Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kuridhisha matakwa Yangu kikamilifu, kwa hiyo lazima Niseme kile hasa ninachotaka kusema na kuwafafanulia mapenzi Yangu. Kwa kuwa utambuzi wenu ni ndogo na shukrani yenu pia ni ndogo, karibu mmekosa kabisa kujua tabia Yangu na dutu Yangu pia, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuyahusu. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kujaribu kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani. Masuala haya si mageni kabisa kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo ndani yao. Wengi wenu mnao ufahamu dhaifu tu na aidha ufahamu kiasi na usiokamilika. Ili kuwasaidia kutenda ukweli kwa njia bora zaidi, yaani, kuweka maneno Yangu katika matendo kwa njia bora zaidi, Nafikiri kwamba ni masuala haya ambayo lazima kwanza myajue. Vinginevyo, imani yenu itabakia isiyo wazi, ya unafiki, na iliyopambwa sana na dini. Kama huelewi tabia ya Mungu, basi haitawezekana kwako kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, haitawezekana wewe kumwonyesha heshima na uchaji, lakini badala yake utakuwa tu mzembe asiyejali na kuepuka kusema ukweli wote, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Ingawa kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakini au kudadisi masuala haya. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuzilia mbali amri za utawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na tunda la msingi la tendo lako linakuwa ni kosa dhidi ya amri ya utawala. Sasa unafaa kutambua kwamba kuelewa tabia ya Mungu huja na kujua dutu Yake, nakwamba pamoja na kuelewa tabia ya Mungu huja kuelewa amri za utawala. Bila shaka, amri nyingi za utawala zinahusisha tabia ya Mungu, lakini tabia Yake haijaonyeshwa ndani yao kikamilifu. Kwa hivyo mnawahitaji kuongeza hatua nyingine katika kukuza ufahamu wenu wa tabia ya Mungu.

Ninaongea nanyi leo si katika hali ya mazungumzo ya kawaida, kwa hiyo lazima myachukulie maneno Yangu kwa uangalifu na, zaidi, kuyatafakari kwa kina. Kile Ninachomaanisha na haya ni kwamba mmetoa jitihada ndogo sana kwa maneno ambayo Nimeyazungumza. Tunapokuja kwa tabia ya Mungu, hamko radhi hata zaidi kutafakari juu ya suala hili, na ni mara chache sana ambapo yeyote analiwekea juhudi. Kwa hiyo, Nasema kwamba imani yenu ni mazungumzo ya kujionyesha tu. Hata sasa, hakuna hata mmoja wenu ametoa jitihada yoyote ya dhati kwa udhaifu wenu mkuu zaidi. Mmenisikitisha baada ya maumivu yote Niliyoyapitia kwa ajili yenu. Si ajabu kwamba hammjali Mungu na mnaishi maisha yasiyo na ukweli. Ni vipi watu kama hawa wanaweza kuchukuliwa kama watakatifu? Sheria ya mbinguni haitavumilia kitu kama hiki! Kwa sababu mnao uelewa mdogo sana wa hili, basi itabidi Nitumie pumzi zaidi.

Tabia ya Mungu ni mada ambayo inaonekana kuwa ya dhahania sana kwa kila mtu na aidha ambayo haikubaliwi kwa urahisi, kwani tabia Yake ni tofauti na hulka ya binadamu. Mungu, vilevile, anazo hisia za raha, hasira, huzuni, na furaha, lakini hisia hizo zinatofautiana na zile za binadamu. Mungu ndicho kile Alicho na Anacho kile anacho. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukifichua ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Kila alicho na anacho, pamoja na dutu na utambulisho Wake vyote ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, tulizo kwa binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa binadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Aidha, ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye ambaye hawezi kukosewa (wala Hatavumilia kukosewa)[b] na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanao uwezo au wanaoweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini hulka ya binadamu ni ishara tu ya mamlaka kidogo ya binadamu juu ya wanyama. Binadamu mwenyewe hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuzidi nafsi, bali katika dutu yake ni yule ambaye kwa woga yuko chini ya watu, matukio na mambo ya kila aina. Raha ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa wanadamu; raha Yake ni raha ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi, ishara ya fadhili. Hasira ya Mungu inatokana na uharibifu ambao kuwepo na kuingilia kwa dhuluma kunaleta kwa wanadamu Wake, kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na chema. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya wanadamu, ambao Amekuwa na matumaini nao lakini ambao wameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya wanadamu wasio na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule mwanadamu mzuri lakini mwenye upungufu katika maoni yake mwenyewe. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya uzuri na ukarimu. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na kwa sababu wanadamu hupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na raha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko raha. Furaha Yake ni ishara ya wanadamu kuwa huru dhidi ya mateso kutoka wakati huu kuendelea, na ishara ya wanadamu kuingia katika ulimwengu wa mwangaza. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote huibuka kwa ajili ya masilahi yake mwenyewe, na wala si kwa ajili ya haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, sembuse neema inayotolewa na Mbinguni. Hisia za wanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa hapohapo. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na ni mwenye heshima kila wakati, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote asiye na thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa wanadamu; mwanadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na kujitahidi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia kwa dhati kuendelea kuishi kwa wanadamu, ilhali mwanadamu kamwe hachangii kitu kwa ajili ya mwangaza au haki. Hata kama mwanadamu anajitahidi sana kwa muda, ni dhaifu sana kiasi cha kutoweza kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mwenye ubinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vya uzuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa Mungu.

Kila sentensi Niliyoizungumza ina tabia ya Mungu ndani yake. Mngefanya vizuri endapo mngetafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka kwa maneno hayo. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuelewa, lakini Ninaamini kwamba nyinyi nyote mnayo angalau mawazo fulani kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatulizwa moyo. Kwa mfano, mweke Mungu katika moyo wako siku zote. Unapochukua hatua, fanya hivyo kulingana na maneno Yake. Tafuta nia Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Hata zaidi usimweke Mungu nyuma ya akili zako ili ukajaze uwazi wa baadaye katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umekosea tabia ya Mungu. Tena, tuchukulie kwamba kamwe hutamki matamshi ya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu maisha yako yote, na tena, tuchukulie kwamba unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho amekuaminia wewe na pia kutii maneno Yake yote katika maisha yako yote, basi utakuwa umeweza kuepuka kwa kukosea amri za utawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya ni nuru kiasi ya Roho Mtakatifu tu,” “Katika maoni yangu, si kila kitu ambacho Mungu anakifanya lazima ni sahihi,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukubwa zaidi kuliko wangu,” “Maneno ya Mungu hayaiaminiki kabisa,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakusihi wewe kukiri na kutubu dhambi zako mara nyingi zaidi. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani hukosei mwanadamu, ila Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unamhukumu mtu tu, lakini Roho wa Mungu haichukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia Yeye heshima. Kama hali ni hivi, basi si ni kweli kwamba umekosea tabia ya Mungu? Lazima ukumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu kinafanywa ili kukinga kazi Yake katika mwili na ili kazi hii ifanywe vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ni mtu ambaye kamwe hataweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, kwa hivyo Atatumia adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.

Kupata kujua dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole na bila kujua, utaanza kujua dutu ya Mungu. Wakati umeingia katika maarifa haya, utajipata ukisonga mbele hadi kwa hali iliyo ya juu na ya kupendeza zaidi. Hatimaye, utaaibika kutokana na nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unahisi hakuna mahali pa kujificha. Wakati huo, kutakuwa na machache zaidi na zaidi katika mwenendo wako ya kukosea tabia ya Mungu, moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utakua ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya wanadamu kuingia katika hali nzuri. Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Mnaposhughulika huku na kule kwa ajili ya majaaliwa yenu, ni nani angefikiria kujaribu kujua dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, nyinyi mtazikosea amri za utawala bila kujua, kwani mnafahamu kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kile mfanyacho sasa hakiweki msingi wa makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaomba muelewe tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkikosea amri za utawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, basi kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Naomba kwamba, pamoja na kuchunguza mienendo yenu binafsi, muwe waangalifu zaidi na hatua mnazochukua. Haya ndiyo yatakuwa mahitaji ya juu zaidi nitakayowaomba, na Ninatumai kwamba nyote mtayafikiria kwa umakini na kuyaona kuwa muhimu kabisa. Endapo siku ifike ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa yenu pekee kufikiria, na hakutakuwa na mwingine yeyote atakayevumilia adhabu hiyo kwa niaba yenu.

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yanasema “ni ishara ya kutoweza.”

b. Maandishi asilia yanasema “na vilevile ishara ya kutoweza kukosewa kuwa (na kutovumilia kukosewa).”

Iliyotangulia: Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

Inayofuata: Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp