Kazi na Kuingia (4)

Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani. “Wanajificha wenyewe katika unyenyekevu.” Ukweli ni kwamba, ni wachache miongoni mwenu mnaojua makusudi ya Mungu kuhusu siku za mwisho. Ni wachache sana miongoni mwenu wanaojua nyayo za Mungu, lakini hata mbaya zaidi, hakuna anayejua utimilifu wa mwisho wa Mungu utakavyokuwa. Halafu kila mtu, kwa utashi tupu, anakubali kufundishwa nidhamu na kushughulikiwa na wengine, kana kwamba wanapiga misuli na kujitayarisha kwa vita[1] wakiwa wakisubiri wakati wao wa ushindi. Sitatoa maoni yoyote juu ya “maajabu” haya miongoni mwa watu, lakini kuna hoja moja ambayo wote mnapaswa kuielewa. Kwa sasa watu wengi wanakua wakielekea katika hali isiyo ya kawaida,[2] na kwa hatua zao za kuingia ndani wanaandamana kuelekea mwisho kabisa.[3] Kunaweza kuwa na watu wengi wanaofikiri kwamba ni jamii nje ya ulimwengu wa mwanadamu ambao mwanadamu anatamani, akiuamini kuwa ufalmewa uhuru, lakini kwa hakika sivyo ilivyo. Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekwishapotoka tayari. Lakini bila kujali kile watu wanachokifanya, bado Nahitaji kuzungumza juu ya kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia ndani. Ustahilifu na kasoro za umati sio mada ya msingi ya majadiliano haya. Natumaini kwamba ndugu wote wataweza kupokea maneno Yangu kabisa na kwa usahihi na sio kuelewa visivyo nia Yangu.

Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu Anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajiachilii mbali. Mtu anaweza kusema kwamba inaonekana kama hatua hii ya kazi Yake inafanyika mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu Atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, binadamu wote wataachana na mtazamo wao wa kawaida,[4] na kuamka kutoka katika ndoto yao ndefu. Nakumbuka Mungu Alishawahi kusema, “Kuja katika mwili wakati huu ni sawa na kuanguka katika tundu la duma.” Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika Mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, hata kuliko awali, Anakumbwa na hatari kubwa kwa kuja duniani wakati huu. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na kumbi za starehe; Anavyokabiliana navyo ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura za wauaji. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote. Mungu Alikuja na ghadhabu. Hata hivyo, Alikuja ili Aweze kufanya kazi ya utakasaji, ikiwa na maana kwamba kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake inayoendelea baada ya kazi ya wokovu. Kwa ajili ya hatua hii ya kazi Yake, Mungu Amejitolea mawazo na uangalizi wa hali ya juu kabisa na Anatumia njia yoyote inayoweza kufikiriwa ili kuepuka mashambulio ya majaribu, Anajificha katika unyenyekevu Wake na kamwe haringii utambulisho Wake. Katika kumwokoa mwanadamu msalabani, Yesu Alikuwa Anakamilisha tu kazi ya wokovu; Alikuwa hafanyi kazi ya utakasaji. Hivyo ni nusu tu ya kazi ya Mungu ndiyo ilikuwa inafanywa, na kukamilisha kazi ya ukombozi ilikuwa ni nusu ya mpango Wake mzima. Kwa kuwa enzi mpya ilikuwa inakaribia kuanza na ile ya zamani kukaribia kutoweka, Mungu Baba Alianza kukusudia sehemu ya pili ya kazi Yake na Akaanza kujiandaa kwa ajili yake. Wakati uliopita, kupata mwili huku katika siku za mwisho huenda hakukutolewa unabii, na hivyo kuweka msingi wa usiri mkubwa unaozunguka ujio wa Mungu katika mwili kipindi hiki. Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu Alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari Amekwishawasili duniani. Mungu Alifanya hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwishakamilika zamani sana na Ataondoka, na kufunga maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani. Kwa kuwa kazi ya Mungu inamtaka Mungu kutenda na kuzungumza kwa nafsi Yake mwenyewe, na kwa kuwa hakuna namna ambayo mwanadamu anaweza kuingilia kati, Mungu Ameyavumilia maumivu makali ya kuja duniani kufanya kazi Yeye Mwenyewe. Mwanadamu hawezi kushikilia nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hiyo Mungu Alijihatarisha mara elfu kadhaa kuliko ilivyokuwa katika wakati wa Enzi ya Neema na kuja chini mahali ambapo joka kuu jekundu linaishi ili kufanya kazi Yake, kuweka mawazo Yake yote na uangalizi katika kuokoa kundi hili la watu maskini, kulikomboa kundi hili la watu lililogeuka na kuwa rundo la samadi. Ingawa hakuna anayejua uwepo wa Mungu, Mungu Hahangaiki kwa sababu ni faida kubwa kwa kazi ya Mungu. Kila mtu ni mwovu sana, sasa inawezekanaje kila mtu avumilie uwepo wa Mungu? Ndiyo maana duniani, Mungu Anakuwa kimya siku zote. Haijalishi mwanadamu ni katili kiasi gani, Mungu wala Hazingatii hayo moyoni Mwake hata kidogo, bali Anaendelea kufanya kazi Anayotaka kufanya ili kutimiza agizo kuu ambalo Baba wa mbinguni Alimpatia. Ni nani miongoni mwenu aliyetambua upendo wa Mungu? Ni nani anayejali sana mzigo Alionao Mungu Baba kuliko Mwana Wake Anavyofanya? Ni nani awezaye kuelewa mapenzi ya Mungu Baba? Roho wa Mungu Baba Aliyeko mbinguni Anasumbuka kila mara, na Mwana Wake duniani Anaomba mara kwa mara juu ya mapenzi ya Mungu Baba, Akihofia moyo Wake kuumia. Kuna mtu yeyote anayejua kuhusu upendo wa Mungu Baba kwa Mwana Wake? Kuna mtu yeyote anayejua jinsi ambavyo Mwana mpendwa Anavyomkumbuka Mungu Baba? Wakipata shida ya kuchagua kati ya mbingu na nchi, utaona wawili Hawa wanatazamana wakati wote kutoka kwa mbali, sambamba na Roho. Ee binadamu! Ni lini mtaufikiria moyo wa Mungu? Ni lini mtaielewa nia ya Mungu? Baba na Mwana siku zote Wamekuwa Wakitegemeana. Kwa nini tena Watengane, mmoja juu mbinguni na mmoja chini duniani? Baba Anampenda Mwana Wake kama vile Mwana Anavyompenda Baba Yake. Kwa nini sasa asubiri kwa muda mrefu huku Akiwa na shauku hiyo? Ingawa Hawajatengana kwa muda mrefu, je, mtu yeyote anajua kwamba Baba tayari Amekuwa Akitaka sana kwa shauku kwa siku nyingi na Amekuwa Akitarajia kwa muda mrefu kurudi haraka kwa Mwana Wake mpendwa? Anatazama, Anakaa kwa utulivu, Anasubiri. Hii yote ni kwa ajili ya kutaka Mwana Wake mpendwa Arudi haraka. Ni lini Atakuwa tena na Mwana ambaye Anazungukazunguka duniani? Ingawa watakapokuwa pamoja tena, Watakuwa pamoja milele, Anawezaje kustahimili maelfu ya siku za utengano, mmoja juu mbinguni na mwingine chini duniani. Makumi ya miaka duniani ni kama maelfu ya miaka mbinguni. Mungu Baba Anawezaje kutokuwa na wasiwasi? Mungu Anapokuja duniani, Anakabiliana na mabadiliko mengi ya ulimwengu wa kibinadamu kama mwanadamu. Mungu Mwenyewe hana hatia, sasa kwa nini Mungu Ateseke kwa maumivu kama mwanadamu? Pengine ndiyo maana Mungu Baba Anatamani sana Mwana Wake Arudi haraka; nani awezaye kuujua moyo wa Mungu? Mungu Anampatia mwanadamu vitu vingi sana; mwanadamu anawezaje kuulipa moyo wa Mungu kikamilifu? Lakini mwanadamu anampatia Mungu kidogo sana; sasa Mungu Atawezaje kutokuwa na wasiwasi?

Ni wachache sana miongoni mwa wanadamu wanaouelewa moyo wa Mungu kwa sababu tabia za watu ni duni sana na hisia zao za kiroho zimepoa sana, na kwa sababu hawaoni wala kutilia maanani kile ambacho Mungu anafanya. Hivyo Mungu Anaendelea kuwa na hofu juu ya mwanadamu, kana kwamba asili ya tabia ya wanyama ndani ya mwanadamu inaweza kuonekana muda wowote. Hii inaonyesha zaidi kwamba kuja kwa Mungu duniani kunaambatana na majaribu makubwa. Lakini kwa ajili ya kukamilisha kundi la watu, Mungu, Akiwa na utukufu, Alimwambia mwanadamu juu ya kila kusudi lake, bila kuficha kitu. Ameamua kwa dhati kukamilisha kundi hili la watu. Kwa hiyo, ije shida yoyote au jaribu, Anatazama mbali na kuyapuuzia yote. Anafanya kazi yake kimyakimya tu, Akiamini kwamba siku moja ambapo Mungu Atapata utukufu, mwanadamu atamjua Mungu, na kuamini kwamba mwanadamu atakapokuwa amekamilishwa na Mungu, atakuwa ameuelewa moyo wa Mungu kikamilifu. Sasa hivi kunaweza kuwepo watu wanaomjaribu Mungu au kumwelewa vibaya Mungu au kumlaumu Mungu; Mungu wala hayazingatii haya moyoni. Mungu atakapoingia katika utukufu, watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa ajili ya mema ya binadamu, na watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa sababu binadamu aweze kuishi vizuri. Ujio wa Mungu umeambatana na majaribu, na Mungu pia Anakuja katika adhama na ghadhabu Yangu. Muda ambapo Mungu Anamwacha mwanadamu, Atakuwa tayari Amepata utukufu, na Ataondoka Akiwa Amejawa na utukufu mwingi na furaha ya kurudi. Mungu Anayefanya kazi duniani Hazingatii mambo moyoni Mwake haijalishi watu wamemkataa kiasi gani. Yeye Anafanya tu kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa ulimwengu unaanzia mbali maelfu ya miaka huko nyuma, Amekuja duniani kufanya kazi isiyoweza kupimika, na Amepitia uzoefu mkubwa wa kukataliwa na kashfa. Hakuna anayekaribisha ujio wa Mungu; kila mtu anamwangalia tu kwa jicho kavu. Katika kipindi hiki cha maelfu ya miaka ya taabu, matendo ya mwanadamu yamevunjavunja moyo wa Mungu tangu zamani sana. Wala Hazingatii tena uasi wa watu, lakini badala yake Anatengeneza mpango tofauti ili kumbadilisha na kumsafisha mwanadamu. Dhihaka na kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu Alipitia Akiwa katika mwili, Mungu Amepitia ya kutosha. Dhihaka na kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu Alipitia Akiwa katika mwili, Mungu Amepitia ya kutosha. Mungu katika mwili Ameteseka kikamilifu na shida za ulimwengu wa wanadamu. Roho wa Mungu Baba wa mbinguni Aliona mambo hayo hayavumiliki na Akarudisha kichwa Chake nyuma na kufumba macho Yake, Akisubiri Mwana Wake mpendwa kurudi. Yote Anayoyatamani ni kwamba watu wote wasikie na kutii, waweze kuhisi aibu kubwa mbele ya mwili Wake, na wasiasi dhidi Yake. Anachokitamani ni kwamba watu wote waamini kwamba Mungu yupo. Aliacha zamani sana kutaka mambo makubwa kutoka kwa mwanadamu kwa sababu Mungu Amelipa gharama kubwa sana, lakini mwanadamu bado anajistarehesha,[5] na kamwe haiweki kabisa kazi ya Mungu moyoni mwake hata kidogo.

Ingawa vitu Ninavyozungumzia leo juu ya kazi ya Mungu vinaweza kuwa na mengi ambayo ni ya upuuzi kimsingi,”[6] hata hivyo kina makubwa yaliyo muhimu kwa kuingia kwa binadamu. Ninazungumza tu kiasi juu ya kazi na kisha kuzungumza kiasi juu ya kuingia, lakini kati ya vipengele hivi viwili, hakuna kisicho cha muhimu, na vikiunganishwa, vipengele hivi viwili ni vyenye manufaa zaidi kwa maisha ya mwanadamu. Hivi vipengele viwili ni vya kusaidiana[7] na ni vyenye manufaa sana, vikiwezesha watu kuyaelewa bora mapenzi ya Mungu na kuwezesha mawasiliano kati ya watu na Mungu. Kupitia kwa majadiliano ya leo juu ya kazi, uhusiano wa watu na Mungu unaboreshwa zaidi, kuelewa kwa pande mbili kunaongezeka, na mwanadamu anaweza kuzingatia zaidi na kujali kwa mzigo wa Mungu; mwanadamu anaweza kuhisi kile ambacho Mungu anahisi, kuwa na ujasiri zaidi juu ya kubadilishwa na Mungu, na kusubiri kuonekana tena kwa Mungu. Hili ni ombi pekee la Mungu kwa mwanadamu leo—kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu anayempenda Mungu, kuufanya ili kwamba mwanga wa kudhihirika kwa hekima ya Mungu utamulika katika enzi ya giza na ili kuishi kwa kudhihirisha kwa mwanadamu kuweze kuachaukurasa wa kung’aa katika kazi ya Mungu, uangaze milele katika Mashariki ya ulimwengu, ukiamuru uangalifu wa ulimwengu na uvutiwaji wa wote. Huku, kwa hakika, ni kuingia bora kwa wale wanaompenda Mungu leo.

Tanbihi:

1. “Wanapiga misuli na kujitayarisha kwa vita” imetumika kwa dhihaka.

2. “Isiyo ya kawaida” inamaanisha kwamba kuingia kwa watu kumeacha maadili na uzoefu wao unaegemea upande mmoja.

3. “Mwisho kabisa” kunamaanisha kwamba njia ambayo watu wanaifuata inaenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

4. “Kubadilika kutokana na mtazamo wao wa kawaida” inahusu jinsi fikira za watu na maoni kumhusu Mungu hubadilika mara tu wanapokuja kumjua Mungu.

5. “Anajistarehesha” inamaanisha kwamba watu hawapendezwi kuhusu kazi ya Mungu na hawaizingatii kama muhimu.

6. “Upuuzi usio na msingi” linamaanisha kwamba kimsingi watu hawawezi kuafikia chanzo cha maneno anayosema Mungu na hawajui kile Anachokizungumzia. Msemo huu hutumiwa kwa kejeli.

7. “Kupeana mkono” kunamaanisha kwamba kuchanganya “kazi” na “kuingia katika ushirika” kutakuwa kwa manufaa zaidi kwa ujuzi wetu kumhusu Mungu.

Iliyotangulia: Kazi na Kuingia (3)

Inayofuata: Kazi na Kuingia (5)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp