Jinsi ya Kujua Uhalisi
Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi zaidi, ndivyo wanavyokuwa na dhana chache zaidi; kadiri watu wanavyopitia uhalisi zaidi, kadiri wanavyojua zaidi matendo ya Mungu wa uhalisi, na ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kujiweka huru kutokana na tabia zao potovu na za kishetani; kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyomjua Mungu zaidi na kuuchukia mwili zaidi na kupenda ukweli; na kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyofika karibu na ubora wa mahitaji ya Mungu. Watu waliopatikana na Mungu ni wale walio na uhalisi, na wanaojua uhalisi; wale ambao wamepatikana na Mungu wamepata kuyajua matendo halisi ya Mungu kutokana na kupitia katika uhalisi. Kadiri hasa unavyoshirikiana zaidi na Mungu na kuudhibiti mwili wako, ndivyo utakavyopokea zaidi kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo utakavyopata uhalisi zaidi, na ndivyo utapatiwa nuru zaidi na Mungu—na hivyo ukubwa wa ufahamu wako wa matendo halisi ya Mungu. Ikiwa unaweza kuishi katika mwangaza wa sasa wa Roho Mtakatifu, njia ya sasa ya kutenda itakuwa wazi kwako, na utaweza kujitenga zaidi na dhana za kidini na vitendo vilivyopita zamani. Leo tunalenga uhalisi: Kadiri watu walivyo na uhalisi zaidi, ndivyo ufahamu wao wa ukweli unavyokuwa wazi, na ufahamu wao wa mapenzi ya Mungu unaongezeka. Uhalisi unaweza kuzishinda nyaraka zote na mafundisho yote ya kidini, unaweza kushinda nadharia na utaalamu wote, na kadiri watu wanavyoangazia uhalisi zaidi, ndivyo wanavyompenda Mungu kwa dhati zaidi na kuyatamani maneno Yake. Ikiwa daima unalenga uhalisi, falsafa yako ya maisha, dhana za kidini, na tabia asilia zitafutwa kutokana na kazi ya Mungu. Wale wasiouandama uhalisi, na hawafahamu uhalisi, wanaelekea kutafuta kile kilicho na nguvu za juu, na watalaghaiwa kwa urahisi. Roho Mtakatifu hana namna ya kufanya kazi ndani ya watu kama hao, na kwa hivyo wanajisikia watupu, na kwamba maisha yao hayana maana.
Roho Mtakatifu anaweza tu kufanya kazi ndani yako ukijifunza kweli, ukitafuta kweli, ukiomba kweli, na ukiwa radhi kuteseka kwa ajili ya kuutafuta ukweli. Wale ambao hawautafuti ukweli hawana chochote ila tu nyaraka na mafundisho ya kidini, na nadharia tupu, na wale wasio na ukweli kiasili wana dhana nyingi kuhusu Mungu. Watu kama hawa hutamani tu Mungu aibadilishe miili yao ya nyama kuwa miili ya kiroho ili kwamba waweze kupaa katika mbingu ya tatu. Hawa watu ni wapumbavu kiasi gani? Wote wasemao mambo sampuli hii hawana ufahamu wa Mungu, au uhalisi; watu kama hawa hawawezi kushirikiana na Mungu, na wanaweza tu kusubiri bila kufanya chochote. Ikiwa watu wanataka kuelewa ukweli, na kuuona ukweli wazi wazi, na ikiwa, aidha, wanataka kuingia ndani ya ukweli, na kuuweka katika vitendo, ni sharti wajifunze kweli, watafute kweli, na wawe na hitaji la kweli. Unapotamani, na unaposhirikiana na Mungu kweli, Roho wa Mungu kwa hakika atakugusa na kufanya kazi ndani yako, jambo ambalo litakuletea nuru zaidi na kukupa ufahamu zaidi kuhusu uhalisi na kuwa wa msaada mkubwa kwa maisha yako.
Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu, ni sharti kwanza wajue kuwa Mungu ni Mungu halisi, na ni sharti wajue maneno ya Mungu, kuonekena halisi kwa Mungu katika mwili, kazi halisi ya Mungu. Ni baada tu ya kujua kwamba kazi ya Mungu ni halisi ndiyo utaweza kweli kushirikiana na Mungu, na ni kupitia kwa njia hii tu ndipo utaweza kutimiza ukuaji wa maisha yako. Wale wote wasiokuwa na ufahamu wa uhalisi hawana namna ya kuyapitia maneno ya Mungu, wametekwa katika dhana zao, wanaishi katika mawazo yao, na hivyo hawana ufahamu wa maneno ya Mungu. Kadiri ufahamu wako kuhusu uhalisi ulivyo mkubwa, ndivyo unakuwa karibu zaidi na Mungu, na ndivyo unakuwa rafiki Yake wa karibu zaidi; jinsi unavyotafuta zaidi kutokuwa yakini na udhahania, na mafundisho ya kidini, ndivyo unavyojitenga zaidi na Mungu, na ndivyo utakavyohisi zaidi kuwa kuyapitia maneno ya Mungu ni kazi na ni kugumu, na kwamba huna uwezo wa kuingia. Ikiwa unataka kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, na katika njia sahihi ya maisha yako ya kiroho, ni sharti kwanza ujue uhalisi na ujitenge na vitu visivyo yakini na vya miujiza—ambako ni kumaanisha kuwa, kwanza ni sharti uelewe jinsi Roho Mtakatifu anapeana nuru na kukuongoza kutoka ndani. Kwa njia hii, ikiwa kwa kweli unaweza kuielewa kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako, utakuwa umeingia katika njia sahihi ya kufanywa mkamilifu na Mungu.
Leo, kila kitu kinaanza kwa uhalisi. Kazi ya Mungu ndiyo halisi zaidi, na inaweza kuguswa na watu; ndicho kitu kinachoweza kupitiwa na wanadamu, na kufanikisha. Ndani ya watu mna mengi ambayo si yakini na ya miujiza, ambayo yanawazuia kuijua kazi ya sasa ya Mungu. Hivyo katika mazoea yao mara zote hupotoka na kuhisi vigumu, ambayo yote yanasababishwa na dhana zao. Watu wanashindwa kuelewa kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, hawajui uhalisi, na kwa hivyo daima njia zao za kuingia ni hasi. Wanatazama mahitaji ya Mungu kwa mbali, bila kuweza kuyatimiza; wanaona tu kwamba maneno ya Mungu kwa hakika ni mazuri, ila hawawezi kupata njia ya kuingilia. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kanuni hii: kupitia ushirikiano na watu, kupitia kwa wao kuomba kimatendo, kumtafuta na kusonga karibu na Mungu, matokeo yanaweza kupatikana na wanaweza kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Si kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kivyake, au mwanadamu anafanya kazi kivyake. Wote ni wa muhimu, na jinsi wanadamu wanavyoshiriki zaidi na jinsi wanavyotaka zaidi kufikia viwango vya mahitaji ya Mungu, ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu inaimarika. Ni ushirikiano halisi tu wa wanadamu, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo vinaweza kutoa matukio halisi na ufahamu wa kweli wa kazi ya Mungu. Hatua kwa hatua, kupitia kwa mazoea kwa njia hii, mwanadamu mkamilifu hatimaye huzalishwa. Mungu hafanyi vitu vya miujiza; katika dhana za mwanadamu, Mungu ni mwenye uweza, na kila kitu kinafanywa na Mungu—na hutokea kwamba watu wanasubiri tu bila kufanya chochote, hawasomi maneno ya Mungu au kuomba, na wanasubiri tu kuguswa na Roho Mtakatifu. Walio na ufahamu sahihi, hata hivyo, wanaamini hili: matendo ya Mungu yanaweza kufikia pale ambapo ushirikiano wangu umefikia, na athari ya kazi ya Mungu kwangu inategemea namna ninavyoshirikiana. Mungu anenapo, ninapaswa kufanya lolote niwezalo na kuyaelekea maneno ya Mungu; hili ndilo ninapaswa kufanikisha.
Kati ya Petro na Paulo, mnaweza kuona wazi kuwa Petro ndiye alikuwa makini kwa uhalisi. Kutokana na yale aliyoyapitia Petro, inaweza kuonekana kuwa matukio aliyopitia yalijumlisha mafunzo kutoka kwa wale walioanguka awali, na kwamba alipokea nguvu za watakatifu wa zamani—na kutokana na hili inaonekana hasa jinsi matukio aliyopitia Petro yalivyokuwa, kwamba yalitosha kuwapa watu fursa ya kuyagusa, na kuwa na uwezo wake, na kwamba yalitimizwa na watu. Paulo, ijapokuwa alikuwa tofauti: yale aliyonena kuhusu hayakuwa yakini na hayakuonekana, mambo kama kwenda katika mbingu ya tatu, kupanda katika kiti cha ufalme, na taji la wenye haki. Aliangazia masuala ya nje: kuhusu hadhi, na kuwakemea watu, na kujivunia ukuu wake, kuguswa na Roho Mtakatifu, na kadhalika. Hakuna lililokuwa halisi miongoni mwa mambo aliyoyatafuta, na mengi yake yalikuwa ndoto, na kwa hivyo inaweza kuonekana kwamba yote ambayo ni miujiza, kwa mfano ni mara ngapi Roho Mtakatifu anawagusa watu, furaha kubwa ambayo watu wanafurahia, kwenda katika mbingu ya tatu, au mafunzo ya mara kwa mara na kuyafurahia kwa kiwango fulani, kusoma maneno ya Mungu na kuyafurahia kwa kiwango fulani—hakuna lililo halisi miongoni mwa haya. Kazi yote ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida, na halisi. Usomapo maneno ya Mungu na kuomba, ndani unang’aa na kuwa imara, dunia ya nje haiwezi kuhitilafiana na wewe, ndani unakuwa radhi kumpenda Mungu, uko radhi kushughulika na mambo chanya, na unachukia dunia potovu; huku ni kuishi ndani ya Mungu. Si kama watu wasemavyo, kufurahia kupindukia—maneno kama hayo si halisi. Leo, kila kitu kinapaswa kuanzia kwa uhalisi. Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni halisi, na katika matukio unayoyapitia, unapaswa kuwa makini kumjua Mungu kweli, na kuzitafuta nyayo za kazi ya Mungu na namna ambazo Roho Mtakatifu anawagusa na kuwapa watu nuru. Ikiwa unakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuomba, na kushirikiana kwa njia iliyo halisi zaidi, kuchukua kilichokuwa kizuri zama zilizopita, na kukataa kilichokuwa kibaya kama Petro, ukisikiliza na masikio yako na kuangalia na macho yako, na kuomba mara kwa mara na kutafakari moyoni mwako, na kufanya lolote uwezalo kushirikiana na kazi ya Mungu, basi kwa hakika Mungu atakuongoza.