Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 48

Mimi nina wasiwasi, lakini wangapi kati yenu wanaweza kuwa na nia moja na mawazo sawa na Mimi? Ninyi hamyasikilizi tu maneno Yangu, mkipuuza kabisa na kushindwa kuyatilia maanani, badala yake mkizingatia tu mambo yenu wenyewe ya juu juu. Mnachukulia kujali Kwangu kwa bidii na juhudi kama jitihada za bure; je, dhamiri yenu haiwahukumu? Ninyi ni wajinga na hamna mantiki; ninyi ni wapumbavu, na hamwezi kuniridhisha kabisa. Niko upande wenu kabisa—ninyi mnaweza kuwa upande Wangu kiasi gani? Mmeelewa visivyo nia Yangu, na hakika huu ni upofu wenu na kutoweza kuona mambo, daima mkinifanya Niwe na wasiwasi kuwahusu na kutumia muda kwenu. Sasa, ni kiasi gani cha muda wenu ambao mnaweza kuutumia na kutenga kwa ajili Yangu? Mnapaswa kujiuliza zaidi.

Nia Yangu yote ni kwa sababu yenu—je, mnaelewa hili kweli? Kama kweli mngeelewa, mngekuwa mmekwisha kufahamu nia Yangu na kuufikiria mzigo Wangu. Msiwe wazembe tena, la sivyo Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yenu, jambo ambalo litazifanya roho zenu zife and kuanguka kuzimuni. Je, hilo si jambo baya sana kwako? Hakuna haja ya Mimi kuwakumbusha tena. Mnapaswa kuchunguza dhamiri zenu na kujiuliza: Je, ni kwamba Ninawahurumia sana, au kwamba ninyi mna madeni Yangu mengi sana? Msichanganye mema na mabaya na muwe bila akili! Sasa si wakati wa kupigania nguvu na faida au kushiriki katika kula njama, badala yake lazima muweke kando kwa haraka mambo haya ambayo ni yenye kuleta madhara kwa maisha na kutafuta kuingia ndani ya ukweli. Ninyi ni wazembe sana! Hamwezi kuuelewa moyo Wangu au kutambua nia Yangu. Kuna mambo mengi ambayo Sikupaswa kuyasema, lakini ninyi ni watu mliochanganyikiwa sana ambao hamwelewi, imenibidi Niyaseme mara kwa mara, na hata hivyo, ninyi bado hamjauridhisha moyo Wangu.

Nikiwahesabu mmoja mmoja, ni wangapi wanaoweza kuufikiria moyo Wangu kwa hakika?

Iliyotangulia:Sura ya 47

Inayofuata:Sura ya 49

Maudhui Yanayohusiana

 • Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

  Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na…

 • Utendaji (8)

  Ninyi bado hamwelewi vipengele mbalimbali vya ukweli, na bado kuna makosa machache na mikengeuko katika kutenda kwenu; katika mambo mengi mnaishi ku…

 • Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

  Kunayo siri kubwa moyoni mwako, ambayo hujawahi kuifahamu kamwe, kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu bila mwanga. Moyo wako na roho yako vime…

 • Maonyo Matatu

  Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata h…