Sura ya 82

Wote wanaogopa wanaposikia neno Langu. Wote wamejawa na hofu. Mnaogopa nini? Sitawaua! Ni kwa sababu mnahisi hatia na mnaogopa kugunduliwa. Yale unayoyafanya nyuma Yangu ni ya upuuzi na yasiyo na maana kabisa. Hili limenifanya Nikuchukie sana hivi kwamba Ninatamani sana Ningekuwa nimewatupa wale ambao Sikuwa nimewajaalia wala kuwachagua katika shimo lisilokuwa na mwisho wavunjwe vipande vipande. Hata hivyo, Nina mpango Wangu, Nina malengo Yangu. Nitayahurumia maisha yako kwa sasa, kutokufukuza hadi baada ya huduma yako Kwangu kufika mwisho. Sitaki kuona viumbe kama hawa, wao ni aibu kwa jina Langu! Je, unajua hili? Unaelewa? Maskini usiye na thamani! Elewa hili waziwazi! Unapotumiwa ni Mimi Ninayefanya hivyo na wakati ambapo hutumiwi pia ni kwa sababu Yangu. Yote yamepangwa na Mimi, na mikononi Mwangu yote ni tiifu na ya utaratibu. Yeyote athubutuye kuondoka nje ya foleni atapigwa mara moja na mikono Yangu. Mara nyingi Mimi husema “kupigwa”; je, unafikiri kwamba Mimi hufanya hivyo kwa mikono Yangu? Sihitaji kufanya hivyo! Vitendo Vyangu si vya upumbavu kama wanadamu wanavyofikiri. Ina maana gani inaposemekana kwamba kila kitu kinaanzishwa na kukamilishwa na neno Langu? Kila kitu hukamilishwa bila Mimi hata kuinua kidole. Je, unaelewa maana halisi ya neno Langu?

Kamwe Sitamwokoa yeyote kati ya wale wanaotoa huduma Kwangu. Hawana mgawo katika ufalme Wangu Hii ni kwa sababu watu hawa wanajihusisha tu na mambo ya nje badala ya kufanya mapenzi Yangu. Ingawa Ninawatumia sasa, kwa kweli wao ni watu ambao Ninawachukia zaidi, watu ambao Ninawakirihi zaidi. Leo, Ninampenda yeyote anayefanya mapenzi Yangu, yeyote anayeweza kuidhukuru mizigo Yangu, na yeyote anayeweza kutoa kila kitu chake kwa moyo wa kweli na uaminifu, na Nitampa nuru daima, kutomwacha aende mbali na Mimi. Mara nyingi Mimi husema, “Kwa wale wanaotumia rasilmali kwa dhati kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki sana.” “Bariki” ina maana gani? Je, unajua? Kuhusu kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, inaonyesha mizigo Ninayokupa. Wote wanaoweza kuubebea kanisa mzigo, ambao hujitolea kwa dhati kwa ajili Yangu, mzigo wao na moyo wao wa kweli ni baraka kutoka Kwangu. Aidha, ufunuo Wangu kwao pia ni baraka kutoka Kwangu. Hii ni kwa sababu wale ambao hawana mzigo sasa hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi; laana Yangu tayari imeshuka juu yao. Yaani, wale ambao Nimewajaalia na kuwachagua wana mgawo katika vipengele chanya vya kile Nilichosema, huku wale ambao Sijawaamulia kabla na kuwateua wana mgawo katika vipengele hasi tu vya matamko Yangu. Kadiri maneno Yangu yanavyozidi kunenwa, ndivyo maana yake inavyozidi kueleweka; kadiri Ninavyoyasema, ndivyo yanavyokuwa wazi zaidi. Kila mmoja wa wale wadanganyifu na wenye hila ambao Sijawajaalia alilaaniwa na Mimi kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Kwa nini inasemekana kwamba mwaka, mwezi, siku, hata saa, dakika, na sekunde ya kuzaliwa kwenu kote kumepangwa vizuri na Mimi? Nilishaamua kitambo kabla ni wagani ambao watapata nafasi ya wazaliwa wa kwanza. Wako machoni Pangu; kwa muda mrefu wameonekana kuwa wa thamani na Mimi, na kwa muda mrefu wamekuwa na nafasi katika moyo Wangu. Kila neno Nilisemalo lina uzito na hubeba mawazo Yangu. Mwanadamu hana maana! Isipokuwa wale wachache ambao Ninawapenda walio na vyeo vya wazaliwa wa kwanza, ni kina nani wachache ambao huonyesha wema kwa mapenzi Yangu? Wana wangu wana thamani gani? Watu Wangu wana thamani gani? Hapo zamani, neno “Wana Wangu” lilikuwa jina la wazaliwa Wangu wa kwanza. Lakini wale kati ya wana Wangu na watu Wangu ambao hawana aibu yoyote walidhani kuwa lilikuwa jina la heshima waliloitwa. Msichukue wajibu wa wana Wangu wazaliwa wa kwanza bila aibu, je, unastahili hili? Leo ni wale pekee ambao wamethibitishwa ndio ambao wamewekwa katika nafasi muhimu mbele Yangu. Wamepata vyeo vya wazaliwa wa kwanza. Tayari wana mgawo wa kiti Changu cha enzi, taji Langu, utukufu Wangu, na ufalme Wangu. Kila kitu kimepangwa kwa uangalifu na Mimi. Wale wote wanaopokea vyeo vya wazaliwa wa kwanza leo wote wamepitia maumivu makubwa, mateso, na shida, kama vile yale waliyoyakabili katika familia zao tangu kuzaliwa, matarajio yao wenyewe, kazi, ndoa, nk. Hawa wazaliwa wa kwanza hawajashinda vyeo hivi bila kulipa gharama; badala yake, tayari wamepitia vipengele vyote vya maisha: vizuri na vibaya, milima na mabonde. Wote ambao hapo zamani waliheshimiwa sana na watu wa dunia na wanaoishi katika faraja nyumbani hawana mgawo katika wazaliwa wa kwanza. Hawastahili kuwa wana wa kwanza; wao huliletea aibu jina Langu, Siwataki kabisa. Kwa wana Wangu na watu Wangu ambao Nimewachagua, pia wana sifa nzuri duniani, lakini wako mbali sana na wazaliwa Wangu wa kwanza. Sasa Ninawatumia watu fulani, lakini miongoni mwao wengi hawastahili kuwa watu Wangu, ni walengwa wa uharibifu wa milele; wanatumiwa kutoa huduma Kwangu kwa muda, sio kwa matumizi ya muda mrefu. Wale ambao watatumiwa kwa muda mrefu tayari wameamuliwa katika moyo Wangu. Yaani, wale ambao Mimi huwaweka katika nafasi muhimu ni wale Ninaowapenda na ambao Nilianza kuwatumia muda mrefu ulipoita. Yaani, kazi yao tayari imewekwa. Kwa mintarafu ya wale ambao Ninawachukia, katika hatua ya sasa wao wanatumika tu kwa muda. Wageni watakapokuja, wazaliwa wa kwanza watafichuliwa kwenu waziwazi wakati huo.

Leo Ninawahitaji mkue kwa haraka na kuonyesha wema kwa mzigo Wangu, mzigo huu sio mzito sana, na Nitawafanya mfanye tu kilicho chini ya uwezo wenu. Najua vimo vyenu, Najua kazi mnayoweza kufanya. Najua haya yote na Ninaelewa mambo haya. Ninatamani tu kuwa wana Wangu wajinyime wenyewe kwa hiari, kwa kweli wakipenda kile Ninachopenda, kuchukia kile Ninachokichukia, kufanya kile Ninachofanya, na kusema kile Ninachosema. Msidhibitiwe na nafasi, jiografia, wakati, au mtu yeyote. Natamani kuwa roho zenu ziwe huru kila mahali na kila mmoja wenu aweze kusimama katika nafasi ya wazaliwa wa kwanza. Ni nani anayejitoa Kwangu leo? Ni nani ambaye hutumia rasilmali kwa uaminifu kwa ajili Yangu? Nani akeshaye mchana na usiku kwa ajili Yangu? Ni nani ambaye huendesha mambo ya nyumba Yangu? Ni nani ambaye hupunguza mzigo uliopo mabegani Pangu kwa ajili Yangu? Je, sio wana Wangu? Kila kitu Ninachofanya ni ili kuwafanya kamili wana Wangu na katika huduma kwa wana Wangu, unaelewa? Yote ni kwa ajili ya wazaliwa Wangu wa kwanza na Sifanyi makosa. Usifikiri Mimi huwakadiria watu vibaya. Usifikiri kwamba Ninakuchukia. Usifikiri Situmii kikamilifu vipaji bora. Usifikiri kwamba Nimekosea katika kutokujaalia. Badala yake, hustahili hilo! Je, unajua? Sasa Nitawahakikishia mambo mengine: Kila mtu anayeisisimua ghadhabu Yangu mara nyingi, yeyote ambaye ni mlengwa wa mara kwa mara wa ukosoaji Wangu au kushughulikiwa na Mimi, hakika ni mlengwa wa chuki Yangu. Hakika atakufa, hilo halina budi. Nimesema kuwa Sitawashughulikia tena wana Wangu wazaliwa wa kwanza kwa sababu watu hawa wamepitia majaribio Yangu makubwa na wamepata idhini Yangu. Yeyote Nitakayemwangalia kwa sura ya ukali atakabiliana na hatari, je, huogopi? Wengi watakufa mara tu maneno Yangu yatakapotoka kinywani Mwangu. Hata hivyo, wengine bado wanadumisha mwili wao, ni kwamba tu roho yao imekufa. Dalili ya wazi ni kwamba hawana kazi ya Roho Mtakatifu na hawana chochote kinachowazuia. (Tayari wamepotoshwa na Shetani, kufikia kiwango fulani). Kila mwili wao unapofishwa, hilo hufanyika kwa mpango Wangu unaofaa na kwa wakati ambao Nimeeleza bayana. Kifo chao cha kiroho hakiwezi kufanya huduma bora Kwangu; Nitatumia mwili wao kuonyesha maajabu ya matendo Yangu. Kutoka kwa hili watu wataondoa mashaka, watasifu bila kukoma, hakutakuwa na mmoja ambaye hatakuwa na uchaji Kwangu, na hakuna wowote ambao hawaniogopi. Sichukulii mambo yoyote kwa urahisi; wote husihi au kufa kwa sababu Yangu na hakuna yeyote anayeweza kuondoka hadi atakapotekeleza huduma yake Kwangu. Hata Shetani hawezi kurudi kwenye shimo lisilokuwa na mwisho hadi atimize huduma yake Kwangu. Kila hatua Ninayochukua ni thabiti na salama na iliyo na msingi thabiti. Hakuna hatua ambayo Mimi huchukua iliyo ya juujuu, hata kidogo.

Ni nani anayeweza kuthubutu kulinganishwa na mimi? Ni nani anayeweza kuthubutu kunipinga? Nitakupiga mara moja! Sitaacha dalili, na mwili wako utaondolewa kabisa; hii ni bila shaka. Nitaiweka katika vitendo mara Nisemapo na hakutakuwa na kurudi nyuma. Dunia inavunjika kila siku. Watu wanaangamia kila siku. Ufalme Wangu unapata umbo kila siku. Wana Wangu wazaliwa wa kwanza wanakua kila siku. Hasira Yangu inakua kila siku, kuadibu Kwangu kunakuwa kubaya zaidi kwa siku, na neno Langu linazidi kuwa kali kwa siku. Bado mnasubiri lugha Yangu juu yenu iwe yenye huruma, sauti Yangu iwe yenye ucheshi, fikiria tena! Inategemea ni nani Ninayemshughulikia. Kwa wale Niwapendao, sauti Yangu ni ya upole, daima inayofariji. Kwenu, Naweza tu kuwa mkali na mwenye hukumu, na kuongeza juu ya hayo kuadibu na hasira. Bila kujua, hali katika kila nchi ya dunia inazidi kuwa ya fadhaa, kila siku zikivunjika, kila siku zikipata machafuko. Viongozi wa kila nchi wanatumai kushinda mamlaka mwishoni. Hawatarajii hili, lakini kuadibu Kwangu tayari iko juu yao. Wanajaribu sana kushika mamlaka Yangu, lakini wanaota tu! Hata kiongozi wa Umoja wa Mataifa lazima pia aombe msamaha kutoka Kwangu. Matendo maovu aliyoyafanya ni mengi. Sasa ni wakati wa adhabu. Mimi Simhurumii kwa urahisi. Wote walio mamlakani ni lazima wavue mataji yao. Ni Mimi pekee Ninayestahili kutawala juu ya vitu vyote. Kila kitu kinanitegemea Mimi. Yote yananitegemea, bila kutaja wageni wachache. Nitawapiga mara moja wale wanaonichunguza kwa makini kwa sababu kazi Yangu tayari imefika hapa. Kila siku kuna ufunuo mpya, kila siku kuna mwanga mpya. Yote yanazidi kuwa kamili. Siku ya mwisho ya Shetani inakaribia zaidi na zaidi na kuzidi kuwa wazi zaidi kuliko hapo awali.

Iliyotangulia: Sura ya 81

Inayofuata: Sura ya 83

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp