Sura ya 47

Ili kuwafanya wanadamu wawe wakomavu katika maisha na kuwafanya wanadamu na Mimi tuweze kutimiza matokeo katika udhanifu wetu wa pamoja, Nimewaendeka wanadamu kila mara, Nikiwakubalia kupata chakula na riziki kutoka kwa neno Langu na kupokea utele Wangu kutoka kwake. Sijawahi kuwapa wanadamu sababu ya kuaibika, lakini mwanadamu hafikirii hisia Zangu kamwe. Hii ni kwa sababu wanadamu hawana hisia na “hudharau” vitu vyote isipokuwa Mimi. Kutokana na dosari za wanadamu, Nawasikitikia sana na hivyo Nimefanya kila Niwezalo, ili waweze kufurahia utele wa dunia hadi kiasi cha kuiridhisha mioyo yao kwa wakati wao duniani. Simtendei mwanadamu bila haki na kwa kuzingatia watu walionifuata kwa miaka mingi, Nimekuwa na moyo wa huruma kwao. Ni kama kwamba Siwezi kujizuia kuweka mikono Yangu juu yao ili kufanya kazi Yangu. Kwa hiyo, Nawaangalia watu waliokonda wanaonipenda jinsi wanavyojipenda wenyewe na katika moyo Wangu daima huwa kuna hisia za maumivu zisizoweza kuelezeka, lakini ni nani angevunja mkataba kwa sababu ya hili? Ni nani angesumbua kwa sababu ya hili? Hata hivyo, Nimewakirimu wanadamu zawadi Zangu zote ili waweze kuzifurahia kwa ukamilifu, nami Sijawatesa wanadamu kuhusu suala hili. Ndio maana wanadamu bado wanauona uso Wangu wa huruma na wenye ukarimu. Nimevumilia na kusubiri kila mara. Wakati ambapo wanadamu wanafurahia kwa kuridhika na kisha kuchoshwa, Nitaanza “kukidhi” maombi yao na kuwaruhusu wanadamu wote kuepuka maisha yao matupu, na kisha Sitakuwa na shughuli tena na watu. Juu ya dunia, hapo awali Nilikuwa Nimewameza binadamu na maji ya bahari, Nilikuwa Nimewadhibiti kwa njaa, Nilikuwa Nimewatisha kwa tauni za wadudu, na Nilikuwa Nimetumia mvua nzito “kuwanyunyizia”, lakini mwanadamu hakuhisi utupu wa maisha hata kidogo. Sasa bado mwanadamu haelewi umuhimu wa kuishi duniani. Yawezekana kuwa kuishi katika kuwepo Kwangu ni kipengele muhimu sana cha maisha ya binadamu? Je, kuishi ndani Yangu kunamruhusu mtu kuepuka tishio la maafa? Ni miili mingapi ya nyama duniani imeishi katika uhuru wa kujifurahisha? Ni nani ameepuka utupu wa kuishi katika mwili? Na nani angeujua? Tangu uumbaji Wangu wa wanadamu hadi sasa, hakuna ambaye ameishi maisha muhimu sana duniani, na hivyo mwanadamu daima amekuwa mzembe kwa kuishi maisha yasiyo na umuhimu kabisa, lakini hakuna yeyote aliye na nia ya kuepuka mashaka haya na hakuna yeyote aliye na nia ya kuepukana na maisha yake matupu na ya uchovu. Katika uzoefu wa wanadamu, hakuna hata mmoja wa wale wanaoishi katika mwili ameepukana na desturi za ulimwengu wa mwanadamu, hata ingawa wanaitumia kwa faida ya kunifurahia Mimi. Badala yake, daima wameruhusu tu asili ifuate mkondo wake na kujidanganya.

Wakati Nitakapomaliza kabisa kuwepo kwa wanadamu, hakutakuwa na mtu aliyeachwa kuvumilia mateso kutoka duniani, na kisha kazi Yangu kuu inaweza kusemwa kuwa imetimizwa kwa ukamilifu. Katika siku za mwisho wakati Mimi Nimefanyika mwili, kile Ninachotaka kukamilisha katika kazi Yangu ni kuwawezesha wanadamu kuelewa utupu wa kuishi katika umbo la mwili, na hivyo Nitauzima mwili. Baadaye, hakutakuwa na watu duniani, hakuna mtu atakayelia tena kuhusu utupu wa dunia, hakuna mtu atakayeongea tena juu ya matatizo ya mwili, hakuna mtu atakayelalamika tena kuwa mimi Sifanyi haki, na watu na vitu vyote vitaingia katika pumziko. Baadaye, hakuna mtu atakayekuwa akirupuka, wala kutafuta hapa na pale duniani kwa sababu watu watakuwa wamejipatia hatima ya kufaa. Wakati huo, watakuwa na tabasamu kwenye nyuso zao. Halafu Sitamwuliza mwanadamu chochote tena na Sitakuwa na mgogoro zaidi naye; hapatakuwa na mkataba wa amani tena kati yetu. Naishi juu ya dunia na wanadamu wanaishi juu ya dunia; Naishi na kukaa pamoja nao. Wanadamu wanahisi furaha ya kuwepo Kwangu; kwa hivyo wanadamu hawako radhi kuondoka bila sababu, na badala yake, wangependelea kuwa Nikae tu kwa muda kidogo zaidi. Ningewezaje kuvumilia kuona matukio ya taabu yaliyoenea ulimwenguni huku Nikose kujitahidi hata kidogo ili kusaidia? Mimi si wa dunia. Ni kupitia uvumilivu ndio Nabaki duniani hadi siku hii, ingawa Nafanya hivyo kwa kusita. Isingalikuwa kwa ajili ya kuomba kwa wanadamu kusio na mwisho, Ningeliondoka zamani. Siku hizi wanadamu wanaweza kujitunza na hawahitaji msaada Wangu kwa sababu wamekomaa nao hawahitaji Niwalishe. Kwa hiyo Napanga kufanya sherehe ya ushindi na wanadamu, baada ya hapo Nitawaaga, ili waweze kujua jambo hili. Bila shaka, kutengana tukiwa tumekosana halingekuwa jambo jema kwa sababu hakuna machukio kati yetu. Kwa hivyo urafiki ulioko kati yetu utakuwa wa milele. Natumaini kwamba baada ya sisi kutengana, wanadamu wanaweza kutekeleza “urithi” Wangu na kutosahau kuhusu mafundisho ambayo Nimetoa wakati wa maisha Yangu, kutofanya lolote ambalo lingeleta aibu kwa jina Langu, na kukumbuka neno Langu. Natumaini kwamba binadamu watajitahidi kabisa kuniridhisha Mimi Nitakapokuwa Nimeondoka. Natumaini kuwa binadamu watatumia neno Langu kama msingi wa maisha yao. Msinivunje moyo kwa sababu moyo Wangu daima umekuwa ukiwajali wanadamu na Mimi Nimewapenda daima. Binadamu na Mimi tulikusanyika pamoja wakati mmoja na kufurahia duniani baraka hizo hizo zilizo mbinguni. Niliishi pamoja na wanadamu na kukaa pamoja nao, wanadamu walinipenda daima, nami Niliwapenda daima; tulikuwa na uhusiano kati yetu. Ninapokumbuka wakati Wangu pamoja na wanadamu, Nakumbuka siku zetu zikijawa na kicheko na furaha, na zaidi ya hayo, kulikuwa na ugomvi. Hata hivyo, upendo kati yetu uliimarishwa kwa msingi huu na kushughulikiana kwetu hakukuwahi kuvunjika. Kati ya miaka yetu mingi ya mawasiliano, wanadamu wameacha alama kubwa juu Yangu nami Nimewapa wanadamu mambo mengi ili wafurahie, ambayo wanadamu daima wameonyesha shukrani kubwa kuyahusu. Sasa, mkutano wetu ni tofauti na kitu chochote cha awali; nani angeweza kukosa wakati huu wa kuagana kwetu? Wanadamu wananipenda sana, nami Nina upendo usio na mwisho kwao, lakini ni nini kinaweza kufanywa kuhusu hilo? Nani angethubutu kwenda kinyume na mahitaji ya Baba wa mbinguni? Nitarejea kwenye makao Yangu, ambapo Nitakamilisha sehemu nyingine ya kazi Yangu. Pengine tutapata nafasi ya kukutana tena. Ni matumaini yangu kuwa wanadamu hawatahisi huzuni sana na kwamba wataniridhisha Mimi duniani; mara nyingi Roho Wangu aliye mbinguni Atawapa neema.

Katika wakati wa uumbaji, Nilikuwa nimetabiri kwamba katika siku za mwisho Nitafanya kundi la watu ambao wana nia moja na Mimi. Nilikuwa nimetabiri kwamba baada ya kuanzisha mfano duniani katika siku za mwisho, Nitarudi kwenye makao Yangu. Wakati wanadamu wote wameniridhisha Mimi, watakuwa wametimiza matakwa Yangu, na Mimi Sitahitaji tena kitu chochote kutoka kwao. Badala yake, wanadamu na Mimi tutasimuliana hadithi za siku zetu za zamani na baada ya hapo tutaagana. Naanza kuifanya kazi hii na kuwawezesha wanadamu kujiandaa kiakili. Nitawawezesha wanadamu wote kuelewa nia Zangu ili wasinielewe vibaya au kufikiria kuwa Mimi ni katili au asiye na huruma, ambayo sio nia Yangu. Je, wanadamu wananipenda lakini wanakataa kuniacha Niwe na mahali pa kupumzika pa kufaa? Je, wanadamu hawataki kumsihi Baba wa mbinguni kwa ajili yangu? Je, wanadamu hawajalia machozi ya huruma pamoja na Mimi? Je, wanadamu hawajasaidia katika kufanikisha mkutano wa haraka wa Sisi Baba na Mwana? Kwa nini hawataki sasa? Huduma Yangu duniani imetimizwa na baada ya kuagana na wanadamu bado Nitaendelea kuwasaidia wanadamu, je, hivi si vizuri? Ili kazi Yangu ipate kuwa na ufanisi zaidi na ili iwe ya manufaa pande zote, lazima tuagane ingawa ni uchungu kufanya hivyo. Machozi yetu yatatiririka kimyakimya na Sitawashutumu wanadamu tena. Katika wakati uliopita, Nilisema mambo mengi ambayo yaliichoma moyo halisi wa wanadamu, yakiwasababisha kutoa machozi ya huzuni. Kwa hiyo, Naomba radhi kwa wanadamu na kuomba msamaha wa wanadamu; msinionee kijicho na kunichukia, kwa kuwa haya yote ni kwa ajili ya manufaa yao wenyewe. Kwa hiyo, Natumaini kwamba wanadamu watauelewa moyo wangu. Katika nyakati za awali, tulikuwa na migogoro yetu, lakini tukiangalia nyuma, sisi sote tulifaidika. Kupitia kwa migogoro hii Mungu na wanadamu wamekuza daraja la urafiki kati yao, je, hili si tunda la jitihada zetu za ushirikiano? Sote tunapaswa kufurahia hili. Namwomba mwanadamu anisamehe kwa “makosa” Yangu ya awali na dhambi za wanadamu pia zitasahauliwa. Maadamu mwanadamu anaweza kurudisha upendo Wangu katika siku zijazo, basi hilo litaifariji Roho Yangu mbinguni. Sijui ni nini azimio la wanadamu katika suala hili, au kama mwanadamu ana nia ya kutimiza ombi Langu la mwisho au la. Siombi chochote kingine kutoka kwa wanadamu, ila tu wanipende na hiyo inatosha. Je, hili linaweza kufanywa? Yaache mambo yote mabaya yaliyotokea kati yetu yawe katika wakati uliopita, acha kuwe na upendo kati yetu daima. Nimewapa wanadamu upendo mwingi sana na wanadamu wamelipa gharama kubwa sana kwa ajili ya kunipenda Mimi. Hivyo, Natumaini kwamba binadamu watathamini upendo safi na takatifu kati yetu ili upendo wetu uenee kote katika dunia ya wanadamu na kupitishwa kwa vizazi vingine milele. Tutakapokutana tena, hebu tuungane katika upendo ili upendo wetu uweze kuendelea milele na kusifiwa na kuzungumziwa na watu wote. Hili lingeniridhisha na Ningewaonyesha wanadamu uso Wangu wenye tabasamu. Natumaini kwamba wanadamu watakumbuka yote Niliyowakabidhi.

Juni 1, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 46

Inayofuata: Sura ya 1

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp