Sura ya 19

Inaonekana kwamba katika mawazo ya watu, Mungu ni wa fahari sana naye Haeleweki. Ni kana kwamba Mungu haishi miongoni mwa wanadamu, kana kwamba anawadharau watu kwa sababu Yeye ni wa fahari sana. Mungu, hata hivyo, Huziseta fikira za wanadamu na kuzifuta zote, Akizika fikira zao zote ndani ya “makaburi” ambamo zinageuka kuwa majivu. Mtazamo wa Mungu kwa fikira za wanadamu ni sawa na mtazamo Wake kwa wafu, Akiwafafanua apendavyo. Ni kana kwamba hakuna athari kutokana na fikira. Kwa hiyo tangu uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa, Mungu amekuwa Akifanya kazi hii na Hajaacha kamwe. Kwa sababu ya mwili, wanadamu hupotoshwa na Shetani, na kwa sababu ya matendo ya Shetani duniani, wanadamu huunda kila aina ya fikira wakati wa uzoefu wao. Huu unaitwa “muundo asilia.” Hii hatua ya kazi ni sehemu ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani, kwa hiyo mbinu ya kazi ya Mungu imefikia kilele chake, naye Anazidisha mafunzo Yake kwa mwanadamu ili waweze kufanywa wakamilifu katika kazi Yake ya mwisho, na mapenzi ya Mungu yataridhishwa mwishowe. Awali, kulikuwa tu na kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu miongoni mwa wanadamu, lakini hakuna maneno yaliyonenwa na Mungu Mwenyewe. Wakati ambapo Mungu alinena kwa sauti Yake Mwenyewe, kila mtu aligutushwa, na leo maneno Yake yanakanganya hata zaidi. Ni vigumu hata zaidi kuelewa maana ya maneno Yake, na wanadamu wanaonekana kuwa katika hali ya kuvutiwa sana, kwa sababu asilimia hamsini ya maneno Yake huja katikati ya alama za kudondoa. “Ninapozungumza, mwanadamu husikiza sauti Yangu kwa makini; lakini Ninapokoma kuzungumza, anaanza tena ‘biashara’ yake.” Kuna neno katika hilo fungu lililo katika dondoo. Kadri maneno ya Mungu yalivyo ya kuchekesha, ndivyo yanavyoweza kuwavutia zaidi watu kuyasoma. Kipengele kimoja ni kwamba watu wanaweza kukubali kushughulikiwa wakati ambapo wamepumzika. Kipengele cha msingi ni kuwazuia watu wengi kuvunjika moyo au kusikitika kwa sababu hawafahamu maneno ya Mungu. Hii ni mbinu katika vita vya Mungu dhidi ya Shetani. Ni kwa njia hii tu ndiyo watu watavutiwa na maneno ya Mungu na bado wayazingatie hata wanapokanganyikiwa. Lakini pia kuna uzuri mwingi katika maneno yote ambayo hayako katika dondoo, na kwa hiyo yanatambulika zaidi na huwafanya watu kuyapenda maneno ya Mungu hata zaidi, yakiwaruhusu kuhisi utamu wa maneno Yake ndani ya mioyo yao wenyewe. Kwa kuwa maneno ya Mungu huja katika miundo mingi mbalimbali nayo ni mazuri na tofauti, na kwa kuwa hakuna urudiaji wa majina miongoni mwa maneno mengi ya Mungu, katika hisia yao ya tatu, watu wote huamini kuwa Mungu ni mpya daima naye si wa kale kamwe. Kwa mfano: “Simtaki mwanadamu awe ‘mtumiaji’ tu, lakini Namtaka awe ‘mzalishaji’ anayeweza kumshinda Shetani.” Maneno “mtumiaji” na “mzalishaji” katika sentensi hiyo yana maana sawa na maneno mengine yaliyonenwa katika nyakati za awali, lakini Mungu si mgumu. Bali, Humfanya mwanadamu afahamu upya Wake, na hivyo kuthamini upendo wa Mungu. Ucheshi katika hotuba ya Mungu una hukumu Yake na madai Yake kwa mwanadamu. Kwa kuwa maneno yote ya Mungu yana malengo, yote yana maana, ucheshi Wake haukusudiwi tu kuleta raha katika mazingira au kuwafanya watu wapasue waangue kicheko, au kulegeza misuli yao tu. Bali, ucheshi wa Mungu unanuiwa kumkomboa mwanadamu kutoka kwa kifungo cha miaka elfu tano na kamwe asifungwe tena, ili aweze kukubali maneno ya Mungu vizuri zaidi. Mbinu ya Mungu ni “kijiko kimoja cha sukari husaidia dawa kumezeka”; Huwa Hamlazimishi wanadamu kumeza dawa chungu. Kuna uchungu ndani ya kilicho tamu, na pia utamu ndani ya kilicho chungu.

“Mwangaza hafifu unapoanza kuonekana Mashariki, watu wote ulimwenguni kwa sababu hii wanaupa kipaumbele mwangaza ulio Mashariki. Bila kujawa na usingizi, wanadamu huenda kuchunguza chanzo cha mwangaza wa mashariki, lakini kwa sababu ya vikwazo vya uwezo wa binadamu, hakuna anayeweza kuona mahali unapotokea mwangaza.” Hiki ndicho kinachofanyika kila mahali ulimwenguni, sio tu miongoni mwa wana na watu wa Mungu. Makundi ya kidini na wasioamini wote hupitia athari hii. Wakati ambapo nuru ya Mungu hung’aa, moyo wa kila mtu hubadilika polepole, na wao huanza kugundua bila kujua kwamba kuishi hakuna maana, kwamba maisha ya binadamu hayana thamani. Wanadamu hawafuatilii siku za baadaye, hawafikirii kuhusu kesho, au kuwa na wasiwasi kuhusu kesho, bali hushikilia wazo kwamba wanapaswa kula na kunywa zaidi wakati bado ni “vijana,” kwamba itakuwa imestahili mara tu siku ya mwisho itakapowadia. Mwanadamu hana hamu ya kuuweka ulimwengu katika mpango. Nguvu za upendo wa mwanadamu kwa ulimwengu ziliibwa na “shetani,” lakini hakuna ajuaye sababu ni gani, na wanakimbia tu nyuma na mbele wakiarifiana, kwa sababu siku ya Mungu bado haijafika. Siku moja, kila mtu ataona majibu kwa mafumbo yote yasiyoeleweka. Hii ni maana ya kweli ya maneno ya Mungu kwamba “mwanadamu atazinduka kutoka usingizi na ndoto, na hapo tu ndipo atakapotambua kwamba siku Yangu inawadia polepole duniani.” Wakati huo utakapofika, watu wote ambao ni wa Mungu watakuwa kama majani ya kijani kibichi “yakisubiri kutakasa sehemu yao binafsi Kwangu wakati Niko duniani.” Watu wengi sana miongoni mwa watu wa Mungu Uchina bado hurudia hali mbaya baada ya Mungu kutamka sauti Yake, na kwa hiyo Mungu asema, “bila uwezo wa kubadilisha ukweli uliotimia, wanaweza tu kunisubiri kutamka hukumu.” Bado kutakuwa na wengine miongoni mwao wa kuondolewa—sio wote watabaki bila kubadilishwa. Kwa usahihi zaidi, watu wanaweza tu kufikia matarajio baada ya kupitia majaribio, na hivyo watapewa “ vyeti vya ubora”; la sivyo watakuwa takataka juu ya rundo la takataka. Siku zote Mungu huonyesha hali halisi ya mwanadamu, kwa hiyo mwanadamu huendelea kuhisi usiri wa Mungu. “Kama Hangekuwa Mungu, Angewezaje kujua vizuri sana hali yetu halisi?” Lakini kwa ajili ya udhaifu wa wanadamu, “Katika mioyo ya wanadamu, Mimi siko juu, wala chini. Wanadamu hawajali iwapo Nipo au la.” Je, hii hasa si hali ya watu wote inayolingana vizuri na uhalisi? Kulingana na wanadamu, Mungu yupo wakati ambapo wanamtafuta na hayupo wakati ambapo hawamtafuti. Kwa maneno mengine, Mungu yupo ndani ya mioyo ya wanadamu mara tu wanapohitaji msaada Wake, lakini wakati hawamhitaji, Hayupo tena. Hiki ndicho kiko ndani ya mioyo ya wanadamu. Kwa kweli, kila mtu duniani hufikiria hivi, pamoja na wakana Mungu wote, ambao fikira yao kuhusu Mungu ni nyeusi na ya dhahania.

“Kwa hiyo, milima inakuwa mipaka kati ya mataifa ulimwenguni, maji yanakuwa vikwazo vya kuwatenga watu kati ya nchi, na hewa inapuliza kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi mwingine katika uwanda wa dunia.” Hii ndiyo kazi ambayo Mungu alifanya wakati Alipokuwa Akiuumba ulimwengu. Kulitaja hili hapa kunawakanganya watu: Yawezekana kwamba Mungu anataka kuumba ulimwengu mwingine? Ni haki kusema hivi: Kila wakati Mungu anaponena, maneno Yake huwa na uumbaji, usimamizi, na uharibifu wa ulimwengu; ni kwamba tu wakati mwingine ni dhahiri, na wakati mwingine tata. Usimamizi wote wa Mungu unajumuishwa katika maneno Yake; tatizo la pekee ni kwamba wanadamu hawawezi kuyabainisha. Baraka ya Mungu kwa wanadamu huifanya imani yao kukua mara mia moja. Kutoka nje, inaonekana kana kwamba Mungu anafanya ahadi kwa wanadamu, lakini la muhimu ni kigezo kwa madai ya Mungu kwa watu wa ufalme Wake. Atawahifadhi wale wanaotii, na wale wasiotii watamezwa katika janga ambalo limetupwa chini kutoka mbinguni. “Radi, inayovingirika angani, inamwangusha chini mwanadamu, milima ya juu, inapoanguka, inamzika; wanyama pori kwa njaa yao wanamla kwa ulafi; na bahari, zinapobingirika, zinazingira kichwa chake. Binadamu wanapojishughulisha na migogoro ya mauaji ya jamii, wanadamu wote watatafuta maangamizo yao katika majanga yatokayo katikati ya binadamu.” Huku ni “kutendewa kwa njia ya pekee kutakaotolewa kwa wale ambao hawafikii matarajio, ambao hawataokolewa katika ufalme wa Mungu baadaye. Kadri Mungu anavyosema mambo kama, “Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza,” ndivyo wanadamu wanafahamu zaidi heshima yao wenyewe, na hivyo huwa na imani zaidi ya kutafuta maisha mapya. Mungu huwapa wanadamu jinsi wanavyomwomba. Wakati Mungu anawafichua kwa kiasi fulani, Yeye hubadilisha mtindo Wake wa kunena, na Hutumia sauti ya kubariki ili kupata matokeo bora zaidi. Kumdai mwanadamu kwa njia hii hutoa matokeo zaidi ya kiutendaji. Kwa kuwa wanadamu wote wako radhi kuzungumza kuhusu biashara na wenzi wao—wote ni watalaam katika biashara—hiki ndicho Mungu anacholenga moja kwa moja hasa katika kusema hivi. Kwa hiyo “Sinim” ni nini? Maana ya Mungu hapa si ufalme ulio duniani ambao umepotoshwa na Shetani, bali ni kusanyiko la malaika wote waliotoka kwa Mungu. Maneno “shujaa na imara” yanadokeza kwamba malaika watapenyeza nguvu zote za Shetani na kwa hiyo Sinim itaanzishwa katika ulimwengu mzima. Kwa hiyo maana halisi ya Sinim ni kusanyiko la malaika wote duniani; hapa inahusu wale walio duniani. Kwa hiyo ufalme utakaokuweko baadaye duniani utaitwa “Sinim,” na sio “ufalme.” Hakuna maana halisi kwa “ufalme” ulio duniani, na hususa ni Sinim. Kwa hiyo kwa kuunganisha tu kwa maana ya Sinim ndio mtu anaweza kujua maana halisi ya maneno “hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.” Hili linaonyesha kuwapanga katika madaraja watu wote duniani katika siku za baadaye. Watu wote wa Sinim watakuwa wafalme watakaowaongoza watu wote duniani baada ya wao kupitia kuadibu. Kila kitu duniani kitatenda kazi kama kawaida kwa sababu ya usimamizi wa watu wa Sinim. Hiki ni kielelezo cha kukadiria tu hali hiyo. Watu wote watabaki ndani ya ufalme wa Mungu, kumaanisha kwamba wataachwa ndani ya Sinim. Wanadamu walio duniani wataweza kuwasiliana na malaika. Kwa hiyo, mbingu na dunia zitaunganishwa, au kwa maneno mengine, wanadamu wote walio duniani watatii na kumpenda Mungu kama vile malaika mbinguni hufanya. Wakati huo, Mungu ataonekana kwa dhahiri kwa watu wote duniani na Atawaruhusu wauone uso Wake halisi kwa macho yao, na Ataonekana kwa wanadamu wakati wowote.

Iliyotangulia: Sura ya 18

Inayofuata: Sura ya 20

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Sura ya 12

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangazwa, na nyota zote zinaanza...

Amri za Enzi Mpya

Katika kupitia kazi ya Mungu, ninyi lazima msome maneno ya Mungu kwa makini na mjiandae na ukweli. Lakini kuhusu kile mnachotaka kufanya...

Fumbo la Kupata Mwili (2)

Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki