Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amekuja katika Uzima?
Ni wakati tu umetupa mbali tabia zako potovu na kufanikisha kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida ndiyo utafanywa kuwa mtimilifu. Ingawa hutaweza kunena unabii, au kuhusu mafumbo yoyote, utakuwa unaishi kwa kudhihirisha na kufunua mfano wa binadamu. Mungu alimuumba mwanadamu, lakini mwanadamu akapotoshwa na Shetani, hivi kwamba watu wakawa “waliokufa.” Hivyo, baada ya wewe kubadilika, hutakuwa kama hawa waliokufa tena. Ni maneno ya Mungu ndiyo yanayofanya roho za watu kufufuka na kuzifanya ziamke, na roho za watu zitakapoamshwa, basi watakuwa wamekuja katika uzima. Ninapozungumzia “waliokufa,” ninazungumza kuhusu maiti zisizo na roho, kuhusu watu ambao roho zao zimekufa ndani yao. Roho za watu zinapoamshwa, basi watu wanakuja katika uzima. Wale watakatifu waliozungumziwa awali wanarejelea watu ambao wamekuja katika uzima, wale ambao walikuwa chini ya ushawishi wa Shetani lakini walimshinda Shetani. Watu wateule wa Uchina wamevumilia mateso ya kikatili na kinyama na udanganyifu wa joka kuu jekundu, ambalo limewaacha wakiwa wenye akili iliyoharibiwa na bila ujasiri hata kidogo wa kuishi. Hivyo, kuamshwa kwa roho zao lazima kuanze na kiini chao: Kidogo kidogo, katika kiini chao, roho zao lazima ziamshwe. Watakapokuja katika uzima siku moja, hakutakuwa na vizuizi tena, na yote yataendelea bila taabu. Wakati huu, hili linabakia kuwa kitu kisichoweza kufanikishwa. Watu wengi wanaishi kwa njia ambayo inatoa hali nyingi za mauti; wamegubikwa katika hali ya kuwepo kwa mauti, na kuna mengi ambayo wanakosa. Maneno ya watu wengine yamebeba mauti, matendo yao yamebeba mauti, na karibu kila kitu wanachoishi kwa kudhihirisha kinajumuisha mauti. Iwapo, leo, watu wanatoa ushuhuda kwa Mungu hadharani, basi watashindwa katika kazi hii, kwa kuwa bado hawajakuja katika uzima kwa ukamilifu, na kuna wengi sana waliokufa miongoni mwenu. Leo, watu wengine wanauliza ni kwa nini Mungu haonyeshi ishara na maajabu ili kuweza kueneza kazi Yake kwa haraka kwa watu wa Mataifa. Watu waliokufa hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu; hicho ni kitu ambacho walio hai tu wanaweza kufanya, na bado watu wengi leo hawana uzima; wengi sana wanaishi chini ya gubiko la mauti, chini ya ushawishi wa Shetani, na hawawezi kuushinda. Kwa sababu hiyo, je, watawezaje kutoa ushuhuda kwa Mungu? Je, watawezaje kueneza kazi ya injili?
Wale wote wanaoishi chini ya ushawishi wa giza ni wale ambao wanaishi kati ya mauti, hao wanamilikiwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu hawawezi kuepuka ushawishi wa mauti; hawawezi kuwa wenye uzima. Waliokufa kama hao hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, au kutumiwa na Mungu, sembuse kuingia katika ufalme. Mungu anataka ushahidi wa walio hai, sio wa waliokufa, na Anataka walio hai, sio waliokufa, wamfanyie kazi. “Waliokufa” ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu; ni wale ambao wamekufa ganzi kiroho na hawaelewi maneno ya Mungu; ni wale ambao hawaweki ukweli katika vitendo na hawana uaminifu hata kidogo kwa Mungu, na ni wale ambao wanaishi chini ya nguvu za Shetani na wanatumiwa na Shetani. Maonyesho ya waliokufa ni kupinga ukweli, kumwasi Mungu, na kuwa duni, hafifu, wakatili, wadhalimu, wajanja, na wenye hila. Hata watu kama hao wakila na kunywa maneno ya Mungu, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; ingawa ni wazima, wao ni maiti zinazotembea, waliokufa wanaopumua. Waliokufa hawana uwezo hata kidogo wa kumridhisha Mungu, wala kuwa watiifu kabisa Kwake. Wanaweza tu kumdanganya, kumkufuru, na kumsaliti, na yale wanayoishi kwa kudhihirisha kwa ukamilifu ni ufunuo wa asili ya Shetani. Iwapo watu wanataka kuwa walio hai na kutoa ushuhuda kwa Mungu, na kuonekana wenye kustahili kwa Mungu, basi wapaswa kuukubali wokovu wa Mungu; lazima watii hukumu na kuadibu Kwake kwa ukunjufu na lazima wakubali upogoaji wa Mungu kwa ukunjufu. Ni wakati huo tu ndiyo wataweza kuweka ukweli wote unaohitajika na Mungu katika vitendo, na ni wakati huo tu ndiyo watapata wokovu wa Mungu na kuwa viumbe hai kweli. Walio wazima ndio wale ambao wameokolewa na Mungu; wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wako radhi kujitoa na wana furaha kutoa uhai wao kwa ajili ya Mungu, na wana furaha kutumia maisha yao yote kwa Mungu. Ni wakati tu ambapo walio hai wanatoa ushuhuda kwa Mungu ndipo Shetani ataaibishwa; ni walio hai tu ndio wanaoweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaopatana na nia ya Mungu, na walio hai tu ndio watu halisi. Mwanzoni mwanadamu aliyeumbwa na Mungu alikuwa na uzima, lakini kwa sababu ya upotovu wa Shetani mwanadamu anaishi kati ya mauti na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo, kwa njia hii, watu wamekuwa waliokufa wasio na roho, wamekuwa maadui wanaompinga Mungu, wamekuwa vifaa vya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu walio hai walioumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda Wake, na Amewapoteza binadamu, ambao Aliwaumba na ambao ndio kitu pekee kilicho na pumzi Yake. Kama Mungu atarejesha ushuhuda Wake na kuwarejesha wale walioumbwa kwa mkono Wake lakini wamechukuliwa mateka na Shetani, basi lazima Awafufue ili wawe viumbe hai, na lazima Awakomboe wote ili waishi katika mwanga Wake. Waliokufa ni wale ambao hawana roho, ambao wamekufa ganzi kabisa, ambao wanampinga Mungu, na hata zaidi, ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata kidogo ya kumtii Mungu; wao wanamwasi na kumpinga Yeye tu na hawana uaminifu hata kidogo. Walio hai ni wale ambao roho zao zimeamshwa, wanaojua kumtii Mungu, ambao ni waaminifu kwa Mungu, na ambao wana ukweli na ushuhuda—hawa watu pekee ndio wanaomfurahisha Mungu katika nyumba Yake. Mungu anawaokoa wale ambao wanaweza kuja katika uzima, ambao wanaweza kuona wokovu wa Mungu, ambao wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu, ambao wako radhi kumtafuta Mungu, ambao wanaamini kupata mwili kwa Mungu, na ambao wanaamini katika kuonekana Kwake. Watu wengine wanaweza kuja katika uzima, na wengine hawawezi; hili linategemea kama asili yao inaweza kuokolewa au la. Watu wengi wamesikia maneno mengi ya Mungu lakini hawaelewi nia za Mungu, na bado hawana uwezo wa kuyatia katika vitendo. Watu kama hao hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli wowote na pia wanasumbua kazi ya Mungu kwa makusudi. Hawana uwezo wa kumfanyia Mungu kazi yoyote, na hawawezi kujitumia kwa ajili Yake—badala yake, wanatumia pesa za kanisa kwa siri na kuidoea nyumba ya Mungu. Hawa ni watu waliokufa ambao hawawezi kuokolewa. Mungu anawaokoa wale wote ambao wako katikati ya kazi Yake, lakini kuna sehemu ya watu ambao hawawezi kupokea wokovu Wake; ni wachache tu ndio wanaoweza kupokea wokovu Wake. Hii ni kwa sababu watu wengi wamepotoshwa sana na wamekuwa waliokufa, na hawawezi kuokolewa tena; wametumiwa kikamilifu na Shetani, na asili yao ni ya uovu sana. Watu hawa wachache pia hawawezi kumtii Mungu kabisa. Hao sio wale ambao wamekuwa waaminifu kabisa kwa Mungu tangu mwanzo, au ambao wamekuwa na upendo mkubwa kwa Mungu tangu mwanzo; bali, wamekuwa watiifu kwa Mungu kwa sababu ya kazi Yake ya ushindi, wanamwona Mungu kwa sababu ya upendo Wake mkuu, wanafanikisha mabadiliko ya tabia kwa sababu ya tabia ya Mungu yenye haki, na wamemjua Mungu kwa sababu ya kazi Yake, kazi Yake ambayo ni ya vitendo na ya kawaida. Bila kazi hii ya Mungu, haijalishi watu hao ni wazuri kiasi gani, bado wangekuwa wa Shetani, na bado wangekuwa wa mauti, bado wangekuwa waliokufa. Uhakika kwamba watu hawa wanaweza kupokea wokovu wa Mungu leo ni kwa sababu tu kwamba wao wako radhi kushirikiana na Mungu.
Kwa sababu ya uaminifu wao kwa Mungu, walio hai watapatwa na Mungu na kuishi kati ya ahadi Zake, na kwa sababu ya kumpinga Mungu, waliokufa watachukiwa na Mungu na kuishi kati ya adhabu na laana Zake. Hivyo ndivyo ilivyo tabia ya Mungu yenye haki, ambayo haibadilishwi na mwanadamu yeyote. Kwa sababu ya kutafuta kwao, watu wanapokea kibali cha Mungu na kuishi katika mwanga; kwa sababu ya mipango yao ya ujanja, watu wanalaaniwa na Mungu na kuingia katika adhabu; kwa sababu ya vitendo vyao viovu, watu wanaadhibiwa na Mungu, na kwa sababu ya kiu na uaminifu wao, watu wanapokea baraka za Mungu. Mungu ni mwenye haki: Yeye huwabariki walio hai, na kuwalaani waliokufa ili wawe kati ya mauti daima na kamwe hawataishi katika mwanga wa Mungu. Mungu atawachukua walio hai katika ufalme Wake na kwenye baraka Zake, kuwepo pamoja na Yeye kwa wakati wote. Lakini kwa wale waliokufa, Atawapeleka kwenye mauti ya milele; hao ndio walengwa wa maangamizo Yake na daima watakuwa wa Shetani. Bila shaka Mungu hawezi kumtendea mtu yeyote bila haki. Wale wote wanaomtafuta Mungu kwa kweli watabakia katika nyumba ya Mungu, na wale wote wanaomwasi Mungu na hawalingani na Yeye kwa hakika wataishi kati ya adhabu Yake. Pengine huna uhakika kuhusu kazi inayofanywa na Mungu mwenye mwili—lakini siku moja, mwili wa Mungu hautapanga matokeo ya mwanadamu moja kwa moja; badala yake, Roho Wake atapanga hatima ya mwanadamu, na wakati huo watu watajua kwamba mwili wa Mungu na Roho Wake ni mmoja, kuwa mwili Wake haufanyi makosa, na Roho Wake vile vile hata zaidi. Hatimaye, kwa hakika Atawachukua wale ambao wamekuja katika uzima kwenye ufalme Wake; kwa idadi kamili. Kwa wale waliokufa, ambao hawajakuja katika uzima, kwa hakika watatupwa kwenye tundu la Shetani.