kubwa jekundu iliyofichuliwa kwa wingi zaidi, na kwa dhahiri zaidi, ndani yao. Lakini Mungu hazungumzi kuhusu hili moja kwa moja, Akitaja tu kidogo kuhusu sumu ya joka kubwa jekundu. Kwa njia hii, Hayafichui makovu ya mwanadamu moja kwa moja, ambalo ni la manufaa zaidi kwa maendeleo ya mwanadamu. Watoto wa joka kubwa jekundu hawapendi kuitwa ukoo wa joka kubwa jekundu mbele ya wengine. Ni kana kwamba maneno “joka kubwa jekundu” huleta aibu kwao; hakuna yeyote kati yao aliye radhi kuzungumza kuhusu maneno haya, na hivyo Mungu husema tu, “hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina.” Kwa usahihi zaidi, Mungu amekuja hasa kuwashinda wawakilishi wa kiumboasili wa watoto wa joka kubwa jekundu, ambalo ni umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu Uchina.

“Nijapo binafsi miongoni mwa binadamu, malaika wanaanza kazi ya uchungaji wakati huo huo.” Kwa kweli, haichukuliwi neno kwa neno kwamba Roho wa Mungu huwasili tu katika ulimwengu wa mwanadamu wakati ambapo malaika huanza kazi yao miongoni mwa watu wote. Badala yake, sehemu hizi mbili za kazi—kazi ya uungu na uchungaji wa malaika—hutekelezwa sawia. Linalofuata, Mungu huzungumza kidogo kuhusu uchungaji wa malaika. Wakati ambapo Yeye husema kwamba “wana na watu wote hawapati tu majaribio na uchungaji, lakini wanaweza pia kuona, na macho yao wenyewe, tukio la kila aina za maono,” watu wengi sana huwa na mawazo tele kuhusu neno “maono.” Maono yanahusu matukio ya rohoni katika mawazo ya watu. Lakini yaliyomo katika kazi husalia ufahamu wa Mungu Mwenyewe wa vitendo. Maono ni njia ambayo kwayo malaika hufanya kazi. Yanaweza kuwapa watu hisia au ndoto, yakiwakubalia kutambua kuweko kwa malaika. Lakini malaika husalia wasioonekana kwa mwanadamu. Mbinu ambayo kwayo wao hufanya kazi miongoni mwa wana na watu wa Mungu ni kuwapa nuru na kuwaangaza moja kwa moja, kuongezea kwayo ni kuwashughulikia na kuwavunja. Wao hutoa mahubiri mara chache. Kwa kawaida, mawasiliano kati ya watu ni jambo la pekee; hili ndilo linalofanyika katika mataifa nje ya Uchina. Ndani ya maneno ya Mungu kuna ufunuo wa hali za kuishi za wanadamu wote—kwa kawaida, hili linaelekezwa hasa kwa watoto wa joka kubwa jekundu. Kati ya hali mbalimbali za kiroho za wanadamu wote, Mungu huteua zile ambazo ni za uwakilishi ili zitumike kama mifano. Hivyo, maneno ya Mungu huwavua watu wakawa uchi, na hawaoni aibu yoyote, ama sivyo hawana muda wa kujificha kutoka kwa nuru iangazayo, na wao hushindwa katika ujanja wao. Tabia nyingi za mwanadamu ni picha nyingi kupita kiasi, ambazo Mungu amechora kutoka nyakati za kale mpaka leo, na ambazo Atachora kutoka leo mpaka kesho. Yote ambayo Yeye huchora ni ubaya wa mwanadamu: Wengine hutokwa na machozi gizani, inavyoonekana kwa nje wao husikitishwa kwa ajili ya kutoona tena, wengine hucheka, wengine hupigwa kwa nguvu na mawimbi makubwa, wengine hutembea juu ya barabara za mlima zinazoinuka na kushuka, wengine hutafuta katikati ya nyika kubwa mno, wakitetemeka kwa woga, kama ndege aliyegutushwa na mlio tu wa uzi wa uta, wakitishwa kabisa na kuliwa na wanyama wa mwitu katika milima. Mikononi mwa Mungu, hizi tabia nyingi mbaya hugeuka kuwa za kugusa, uwakilishaji wa picha kama za maisha, nyingi ya hizo za kutisha sana kutazama, la sivyo za kiasi cha kutosha kuwaogofya watu na kuwaacha waliokanganyikiwa na kutatanishwa. Machoni pa Mungu, vyote vinavyoonyeshwa ndani ya mwanadamu ni ubaya tu, na hata ingawa kinaweza kuchochea huruma, bado ni ubaya. Sehemu maalum ya tofauti kati ya mwanadamu na Mungu ni kwamba udhaifu wa mwanadamu upo katika mwelekeo wake wa kuonyesha ukarimu wake kuelekea wengine. Mungu, hata hivyo, Amekuwa yule yule kila mara kwa mwanadamu, ambalo lina maana kwamba Yeye kila mara Amekuwa na mtazamo ule ule. Yeye kila mara si mkarimu jinsi watu hufikiria, kama mama mwenye tajiriba ambaye watoto wake kila mara huwa katika sehemu ya mbele kabisa ya mawazo yake. Kwa kweli, kama Mungu hangetaka kutumia mbinu nyingi ili kulishinda joka kubwa jekundu, hakuna vile ambavyo Angejisalimisha kwa aibu kama hiyo, Akijiruhusu kutiishwa chini ya udhaifu wa mwanadamu. Kulingana na tabia ya Mungu, yote ambayo watu hufanya na kusema huchochea ghadhabu ya Mungu, na wao wanapaswa kuadibiwa. hina ni taifa la joka kubwa jekundu, na nchi ambayo kwayo Mungu mwenye mwili huishi, Mungu lazima amezee hasira Yake na kuwashinda watoto wote wa joka kubwa jekundu; ilhali Yeye kila mara Atawachukia sana watoto wa joka kubwa jekundu, yaani, Yeye kila mara Atayachukia sana yote ambayo hutoka kwa joka kubwa jekundu—na hili halitabadilika kamwe.

Hakuna ambaye amewahi kufahamu matendo yoyote ya Mungu, wala matendo Yake hayajawahi kutazamwa na chochote. Wakati ambapo Mungu alirudi Sayuni, kwa mfano, ni nani aliyefahamu hili? Hivyo, maneno kama “Naja polepole miongoni mwa wanadamu, na Naondoka taratibu. Kuna yeyote aliyewahi kuniona?” yanaonyesha kwamba mwanadamu kweli hukosa welekevu wa kukubali matukio ya ufalme wa kiroho. Zamani, Mungu alisema kwamba “jua ni la joto, mwezi ni wa mng’aro” wakati wa kurudi Kwake Sayuni. Kwa sababu watu bado wameshughulishwa na kurudi kwa Mungu Zayuni—kwa sababu bado hawajaliacha—Mungu hutamka moja kwa moja maneno “jua ni la joto, na mwezi ni wa mng’aro” ili kupatana na dhana za watu. Kutokana na hilo, wakati ambapo dhana za watu hugongwa na maneno ya Mungu, wao huona kwamba matendo ya Mungu ni ya ajabu sana, na huona kwamba maneno Yake ni ya maana sana na yasiyoweza kueleweka, na yasiyotambulikana kwa wote; hivyo, wao huliweka jambo hili pembeni kabisa, na kuhisi ubayana kidogo ndani ya roho zao, kana kwamba Mungu amerudi Sayuni tayari, na kwa hiyo watu hawazingatii sana jambo hili. Kuanzia wakati huo kuendelea, wao hukubali maneno ya Mungu kwa moyo mmoja na fikira moja, na hawawi na wasiwasi tena kwamba watafikwa na msiba mkuu baada ya kurudi kwa Mungu Sayuni. Ni wakati huo tu ndiyo huwa rahisi kwa watu kuyakubali maneno ya Mungu, kulenga zingatio lao lote kwa maneno ya Mungu, wakiachwa bila hamu ya kufikiria jambo lingine lolote.

Iliyotangulia: Sura ya 10

Inayofuata: Nyongeza: Sura ya 2

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp