Kazi na Kuingia (5)

Leo wote mnajua kwamba Mungu anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuchukua hatua inayofuata kuingia katika enzi nyingine, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuvuka mipaka ya enzi hii ya kale ya giza, kutoka katika mwili, kutoka kwenye ukandamizaji wa nguvu za giza na ushawishi wa Shetani, ili kila mtu aweze kuishi katika ulimwengu wa uhuru. Kwa ajili ya kesho ya kupendeza, ili kwamba watu wawe wakakamavu katika hatua zao kesho, Roho wa Mungu anapanga kila kitu kwa ajili ya mwanadamu, na ili mwanadamu aweze kuwa na furaha kubwa zaidi, Mungu anajitolea jitihada Zake zote katika mwili Akiandaa njia mbele ya mwanadamu, ili siku ambayo mwanadamu anaitamani sana iweze kuja haraka. Nyote mngeweza kufurahia wakati huu mzuri; si tendo rahisi kufanya mkutano na Mungu. Ingawa hamjawahi kumjua, tayari mmekuwa pamoja naye tangu kitambo. Laiti kila mtu angeweza kukumbuka milele siku zote hizi nzuri lakini fupi, na kuzifanya kuwa mambo yao ya kuwafurahisha duniani. Kazi ya Mungu tangu zamani imefichuliwa kwa mwanadamu—lakini kwa sababu mioyo ya watu ni yenye utata sana, na kwa sababu hawajawahi kuwa na shauku kwayo, kazi ya Mungu imebaki ikiwa imesitishwa juu ya msingi wake wa asili. Mawazo yao, fikira, na mtazamo wa akili, ingeonekana, inasalia iliyopitwa na wakati, kiasi kwamba mtazamo wa akili wa wengi wao unafanana na ule wa washenzi wa nyakati za kale, na haujabadilishwa hata kidogo. Kutokana na hilo, watu bado wamekanganyikiwa na hawajui kuhusu kazi ambayo Mungu anafanya. Wao hata hawajui zaidi kuhusu kile wanachofanya na kile wanachopaswa kuingia ndani. Mambo haya yanaleta matatizo makubwa kwa kazi ya Mungu na kuzuia maisha ya watu kwenda mbele. Kwa sababu ya kiini cha mwanadamu na ubora wake duni wa tabia, hawezi kuifahamu kazi ya Mungu, na kamwe hayachukulii mambo haya kuwa muhimu. Ikiwa mnataka maendeleo katika maisha yenu, lazima mwanze kuzingatia utondoti wa kuishi kwenu, mkifahamu kila mojawapo ili kudhibiti kuingia kwenu katika maisha, mbadilishe kabisa moyo wa kila mmoja wenu, na kutatua matatizo ya utupu ndani ya mioyo yenu na kuwepo kwa uchachu na kuchosha ambako kunawaumiza, ili kila mmoja wenu atafanywa upya kutoka ndani hadi nje na kufurahia kweli maisha ambayo yamerefushwa, ya miujiza, na huru. Lengo ni kwamba kila mmoja wenu ataweza kuwa hai, kuhuishwa katika roho zenu, na kuwa na mfano wa kiumbe hai. Kati ya ndugu wote mnaowasiliana nao, ni mara chache kuna yeyote ambaye ni mwenye kusisimua na wa kupendeza. Wote ni kama sokwe watu wa kale, punguani na wajinga, inavyoonekana bila matarajio yoyote ya maendeleo. Jambo baya hata zaidi, ndugu ambao Nimewasiliana nao wamekuwa fidhuli na wasiostaarabika kama nduli wa mlimani. Hawajui chochote kuhusu tabia, seuze mambo ya msingi ya jinsi ya kutenda. Kuna dada wadogo wengi ambao, ingawa wanaweza kuonekana wenye akili na wenye sura nzuri, na wamekua wazuri kama maua, bado wanajiingiza katika mtindo “mbadala.” Nywele za dada[a] mmoja zinaufunika uso wake wote, bila kuonyesha macho yake hata kidogo. Ingawa sehemu za uso wake ni safi na zenye heshima, mtindo wa nywele zake ni wa kukirihi, ukitoa hisi ya kuogofya, kama kwamba yeye ni mkosaji mkuu katika jela ya vijana. Macho yake, yaliyo meupe na maangavu kama zumaridi katika maji, yanasawazishwa na mavazi na mtindo wa nywele zake, na kuyafanya kuwa kama taa mbili, zinazoonekana ghafla usiku wa giza kuu, yanayomulika kwa vipindi kwa mng’aro wa kupofusha ambao hutia hofu katika mioyo ya wanaume, na bado inaonekana kana kwamba anajificha kwa makusudi kutoka kwa mtu fulani. Wakati Ninapokutana naye, daima yeye hujaribu kupanga njia za kuondoka katika “mandhari” hayo, kama mwuaji ambaye amemwua mtu fulani na, kwa hofu kuu ya kupatikana, daima anakwepa; kwa hiyo, pia, yeye ni kama Waafrika weusi[1] ambao wamekuwa watumwa kwa vizazi vingi na hawawezi kuinua vichwa vyao mbele ya wengine. Mpangilio huu maalum wa tabia, hadi jinsi watu hawa huvaa na kujinadhifisha, ingechukua miezi kadhaa ya kazi ili kuiboresha.

Kwa maelfu ya miaka, Wachina wameishi maisha ya utumwa na hii imebana sana fikira, mawazo, maisha, lugha, tabia, na matendo yao kiasi kwamba wamebaki bila uhuru wowote. Maelfu kadhaa ya miaka ya historia imewachukua watu muhimu waliomilikiwa na roho na kuwadhoofisha hadi kuwa kitu kinachofanana na maiti iliyoondokewa na roho. Wengi ni wale wanaoishi chini ya kisu cha kuchinja cha Shetani, wengi wanaishi katika makazi yanayofanana na pango la mnyama, wengi wanakula chakula kama wanachokula ng’ombe au farasi, wengi wapo katika mchafuko huko “ahera” na hawana maana kabisa. Katika umbo la nje, watu hawana tofauti na watu wa zamani, sehemu yao ya kupumzika ni kama kuzimu, na wote wanaowazunguka ni mashetani na pepo wachafu. Kwa umbo la nje, wanadamu wanaonekana kuwa ni “wanyama” wa tabaka ya juu; kwa kweli wanaishi na kukaa na mashetani wachafu. Bila mtu yeyote kuwashughulikia, watu wanaishi katika mtego uliojificha wa Shetani, na wamenaswa kabisa katika kazi zake za taabu kiasi kwamba hawawezi kutoroka. Hawakusanyiki na wapendwa wao katika makazi yao ya furaha, kuishi kwa furaha na kuyaishi maisha ya kuridhisha, bali wanaishi Kuzimu, wakishughulika na pepo na kushirikiana na mashetani. Kwa kweli, watu bado wamefungwa na Shetani, wanaishi mahali ambapo pepo wachafu wanakusanyika, na wanatawaliwa na hawa pepo wachafu, na ni kana kwamba vitanda vyao ni mahali ambapo maiti zao zimelala, kana kwamba ni sehemu zao za kustarehe. Uingiapo nyumbani kwao, uwanja ni baridi na pweke, upepo wa kuzizima ukipiga mluzi kupitia matawi makavu. Kufungua mlango kuelekea “eneo la kuishi,” chumba ni cheusi kabisa—ungeweza kunyoosha mkono wako na usione vidole vyako. Mwangaza mdogo unapenya ndani kupitia ufa katika mlango, ambao unafanya chumba kusononesha hata na kutisha hata zaidi. Mara kwa mara, panya hutoa vilio vyembamba vya ajabu, kana kwamba wanajifurahisha. Yote ndani ya chumba ni ya kutia kinyaa na ya kutisha, kama nyumba ambayo mtu aliyekuwa akiishi ndani amewekwa kwenye jeneza sasa hivi. Kitanda, mafarishi, na kabati dogo lisilo la kawaida ndani ya chumba vyote vimefunikwa kwa vumbi, chini kuna vigoda kadhaa vidogo vikikenua meno yao na kutia tahabibu kucha zao, na utando wa buibui unaning’inia juu ya kuta. Kioo kiko juu ya meza, kitana cha mbao kikiwa karibu nacho. Unapotembea kuelekea kwa kioo, unachukua mshumaa na kuuwasha. Unaona kwamba kioo kimefunikwa na vumbi, na kufanya aina ya “vipodozi” juu ya picha za watu[b] ili kwamba wanaonekana kana kwamba wametoka kaburini hivi sasa. Kitana kimejaa nywele. Vitu hivi vyote ni vya zamani na, visivyostaarabika na vinaonekana kana kwamba vimetumika hivi sasa na mtu aliyekufa hivi sasa. Ukiangalia kitana, unahisi kana kwamba kuna maiti iliyolala kwa upande mmoja. Nywele zilizo katika kitana, bila damu kuzunguka ndani yake, zina harufu ya wafu juu yake. Upepo wa kuzizima unaingia kupitia kwa ufa ulio katika mlango, kana kwamba pepo anajipenyeza kupitia kwa ufa, akirudi kuishi ndani ya chumba. Kuna mzizimo wa kukandamiza katika chumba, na ghafla, uvundo kama wa maiti inayooza, na kwa wakati huu inaweza kuonekana kuwa kuna mchanganyiko wa vitu vinavyoning’inia juu ya kuta, juu ya kitanda kuna matandiko yasiyo nadhifu, machafu na yenye harufu mbaya, kuna nafaka pembeni, kabati limefunikwa kwa vumbi, sakafu imefunikwa kwa matawi na uchafu, na kadhalika—kana kwamba vimetumika sasa hivi na mtu aliyekufa, akielemea mbele, akisaga meno yake na kupapura hewa. Hii inatosha kukutetemesha. Hakuna dalili ya uhai mahali popote katika chumba, chote ni giza na chenye unyevu, kama Kuzimu na jahanamu zilizotajwa na Mungu. Hili ni kama tu kaburi la mwanadamu, likiwa na kabati ambalo halijapakwa rangi, vigoda, viunzi vya madirisha, na milango iliyovishwa nguo za kuomboleza na kuwatukuza wafu kwa kimya. Mwanadamu amekuwa akiishi katika ahera hii kwa miongo kadhaa, au karne kadhaa, au hata milenia kadhaa, akienda nje mapema na kurudi akiwa amechelewa. Anajitokeza kwa “kaburi” lake alfajiri, wakati majogoo wanapowika, na kuangalia juu angani na kutazama chini ardhini, na kuanza shughuli zao za siku. Wakati jua linapotua, yeye hukokota mwili wake uliochoka na kurudi “kaburini”; kufikia wakati anapojaza tumbo lake inakuwa ni magharibi. Kisha, baada ya kumaliza maandalizi yake ya kuondoka “kaburini” tena keshoye, yeye huizima taa, ambayo inaonekana kutoa miali ya mioto ya mmemetuko. Wakati huu, yote ambayo yanaweza kuonekana chini ya mbalamwezi ni matuta ya makaburi yaliyoenea kama viduta vidogo katika kila pembe. Kutoka ndani ya “makaburi” inatokea sauti ya mikoromo ya mara kwa mara, ikiinuka na kushuka. Watu wote wanalala fofofo, na pepo wachafu na vizuka pia wanaonekana wakipumzika kwa amani. Mara kwa mara, mtu anasikia kunguru wakilia kutoka mbali—sauti ya vilio hivi vya huzuni katika usiku mtulivu na ulio kimya kama huu inatosha kusababisha kuwa na wasiwasi mkuu na kukuogofya sana.... Ni nani anayejua ni miaka mingapi waliyoishi katika mazingira kama haya, wakifa na kuzaliwa upya, nani ajuaye ni muda gani wamebakia katika ulimwengu wa binadamu ambapo watu na vizuka huchanganyika, na zaidi, ni nani anayejua mara ngapi wameuaga ulimwengu! Katika jahanamu hii iliyo duniani wanadamu huishi maisha ya furaha, kana kwamba hawana lalamiko hata moja, kwani kwa muda mrefu wamezoea maisha Kuzimuni. Na kwa hiyo, watu huvutiwa sana na mahali hapa ambapo pepo wachafu hukaa, kana kwamba pepo wachafu ni marafiki wao na wenzi wao, kana kwamba ulimwengu wa mwanadamu ni kikosi cha majambazi[2]—kwani kiini cha asili cha mwanadamu kwa muda mrefu kimetoweka bila mnong’ono, kimepotea kisionekane tena. Kuonekana kwa watu kuna kitu fulani cha pepo mchafu; zaidi ya hayo, matendo yao yanaendeshwa na pepo wachafu. Leo, wao hawaonekani tofauti na pepo wachafu, ni kana kwamba walizaliwa kutoka kwa pepo wachafu. Zaidi ya hayo, watu pia wanapenda sana, na kuwaunga mkono, mababu zao. Hakuna ajuaye kwamba tangu wakati huo mwanadamu amekandamizwa sana na Shetani mpaka amekuwa kama sokwe milimani. Macho yao mekundu yana mtazamo wa kusihi, na katika nuru iliyofifia iangazayo kutoka kwao ni dalili hafifu ya uovu wa chuki wa pepo mchafu. Nyuso zao zimefunikwa na kunyanzi, zimepasuka kama ganda la msonobari, midomo yao inachomoza nje, kana kwamba imeundwa na Shetani, masikio yao yamefunikwa na masizi ndani na nje, migongo yao imepindwa, miguu yao inang’ang’ana kuhimili miili yao, na mikono yao myembamba inacheza nyuma na mbele kwa mahadhi safi. Ni kana kwamba ni ngozi na mfupa tu, lakini tena wao ni wanene kama dubu wa mlimani. Ndani na nje, wamejipamba na kuvaa kama sokwe kutoka nyakati za zamani—ni kana kwamba, leo, hawa sokwe bado hawajageuka kuwa na[3] umbo la mtu wa kisasa, hivyo ndivyo walivyo nyuma!

Mwanadamu anaishi bega kwa bega na wanyama, na wanatembea pamoja kwa amani, bila ugomvi au vita vya maneno. Mwanadamu ni mgumu kuridhika vile anavyowajali na anavyohusika na wanyama, na wanyama wapo kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu, hasa kwa manufaa ya mwanadamu, bila wao kunufaika na chochote na kwa kumtii mwanadamu kikamilifu. Kwa namna zote, uhusiano kati ya mwanadamu na mnyama ni wa karibu[4] na wa kukubaliana[5]—na pepo wachafu, inaweza kuonekana, ni muungano kamilifu wa mwanadamu na mnyama. Hivyo, mwanadamu na pepo wachafu walio duniani hata ni marafiki wema zaidi na wasiotengana: Mwanadamu anaonekana kufarakana na pepo wachafu, lakini kimsingi ameunganika nao; wakati huo, pepo wachafu hawamnyimi mwanadamu kitu chochote, na “wanatoa” vyote walivyonavyo kwao. Kila siku, watu wanachacharika katika “kasri la mfalme wa kuzimu,” wakichezacheza na “mfalme wa kuzimu” (babu yao) na kutawaliwa naye, ili kwamba, leo, watu wamepakwa masizi, na, baada ya kuishi muda mrefu sana Kuzimuni, wana muda mrefu toka waache kutamani kurudi katika “dunia ya walio hai.” Hivyo, mara tu wanapoiona nuru, na kutazama matakwa ya Mungu, na tabia ya Mungu, na kazi ya Yake, wanahisi dukuduku na wasiwasi; bado wakitamani sana kurudi kuzimu na kuishi na mizimu. Walimsahau Mungu zamani sana, na hivyo wamekuwa wakizungukazunguka katika makaburi. Ninapokutana na mtu, Najaribu kuzungumza naye, na wakati huu tu ndipo Nagundua kwamba mtu aliyesimama mbele Yangu si mwanadamu kabisa. Nywele zake ni chafu, uso wake ni mchafu, na kuna kitu kama mbwa-mwitu kuhusu tabasamu lake la kuonyesha jino. Kwa hiyo, pia, anaonekana kuwa na ukorofi wa pepo ambaye ametoka tu kaburini na kumwona mwanadamu wa dunia iliyo hai. Mtu huyu daima hujaribu kuunda midomo yake kuwa tabasamu; inaonekana kuwa yenye kudhuru kwa siri na mbaya. Anaponionyesha tabasamu, ni kama kwamba ana jambo la kusema lakini anaonekana hana maneno ya kueleza, na kwa hiyo anaweza tu kusimama upande mmoja, akionekana kukosa ufahamu na mjinga. Kutoka nyuma, anaonekana kuwasilisha “sura ya nguvu ya watu wa Kichina wanaofanya kazi”; nyakati hizi anaonekana wa kuchukiza sana hata zaidi, ukikumbuka sura ya vizazi vya Yan Huang/Yan Wang wa zamani[c] ambavyo watu huzungumzia. Ninapomwuliza, anainamisha kichwa chake akiwa kimya. Inamchukua muda mrefu kujibu, na amejizuia sana anapofanya hivyo. Yeye hawezi kutuliza mikono yake, na anavinyonya vidole vyake viwili kama paka. Sasa tu ndio Natambua kwamba mikono ya yule mtu inaonekana kama kwamba imekuwa ikipekua katika takataka sasa hivi, na makucha yenye umbo lisilo sawa yaliyogeuka rangi sana kiasi kwamba mtu hawezi kamwe kujua kwamba yalitakiwa kuwa meupe, makucha “membamba” ambayo yamezungukwa sana na uchafu. Hata la kuchukiza zaidi, pande za nyuma za mikono yake zinafanana na ngozi ya kuku ambaye amenyonyolewa hivi sasa. Mistari iliyo mikononi mwao karibu yote imejaa thamani ya damu na jasho la kazi za mwanadamu, ndani ya kila mstari kuna kitu ambacho kinafanana na uchafu, kinachoonekana kuwa kinatoa “harufu nzuri ya udongo,” bora zaidi kuwakilisha thamani na kustahili kusifiwa kwa roho ya mwanadamu ya kuteseka—ili roho hii ya kuteseka imetiwa hata ndani zaidi ya kila mstari ulio juu ya mikono ya mwanadamu. Kutoka utosini hadi kidoleni, hakuna nguo anayovaa mwanadamu inayofanana na ngozi ya mnyama iliyo na manyoya, lakini hawajui kwamba, hata wakiwa “waheshimiwa” sana, thamani yao kwa kweli ni ya chini kuliko ile ya manyoya ya mbweha—chini, hata, kuliko unyoya mmoja wa tausi, kwa kuwa kwa muda mrefu nguo zake zimemfanya kuwa mbaya sana kiasi cha kuonekana mbaya kuliko nguruwe na mbwa. Vazi lake dogo mno la juu linaning’inia nusu chini ya mgongo wake, na miguu ya suruali yake ndefu—kama matumbo ya kuku—inaonyesha kwa ukamilifu ubaya wake kwa nuru ya jua yenye kung’aa. Nguo hizo ni fupi na nyembamba, kana kwamba kwa ajili ya kuonyesha kwamba miguu yake imefunguliwa kwa muda mrefu: Ni miguu mikubwa, sio tena “inchi tatu ya yungiyungi za dhahabu za inchi tatu” za jamii ya zamani. Mavazi ya mtu huyu yamefanywa ya kimagharibi sana, lakini pia ni duni mno. Nikutanapo naye, yeye daima ni mwenye haya, uso wake ukibubujika kwa wekundu, na hawezi kuinua kichwa chake kabisa, kana kwamba amekanyagiwa chini na pepo wachafu, na hawezi kuwa na ujasiri wa kuwaangalia watu usoni tena. Vumbi hufunika uso wa mwanadamu. Vumbi hili, ambalo limeanguka kutoka angani, linaonekana kuanguka kwa njia isiyo ya haki juu ya uso wa mwanadamu, na kuufanya uonekane kama manyoya laini ya jurawa. Macho ya mwanadamu ni kama ya jurawa, pia: madogo na makavu, bila mng’aro wowote. Anapozungumza, kwa kawaida kunena kwake ni kwa kusitasita na kuepaepa, kunachukiza sana na kuwaudhi wengine. Hata hivyo wengi huwatukuza watu hao kama “wawakilishi wa taifa.” Je, huu sio utani? Mungu anataka kuwabadilisha watu, kuwanusuru, kuwaokoa kutoka kwa kaburi la kifo, ili waweze kuepukana na maisha wanayoishi Kuzimu na jahanamu.

Tanbihi:

1. “Waafrika weusi” inahusu watu weusi ambao walilaaniwa na Mungu, ambao wamekuwa watumwa kwa vizazi vingi.

2. “Kikosi cha majambazi” ni sitiari inayomaanisha kundi la waovu. Inahusu upotovu wa wanadamu, na jinsi hakuna watu watakatifu miongoni mwa wanadamu.

3. Sentensi hii inahusu “mageuzi” ya sokwe watu kuwa na umbo la watu wa kisasa. Lengo ni la tashtiti: Hakuna, kwa kweli, kitu kama nadharia ya sokwe wa kale kugeuka kuwa wanadamu wanaotembea wima.

4. “Wa karibu” inatumiwa kwa dhihaka.

5. “Wa kukubaliana” inatumiwa kwa mzaha.

a. Maandishi ya asili yanasoma “Yeye.”

b. Maandishi ya asili yanasoma “nyuso za watu.”

c. “Yan” na “Huang” ni majina ya watawala wawili wa mithiolojia ambao walikuwa miongoni mwa watoaji wa kwanza wa utamaduni wa China. “Yan Wang” ni jina la Kichina la “mfalme wa kuzimu.” “Yan Huang” na “Yan Wang” yanakaribia kuwa homofonia yanapotamkwa katika lugha ya Mandarin.

Iliyotangulia: Kazi na Kuingia (4)

Inayofuata: Kazi na Kuingia (6)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp