Sura ya 21

Machoni pa Mungu, watu ni kama wanyama katika ulimwengu wa wanyama. Wao hupigana, huchinjana, na huwa na ushirikiano wa pekee mmoja kwa mwingine. Machoni pa Mungu, wao pia ni kama sokwe, wakipangiana hila bila kujali umri au jinsia. Kwa hivyo, yote ambayo wanadamu wote hufanya na kuonyesha hayajawahi kuupendeza moyo wa Mungu. Wakati ambao Mungu hufunika uso Wake ndio hasa wakati ambao watu duniani kote wanajaribiwa. Watu wote wanapiga kite kwa uchungu, wote wanaishi chini ya tishio la msiba, na hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuepuka kutoka kwa hukumu ya Mungu. Kwa kweli, lengo kuu la Mungu kupata mwili ni kumhukumu mwanadamu na kumshutumu katika mwili Wake. Katika mawazo ya Mungu, imeamuliwa kitambo ni nani, kwa mujibu wa kiini chake, ataokolewa au kuangamizwa, na hili litafanywa wazi polepole wakati wa awamu ya mwisho. Kadri siku na miezi inavyopita, watu hubadilika na umbo lao la asili hufichuliwa. Inakuwa wazi iwapo kuna kuku au bata katika yai wakati linapofunguka. Wakati ambapo yai huvunjika ndio wakati hasa ambapo maafa duniani yatafikia kikomo. Kutokana na hili inaweza kuonekana kuwa, ili kujua kama kuna “kuku” au “bata” ndani, lazima “yai” livunjwe. Huu ndio mpango katika moyo wa Mungu, na ni lazima utimizwe.

“Ole wao, maskini wanadamu! Kwa nini mwanadamu ananipenda lakini hawezi kufuata nia za Roho Wangu?” Kwa sababu ya hali hii ya mwanadamu, lazima apitie kushughulikiwa ili apate kuridhisha mapenzi ya Mungu. Na kwa sababu ya Mungu kuwachukia sana wanadamu, Ametangaza mara nyingi: “Enyi waasi wa wanadamu wote! Lazima waharibiwe chini ya miguu Yangu, ni lazima watokomee kabisa katikati ya kuadibu Kwangu, na lazima, siku ambayo mpango Wangu mkubwa utakamilika, watatupiliwa mbali kutoka kati ya wanadamu, ili wanadamu wote wazijue nyuso zao mbaya.” Mungu ananena kwa watu wote katika mwili, na pia Ananena kwa Shetani katika ulimwengu wa kiroho, yaani, juu ya ulimwengu wote. Haya ni mapenzi ya Mungu, na ndiyo yanayohitajika kutimizwa kwa mpango wa Mungu wa miaka 6,000.

Kwa kweli, Mungu ni wa kawaida hasa, na kuna mambo mengine ambayo yanaweza tu kutimizwa ikiwa Atayatekeleza mwenyewe na kuyaona kwa macho Yake Mwenyewe. Sivyo kama watu wanavyofikiria, Mungu hulala tu pale huku yote yanaenda kama Atakavyo; haya ni matokeo ya usumbufu wa Shetani katika watu, jambo ambalo huwafanya watu kutofahamu uso halisi wa Mungu. Kwa hivyo, wakati wa enzi ya mwisho, Mungu amepata mwili ili kufichua wazi uhalisi Wake kwa mtu, bila kuficha chochote. Maelezo mengine ya tabia ya Mungu ni kutia chumvi kutupu, kama vile inaposemwa kwamba Mungu anaweza kuiharibu dunia kwa neno moja au wazo dogo. Kwa hiyo, watu wengi husema mambo kama, Kwa nini Mungu ni Mwenye kudura, lakini Hawezi kummeza Shetani kwa funda moja? Maneno haya ni ya upuuzi, na huonyesha kuwa watu bado hawamjui Mungu. Kwa Mungu kuwaangamiza maadui Zake kunahitaji mchakato, hata hivyo ni kweli kusema kwamba Mungu ni Mshindi kwa yote: Hatimaye Mungu atawashinda maadui Zake. Kama vile tu nchi yenye nguvu huishinda nchi dhaifu, ni lazima itimize ushindi yenyewe, hatua kwa hatua, wakati mwingine kwa kutumia nguvu, wakati mwingine kwa kutumia mkakati. Kuna mchakato, lakini haiwezi kusema kuwa, kwa kuwa nchi yenye nguvu ina silaha za nyuklia za kizazi kipya na nchi dhaifu ni duni sana, nchi dhaifu itakata tamaa bila kupigana. Hiyo ni hoja ya upuuzi. Ni haki kusema kwamba nchi yenye nguvu itashinda bila shaka na nchi dhaifu itapoteza bila shaka, lakini nchi yenye nguvu inaweza tu kusemwa kuwa na nguvu zaidi wakati inapovamia binafsi nchi dhaifu. Hivyo, daima Mungu amesema kwamba mwanadamu hamjui. Kwa hiyo, kile kilichosemwa hapo juu ni upande mmoja wa kwa nini mwanadamu hamjui Mungu? Je, hizi ni dhana za mwanadamu? Kwa nini Mungu anataka tu mwanadamu ajue uhalisi Wake, na mwenyewe na hivyo kuwa mwili? Hivyo, watu wengi waliabudu Mbinguni kwa dhati, lakini “Mbingu haijawahi kuathiriwa na matendo ya mwanadamu hata kidogo, na iwapo kumtendea Kwangu mwanadamu kungetegemea matendo yake yote, basi wanadamu wote wangeishi katikati ya kuadibu Kwangu.”

Mungu hutambua kiini cha mwanadamu. Katika matamko ya Mungu, Mungu anaonekana “kuteswa” sana na mwanadamu kiasi kwamba Hana haja ya kumzingatia zaidi mwanadamu, wala tumaini ndani yake hata kidogo; ingeonekana kwamba mwanadamu hawezi kuokolewa. “Nimewaona watu wengi wakitiririkwa na machozi, na Nimewaona watu wengi wakitoa nyoyo zao ili wapate utajiri Wangu. Licha ya ‘uchaji Mungu’ kama huu, Sijawahi kujitoa kwa mwanadamu kikamilifu kwa sababu ya hisia zake za ghafla, kwa sababu mwanadamu hajawahi kuwa radhi kujitoa kwa furaha mbele Yangu.” Mungu anapofichua asili ya mwanadamu, mwanadamu anaona aibu, lakini huu ni ufahamu wa juujuu tu, na hawezi kujua kweli asili yake katika maneno ya Mungu; hivyo, watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu, hawawezi kupata njia kwa ajili ya maisha yao katika maneno ya Mungu, na kwa hiyo, kadri wanavyokuwa wapumbavu, ndivyo Mungu anavyowadhihaki zaidi. Kwa hivyo, wao huingia katika jukumu la mwovu kwa kutojua—na kwa hiyo, wanakuja kujijua wanapochomwa kwa “upanga mwepesi.” Maneno ya Mungu yanaonekana kuyasifu matendo ya mwanadamu, na kuyahimiza matendo ya mwanadamu—na bado watu daima huhisi kwamba Mungu anawadhihaki. Na hivyo, wanapoyasoma maneno ya Mungu, misuli katika nyuso zao hutetemeka mara kwa mara, kama kwamba wanasukasuka. Huu ni uchafu wa dhamiri zao, na ni kwa sababu hii ndio wanatetemeka pasipo kutaka. Maumivu yao ni aina ambayo kwayo wanataka kucheka lakini hawawezi—wala hawawezi kulia, kwa sababu utani wa watu unachezwa kwenye kidhibiti cha mbali cha “mashine ya video” “VCR,” lakini hawawezi kuizima, na wanaweza tu kuivumilia. Ijapokuwa “kuzingatia maneno ya Mungu” huhubiriwa wakati wa mikutano yote ya wafanyikazi wenza, ni nani asiyejua asili ya mayai ya joka kubwa jekundu? Ana kwa ana, wao ni watiifu kama wanakondoo, lakini wanapogeuka wao ni katili kama mbwa mwitu, ambalo linaweza kuonekana katika maneno ya Mungu kwamba “watu wengi hunipenda kwa dhati Ninapotoa maneno Yangu, lakini hawathamini maneno Yangu katika roho zao, badala yake wakiyatumia kwa kawaida kama mali ya umma na kuyatupa yalipotoka wakati wowote wanapotaka.” Kwa nini Mungu daima amemfunua mwanadamu? Hili linaonyesha kwamba asili ya mwanadamu ya kale ni thabiti na imara. Kama Mlima wa Tai, ni mrefu kwa mamia ya mamilioni ya mioyo ya watu, lakini siku itakuja ambapo Yu Gong atauhamisha mlima huo, na huu ndio mpango wa Mungu. Katika matamko Yake, hakuna wakati ambapo Mungu hatoi matakwa kwa mwanadamu, kumwonya mwanadamu, au kuonyesha asili ya mwanadamu inayofichuliwa katika maisha yake: “Wakati mwanadamu yuko mbali nami, na wakati ananijaribu, Mimi hujificha kutoka kwake kati ya mawingu. Na hivyo, hawezi kunipata hata kidogo, na huishi tu mikononi mwa waovu, akifanya yote watakayo.” Kwa kweli, watu huwa na nafasi ya kuishi mbele ya uwepo wa Mungu kwa nadra sana, kwa sababu wana hamu kidogo sana ya kutafuta; kwa hiyo, ingawa watu wengi wanampenda Mungu, wanaishi chini ya mkono wa yule mwovu, wanaongozwa tu na yule mwovu. Kama kweli watu wangeishi katika nuru ya Mungu, wakimtafuta Mungu kila dakika ya kila siku, hakungekuwa na haja ya Mungu kunena hivi, ndiyo? Watu wanapoweka maandiko kando, papo hapo wanamweka Mungu kando pamoja na kitabu, na hivyo wanajihusisha na shughuli yao wenyewe, baada ya hapo Mungu hutoweka mioyoni mwao. Lakini wanapokichukua kitabu tena, huwajia ghafla kwamba hawakuwa wakimfikiria Mungu. Hivyo ndivyo maisha ya mwanadamu yalivyo “bila kumbukumbu.” Kadri Mungu anavyonena, ndivyo maneno Yake yanavyokuwa makuu zaidi. Yanapofikia kilele chake, kazi yote inakamilika, na kwa hiyo, Mungu hukomesha matamshi Yake. Kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi ni kumaliza kazi Yake wakati inapofikia upeo wake; Haendelei kufanya kazi wakati inapofika upeo wake, lakini Huacha ghafla. Yeye kamwe Hafanyi kazi ambayo si ya lazima.

Iliyotangulia: Sura ya 20

Inayofuata: Sura ya 22 na 23

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp