Sura ya 3

Kwa kuwa mnaitwa watu Wangu, mambo hayapo kama yalivyokuwa; mnapaswa kusikiliza na kutii matamshi ya Roho Wangu, fuateni kwa karibu kazi Yangu, na msitenganishe Roho Wangu na mwili Wangu, maana kwa asili Sisi ni wamoja, na Hatujatengana. Yeyote ambaye angegawanya Roho na mwanadamu na kuzingatia kwa mwanadamu au Roho atapata hasara na ataweza tu kunywa kutoka kwenye kikombe chake chungu—ni hayo tu. Ni wale tu ambao wanaweza kumtazama Roho na mwanadamu kama kitu kizima kisichoweza kutenganishwa ndio wataweza kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu Mimi, na ni hapo tu ndipo mabadiliko yanaweza kutokea taratibu katika maisha yaliyomo ndani yao. Ili kwamba hatua inayofuata ya kazi Yangu iweze kuendelea taratibu na bila kizuizi, Ninatumia usafishaji wa maneno kuwajaribu wale wote ambao wapo katika nyumba Yangu, Nikitumia mbinu ya kufanya kazi kuwajaribu wale ambao hunifuata Mimi. Katika mazingira haya, ni haki kusema kwamba wote wanapoteza matumaini; kama watu, hakuna mmoja miongoni mwao ambaye hali zake si hasi na za baridi, kana kwamba nafasi yao yote imebadilika. Baadhi ya watu wanaishutumu Mbingu na nchi; baadhi, katika kukata tamaa kwao, bado wanastahimili ugumu na kukubali jaribio la maneno Yangu; baadhi wanatazama angani na kushusha pumzi ndefu, machozi yanajaza macho yao, kana kwamba wanahangaikia kifo cha mapema mno cha mtoto mchanga aliyezaliwa; baadhi hata wanahisi kuna aibu katika kuishi hivyo, na wanamwomba Mungu awachukue karibuni; baadhi wanashinda siku nzima wakiwa wamepigwa bumbuwazi, kana kwamba wamekuwa wagonjwa sana na bado hawajarejea katika hali yao ya kawaida; baadhi, baada ya kulalamika, wanaondoka kimyakimya; na baadhi bado hunisifu Mimi kutoka mahali pao, lakini wao bado ni hasi kidogo. Leo, ambapo yote yamefichuliwa, Sihitaji kuzungumzia zaidi yaliyopita; jambo la muhimu mkubwa ni kwamba mnapaswa bado muwe na uwezo wa utiifu mkubwa sana kutoka kwa mahali Ninayowapa leo, ili kwamba yote mnayofanya yakidhi idhini Yangu, na yote msemayo ni zao la mwangaza na nuru Yangu, na hatimaye kile mnachoishi kwa kudhihirisha ni sura Yangu, ni udhihirisho Wangu kabisa.

Maneno Yangu yanatolewa na kuonyeshwa wakati wowote au mahali popote, na hivyo, nyinyi pia, mnapaswa kujijua wenyewe mbele Yangu wakati wote. Kwani leo ni, hata hivyo, tofauti na kile kilichokuja kabla, na hamwezi tena kutimiza chochote mnachotamani. Badala yake, kwa kuongozwa na maneno Yangu, mnapaswa kuweza kuihini miili yenu, mnapaswa kutumia maneno Yangu kama nguzo, na hampaswi kutenda kizembe. Njia zote kuelekea matendo ya kweli kwa ajili ya kanisa zinaweza kupatikana katika maneno Yangu. Wale ambao hawatendi kulingana na maneno Yangu wanakosea Roho Wangu moja kwa moja, na Nitawaangamiza. Kwa kuwa mambo yamefikia hali ilivyo leo, hamhitaji kujihisi kutiwa uchungu na kujuta kuhusu matendo yenu ya zamani. Ukarimu Wangu hauna mipaka kama ilivyo bahari na anga—uwezo na ufahamu wa mwanadamu kunihusu Mimi unawezaje kukosa kujulikana Kwangu kama kiganja Changu? Ni nani miongoni mwa wanadamu ambaye hayupo mikononi Mwangu? Unadhani Sijui chochote juu ya jinsi ukubwa wa kimo chako ulivyo unaamini Mimi sijui kabisa kuhusu hili? Hilo haliwezekani! Hivyo, wakati ambapo watu wote wapo katika hali yao ya kukata tama zaidi, wakati ambapo hawawezi kusubiri zaidi, na wanatamani kuanza upya, wakati wanapotaka kuniuliza nini kinaendelea, wakati ambapo baadhi wanajiendekeza katika ubadhirifu na baadhi wanataka kuasi, wakati baadhi bado ni watiifu wakifanya huduma, Ninaanza sehemu ya pili ya enzi ya hukumu: kuwatakasa na kuwahukumu watu Wangu. Ambayo ni kusema, Ninaanza rasmi kuwafundisha watu Wangu, kuwawezesha si tu kunitolea ushuhuda unaopendeza, bali, zaidi, kutimiza ushindi mzuri katika vita kwa ajili Yangu kutoka kwa kiti cha watu Wangu.

Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani, walinde lango la nyumba Yangu kwa ajili Yangu, waweze kusaidiana na kupeana mahitaji, kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati mtakapokuwa na majuto ya kuchelewa sana. Kwa nini Ninawafundisha kwa hali hiyo ya dharura? Kwa nini Ninawaelezea ukweli wa ulimwengu wa kiroho? Kwa nini Ninawakumbusha na kuwaonya mara kwa mara? Je, mmewahi kufikiri juu ya hili? Je, mmewahi kulielewa? Hivyo, hamhitaji tu kuweza kuwa wazoefu kwa kutegemeza juu ya msingi wa zamani, bali, zaidi, kuondoa uchafu ndani yenu chini ya uongozi wa maneno ya leo, mkiruhusu kila maneno Yangu kukita mzizi na kustawi ndani ya roho zenu, na muhimu zaidi, kuzaa matunda zaidi. Hiyo ni kwa sababu kile Ninachokiomba si maua angavu yaliyostawi sana, bali matunda mengi—matunda, zaidi ya hayo, ambayo hayaharibiki. Je, mnaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu? Ingawa maua katika nyumba ya kioo ya kuhifadhi mimea ni yasiyohesabika kama nyota, na huwavuta watalii wote, mara yanaponyauka yanakuwa mabovu mabovu kama hila danganyifu za Shetani, na hakuna mtu anayevutiwa nayo. Lakini kwa wale ambao wamerushwa na upepo na kuchomwa na jua na kuwa na ushuhuda Kwangu, ingawa maua haya si mazuri, mara yanaponyauka, hapo panatokea tunda, maana haya ndiyo matakwa Yangu. Ninapozungumza maneno haya, mnaelewa kiwango kipi? Mara maua yanaponyauka na kuzaa matunda, na mara matunda haya yote yanaweza kutolewa kwa ajili ya furaha Yangu, Nitakamilisha kazi Yangu yote duniani, na Nitaanza kufurahia udhihirisho wa hekima Yangu!

Februari 22, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 2

Inayofuata: Sura ya 4

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp