Sura ya 9

Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong’aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. Kwa sababu Nilitoka katika nchi takatifu, si kama yungiyungi, ambalo lina jina tu na halina dutu kwa sababu lilikuja kutoka katika matope na si kutoka nchi takatifu. Wakati ambapo mbingu mpya inashuka duniani na nchi mpya kuenea juu ya anga ndio pia wakati hasa ambao Ninafanya kazi kirasmi miongoni mwa binadamu. Ni nani kati ya wanadamu anayenijua Mimi? Ni nani aliyeona wakati wa kuwasili Kwangu? Ni nani ameona kwamba Mimi sina jina tu, bali zaidi ya jina Nina dutu? Mimi huyasongeza mawingu meupe kwa mkono wangu na kwa karibu Naichunguza anga; katika anga, hakuna kitu kisichopangwa kwa mkono wangu, na chini ya anga, hakuna mwanadamu asiyechangia juhudi yake ndogo kwa ukamilishaji wa shughuli Yangu kuu. Mimi Simwekei mwanadamu madai mazito duniani, kwa maana Mimi daima Nimekuwa Mungu wa vitendo, na kwa sababu Mimi ni Mwenyezi Aliyeumba mwanadamu na Anayejua mwanadamu vizuri. Watu wote wako machoni pa Mwenyezi. Hata wale walio katika pembe zote mwisho wa dunia watawezaje kuepuka uchunguzi wa Roho Yangu? Ingawa mwanadamu “anajua” Roho Wangu, yeye pia huikosea Roho Wangu. Maneno Yangu yanaweka wazi uso mbaya wa wanadamu wote, na kuweka wazi mawazo ya ndani kabisa ya watu wote, na kusababisha wote duniani kufanywa wazi na mwanga Wangu na kuanguka chini ndani ya uchunguzi Wangu. Ijapokuwa mwanadamu anaanguka chini, moyo wake hauthubutu kwenda mbali Nami. Miongoni mwa viumbe, ni nani asiyekuja kunipenda kwa sababu ya matendo Yangu? Ni nani asiyekuwa na hamu kwa ajili ya kuyasikia maneno Yangu? Ni nani asiyezaliwa ndani mwake na hisia za ibada kwa sababu ya upendo Wangu? Ni kwa sababu tu ya ufisadi wa Shetani ndio maana mwanadamu anashindwa kuufikia ulimwengu kama Ninavyomhitaji kufika. Hata viwango vya chini kabisa ambavyo Mimi Namhitaji kufika huzalisha mashaka ndani yake, bila kutaja chochote cha leo, enzi ambayo Shetani anaendesha ghasia na ni mdhalimu mkuu, au wakati ambapo mwanadamu amekanyagwa sana na Shetani mpaka mwili wake mzima umejaa uchafu. Ni lini ambapo kutojali kwa mwanadamu kuhusu moyo Wangu kwa sababu ya upotovu wake hakujanisababishia Mimi huzuni? Je, inawezekana kwamba Mimi namwonea Shetani huruma? Je, inawezekana kwamba Mimi Nimekosea katika upendo wangu? Wakati mwanadamu ananikaidi, Moyo wangu unaomboleza kwa siri; wakati mwanadamu ananipinga, Ninamwadibu; wakati Ninamwokoa mwanadamu na kumfufua kutoka wafu, Mimi Huwalisha kwa uangalifu wanaponyenyekea mbele zangu, Moyo Wangu unatulia tuli na mara moja Ninahisi mabadiliko makubwa katika mbinguni na duniani na vitu vyote. Wanadamu wanaponisifu Mimi, itawezekanaje Nisiwe na furaha? Wakati mwanadamu ananishuhudia na kupatwa na Mimi, itawezekanaje Nisitukuzwe? Inawezekana kwamba kila anachofanya mwanadamu hakiongozwi na kutolewa na Mimi? Wakati ambapo Sitoi mwelekeo, wanadamu wanazembea na kuwa wanyamavu, na, nyuma Yangu, wao wanashiriki katika zile shughuli chafu “zenye kusifika.” Je, unafikiri kwamba mwili Ninaouvaa, haufahamu chochote kuhusu matendo yako, tabia zako, na maneno yako? Nimestahimili mvua na upepo kwa miaka mingi, na vile vile Nimepitia machungu ya ulimwengu wa binadamu, lakini ukitafakari kwa karibu, hakuna kiasi cha mateso kinachoweza kumfanya mwanadamu aliye katika nyama za mwili kupoteza matumaini ndani Yangu, kama vile hakuna utamu wowote unaoweza kumfanya mwanadamu wa mwili awe bila hisia, mwenye kuvunjika moyo au mwenye kunipuuza Mimi. Je, upendo wa mwanadamu Kwangu una mipaka kwa hali ya kutokuwa na maumivu au kutokuwa na utamu?

Leo hii, Mimi niko katika nyama na nimeanza kirasmi kutekeleza kazi ambayo lazima Niifanye, na hata ingawa mwanadamu anaogopa sauti ya Roho Wangu, yeye huasi kiini cha Roho Yangu. Sihitaji kufafanua jinsi ni vigumu kwa mwanadamu kunijua Mimi Niliye katika mwili kupitia kwa maneno Yangu. Kama Nilivyosema awali, Mimi Simlazimishi mwanadamu katika matarajio Yangu, na si lazima muwe na ufahamu wote kunihusu Mimi (kwa maana mwanadamu amepungukiwa; hii ni hali asili, na ujuzi wa kujipatia hauwezi kubadili hali hii). Mnahitaji kujua tu mambo yote yanayofanyika na kusemwa na Mimi katika hali ya mwili. Na kwa maana mahitaji Yangu si ya kulazimisha, ni matumaini Yangu kwamba mnaweza kuja kujua, na kwamba mnaweza kufaulu. Lazima mjitoe katika uovu wenu kwenye ulimwengu huu mchafu, lazima mjitahidi kufanya maendeleo katika hii “jamii ya wafalme wakuu” iliyo nyuma kimaendeleo, na msijiruhusu wenyewe kuzembea. Hupaswi kujihurumia hata kidogo: Unastahili kutenga muda mwingi na kuweka juhudi ili ujue lile Nitamkalo kwa siku moja, na maarifa ya hata sentensi moja Ninayonena ina thamani ya mafunzo ya maisha marefu. Maneno Ninayonena ni yakini na dhahania, sio maneno matupu. Watu wengi wanayo matumaini ya kufaidi kutokana na maneno Yangu, lakini Siwapi sikio; watu wengi wanatamani unene Wangu, lakini Mimi Siwapi hata kidogo; watu wengi wanatamani kuuona uso Wangu, lakini kamwe Mimi nimeuficha; watu wengi husikiliza kwa makini sauti Yangu, lakini Mimi hufunga macho Yangu na kupindua Kichwa changu, kwa kuwa kutotikisika na tamaa yao; watu wengi wanahofia sauti Yangu, lakini maneno Yangu daima ni ya kuanzisha vita; watu wengi wana uoga wa kuuona uso Wangu, lakini Mimi huwatokezea kwa makusudi ili niwacharaze waanguke. Mwanadamu kwa hakika hajawahi kuuona uso Wangu na hajawahi kuisikia sauti Yangu, kwa maana yeye hanijui kwa kweli. Hata ingawa yeye anapata pigo kutoka Kwangu, hata ingawa ananiacha, hata ingawa anaadibiwa kwa mkono wangu, yeye bado hajui kama yote anayofanya ni ya kupendeza Moyo Wangu kwa kweli, na bado hana ufahamu kuhusu ni nani ambaye hufichuliwa Moyo Wangu. Tangu uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa, hakuna mtu aliyewahi kunijua kwa kweli, au kuniona kwa kweli, na ingawa Nimekuwa mwili leo, nyinyi bado hamnijui. Je, huu sio ukweli? Je, umewahi kuona vitendo Vyangu na tabia Yangu hata kidogo katika mwili?

Mbinguni ndiko mahali Ninakojinyoosha kwenye kiti, na chini ya mbingu ndipo ambapo Mimi Hupata mapumziko. Mimi Nina mahali pa kukaa, na Ninao wakati wa kuonyesha nguvu Zangu. Kama Singekuwa duniani, kama Singejificha ndani ya mwili, na kama Singekuwa mnyenyekevu na msiri, je, si mbingu na dunia zingekuwa zimeshabadilishwa muda mrefu uliopita? Je, si nyinyi watu Wangu, mngekuwa tayari mmetumiwa na Mimi? Hata hivyo kuna hekima kwa matendo Yangu, na ingawa Ninafahamu kikamilifu kuhusu udanganyifu wa mwanadamu, Mimi Sifuati mfano wake, na badala yake Ninafanya mabadilishano nao. Hekima Yangu katika ulimwengu wa kiroho haiishi, na pia hekima Yangu katika mwili ni ya kudumu milele. Je, huu sio wakati hasa ambao matendo Yangu yanawekwa wazi? Nimemsamehe na kufuta dhambi za mwanadamu mara nyingi, mpaka leo, katika Enzi ya Ufalme. Nitaweza kuchelewesha wakati Wangu zaidi tena? Ingawa Nimekuwa na huruma kiasi fulani kwa wanadamu mdhaifu, pindi kazi Yangu inapokamilika, Ninaweza kujiletea taabu kwa kufanya kazi ya zamani? Ningeweza kwa makusudi kumruhusu Shetani alete mashtaka? Sihitaji mwanadamu afanye kitu chochote ila kukubali ukweli wa maneno Yangu na maana halisi ya maneno Yangu. Hata ingawa maneno Yangu ni rahisi, katika kiini maneno hayo ni ngumu kufahamika, kwa maana nyinyi ni wadogo mno, na pia mmekuwa wasiosikia. Ninapozionyesha siri Zangu wazi na kufanya wazi mapenzi Yangu katika mwili, hamwoni haya yote; mnaisikiliza sauti, lakini hamwelewi maana yake. Mimi hukumbwa na huzuni kuu. Ingawa Mimi Niko katika mwili, Ninakosa uwezo wa kufanya kazi ya huduma ya mwili.

Ni nani ambaye amekuja kujua matendo Yangu katika mwili kati ya maneno na matendo Yangu? Ninapofichua siri zangu kwa maandishi, au kuzizungumza kwa sauti, watu wote hupigwa na butwaa, na wanafumba macho yao wakiwa kimya. Kwa nini Ninayosema hayaeleweki na mwanadamu? Kwa nini maneno Yangu hayaeleweki na yeye? Kwa nini yeye ni kipofu kwa matendo Yangu? Ni nani anayeweza kuniona na kamwe asiweze kusahau? Ni nani anayeweza kusikia sauti Yangu na asiiruhusu impite tu? Ni nani anayeweza kuhisi mapenzi Yangu na aufurahishe Moyo Wangu? Ninaishi na kutembea miongoni mwa wanadamu, Nimekuja kutambua wanachopitia, na ingawa Nilihisi kwamba kila kitu kilikuwa kizuri baada ya Mimi kuviumba kwa ajili ya mwanadamu, Sipati furaha kutokana na maisha miongoni mwa wanadamu, na Mimi sifurahishwi na kuwepo kwa furaha miongoni mwa wanadamu. Simchukii wala kumkataa mwanadamu, na wala Mimi Sina mvuto wa upendo kwao—kwa vile wanadamu hawanijui Mimi, wao hupata ugumu kuuona uso Wangu gizani, katikati ya kelele wanakuwa na wakati mgumu kuisikia sauti Yangu na hawawezi kutambua Ninayosema. Hivyo, kwa kijuu juu, yote mnayoyafanya ni kwa kunitii, lakini moyoni mwenu, nyinyi bado mnaniasi. Hali asili yote ya zamani ya mwanadamu, inaweza kusemwa, iko namna hii. Ni nani aliye tofauti? Ni nani asiye mmoja wa wale wanaolengwa na kuadibu Kwangu? Lakini ni nani asiyeishi chini ya uvumilivu Wangu? Kama mwanadamu angeangamizwa na ghadhabu Yangu, umuhimu wa kuumba Kwangu kwa mbingu na dunia ungekuwa nini? Wakati mmoja Niliwaonya watu wengi na kuwasihi watu wengi, na kwa uwazi Nikawahukumu watu wengi—je, hili si bora zaidi kuliko kumuangamiza mwanadamu moja kwa moja? Lengo Langu sio kumweka mwanadamu kwenye mauti, bali kumfanya kujua matendo Yangu yote katika hukumu Yangu. Wakati mnapanda kutoka kuzimu, ambayo ni kusema, mnapojiweka huru kutoka kwenye hukumu Yangu, fikira zenu binafsi na mipango yote yatatoweka, na watu wote watanuia kukidhi matakwa Yangu. Na katika hili, je, Mimi Sitakuwa Nimefanikiwa katika Lengo Langu?

Machi 1, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 8

Inayofuata: Sura ya 10

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp