Sura ya 20

Mungu aliwaumba wanadamu wote, na amewaongoza wanadamu wote mpaka leo. Hivyo, Mungu anajua yote yafanyikayo miongoni mwa wanadamu: Anajua uchungu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, Anaelewa utamu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, na kwa hiyo kila siku Yeye hufafanua hali za maisha za wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, hushughulikia udhaifu na upotovu wa wanadamu wote. Si mapenzi ya Mungu kwamba wanadamu wote watupwe jahanamu, au kwamba wanadamu wote waokolewe. Kila mara huwa kuna kanuni kwa matendo ya Mungu, lakini hakuna anayeweza kuelewa sheria za yote Afanyayo. Watu wanapofahamu uadhama na ghadhabu ya Mungu, Mungu hubadilisha sauti mara moja kuwa ya huruma na upendo, lakini watu wanapokuja kujua huruma na upendo wa Mungu, Anaibadilisha sauti mara moja tena, Akiyafanya maneno Yake kuwa magumu kula kana kwamba ni kuku aliye hai. Katika maneno yote ya Mungu, mwanzo haujawahi kurudiwa kamwe, na maneno Yake yoyote hayajawahi kamwe kuzungumziwa kulingana na kanuni za matamko ya jana; hata sauti haifanani, wala hakuna uhusiano wowote katika maudhui—haya yote huwafanya watu wahisi wamekanganywa hata zaidi. Hii ni hekima ya Mungu, na ufichuzi wa tabia Yake. Yeye hutumia sauti na mtindo wa kunena Kwake kutawanya dhana za watu, ili kumtatiza Shetani, Akimnyang’anya Shetani nafasi ya kutia sumu matendo ya Mungu. Ajabu ya matendo ya Mungu husababisha akili za watu kuachwa zikiwa zimeshtushwa na maneno ya Mungu. Wanaweza kuupata mlango wao wa mbele kwa shida, au hata hawajui wakati wanaotarajiwa kula au kupumzika, hivyo wanatimiza kweli “kuacha kulala na kula ili kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu.” Lakini hata wakati huu, Mungu bado haridhiki na hali za sasa, na kila mara huwa Amemkasirikia mwanadamu, Akimlazimisha kuonyesha moyo wake halisi. La sivyo, watu “wangetii” mara moja na kuwa wazembe, wakionyeshwa huruma kidogo tu na Mungu. Huu ni uduni wa mwanadamu; hawezi kubembelezwa, lakini lazima apigwe au alazimishwe ili asonge. “Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao.” Hivyo ndivyo hali za wote walio duniani zilivyo. Hivyo, bila kazi ya mitume au viongozi, watu wote wangekuwa wametawanyika kitambo sana, na kwa hiyo, kotekote katika enzi, hakujakuwa na ukosefu wa mitume na manabii.

Katika matamko haya, Mungu anazingatia kwa hali maalum kufanya muhtasari wa hali za maisha za wanadamu wote. Maneno kama “Maisha ya mwanadamu hayana joto hata kidogo, na hayana dalili yoyote ya binadamu wala mwanga—lakini daima amekuwa mwenye kujishughulisha na mwenyewe, akivumilia maisha yasiyo ya thamani ambayo yeye huenda hapa na pale akiharakisha kufanya mambo bila kufikia kitu chochote. Kwa haraka sana, siku ya kufa inakaribia, na mtu anakufa kifo cha uchungu” yote ni ya aina hii. Ni kwa nini Mungu ameongoza kuishi kwa wanadamu mpaka leo, na bado pia Anafichua utupu wa maisha katika ulimwengu wa mwanadamu? Na kwa nini Anafafanua maisha yote ya watu wote kama “kufika kwa haraka na kuondoka kwa haraka”? Huu, inaweza kusemwa, wote ni mpango wa Mungu, wote umeamuliwa na Mungu, na kwa hivyo, kwa namna moja unaashiria jinsi Mungu anadharau yote isipokuwa maisha katika uungu. Ingawa Mungu aliwaumba wanadamu wote, Hajawahi kamwe kufurahishwa na maisha ya wanadamu wote, na kwa hiyo Yeye huwaruhusu tu wanadamu waishi chini ya upotovu wa Shetani. Baada ya wanadamu kupitia mchakato huu, Atawaangamiza au kuwaokoa wanadamu, na hivyo mwanadamu atatimiza maisha duniani ambayo si matupu. Yote haya ni sehemu ya mpango wa Mungu. Na kwa hiyo, huwa kila mara kuna matamanio ndani ya fahamu ya mwanadamu, jambo ambalo limesababisha kutokuwa na mtu anayekufa kifo maasumu kwa furaha—lakini wale ambao tu hutimiza matamanio haya ni watu wa siku za mwisho. Leo, bado watu huishi katikati ya utupu usiogeuka na bado wanangoja matamanio haya yasiyoonekana: “Ninapoufunika uso Wangu kwa mikono Yangu, na kuwasukuma watu chini ya ardhi, mara moja wao hupungukiwa na pumzi, na ni vigumu waweze kuishi. Wao wote hunililia, wakiwa wenye hofu kwamba Nitawaangamiza, kwa maana wote wanatamani kutazama siku ambayo Nitatukuzwa.” Hivyo ndivyo hali za watu zilivyo leo. Wote huishi katika “ombwe,” bila “oksijeni,” ambalo huwafanya kuwa na ugumu kupumua. Mungu hutumia matamanio ndani ya fahamu ya mwanadamu ili kuwasaidia wanadamu wote kuendelea kuishi; la sivyo, wote “wangeondoka nyumbani ili kuwa watawa wa kiume,” kwa sababu hiyo wanadamu wote wangetoweka, na wangemalizika. Hivyo, ni kwa sababu ya ahadi ambayo Mungu alimpa mwanadamu ndio mwanadamu ameendelea kuishi mpaka leo. Huu ni ukweli, lakini mwanadamu hajawahi kugundua sheria hii, na kwa hiyo hajui ni kwa nini yeye “anahofu sana kwamba kifo kitamjia mara ya pili.” Kwa kuwa ni binadamu, hakuna yeyote ambaye ana ujasiri wa kuendelea kuishi, wala hakuna yeyote ambaye amewahi kuwa na ujasiri wa kufa, na hivyo Mungu asema kwamba watu “hufa kifo cha uchungu.” Hivyo ndivyo hali halisi miongoni mwa wanadamu ilivyo. Labda, katika matarajio yao, watu wengine wamekumbana na vizuizi na wakawaza juu ya kifo, lakini mawazo haya hayajawahi kufaulu; labda, wengine wamewaza juu ya kifo kwa sababu ya ugomvi wa familia, lakini wanawajali wapendwa wao, na wanabaki kutoweza kutimiza matamanio yao; na labda, wengine wamewaza juu ya kifo kwa sababu ya mapigo kwa ndoa yao, lakini hawako radhi kupitia hilo. Hivyo, watu hufa wakiwa na majonzi au majuto ya milele ndani ya mioyo yao. Hivyo ndivyo hali mbalimbali za watu wote zilivyo. Nikitazama juu ya ulimwengu mpana wa mwanadamu, watu huja na kwenda katika mkondo usiokuwa na mwisho, na ingawa wanahisi kwamba kungekuwa na raha zaidi kwa kifo ikilinganishwa na kuishi, wao bado huendelea kusema maneno matupu, na kamwe hakuna yeyote ambaye amewahi kuongoza kwa mfano, kwa kufa na kufufuka, na kuwaambia walio hai namna ya kufurahia furaha ya kifo. Watu ni mafidhuli duni: Hawana haya wala kujiheshimu, nao daima hukosa kutimiza ahadi zao. Katika mpango Wake, Mungu alijaalia kikundi cha watu ambao wangefurahia ahadi Zake, na hivyo Mungu asema, “wengi wameishi katika mwili, na wengi wamekufa na wamezaliwa upya duniani. Hata hivyo kamwe hakuna yeyote kati yao aliyepata nafasi ya kufurahia baraka za ufalme leo.” Wote ambao wanafurahia baraka za ufalme leo wamejaaliwa na Mungu tangu Alipouumba ulimwengu. Mungu alipanga ili roho hizi ziishi ndani ya mwili katika siku za mwisho, na hatimaye, Mungu atalipata kundi hili la watu, na kuwapangia kuwa Sinim. Kwa sababu, hususa, roho za watu hawa ni malaika, Mungu asema “Je, Nimetoweka kabisa katika roho ya mwanadamu?” Kwa kweli, watu wanapoishi katika mwili, wanabaki kutojua mambo ya ulimwengu wa kiroho. Kutokana na maneno haya rahisi hali ya moyo wa Mungu “mwanadamu kunipiga macho ya hadhari”—mhemko wa Mungu unaweza kuonekana. Katika maneno haya rahisi, taaluma tata ya Kisaikolojia ya Mungu inaelezeka. Tangu wakati wa uumbaji mpaka leo, ndani ya moyo wa Mungu daima kumekuwa na majonzi yanayoandamana na ghadhabu na hukumu, kwani watu walio duniani hawana uwezo wa kuyajali mapenzi ya Mungu, kama tu asemavyo Mungu, “Mwanadamu ni kama kiumbe katili cha mlimani.” Lakini Mungu asema pia, “Siku itawadia ambapo mwanadamu ataogelea kuja upande Wangu kutoka katikati ya bahari kuu, ili aweze kufurahia mali yote ya dunia na kuacha hatari ya kumezwa na bahari.” Huu ndio ufanikishaji wa mapenzi ya Mungu, na pia unaweza kuelezwa kama mwelekeo usioepukika, na unaashiria ufanikishaji wa kazi ya Mungu.

Ufalme utakaposhuka duniani kabisa, watu wote watapata tena mfano wao wa asili. Hivyo, Mungu asema, “Nafurahia kutoka juu ya kiti Changu cha enzi, Naishi miongoni mwa nyota. Na malaika wananipa nyimbo mpya na dansi mpya. Udhaifu wao hausababishi machozi kutiririka nyusoni mwao tena. Sisikii tena, mbele Yangu, sauti za malaika wakilia, na hakuna tena anayeninung’unikia kuwa ana shida.” Hili linaonyesha kwamba siku ambayo Mungu atapata utukufu kamili ndiyo siku ambayo mwanadamu atafurahia pumziko lake; watu hawakimbii huku na huko tena kutokana na usumbufu wa Shetani, dunia inaacha kuendelea mbele, na watu wanaishi katika pumziko—kwa kuwa idadi kubwa mno ya nyota angani zinafanywa upya, na jua, mwezi, na nyota, na kadhalika, na milima na mito yote iliyo mbinguni na duniani, vyote vinabadilishwa. Na kwa kuwa mwanadamu amebadilika, na Mungu amebadilika, kwa hiyo, pia, vitu vyote vinabadilika. Hili ndilo lengo la msingi la mpango wa usimamizi wa Mungu, na ule ambao utatimizwa hatimaye. Lengo la Mungu katika kuzungumza maneno haya yote ni hasa kwa mwanadamu kumjua Yeye. Watu hawaelewi amri za utawala za Mungu. Yote ambayo Mungu hufanya yametungwa na kupangwa na Mungu Mwenyewe, na Mungu hayuko radhi kumwacha mtu yeyote aingilie; badala yake, Yeye huwaruhusu watu kuona kwamba yote yamepangwa na Yeye na hayawezi kutimizwa na mwanadamu. Ingawa mwanadamu anaweza kuliona, au kuliona kuwa gumu kuwaza, yote yanadhibitiwa na Mungu pekee, na Mungu hatamani litiwe doa na wazo hata kidogo la mwanadamu. Mungu kwa kweli Hatawasamehe wowote wanaoshiriki, hata kwa kiasi kidogo; Mungu ni Mungu anayemwonea mwanadamu wivu, na inaonekana Roho wa Mungu hasa ni mwepesi wa kuhisi katika suala hili. Hivyo, yeyote aliye na nia hata kidogo ya kuingilia atazongwa mara moja na miale ya moto ya Mungu ya kuangamiza, ikimgeuza kuwa majivu ndani ya moto. Mungu hawaruhusu watu kuonyesha vipaji vyao jinsi wapendavyo, kwani wote walio na vipaji hawana uzima; hivi vipaji vya kudhaniwa humhudumia Mungu tu, na vinatokana na Shetani, na hivyo vinadharauliwa hasa na Mungu, Asiyeruhusu hili. Hata hivyo mara nyingi ni watu wasio na uhai ndio wanaweza kushiriki katika kazi ya Mungu, na, hata zaidi, kushiriki kwao huwa hakugunduliwi, kwani kunafichwa na vipaji vyao. Kotekote katika enzi, wale ambao wana vipawa hawajawahi kusimama imara, kwani hawana uzima, na hivyo wanakosa nguvu zozote za kupinga. Hivyo, Mungu asema, “Kama Sizungumzi waziwazi, mwanadamu kamwe hataacha kufanya upumbavu kamwe, na ataanguka katika kuadibu Kwangu bila kujua—kwa kuwa mwanadamu hanijui katika nafsi ya mwili Wangu.” Wote ambao ni wa mwili na damu wanaongozwa na Mungu, lakini pia wanaishia katika kifungo cha Shetani, na kwa hiyo watu hawajawahi kuwa na uhusiano wa kawaida kati yao, kama ni kwa sababu ya tamaa, au kuabudu, au utaratibu wa mazingira yao. Mahusiano yasiyo ya kawaida kama hayo ndiyo Mungu anayachukua zaidi ya yote, na hivyo ni kwa sababu ya mahusiano kama hayo ndiyo maneno kama “Kile Ninachotaka ni viumbe vilivyo hai ambao wamejawa na uzima, si maiti ambazo zimegubika katika kifo. Kwa kuwa Ninaketi mezani pa ufalme, Nitatoa amri kwa watu wote duniani ili wapate ukaguzi Wangu” yanatoka kinywani mwa Mungu. Mungu anapokuwa juu ya ulimwengu mzima, kila siku Yeye huangalia kwa makini kila kitendo cha wale wa mwili na damu, na Hajawahi kumpuuza hata mmoja wao. Haya ni matendo ya Mungu. Na kwa hiyo, Nawasihi watu wote wachunguze fikira, mawazo, na matendo yao wenyewe. Siwataki muwe ishara ya aibu kwa Mungu, bali dhihirisho la utukufu wa Mungu, kwamba katika matendo, maneno, na maisha yenu yote, msiwe shabaha ya mizaha ya Shetani Haya ni matakwa ya Mungu kwa watu wote.

Iliyotangulia: Sura ya 19

Inayofuata: Sura ya 21

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp