Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa

Kuwa na ujuzi wa utendaji na kuwa na uwezo wa kuona wazi kazi ya Mungu—yote haya yanaonekana katika maneno Yake. Ni katika maneno ya Mungu tu ndio unaweza kupata nuru, hivyo unapaswa kujitayarisha na maneno Yake zaidi. Gawa ufahamu wako kutoka kwa maneno ya Mungu katika ushirika, na kupitia katika ushirika wako wengine wanaweza kupata nuru na unaweza kuwaongoza watu kwenye njia—njia hii ni ya utendaji. Kabla ya Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili yenu, kila mmoja wenu lazima kwanza ajitayarishe na maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kufanya—ni kipaumbele cha haraka. Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuwa na uwezo wa kula na kunywa maneno Yake. Kwa mambo ambayo huwezi kufanya, tafuta njia ya kutenda kutoka kwa maneno Yake, na angalia katika maneno Yake masuala yoyote ambayo hujui au matatizo yoyote uliyo nayo. Yafanye maneno ya Mungu yawe ruzuku yako, na uyaruhusu yaweze kukusaidia katika kutatua shida na matatizo yako ya vitendo; pia yaruhusu maneno Yake yawe msaada wako katika maisha. Mambo haya yanahitaji jitihada kwa upande wako. Katika kula na kunywa neno la Mungu, lazima ufanikishe matokeo; lazima uweze kuutuliza moyo wako mbele Yake, na kutenda kulingana na maneno Yake unapokabili masuala. Wakati hujakutana na masuala yoyote, kula na kunywa tu. Wakati mwingine unaweza kuomba na kutafakari juu ya upendo wa Mungu, kuwa na ushirika juu ya ufahamu wako wa maneno Yake, na kuwasiliana juu ya kupata nuru na kupata mwanga unaoupitia ndani yako mwenyewe na majibu ambayo umekuwa nayo unapoyasoma matamko haya. Aidha, unaweza kuwapa watu suluhisho. Hili pekee ndilo la utendaji. Lengo la kufanya hili ni kuyaruhusu maneno ya Mungu kuwa utoaji wako wa vitendo.

Kitika kipindi cha siku moja, unatumia saa ngapi kwa hakika mbele ya Mungu? Ni kiasi gani cha siku yako kinachotolewa kwa Mungu? Ni kiasi gani kinachopewa kwa mwili? Moyo wa mtu kuelekea daima kwa Mungu ndiyo hatua ya kwanza kwenye njia sahihi ya kufanywa mkamilifu na Mungu. Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua neno la Mungu kama kanuni, kama msingi. Hivyo, malengo yako na mtazamo wako yote yatakuwa mahali sahihi, na utakuwa mtu ambaye anapata sifa za Mungu mbele Zake. Wale ambao Mungu hupenda ni watu ambao ni kamili kabisa, watu ambao wamejitolea kwake na hakuna mwingine. Wale ambao Yeye huwachukia ni watu ambao wako shingo upande kumhusu, na ambao wanaasi dhidi Yake. Anawachukia wale wanaomwamini na daima wanataka kumfurahia, lakini hawawezi kujitumia kabisa kwa ajili Yake. Anawachukia wale wanaosema wanampenda lakini wanaomuasi mioyoni mwao. Anawachukia wale wanaotumia maneno matamu ili wafanye udanganyifu. Wale ambao hawajitolei kwa kweli kwa Mungu au hawana utiifu wa kweli Kwake ni watu wasio waaminifu; wao kwa kawaida ni wenye kiburi sana. Wale ambao hawawezi kuwa watiifu kwa kweli mbele ya Mungu wa kawaida, wa vitendo hata ni wenye kiburi zaidi, na hasa wao ni uzao mtiifu wa malaika mkuu. Wale ambao kwa kweli hujitumia wenyewe kwa ajili ya Mungu huweka nafsi zao zote mbele Yake. Wao hutii kwa kweli matamshi Yake yote, na wana uwezo wa kuweka maneno Yake katika matendo. Wao hufanya maneno ya Mungu kuwa msingi wa kuwepo kwao, na wanaweza kutafuta kwa kweli sehemu za matendo katika neno la Mungu. Huyu ni mtu ambaye kwa kweli anaishi mbele ya Mungu. Ikiwa unachofanya ni cha manufaa kwa maisha yako, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yake, unaweza kukidhi mahitaji yako ya ndani na upungufu ili tabia yako ya maisha inabadilishwa, basi hii itatimiza mapenzi ya Mungu. Ikiwa unatenda kulingana na mahitaji ya Mungu, ikiwa huuridhishi mwili lakini unaridhisha mapenzi Yake, huku ni kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Wakati unazungumza juu ya kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu kwa kweli zaidi, kunamaanisha unaweza kutekeleza wajibu wako na kukidhi mahitaji ya Mungu. Aina hizi tu za vitendo ndizo zinazoweza kuitwa kuingia katika uhalisi wa maneno Yake. Ikiwa una uwezo wa kuingia katika uhalisi huu, basi una ukweli. Huu ndio mwanzo wa kuingia katika uhalisi; lazima kwanza ufanye mazoezi haya na ni baada tu ya hayo ndio utakuwa na uwezo wa kuingia katika hali halisi za kina zaidi. Fikiria jinsi ya kushika amri na jinsi ya kuwa mwaminifu mbele ya Mungu. Usifikiri kila muda kuhusu wakati utakapoweza kuingia katika ufalme—ikiwa tabia yako haibadiliki, chochote unachokifikiria kitakuwa bure! Ili kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, lazima kwanza uweze kufanya mawazo yako na fikira zote ziwe kwa ajili ya Mungu—hili ni hitaji la msingi zaidi.

Kuna watu wengi ambao sasa wako katikati ya majaribio; hawaelewi kazi ya Mungu. Lakini Nakwambia—ikiwa huielewi, ni vyema usiihukumu. Labda kutakuwa na siku moja wakati ukweli utajulikana na kisha utaujua. Kutohukumu kutakuwa na manufaa kwako, lakini huwezi kusubiri tu bila kuonyesha hisia. Lazima utafute kuingia ndani kwa matendo—huyu tu ndiye mtu anayeingia kwa vitendo. Kwa sababu ya uasi wao, watu daima wanaendeleza mawazo kuhusu Mungu wa vitendo. Hii inahitaji watu wote kujifunza jinsi ya kuwa watiifu kwa sababu Mungu wa vitendo ni jaribio kubwa kwa wanadamu. Ikiwa huwezi kusimama imara, basi kila kitu kimekamilika; kama huna ufahamu wa utendaji wa Mungu wa vitendo, huwezi kukamilishwa na Mungu. Hatua muhimu katika ikiwa watu wanaweza kufanywa kuwa kamili au sio ni kuelewa uzoefu wa Mungu. Uzoefu wa Mungu mwenye mwili aliyekuja duniani ni jaribio kwa kila mtu. Ikiwa unaweza kusimama imara katika kipengele hiki basi wewe ni mtu anayemjua Mungu, na wewe ni mtu anayempenda kwa kweli. Ikiwa huwezi kusimama imara katika kipengele hiki, ikiwa unamwamini tu Roho na huwezi kuwa na imani kwa utendaji wa Mungu, basi bila kujali jinsi imani yako ilivyo kubwa kwa Mungu, haina maana. Ikiwa huwezi kumwamini Mungu anayeonekana, unaweza kuamini Roho wa Mungu? Je, hujaribu kumdanganya Mungu? Wewe si mtiifu kwa Mungu anayeonekana na Anayeshikika, kwa hivyo unaweza kumtii Roho? Roho haishikiki na haionekani, kwa hiyo wakati unasema kwamba unatii Roho wa Mungu, je, huzungumzi tu upuuzi? Cha msingi katika kushika amri ni kuwa na ufahamu wa Mungu wa vitendo. Mara tu ukiwa na ufahamu wa Mungu wa vitendo, utakuwa na uwezo wa kushika amri. Kuna vipengele viwili katika kuzishika: Kimoja ni kushikilia kiini kiini cha Roho Wake, na mbele ya Roho, kuwa na uwezo wa kukubali uchunguzi wa Roho; kingine ni kuwa na uwezo wa kuwa na ufahamu wa kweli wa mwili wenye mwili, na kufikia utii wa kweli. Ikiwa ni mbele ya mwili au mbele ya Roho, moyo wa kumtii na kumcha Mungu lazima udumishwe daima. Ni mtu wa aina hii pekee ndiye anayestahiki kukamilishwa. Ikiwa una ufahamu wa utendaji wa Mungu wa vitendo—yaani, kama umesimama imara katika jaribio hili—kisha hakuna kitu kitakuwa kikubwa sana kwako.

Watu wengine husema, “Amri ni rahisi kushika. Unahitaji tu kuja mbele ya Mungu, kusema kwa uwazi na kwa dhati bila kutumia mikono, na huku ni kushika amri.” Je, hiyo ni sawa? Kwa hivyo, ukifanya mambo machache bila Mungu kujua ambayo yanampinga, je, hilo linahesabika kama kushika amri? Lazima uwe na ufahamu wa kina kuhusu kushika amri kunajumuisha nini. Linahusiana na ikiwa una ufahamu wa kweli wa utandaji wa Mungu au la; ikiwa una uelewa wa kutenda, na hujikwai na kuanguka katika jaribio hili, hili linahesabika kama wewe kuwa na ushahidi wa nguvu. Kuwa na ushahidi mkuu kwa Mungu hasa kunahusiana na ikiwa una ufahamu wa Mungu wa vitendo au la, na ikiwa unaweza au huwezi kutii mbele ya mtu huyu ambaye ni wa kawaida na kutii mpaka hata kifo. Ikiwa unamshuhudia Mungu kwa kweli kupitia utii huu, hiyo inamaanisha kuwa umepatwa na Mungu. Kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo, na kuwa bila malalamiko mbele Yake, kutohukumu, kutokashifu, kutokuwa na mawazo, na kutokuwa na makusudi mengine—kwa njia hii Mungu atapata utukufu. Utiifu mbele ya mtu wa kawaida ambaye anadharauliwa na mwanadamu na kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo bila mawazo yoyote—huu ni ushuhuda wa kweli. Uhakika ambao Mungu anataka watu waingie ndani ni kwamba unaweza kutii maneno Yake, unaweza kuweka maneno Yake katika matendo, kuweza kuinama mbele ya Mungu wa vitendo na kujua upotovu wako mwenyewe, kuweza kufungua moyo wako mbele Yake, na mwishowe kupatwa na Yeye kupitia maneno haya Yake. Mungu hupata utukufu wakati maneno haya yanakushinda na kukufanya uwe mtiifu kikamilifu Kwake; kwa njia hii Anamwaibisha Shetani na kukamilisha kazi Yake. Wakati huna mawazo yoyote ya utendaji wa Mungu mwenye mwili, yaani, unaposimama imara katika jaribio hili, basi wewe huwa na ushuhuda mzuri. Ikiwa kuna siku ambayo uko na uelewa mkamilifu juu ya Mungu wa matendo na unaweza kutii mpaka kifo kama Petro, utapatwa na Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Kile ambacho Mungu hufanya ambacho hakilingani na mawazo yako ni jaribio kwako. Ikiwa kingelingana na mawazo yako, hakingekuhitaji kuteseka au kusafishwa. Ni kwa sababu kazi Yake ni ya vitendo sana na kwamba hailingani na mawazo yako ndiyo inakuhitaji kuyaachilia mawazo yako. Hii ndiyo sababu ni jaribio kwako. Ni kwa sababu ya utendaji wa Mungu ndiyo maana watu wote wako katikati ya majaribio; kazi Yake ni ya vitendo, siyo ya kawaida. Kwa kuelewa kikamilifu maneno Yake ya vitendo, matamshi Yake ya vitendo bila mawazo yoyote, na kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli zaidi ndivyo kazi Yake ilivyo ya vitendo zaidi, utapatwa na Yeye. Kundi la watu ambao Mungu atapata ni wale wanaomjua Mungu, yaani, ambao wanajua utendaji Wake, na hata zaidi ni wale wanaoweza kutii kazi ya vitendo ya Mungu.

Wakati wa Mungu akiwa ndani ya mwili, utii Anaohitaji kwa watu sio ule ambao watu wanafikiri—kutohukumu au kutopinga. Badala yake, Anahitaji kwamba watu wafanye maneno Yake kuwa kanuni yao ya maisha na msingi wa kuendelea kuishi kwao, kwamba wanaweka kikamilifu kiini cha maneno Yake katika matendo, na kwamba wanayaridhisha kabisa mapenzi Yake. Kipengele kimoja cha kuhitaji watu kumtii Mungu mwenye mwili kinahusu kuweka maneno Yake katika matendo, huku kipengele kingine kinarejelea kuwa na uwezo wa kutii ukawaida na utendaji Wake. Haya yote mawili lazima yawe bila shaka. Wale ambao wanaweza kutimiza vipengele hivi viwili ni wale wote ambao wana moyo wa upendo wa kweli kwa Mungu. Wote ni watu ambao wamepatwa na Mungu, na wote wanampenda Mungu kama wanavyopenda maisha yao wenyewe. Mungu mwenye mwili ana ubinadamu wa kawaida na wa utendaji katika kazi Yake. Kwa njia hii, gamba Lake la nje la ubinadamu wa kawaida na wa utendaji linakuwa jaribio kubwa kwa watu; linakuwa tatizo lao kubwa. Hata hivyo, ukawaida na utendaji wa Mungu hauwezi kuepukwa. Alijaribu kila kitu ili kupata suluhisho lakini hatimaye hakuweza kujiondoa Mwenyewe kutoka kwenye gamba la nje la ubinadamu Wake wa kawaida kwa sababu, hata hivyo, Yeye ni Mungu aliyekuwa mwili, si Mungu wa Roho aliye mbinguni. Yeye si Mungu ambaye watu hawawezi kumuona, lakini Mungu aliyevaa gamba la kiumbe mmoja. Katika hili, kujiondoa Mwenyewe kutoka katika gamba la ubinadamu Wake wa kawaida bila shaka hakuwezi kuwa rahisi. Kwa hivyo bila kujali chochote, bado Yeye hufanya kazi ambayo Yeye hutaka kufanya kutoka kwa mtazamo wa mwili. Kazi hii ni maonyesho ya Mungu wa kawaida na wa matendo, kwa hivyo inawezekanaje kuwa sawa kwa watu kutotii? Ni nini duniani ambacho watu wanaweza kufanya kuhusu matendo ya Mungu? Anafanya chochote Anachotaka kufanya; chochote Anachofurahia kiko jinsi kilivyo. Ikiwa watu hawatii, wanaweza kuwa na mpango gani mwingine thabiti? Hadi sasa, bado ni utiifu tu ambao unaweza kuwaokoa watu; hakuna mawazo mengine ya ujanja. Ikiwa Mungu anataka kuwajaribu watu, wanaweza kufanya nini kuhusu hilo? Lakini yote haya si wazo la Mungu wa mbinguni; ni wazo la Mungu mwenye mwili. Anataka kufanya hili, hivyo hakuna mtu anayeweza kulibadilisha. Mungu aliye mbinguni haingilii kati kile Anachofanya, kwa hivyo watu hawapaswi kumtii hata zaidi? Ingawa Yeye ni wa matendo na wa kawaida, Yeye ni Mungu aliyekuwa mwili kikamilifu. Kulingana na mawazo Yake mwenyewe, Anafanya chochote Anachotaka. Mungu aliye mbinguni Amemkabidhi Yeye kazi zote; lazima utii chochote Anachofanya. Ingawa Ana ubinadamu na Yeye ni wa kawaida sana, yote haya ni yale ambayo Amepanga kwa makusudi, kwa hivyo watu wanaweza kumtazamaje, macho wazi kwa kutokubali? Anataka kuwa wa kawaida, kwa hivyo Yeye ni wa kawaida. Anataka kuishi ndani ya ubinadamu, hivyo Anaishi ndani ya ubinadamu. Anataka kuishi ndani ya uungu, hivyo anaishi ndani ya uungu. Watu wanaweza kuona hilo jinsi wanavyotaka. Mungu daima Atakuwa Mungu na watu daima watakuwa watu. Kiini Chake hakiwezi kukataliwa kwa sababu ya maelezo madogo, wala Hawezi kusukumwa nje ya “nafsi” ya Mungu kwa sababu ya kitu kidogo. Watu wana uhuru wa binadamu, na Mungu ana hadhi ya Mungu; haya hayaingiliani. Je, watu hawawezi kumpa Mungu uhuru kidogo? Je, hawawezi kumvumilia Mungu kuwa wa kawaida zaidi? Usiwe makini sana na Mungu! Kila mtu anapaswa kuwa na uvumilivu kwa kila mmoja; basi si kila kitu kitakuwa kimesuluhishwa? Je, bado kungekuwa na kufarakana kokote? Ikiwa mtu hawezi kuvumilia kitu kidogo kama hicho, anawezaje hata kufikiria kuwa mtu mkarimu, mwanadamu wa kweli? Siye Mungu anayewapa wanadamu wakati mgumu, lakini ni wanadamu wanaompa Mungu wakati mgumu. Daima wanashughulikia vitu kwa kufanya kitu kidogo kionekane kikubwa—kwa kweli wao hufanya kitu kisicho cha maana kuwa kizito, na hiyo si lazima! Wakati Mungu anafanya kazi katika ubinadamu wa kawaida na wa matendo, kile Anachofanya si kazi ya wanadamu, bali ni kazi ya Mungu. Hata hivyo, watu hawaoni kiini cha kazi Yake—daima wanaona gamba la nje la ubinadamu Wake. Hawajaona kazi kubwa kama hiyo, lakini wanasisitiza kuona ubinadamu wa kawaida wa Mungu na hawaachilii wazo hili. Je, hii inawezaje kuitwa kumtii Mungu? Mungu mbinguni sasa “amegeuka kuwa” Mungu duniani, na Mungu duniani sasa ni Mungu wa mbinguni. Haijalishi kama sura Yao ya nje ni sawa au jinsi kazi Yao ilivyo. Kwa ujumla, Yeye anayefanya kazi ya Mungu mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Lazima utii bila kujali ikiwa unataka au la—hiki si kitu ambacho unapata kuchagua! Mungu lazima atiiwe na watu, na watu lazima wamtii kabisa Mungu bila ya kujifanya hata kidogo.

Kikundi cha watu ambao Mungu mwenye mwili Anataka kuwapata leo ni wale wanaokubali mapenzi Yake. Watu wanahitaji tu kutii kazi Yake, sio daima kujishughulisha na mawazo ya Mungu aliye mbinguni, waishi ndani ya hali isiyo dhahiri, au kufanya mambo kuwa magumu kwa Mungu mwenye mwili. Wale ambao wanaweza kumtii ni wale wanaoyasikia kabisa maneno Yake na kutii mipango Yake. Watu hawa hawajali kamwe jinsi Mungu mbinguni alivyo kwa kweli au ni kazi ya aina gani Mungu wa mbinguni Anafanya sasa kwa wanadamu, lakini wao humpa Mungu aliye duniani mioyo yao kabisa na kuweka nafsi zao zote mbele Yake. Kamwe hawazingatii usalama wao wenyewe, wala hawalalamiki kamwe juu ya ukawaida na utendaji wa Mungu katika mwili. Wale wanaomtii Mungu katika mwili wanaweza kukamilishwa na Yeye. Wale wanaomwamini Mungu mbinguni hawatapata kitu. Hii ni kwa sababu si Mungu mbinguni, lakini ni Mungu hapa duniani ndiye Anayetoa ahadi na baraka juu ya watu. Watu hawapaswi daima kumtukuza Mungu aliye mbinguni na kumwona Mungu duniani kama mtu wa wastani. Hii si haki. Mungu mbinguni ni mkuu na wa ajabu na mwenye hekima ya ajabu, lakini hii haipo kabisa. Mungu duniani ni wa wastani sana na asiye na maana; Yeye pia ni wa kawaida sana. Hana mawazo ya ajabu au vitendo vya kimiujiza. Anatenda tu na kuongea kwa njia ya kawaida na ya matendo. Ingawa Hazungumzi kwa njia ya ngurumo au kuita upepo na mvua, Yeye kwa kweli ni mwili wa Mungu aliye mbinguni, na kwa kweli ni Mungu anayeishi kati ya wanadamu. Watu hawapaswi kumtukuza yule wanayeweza kumwelewa na ambaye analingana na mawazo yao wenyewe kama Mungu, au kumwona Yeye ambaye hawawezi kumkubali na kabisa hawawezi kufikiria kama wa chini. Yote haya ni uasi wa watu; yote ni chanzo cha upinzani wa wanadamu kwa Mungu.

Iliyotangulia: Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Inayofuata: Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp