Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 24

Wakati unakaribia hata zaidi. Amkeni! Watakatifu wote! Nitawatamkia ninyi. Wote wanaosikia wataamka. Mimi ni Mungu ambaye mmekuwa na imani katika kwa miaka hii mingi. Leo nimekuwa mwili na kuja mbele ya macho yenu, na hii inafichua yule ambaye ananitaka kwa kweli, ambaye yuko tayari kulipa gharama yoyote kwa ajili Yangu, ambaye husikiliza neno Langu kwa kweli, na yule ambaye yuko tayari kuuweka ukweli katika matendo. Kwa maana mimi ni mwenyezi Mungu, Ninaweza kuona siri zote za binadamu zilizofichwa gizani, Najua ni nani anayenitaka kwa kweli na Ninajua ni nani anayenipinga Mimi; Ninaweza kuchunguza mambo haya yote.

Sasa Ningependa kufanya kikundi cha watu ambao wanaupendeza moyo Wangu haraka iwezekanavyo, wale ambao wanaweza kuihurumia mizigo Yangu. Hata hivyo, Siwezi kuacha kusafisha na kutakasa kanisa Langu; kanisa ni moyo Wangu. Ninawadharau watu wote wabaya wanaowazuia msile na kunywa neno Langu. Hii ni kwa sababu kuna watu fulani wachache ambao hawanitaki Mimi kwa kweli. Watu hawa wamejaa udanganyifu, hawaji karibu na Mimi na moyo wao wa kweli, wao ni waovu, na ni watu ambao huzuia utekelezaji wa mapenzi Yangu; wao sio watu ambao huweka ukweli katika matendo. Watu hawa wamejaa kujidai na majivuno, wao ni wenye kutamani makuu vikali, wanapenda kutenda mema kwa nia ya kusimanga, na maneno wanayosema ni mazuri kusikia, lakini kwa siri hawatendi ukweli. Watu hawa waovu wote watakatwa na kuzolewa kabisa; watateseka katika majanga. Maneno haya ni kuwakumbusha na kuwaonya ili msalie kwenye njia inayoupendeza moyo Wangu. Daima rudini katika roho yenu, kwa sababu Ninawapenda wale wanaonipenda kwa moyo wao wote. Kwa kuwa mnanikaribia Mimi, nitawalinda na kuwaweka mbali na wale waovu, Nitawafanya msimame imara nyumbani Kwangu na kuwalinda mpaka mwisho.

Iliyotangulia:Sura ya 23

Inayofuata:Sura ya 25

Maudhui Yanayohusiana

 • Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

  Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza k…

 • Sura ya 32

  Watu wanapokusanyika pamoja na Mimi, moyo Wangu unajawa na furaha. Mara moja, Ninatoa baraka zilizo mkononi Mwangu miongoni mwa binadamu, ili watu wa…

 • Amri za Enzi Mpya

  Mmeambiwa kuwa mjiandae kwa maneno ya Mungu, ya kuwa pasipo kujali mlichoandaliwa ninyi, yote yamepangwa kwa mkono wa Mungu, na kwamba hakuna haja ya…

 • Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

  Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika watu wa nyota-nyota-nukta-nukt…