Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wako unaegemea upande mmoja sana. Bila kujua hali yako ya kweli au kufahamu kanuni za ukweli, haiwezekani kufikia mabadiliko katika tabia. Bila kujua kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu au kuelewa matokeo yatokayo hapo, itakuwa vigumu kutambua kazi ya pepo wabaya. Lazima ufunue kazi ya pepo wabaya na mawazo ya wanadamu na uende moja kwa moja kwenye kiini cha suala hili; lazima pia uonyeshe mikengeuko mingi katika utendaji wa watu au matatizo katika kumwamini Mungu ili waweze kuyatambua. Kwa kiwango cha kidogo sana, lazima usiwafanye kuhisi hasi au wasiojishughulisha. Hata hivyo, lazima uelewe shida ambazo zipo kwa watu wengi bila upendeleo, hupaswi kuwa bila busara au “ujaribu kumfunza nguruwe kuimba”; hiyo ni tabia ya upumbavu. Ili kutatua matatizo mengi ya wanadamu, lazima uelewe elimumwendo ya kazi ya Roho Mtakatifu, lazima uelewe jinsi Roho Mtakatifu anavyotekeleza kazi kwa watu tofauti, lazima uelewe matatizo ya wanadamu, upungufu wa wanadamu, ubaini masuala muhimu ya shida, na kufikia chanzo cha tatizo, bila mkengeuko au makosa. Ni mtu wa aina hii tu ndiye aliyestahiki kuratibu kumhudumia Mungu.

Bila kujali kama unaweza kuelewa masuala muhimu na kuona kwa dhahiri mambo mengi hutegemea uzoefu wako binafsi. Namna ambavyo unapitia ndiyo pia namna ambavyo unaowaongoza wengine. Ikiwa unaelewa barua na mafundisho, basi unawaongoza wengine kuelewa barua na mafundisho. Njia ambayo unapitia ukweli wa maneno ya Mungu ndiyo njia ambayo unawaongoza wengine kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ikiwa unaweza kuelewa ukweli mwingi na kuona kwa dhahiri mambo mengi katika maneno ya Mungu, basi unaweza kuwaongoza wengine kuelewa ukweli mwingi, na wale unaowaongoza watakuwa na ufahamu wa wazi wa maono. Ukilenga kushika hisia zisizo za kawaida, basi wale unaowaongoza pia watalenga hisia zisizo za kawaida. Ikiwa unapuuza matendo na kusisitiza kuzungumza, basi wale unaowaongoza pia watazingatia kuzungumza, bila utekelezaji wowote, bila mbadiliko wowote katika tabia zao, na watakuwa tu na shauku kwa nje, bila kutenda ukweli wowote. Wanadamu wote huwatolea wengine kile walicho nacho wenyewe. Aina ya mtu huamua njia ambayo anawaongoza wengine kuingia, na aina ya mtu huamua aina ya watu anaowaongoza. Ili kuwa wa kufaa kwa matumizi ya Mungu, hamhitaji tu kuwa na matarajio, lakini mnahitaji pia nuru nyingi kutoka kwa Mungu, mwongozo kutoka kwa maneno ya Mungu, kushughulikiwa na Mungu, na usafishaji wa maneno Yake. Hili likiwa msingi, katika nyakati za kawaida, mnapaswa kutilia maanani uchunguzi, mawazo, kutafakari na hitimisho, na mjishughulishe na uingiaji au uondolewaji inavyopasa. Hizi zote ni njia za kuingia kwenu katika uhalisi na zote ni za msingi—hii ndiyo njia ambayo Mungu hufanya kazi. Ikiwa unapaswa kuingia katika njia hii ambayo Mungu hufanya kazi, basi utakuwa na fursa ya kukamilishwa na Mungu kila siku. Na wakati wowote, bila kujali kama ni mazingira magumu au mazingira mazuri, kama unajaribiwa au unashawishiwa, kama unafanya kazi au la, kama unaishi maisha kama mtu binafsi au kwa pamoja, utapata fursa za kukamilishwa na Mungu kila wakati, bila kukosa hata moja yao. Utakuwa na uwezo wa kugundua zote, na kwa njia hii utakuwa umepata siri ya kupitia maneno ya Mungu.

Iliyotangulia: Mtu Anayepata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Tayari Kutenda Ukweli

Inayofuata: Kuhusu Uzoefu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp