Sura ya 81

Oo, enzi hii mbaya na yenye uzinzi! Nitakumeza! Mlima Sayuni! Simama unisifu Mimi! Kwa kukamilika kwa mpango Wangu wa usimamizi, kwa kukamilika kwa kazi Yangu kuu, ni nani athubutuye kutoinuka na kufurahi! Ni nani athubutuye kutoinuka na kuruka kwa furaha bila kukoma! Atakutana na kifo chake mkononi Mwangu. Mimi hutekeleza haki kwa kila mtu, bila huruma hata kidogo au upendo wa fadhila, na bila kupendelea. Watu wote! Inukeni na mtoe sifa, na mnipeni Mimi utukufu! Utukufu wote usiokoma, kutoka milele hadi milele, upo kwa sababu Yangu na ulianzishwa na Mimi. Nani anayeweza kuthubutu kujichukulia utukufu mwenyewe? Nani anayeweza kuthubutu kuchukulia utukufu Wangu kama kitu cha kimwili? Atauawa kwa mkono Wangu! Ee, wanadamu katili! Niliwaumba na kuwakimu, na Nimewaongoza mpaka leo, ila hamjui angalau hata kidogo juu Yangu na hamnipendi Mimi kabisa. Ninawezaje kuwaonyesha huruma tena? Ninawezaje kuwaokoa? Naweza tu kuwatendea kwa ghadhabu Yangu! Nitawalipa na uharibifu, Niwalipe na kuadibu kwa milele. Hii ni haki; inaweza tu kuwa kwa njia hii.

Ufalme Wangu ni imara na thabiti; hautaanguka kamwe, lakini utakuwapo hadi milele! Wana Wangu, wana Wangu wazaliwa wa kwanza, watu Wangu watafurahia baraka pamoja nami milele na milele! Wale ambao hawaelewi mambo ya kiroho na ambao hawapokei ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu wataondolewa kutoka katika Ufalme Wangu siku moja. Hawataondoka kwa hiari yao wenyewe, lakini watalazimishwa kutoka nje na utawala wa fimbo Yangu ya chuma, na utukufu Wangu, na zaidi ya hayo, watapigwa teke na mguu Wangu. Wale ambao walipagawa na roho wabaya hapo zamani (tangu kuzaliwa) watafichuliwa sasa. Nitakufukuza nje! Je, bado unakumbuka yale ambayo Nimeyasema? Mimi—Mungu mtakatifu na Asiye na waa—Siishi katika hekalu chafu na la kuchukiza. Wale ambao walikuwa wamepagawa na roho wabaya wanajua wenyewe, na Sihitaji kufafanua. Sijakujaalia! Wewe ni Shetani mkongwe, ilhali unataka kupenya katika ufalme Wangu! Hasha! Ninakuambia! Leo Nitakueleza wazi kabisa: Wale Niliowachagua wakati wa uumbaji wa wanadamu, Nimewajaza ubora Wangu na tabia Yangu; kwa hivyo, leo ni waaminifu Kwangu pekee, wanaweza kulibebea kanisa mzigo, na wako radhi kujitoa kwa ajili Yangu na kutoa maisha yao yote Kwangu. Wale ambao Sijawachagua kwa hivyo wamepotoshwa na Shetani kwa kiwango fulani, na hawana sifa Yangu yoyote wala tabia Yangu. Mnafikiri maneno Yangu yanapingana, lakini maneno ya “Umeamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi, lakini mnakubali matokeo ya matendo yenu” yote yanamrejelea Shetani. Sasa Nitaeleza jambo moja: Leo, wale ambao wanaweza kuinuka na kuchukua mamlaka ya makanisa, kuyachunga makanisa, kuudhukuru mzigo Wangu, na kuwa na kazi maalum—hakuna hata moja wa hawa ambaye anamhudumia Kristo. Wote ni wale ambao Nimewajaalia na kuwachagua. Nawaambia hili ili msiwe na wasiwasi zaidi na kuchelewesha maendeleo ya maisha yenu. Ni wangapi wanaoweza kushinda hadhi ya mzaliwa wa kwanza? Yawezekana kuwa hiki ni kitu rahisi kama kupata diploma? Haiwezekani! Kama Singewafanya muwe watimilifu, mngekuwa mmepotoshwa kwa kiasi fulani na Shetani muda mrefu uliopita. Ndiyo maana Nimesisitiza tena na tena kwamba siku zote Nitawatunza na kuwalinda wale walio waaminifu Kwangu na kuwazuia kutokana na madhara na mateso. Wale ambao Sijawajaalia ni wale ambao wamepagawa na roho wabaya, wale ambao hawajali, wapumbavu, na waliodumaa kiroho na hawawezi kuyachunga makanisa (kumaanisha wale walio na shauku lakini hawana hakika kuhusu maono). Mnapaswa kuondolewa kwa haraka mbele Yangu, na mapema iwezekanavyo ili Nisichafuke moyo na kukasirishwa na kukuona. Ukiondoka haraka, utapokea adabu kidogo, lakini kadiri unavyozidi kuchukua muda mrefu ndivyo adabu itakavyokuwa kali zaidi. Unaelewa? Usiwe mtovu wa haya sana! Wewe ni mpotovu na asiye na simile, wa kawaida na asiyejali, pasi kujua wewe ni ovyo jinsi gani! Wewe ni kipofu!

Wale wanaoshikilia mamlaka katika ufalme Wangu wote wamechaguliwa kwa uangalifu na Mimi na wamejaribiwa tena na tena; hakuna mtu anayeweza kuwashinda. Nimewapa nguvu, kwa hiyo hawataanguka kamwe au kupotea. Wamepata idhini Yangu. Kutoka siku hii na kuendelea, wanafiki wataonyesha rangi zao za kweli, na wana uwezo wa kutenda kila aina ya mambo ya aibu, lakini hatimaye hawataweza kuutoroka mkono Wangu ambao huadibu na kumteketeza Shetani. Hekalu Langu litakuwa takatifu na safi. Yote ni ushahidi Kwangu, udhihirisho Wangu, na utukufu kwa jina Langu. Ni makao Yangu ya milele na lengo la upendo Wangu wa milele. Mara nyingi Mimi hulipapasa kwa mkono wa Upendo, kulifariji na lugha ya upendo, kilitunza kwa macho ya upendo, na kulikumbatia ndani ya kifua cha upendo, hivyo halitaanguka katika mitego ya waovu au kudanganywa na Shetani. Leo, wale ambao hunihudumia lakini hawajaokoka watatumiwa na Mimi wakati wa mwisho. Kwa nini Ninaharakisha kuvitoa vitu hivi kutoka katika ufalme Wangu? Kwa nini lazima Niwafukuze watoke mbele Yangu? Nawachukia sana! Kwa nini Siwaokoi? Kwa nini Ninawachukia? Kwa nini lazima Niwapige wafe? Kwa nini lazima Niwaangamize? (Hakuna hata kipande chao kimoja kinachoweza kubaki mbele Yangu, ikiwa ni pamoja na majivu yao.) Kwa nini? Hata joka kuu jekundu, nyoka wa kale, na Shetani wa zamani hutafuta riziki ambayo hastahili katika ufalme Wangu! Msiwe na ndoto tena! Wote wataishia kuwa bure na watageuka kuwa majivu!

Nitaharibu enzi hii, kuibadilisha iwe ufalme Wangu, na kuishi na kufurahia na watu Ninaowapenda hadi milele. Vitu hivyo visivyo safi havifai kufikiri vinaweza kubaki katika ufalme Wangu. Unafikiri kuwa unaweza kuvua samaki katika maji meusi? Sahau ndoto kama hizo! Hujui kwamba kila kitu huchunguzwa na macho Yangu! Hujui kwamba kila kitu hupangwa na mikono Yangu! Usifikiri kuwa unaheshimiwa sana! Kila mmoja wenu lazima achukue nafasi yake inayostahili. Msijifanye kuwa wanyenyekevu (ikirejelea wale waliobarikiwa) au kutetemeka na kuwa na hofu (ikirejelea wale wanaopitia taabu). Sasa, kila mtu anapaswa kujua mwenyewe ndani ya moyo wake. Hata Nisipolitaja jina lako bado unapaswa kuwa na hakika, kwa sababu Nimeelekeza maneno Yangu kwa kila mtu. Bila kujali ikiwa wewe ni mteule Wangu au la, Maneno Yangu yanaelekezwa kwa hali zenu zote za sasa. Yaani, kama ninyi ni miongoni mwa wateule Wangu, basi Nazungumzia hali ya wale Niliowachagua kulingana na maonyesho yako; kwa mintarafu ya wale ambao sio wateule Wangu, Mimi pia nanena kulingana na hali yao. Kwa hivyo, maneno Yangu yamezungumzwa kwa uhakika. Kila mtu anapaswa kuwa na hisia nzuri ya hilo. Msijidanganye! Msiogope! Kwa sababu idadi ya watu ni ndogo, ni wachache pekee, udanganyifu hautafanikisha! Yeyote Nitakayesema ni mteule amechaguliwa na bila kujali unajifanya vizuri jinsi gani, bila sifa Yangu utashindwa. Kwa sababu Mimi hutimiza neno Langu, Sivurugi mipango Yangu bila mpango; Ninafanya chochote Ninachotaka kufanya, kwa sababu kila kitu Ninachofanya ni sahihi, Mimi ni mkuu, na Mimi ni wa pekee. Una hakika juu ya hili? Unaelewa?

Sasa, baada ya kusoma maneno Yangu, wale wanaofanya maovu na walio waovu na wadanganyifu, pia wanajitahidi kutafuta maendeleo na kufanya jitihada zao za kibinafsi. Wanataka kulipa gharama ndogo tu ili kupenya katika ufalme Wangu. Wanapaswa kuweka kando fikira kama hizo! (Watu hawa hawana matumaini kwa sababu Sijawapa fursa ya kutubu.) Mimi hulinda lango la ufalme Wangu. Je, unaamini kwamba watu wanaweza kuingia katika ufalme Wangu kama wanavyotaka? Je, unaamini kwamba ufalme Wangu utakubali aina yoyote ya takataka? Kwamba ufalme Wangu utachukua aina yoyote ya takataka isiyofaa? Umekosea! Leo, wale walio katika ufalme ni wale walio na mamlaka ya kifalme pamoja nami; Nimewakuza kwa uangalifu. Hili si jambo linaloweza kufanikishwa tu kwa kulitaka—lazima ukubaliwe na Mimi. Na hili sio jambo ambalo hujadiliwa na mtu yeyote, bali ni kitu ambacho Mimi Mwenyewe hupanga. Chochote Ninachosema hutendeka. Siri Zangu hufichuliwa kwa wale Ninaowapenda. Wale wanaofanya maovu, yaani, wale ambao Sijawachagua, hawana haki ya kuzipokea. Hata wakizisikia, hawataelewa, kwa sababu Shetani ameyafunika macho yao na kuidhibiti mioyo yao, kuharibu maisha yao yote. Kwa nini inasemwa kwamba vitendo Vyangu ni vya kushangaza na vya busara, na kwamba Mimi huhamasisha kila kitu kwa ajili ya huduma Yangu? Nitawakabidhi wale ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi kwa Shetani awaadhibu na kuwapotosha, na Sitajihusisha katika kuwaadhibu; hivi ndivyo Nilivyo mwenye hekima! Ni nani ambaye amewahi kufikiria hili? Bila jitihada yoyote asilani, kazi Yangu kuu imekamilika, sivyo?

Iliyotangulia: Sura ya 80

Inayofuata: Sura ya 82

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp