Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu
Roho Mtakatifu Anafanya kazi vipi katika kanisa sasa? Je, una ufahamu wa hilo? Ni matatizo gani makubwa zaidi yanayowakumba ndugu na dada? Wamepungukiwa na nini zaidi? Kwa sasa, kuna watu ambao wako hasi katikati ya majaribio, na wengine wao hata wanalalamika, na wengine hawasongi mbele tena kwa sababu Mungu Hazungumzi tena. Watu hawajaingia njia sahihi ya imani katika Mungu. Hawawezi kuishi wakijitegemea, na hawezi kudumisha maisha yao ya kiroho. Kuna watu wengine ambao wanafuata, wanaofuatilia kwa nguvu, na wako tayari kutenda Mungu Akinena. Lakini Mungu Asiponena, hawasongi mbele tena. Watu bado hawajaelewa mapenzi ya Mungu katika mioyo yao na hawana mapenzi kwa Mungu moja kwa moja; kufuata kwao Mungu hapo awali ilikuwa kwa sababu walikuwa wamelazimishwa. Sasa kuna watu ambao wamechoka na kazi ya Mungu. Je, hawako hatarini? Watu wengi wako katika hali ya kuvumilia tu. Ingawa wanakula na kunywa maneno ya Mungu na kumuomba, yote ni kwa kusitasita. Hawana bidii waliyokuwa nayo mwanzoni, na watu wengi hawana shauku katika kazi ya Mungu ya uboreshaji na ukamilisho. Ni kana kwamba hawana bidii ya ndani kamwe, na wanalemewa na maasi hawahisi kuwa wana deni kwa Mungu, wala hawajuti wenyewe. Hawaufuatilii ukweli ama kuondoka kanisani. Wanafuata tu raha za muda. Huyu ni aina ya mjinga mkuu wa kipumbavu! Wakati utakapofika, wote watatupwa nje, na hakuna mmoja atakayeokolewa! Je, unafikiri kuwa kama mtu ameokolewa mara moja ataokolewa kila wakati? Hii ni kujaribu tu kuwapumbaza watu! Wale wote wasiofuata kuingia katika maisha wataadibiwa. Watu wengi hawana shauku hata kidogo ya kuingia katika maisha, katika maono, ama kuweka ukweli katika matendo. Hawafuati kuingia ndani, na kwa hakika hawafuati kuingia ndani zaidi. Je, hawajiangamizi wenyewe? Wakati huu, kuna sehemu ya watu ambao hali zao zinaendelea kuwa nzuri na nzuri zaidi. Roho Mtakatifu Anapofanya kazi zaidi, wanajiamini zaidi, na wanapozoea zaidi ndipo wanapohisi siri ya kushangaza ya kazi ya Mungu. Wanapoingia ndani zaidi, ndipo wanaelewa zaidi. Wanahisi kuwa upendo wa Mungu ni mkubwa sana, na wanahisi imara na kupata nuru ndani. Wana uelewa wa kazi ya Mungu. Hawa ni watu ambao Roho Mtakatifu Anafanya kazi ndani yao. Watu wengine wanasema, “Ingawa hakuna maneno mapya kutoka kwa Mungu, lazima bado niendelee kuingia ndani katika ukweli, lazima niwe na bidii katika kila kitu katika mazoea yangu na kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu.” Mtu kama huyu ana kazi ya Roho Mtakatifu. Ingawa Mungu Haonyeshi uso Wake na Amejifichika kutoka kwa kila mtu, na Haneni neno lolote, na kuna nyakati ambazo watu wanapitia usafishaji wa ndani, ilhali Mungu hajawaacha watu Wake kabisa. Kama mtu hawezi kudumisha ukweli ambao anafaa kutekeleza, hatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika wakati wa usafishaji, wa Mungu kutojionyesha, kama hujiamini na unaogopa, usipo lenga kuwa na uzoefu wa maneno Yake, hii ni kutoroka kutoka kwa kazi ya Mungu. Baadaye, utatupwa nje. Wale ambao hawatafuti kuingia katika neno la Mungu hawana uwezo wa kusimama kama shahidi Wake. Watu ambao wanaweza kutoa ushahidi kwa Mungu na kuridhisha mapenzi Yake wote wanategemea kikamilifu bidii yao kufuatilia maneno ya Mungu. Kazi ambayo Mungu Anaitekeleza katika watu ni kimsingi kuwawezesha kuupata ukweli; Kukufanya wewe kufuatilia maisha ni kwa ajili ya kukukamilisha, na yote ni ya kukufanya ufae kutumika na Mungu. Yote unayofuata sasa ni kusikia siri, kusikiliza maneno ya Mungu, kulisha macho yako, kuona kitu kipya ama kuona ni mwenendo upi, na kuridhisha udadisi wako. Kama hii ndio nia ya moyo wako, hakuna vile utafikia mahitaji ya Mungu. Wale ambao hawafuati ukweli hawezi kufuata mpaka mwisho kabisa. Wakati huu, si kwamba Mungu hafanyi kitu—ni kwamba watu hawashirikiani, kwa sababu wamechoka na kazi Yake. Wanataka tu kusikia maneno ya baraka Yake, na hawataki kusikia maneno ya hukumu Yake na kuadibiwa. Sababu ya hii ni nini? Ni kwa sababu tamaa ya watu kupata baraka haijatimizwa, na wako hasi na wanyonge. Si kwamba Mungu kimakusudi hakubali watu kumfuata, na si kwamba anapeana mapigo kimakusudi kwa wanadamu. Watu wako hasi na wanyonge kwa sababu nia zao hazifai. Mungu ni Mungu Ambaye Anampa mwanadamu maisha, naye hawezi kumleta mwanadamu katika kifo. Uhasi wa watu, unyonge na kurudi nyuma yote yanasababishwa na wao wenyewe.
Kazi ya Mungu ya sasa inawaletea watu usafishaji kiasi, na wale tu ambao wanaweza kusimama imara katika usafishaji huu watapata kibali cha Mungu. Haijalishi ni jinsi gani Anajificha, bila kuongea, ama kufanya kazi, bado unaweza kufuata kwa bidii. Hata kama Mungu Alisema angekukataa, bado ungemfuata Yeye. Hii ni kusimama kama shahidi kwa Mungu. Mungu Akijificha kutoka kwako nawe ukome kumfuata, hii ni kusimama shahidi kwa Mungu? Watu wasipoingia ndani kwa kweli, hawana kimo cha kweli, na wanapokabiliana na jaribio kubwa hasa, wanaanguka. Mungu haneni kwa sasa, ama kile Afanyacho hakilingani na dhana zako, kwa hivyo hauko sawa. Kama Mungu angekuwa sasa anatenda kulingana na dhana zako kwa sasa, kama Angekuwa anayakidhi matakwa yako na ukawa na uwezo wa kusimama na kufuatilia kwa nguvu, basi ni nini ambacho kweli ungekuwa unatumia kuendelea kuishi? Nasema kuwa kuna watu wengi ambao wanaishi wakitegemea kabisa udadisi wa binadamu. Hawana kabisa moyo wa kweli wa kufuata. Wale wote wasiofuata kuingia katika ukweli lakini wanategemea udadisi wao katika maisha ni watu wenye kustahili dharau walio hatarini! Kazi za Mungu tofauti yote ni ya kuwakamilisha wanadamu. Hata hivyo, watu daima ni wadadisi, wanapenda kuuliza kuhusu tetesi, wana wasiwasi kuhusu kinacho endelea nje ya nchi—ni nini kinaendelea Israeli, kama kuna mtetemeko wa ardhi Misri—kila wakati wanatafuta kitu mpya, kitu kisicho cha kawaida kuridhisha tamaa zao za kibinafsi. Hawafuati maisha, wala kufuata kukamilishwa. Wanatafuta tu siku ya Mungu kufika haraka ili ndoto yao nzuri ijulikane na tamaa zao badhirifu zitimie. Mtu kama huyo si wa kweli—ni mtu aliye na mtazamo usio sawa. Kuufuata ukweli ni msingi wa imani ya wanadamu katika Mungu. Watu wasipofuata kuingia katika maisha, wasipotafuta kumridhisha Mungu, basi watatiishwa chini ya adhabu. Wale watakaoadhibiwa ni wale ambao hawajakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu katika wakati wa kazi ya Mungu.
Watu wanafaa kushirikiana na Mungu vipi katika hatua hii ya kazi Yake? Mungu Anawajaribu watu kwa wakati huu. Haneni neno lolote; Anajificha na Hawasiliani na watu moja kwa moja. Kutoka nje, inaonekana kama Hafanyi kazi, lakini ukweli ni kwamba bado Anafanya kazi ndani ya mwanadamu. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ana maono kwa kufuata kwake maisha, na hana mashaka, hata kama haelewi kazi ya Mungu kikamilifu. Katikati ya majaribu, hata kama hajui ni nini Mungu Anataka kufanya na kazi gani Anataka kukamilisha, unafaa kujua kuwa nia za Mungu kwa wanadamu ni nzuri kila wakati. Ukimfuata na moyo wa kweli, Hatawahi kukuacha, na mwishowe kwa kweli Atakukamilisha, na kuwaleta watu katika mwisho unaofaa. Haijalishi ni vipi Mungu Anawajaribu watu kwa sasa, kuna siku moja ambayo Atawatolea watu matokeo yanayofaa na kuwapa adhabu inayofaa kulingana na kile ambacho wamefanya. Mungu Hatawaongoza watu hadi kituo fulani halafu Awatupe tu kando na kuwapuuza. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu mwaminifu. Katika hatua hii, Roho Mtakatifu anafanya kazi ya usafishaji. Anamsafisha kila mmoja. Katika hatua za kazi zilizoundwa na majaribu ya kifo na majaribu ya kuadibu, usafishaji katika wakati huo ulikuwa usafishaji kupitia maneno. Ili watu wapate uzoefu wa kazi ya Mungu, lazima kwanza waelewe kazi Yake ya sasa na kuelewa jinsi wanadamu wanafaa kushirikiana. Hili ni jambo ambalo kila mtu anafaa kuelewa. Haijalishi ni nini Mungu Anafanya, kama ni usafishaji ama kama Haneni, kila hatua ya kazi ya Mungu hailingani na dhana za wanadamu. Yote yanaenda mbali na kupenya katika dhana za watu. Hii ni kazi Yake. Lakini lazima uamini kwamba, kwa kuwa kazi ya Mungu imefika hatua fulani, Hatakubali wanadamu wote waangamie hata iweje. Anawapa ahadi na baraka kwa wanadamu, na wale wote wanaomfuata wataweza kupata baraka Yake, na wale wasiomfuata watatupwa nje na Mungu. Hii inategemea kufuata kwako. Haijalishi chochote, lazima uamini kuwa wakati kazi ya Mungu itakapomalizika, kila mtu atakuwa na mwisho unaofaa. Mungu Amewapa wanadamu matamanio mazuri, lakini wasipofuatilia, hawawezi kuyapata. Unafaa kuweza kuona hii sasa—Mungu kusafisha na kuwaadibu watu ni kazi Yake, lakini kwa watu, lazima wafuate badiliko katika tabia kila wakati. Katika mazoea yako ya kivitendo, lazima kwanza ujue jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu; lazima upate kile unachofaa kuingia ndani na mapungufu yako ndani ya maneno Yake, utafute kuingia katika mazoea yako ya kivitendo, na uchukue sehemu ya kazi ya Mungu inayofaa kuwekwa katika matendo na ujaribu kuifanya. Kula na kunywa maneno ya Mungu ni kipengele kimoja, maisha ya kanisa lazima pia yadumishwe, lazima uwe na maisha ya kiroho ya kawaida, na uweze kumkabidhi Mungu hali zako zote za sasa. Haijalishi ni vipi kazi Yake inabadilika, maisha yako ya kiroho yanapaswa kubaki kawaida. Maisha ya kiroho yanaweza kudumisha kuingia ndani kwako kwa kawaida. Haijalishi kile ambacho Mungu Anafanya, unapaswa kuendeleza maisha yako ya kiroho bila kukatizwa na kutimiza wajibu wako. Hiki ndicho watu wanapaswa kufanya. Yote ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini huku kwa wale walio na hali ya kawaida huku ni kukamilishwa, kwa wale wasio na hali ya kawaida ni majaribu. Katika hatua ya sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu ya kusafisha, watu wengine wanasema kuwa kazi ya Mungu ni kubwa sana na kwamba watu wanahitaji sana usafishaji, vinginevyo kimo chao kitakuwa ndogo sana na hawatakuwa na njia ya kufikia mapenzi ya Mungu. Hata hivyo, kwa wale walio na hali isiyo nzuri, inakuwa sababu ya kutomfuata Mungu, na sababu ya kutohudhuria mikusanyiko ama kula na kunywa neno la Mungu. Katika kazi ya Mungu, haijalishi ni nini Anafanya ama nini kinabadilika, kwa uchache sana watu lazima watu wadumishe hali ya chini zaidi ya maisha ya kawaida ya kiroho. Pengine umekuwa mwangalifu katika hatua hii ya sasa ya maisha yako ya kiroho, lakini bado hujapata mengi; hujavuna pakubwa. Katika hali za aina hizi lazima bado ufuate sheria; lazima ufuate sheria hizi ili usipate hasara katika maisha yako na ili uyakidhi mapenzi ya Mungu. Kama maisha yako ya kiroho si ya kawaida, huwezi kuelewa kazi ya sasa ya Mungu, badala yake kila wakati utahisi kwamba hayalingani kabisa na dhana zako mwenyewe, nawe una hiari ya kumfuata, lakini unakosa bidii ya ndani. Kwa hivyo haijalishi ni nini Mungu Anafanya sasa, lazima watu washirikiane. Watu wasiposhirikiana Roho Mtakatifu Hawezi kufanya kazi Yake, na kama watu hawana moyo wa kushirikiana, basi si rahisi wao kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Kama unataka kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani mwako, na kutaka kupata kibali cha Mungu, lazima udumishe moyo wako wa ibada asili mbele ya Mungu. Sasa, si lazima kwako kuwa na maelewano zaidi ya ndani, nadharia ya juu, ama vitu vingi—yote yanayohitajika ni kwamba ushikilie neno la Mungu juu ya msingi asili. Watu wasiposhirikiana na Mungu na wasipofuata kuingia zaidi, Mungu Atachukua kile walichokuwa nacho wakati mmoja. Ndani, watu wana tamaa kila wakati ya kilicho rahisi na afadhali wajifurahishe na kile ambacho kinapatikana. Wanataka kupata ahadi za Mungu bila kulipa gharama yoyote. Haya ni mawazo badhirifu ndani ya wanadamu. Kupata maisha yenyewe bila kulipa gharama—nini kimewahi kuwa rahisi? Mtu anapoamini katika Mungu na kutafuta kuingia katika maisha na kutafuta badiliko katika tabia yake, ni lazima alipe gharama na kufikia kiwango ambapo atamfuata Mungu daima bila kujali Anachofanya. Hiki ni kitu ambacho watu lazima wafanye. Hata kama unafuata haya yote kama sharti, ni lazima uyazingatie, na haijalishi majaribu yako ni makubwa kiasi gani, huwezi kuachilia uhusiano wako wa kufaa na Mungu. Unapaswa kuweza kuomba, udumishe maisha yako ya kanisa, na uishi na ndugu na dada. Mungu anapokujaribu, bado unapaswa kutafuta ukweli. Hiki ndicho kiwango cha chini cha maisha ya kiroho. Daima kuwa na moyo wa kutafuta na kujitahidi kushirikiana, kutumia nguvu zako zote—Je, hili linaweza kufanywa? Kwa msingi huu, utambuzi na kuingia katika uhalisi kitakuwa kitu ambacho unaweza kufanikisha. Ni rahisi kulikubali neno la Mungu wakati hali yako mwenyewe iko kawaida, na huhisi ugumu katika kuuweka ukweli katika matendo, na unahisi kuwa kazi ya Mungu ni kuu. Lakini kama hali yako ni duni, haijalishi kazi ya Mungu ni kuu vipi na haijalishi mtu anazungumza vizuri kivipi, hutasikiza chochote. Wakati hali ya mtu si ya kawaida, Mungu hawezi kufanya kazi ndani yao, na hawawezi kufanikisha mabadiliko katika tabia zao.
Kama watu hawana imani yoyote, sio rahisi kuendelea katika njia hii. Kila mtu sasa anaweza kuona kuwa kazi ya Mungu hailingani hata kidogo na fikira za watu. Mungu amefanya kazi nyingi sana na kuzungumza maneno mengi sana, ambayo hayalingani kabisa na dhana za binadamu. Hivyo, lazima watu wajiamini na wawe na utashi kuweza kusimama na kile wameshakiona na kile wamepata kutoka kwa uzoefu wao. Haijalishi ni nini Mungu Anafanya kwa watu, lazima washikilie kile walicho nacho, wawe waaminifu mbele za Mungu, na wasalie wenye kujitolea Kwake hadi mwisho. Huu ni wajibu wa wanadamu. Lazima watu watetee kile wanachopaswa kufanya. Imani katika Mungu inahitaji utiifu Kwake na uzoefu wa kazi Yake. Mungu Amefanya kazi nyingi sana—inaweza semekana kuwa kwa watu yote ni kukamilishwa, yote ni usafishaji, na hata zaidi, yote ni kuadibu. Hakujakuwa na hatua hata moja ya kazi ya Mungu ambayo imelingana na dhana za binadamu; kile watu wamefurahia ni maneno makali ya Mungu. Mungu Atakapokuja, watu wanapaswa kufurahia enzi Yake na hasira Yake, lakini haijalishi maneno Yake yalivyo makali, Anakuja kuokoa na kukamilisha binadamu. Kama viumbe, watu wanapaswa watekeleze wajibu ambao wanafaa kufanya, na kusimama shahidi kwa Mungu katikati ya usafishaji. Katika kila jaribio wanapaswa washikilie ushahidi ambao wanapaswa washuhudie, na kushuhudia ushuhuda mkubwa kwa Mungu. Huyu ni mshindi. Haijalishi Mungu Anavyokuboresha, unabaki kuwa na imani kubwa na kutopoteza imani katika Mungu. Ufanye kile mwanadamu anafaa kufanya. Hiki ndicho Mungu Anahitaji kwa mwanadamu, na moyo wa binadamu unapaswa kuweza kurudi Kwake kikamilifu na kumwelekea katika kila wakati. Huyu ni mshindi. Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi. Kama kufuata kwako ni bora kabisa Mungu Anapokubariki, lakini unarudi nyuma bila baraka Zake, si huu ni utakaso? Kwa sababu una uhakika kuwa njia hii ni ya kweli, lazima uifuate hadi mwisho; lazima udumishe ibada yako kwa Mungu. Kwa sababu umeona kuwa Mungu Mwenyewe amekuja duniani kukukamilisha, lazima umpe moyo wako Kwake kabisa. Haijalishi ni nini Anafanya, hata kama Anaamua tokeo lisilofaa kwako mwishowe, bado unaweza kumfuata. Hii ni kudumisha usafi wako mbele za Mungu. Kupeana mwili wa kiroho mtakatifu na bikira safi kwa Mungu inamaanisha kuweka moyo mwaminifu mbele za Mungu. Kwa wanadamu, uaminifu ni usafi, na kuweza kuwa mwaminifu kwa Mungu ni kudumisha usafi. Hii ndiyo unafaa kuweka katika matendo. Unapopaswa kuomba, omba; unapopaswa kukusanyika pamoja katika ushirika, fanya hivyo; unapopaswa kuimba nyimbo za kidini, imba nyimbo za kidini; na unapopaswa kuunyima mwili, unyime mwili. Unapotekeleza wajibu wako hulimalizi kwa kubahatisha; unapokumbana na majaribu unasimama imara. Hii ni ibada kwa Mungu. Usiposhikilia kile ambacho watu wanapaswa kufanya, basi kuteseka kwako na maazimio ya hapo awali yalikuwa ya bure.
Kwa kila hatua ya kazi ya Mungu, kunayo njia ambayo watu wanapaswa washirikiane. Mungu Anawasafisha watu ili wawe na imani katikati ya usafishaji. Mungu Anawakamilisha watu ili wawe na imani ya kukamilishwa na Mungu na wako tayari kuukubali usafishaji Wake na kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Roho wa Mungu Anafanya kazi ndani ya watu ili kuwaletea nuru na mwangaza, na kuwafanya washirikiane Naye na kutenda. Mungu Haneni wakati wa usafishaji. Hatoi sauti Yake, lakini bado kuna kazi ambayo watu wanapaswa kuifanya. Unapaswa kushikilia kile ambacho unacho tayari, unapaswa bado kuwa na uwezo wa kumwomba Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kusimama shahidi mbele ya Mungu; hivi utatimiza wajibu wako mwenyewe. Nyinyi wote mnapaswa muone kwa dhahiri kutoka kwa kazi ya Mungu kuwa majaribu Yake ya imani ya watu na upendo inahitaji kuwa waombe zaidi kwa Mungu, na kwamba waonje maneno ya Mungu mbele Zake mara kwa mara. Mungu Akikupa nuru na kukufanya kuelewa mapenzi Yake lakini huyaweki katika matendo hata kidogo, hutapata chochote. Unapoyaweka maneno ya Mungu katika matendo, unapaswa bado kuwa na uwezo wa kumwomba, na unapoyaonja maneno Yake unapaswa utafute kila wakati mbele Zake na uwe umejaa imani Kwake bila kuvunjika moyo ama kuwa baridi. Wale wasioweka maneno ya Mungu katika matendo wamejawa na nguvu katika mikusanyiko, lakini wanaanguka katika giza wanaporudi nyumbani. Kuna wengine ambao hawataki hata kukusanyika pamoja. Kwa hivyo lazima uone kwa wazi ni wajibu gani ambao watu wanapaswa kutimiza. Unaweza kukosa kujua mapenzi ya Mungu ni nini hasa, lakini unaweza kutekeleza wajibu wako, unaweza kuomba inapopaswa, unaweza kuuweka ukweli katika matendo unapopaswa, na unaweza kufanya kile watu wanapaswa kufanya. Unaweza kushikilia maono yako asili. Hivi, utaweza kukubali zaidi hatua ya Mungu inayofuata. Ni shida ukikosa kutafuta wakati ambapo Mungu anafanya kazi katika njia iliyofichika. Anaponena na kuhubiri katika mabaraza, unasikiza kwa shauku, lakini Asiponena unakosa nguvu na kurudi nyuma. Mtu wa aina gani anafanya hivi? Huyu ni mtu ambaye tu anaenda na mkondo. Hana msimamo, hawana ushuhuda, na hawana maono! Watu wengi wako hivyo. Ukiendelea katika njia hiyo, siku moja utakapopitia jaribio kuu, utateremka katika adhabu. Kuwa na msimamo ni muhimu sana katika kukamilishwa kwa watu na Mungu. Kama huna shaka na hatua yoyote ya kazi ya Mungu, unatimiza wajibu ya mwanadamu, unashikilia kwa uaminifu kile Mungu Amekufanya ukiweke katika matendo, hiyo ni, unakumbuka mawaidha ya Mungu, na haijalishi Anachokifanya sasa husahau mawaidha Yake, huna shaka kuhusu kazi Yake, unadumisha msimamo wako, kushikilia ushahidi wako, na una ushindi katika kila hatua ya njia, mwishowe utakamilishwa kuwa mshindi na Mungu. Kama unaweza kusimama imara katika kila hatua ya majaribu ya Mungu, na bado unaweza kusimama imara hadi mwisho kabisa, wewe ni mshindi, na wewe ni mtu ambaye amekamilishwa na Mungu. Kama huwezi kusimama imara katika majaribu yako ya sasa, baadaye itakuwa hata vigumu zaidi. Ukipitia mateso kidogo yasiyo ya muhimu na usiufuate ukweli, hutapata chochote mwishowe. Utakuwa mkono mtupu. Kuna watu wengine ambao wanaacha kufuata wanapoona kuwa Mungu Haneni, na moyo wao unatawanyika. Je, si huyo ni mjinga? Watu wa aina hii hawana ukweli. Mungu Anenapo, wanakimbia huku na kule kila wakati, wakiwa na shughuli nyingi na kuwa na shauku kwa nje, lakini sasa Haneni, hawatafuti tena. Mtu kama huyu hana maisha ya usoni. Katika usafishaji, lazima uingie ndani kutoka kwa mtazamo halisi na usome masomo unayostahili kusoma; unapomwomba Mungu na kusoma neno Lake, unapaswa kulinganisha hali yako mwenyewe nayo, utambue pungufu zako, na ujue kuwa una somo mengi sana unayofaa kusoma. Unapotafuta kwa uaminifu katikati ya usafishaji, ndipo utakapojipata kuwa una pungufu. Unapokuwa unapitia usafishaji kunayo masuala mengi ambayo unapitia; hautayaona kwa wazi, unalalamika, unatambulisha mwili wako wenyewe—ni kwa njia hii pekee ndiyo unaweza kugundua kwamba una tabia nyingi sana potovu ndani yako.
Watu wanakosa kwa tabia na wanaanguka mbali na kanuni za Mungu, baadaye wanaweza hata kuhitaji imani zaidi ili kutembea njia hii. Kazi ya Mungu katika siku za mwisho inahitaji imani kubwa—inahitaji imani kubwa zaidi hata kuliko ile ya Ayubu. Bila imani, watu hawataweza kuendelea kupata mazoea na hawataweza kukamilishwa na Mungu. Siku itakapokuja ambapo majaribu makuu yanakuja, watu wengine wataondoka kutoka kanisa hili, na wengine wataondoka kutoka kanisa lile. Kutakuwa na wengine ambao walikuwa wakifanya vizuri kiasi katika kufuata kwao katika siku za awali na haiko wazi mbona hawaamini tena. Vitu vingi vitafanyika na hutajua ni nini kinaendelea, na Mungu Hataonyesha dalili zozote ama ishara, ama kufanya chochote kisicho cha kawaida. Hii ni kuona kama unaweza kusimama imara—Mungu Anatumia ukweli kuwasafisha watu. Bado hujateseka sana. Hapo baadaye majaribu makuu yajapo, katika sehemu zingine kila mtu katika kanisa ataondoka, na wale umesikizana nao vizuri sana wataondoka na kuiacha imani yao. Utaweza kusimama imara wakati huo? Sasa, yale majaribu umepitia yamekuwa madogo, na pengine imekuwa vigumu kuyahimili. Hatua hii inajumuisha usafishaji na kukamilishwa kupitia neno pekee. Katika hatua inayofuata, ukweli utakuja juu yako kukusafisha, halafu utakuwa katikati ya hatari. Inapokuwa kubwa sana, Mungu Atakushauri uharakishe na uondoke, na watu wa kidini watajaribu kukushawishi ujiunge. Hii ni ili kuona kama unaweza kuendelea katika njia hiyo. Haya yote ni majaribu. Majaribu ya sasa ni madogo, lakini siku itakuja ambapo kunao wazazi nyumbani ambao hawaamini tena na kunao watoto nyumbani ambao hawaamini tena. Je, utaweza kuendelea mbele? Unapoenda mbele zaidi, ndivyo majaribu yako yanakuwa mengi zaidi. Mtu Anatekeleza kazi Yake ya kuwasafisha watu kulingana na mahitaji yao na kimo chao. Katika hatua ya Mungu kuwakamilisha wanadamu, haiwezekani kuwa idadi ya watu itaendelea kukua—itapunguka tu. Ni kwa kupitia usafishaji huu tu ndipo watu wataweza kukamilishwa. Kushughulikiwa, kuadhibiwa, kujaribiwa, kuadibiwa, kulaaniwa—ndipo unaweza kustahimili haya yote? Unapoona kanisa lililo na hali nzuri hasa, ndugu na dada wote wanatafuta kwa nguvu kubwa, wewe mwenyewe unahisi umetiwa moyo. Siku ikija ambapo wote wameondoka, wengine wao hawaamini tena, wengine wameondoka kufanya biashara ama kuolewa, na wengine wamejiunga na dini, utaweza kusimama imara wakati huo? Je, utaweza kubaki bila mabadiliko ndani? Kukamilishwa kwa wanadamu kwa Mungu siyo jambo rahisi! Anatumia vitu vingi kuwasafisha watu. Watu wanaona haya kama mbinu, lakini kwa nia asili ya Mungu hizi sizo mbinu hata kidogo, ila ni ukweli. Mwishowe, Atakapokuwa Amewasafisha watu kufikia kiwango fulani na hawana malalamishi yoyote tena, hatua hii ya kazi Yake itakuwa imekamilika. Kazi kuu ya Roho Mtakatifu ni kukukamilisha, na wakati ambapo Hafanyi kazi na Anajificha, hata zaidi ni kwa sababu ya kukukamilisha, na hivi inaweza kuonekana hasa kama watu wana upendo kwa Mungu, na kama wana imani ya kweli Kwake. Mungu Anaponena wazi, hakuna haja ya wewe kutafuta; ni wakati tu ambapo Amejificha ndipo unahitaji kutafuta, unahitaji kuhisi njia yako hadi upite. Unapaswa kuweza kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa, na haijalishi matokeo yako ya usoni na hatima yako inaweza kuwa ipi, unapaswa kuweza kufuatilia maarifa na upendo kwa Mungu katika miaka ambayo uko hai, na haijalishi jinsi Mungu anavyokutendea, unapaswa kuweza kuepuka kulalamika. Kuna sharti moja kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya watu. Bora wana hamu na wanatafuta na hawasitisiti ama kuwa na shaka kuhusu matendo ya Mungu, nao wanaweza kushikilia wajibu wao kila wakati, hivi tu ndivyo wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila hatua ya kazi ya Mungu, kinachohitajika kwa wanadamu ni imani kuu na kutafuta mbele za Mungu—kupitia tu kwa mazoea ndipo watu wataweza kugundua jinsi Mungu Anavyopendeka na jinsi Roho Mtakatifu Anavyofanya kazi ndani ya watu. Usipopata uzoefu, usipoihisi njia yako kupitia hayo, usipotafuta, hutapata chochote. Lazima uhisi njia yako kupitia mazoea yako, na kwa kupitia mazoea yako tu ndipo utaona matendo ya Mungu, na kugundua maajabu Yake na mambo Yake yasiyoeleweka.