Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata kwa miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii na uasi wenu mwingi dhidi Yangu kwa hii miaka mingi, kwa sababu hakuna mtakatifu hata mmoja kati yenu, nyinyi pia ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba daima Mimi hujirudia mbele yenu. Sitaki kuishi kuishi pamoja na nyinyi kwa namna hii—lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine. Natumai mtaniendekeza, nami Natumai hata zaidi kwamba mtaweza kuamini kila neno Ninalosema, na bado zaidi, kwamba mtaweza kufahamu kwa kina maana ya maneno Yangu. Msiwe na shaka juu ya yale Ninayosema, au hata kuchukua maneno Yangu mnavyotaka na kuyatupilia mbali kwa hiari, jambo ambalo mimi Ninaona halistahimiliki. Msiyahukumu maneno Yangu, wala kutoyachukulia kwa uzito, au kusema kwamba daima Nawajaribu, au mbaya zaidi, kusema kwamba kile ambacho Nimewaambia kinakosa usahihi. Ninaona kuwa mambo haya hayavumiliki. Kwa sababu mnanichukulia Mimi na kuyachukulia Ninayoyasema kwa shaka kuu na kamwe hamyazingatii, Ninamwambia kila mmoja wenu kwa uzito kabisa: Msiunganishe kile Ninachosema kwa falsafa, msikiweke pamoja na uongo wa matapeli, na hata zaidi, msiyajibu maneno Yangu kwa dharau. Labda katika siku zijazo hakuna mtu yeyote atakuwa na uwezo wa kuwaambia yale Ninayowaambia nyinyi, au kuzungumza na nyinyi kwa huruma sana, sembuse kuwaeleza mambo haya kwa uvumilivu hivi. Siku zijazo zitatumika katika kukumbuka nyakati zile nzuri, au kwa kulia kwa sauti kubwa, au kugumia kwa maumivu, au mtakuwa mkiishi katika usiku wa giza bila hata chembe ya ukweli au kupewa maisha, au kusubiri tu bila matumaini, au katika majuto machungu mengi kiasi kwamba hamwezi kufikiri…. Huu uwezekano mbadala hauwezi kuepukika kabisa kwa mtu yeyote kati yenu. Kwa sababu hakuna hata mmoja wenu ambaye anamiliki kiti ambacho kwacho kwa kweli mnamwabudu Mungu; mnajitumbukiza katika dunia ya uasherati na maovu, kuchanganya ndani ya imani yenu, ndani ya roho zenu, nafsi, na miili, mambo mengi yasiyohusiana na maisha na ukweli na kwa kweli yanapingana nayo. Hivyo kile Ninachotumai kwenu ni kuwa muweze kuletwa kwa njia ya mwanga. Tumaini Langu la pekee ni kwamba muweze kujitunza, muweze kujiangalia, si kuweka mkazo mwingi sana juu ya hatima yenu kiasi kwamba muitazame mienendo na dhambi zenu kwa kutojali.

Watu ambao wanamwamini Mungu kwa muda mrefu sasa wametumainia hatima iliyo nzuri, watu wote ambao wanamwamini Mungu wanatumai kwamba bahati nzuri itawajia ghafla, na wote wanatumai kwamba bila kujua, watajikuta wameketi kwa amani pahali pamoja au pengine mbinguni. Lakini Ninasema watu hawa kwa mawazo yao mazuri hawajawahi kujua kama wana sifa ya kupokea bahati nzuri kama hiyo inayoanguka kutoka mbinguni, au kukaa juu ya kiti huko mbinguni. Kwa sasa nyinyi mna maarifa mazuri kujihusu, lakini bado mnatarajia kwamba mnaweza kuepuka maafa ya siku za mwisho na mkono wa mwenye Uweza ukiwaadhibu wale waovu. Inaonekana kana kwamba kuwa na ndoto tamu na kutaka vitu kama tu wanavyopenda ni jambo la kawaida la watu wote ambao Shetani amewapotosha, si kipaji cha ajabu cha mtu fulani binafsi. Hata hivyo, bado Nataka kukomesha tamaa zenu badhirifu na hamu zenu za kupata baraka. Kwa kuwa dhambi zenu ni nyingi na ukweli wa kutotii kwenu ni mwingi na unaongezeka kila wakati, haya yanawezaje kupatana na ramani zenu nzuri za baadaye? Kama unataka kuendelea unavyopenda kuwa mwenye makosa, bila chochote kinachokuzuia, lakini bado unataka ndoto zitimie, basi Nakusihi uendelee katika usingizi wako na usiamke kamwe, kwa sababu unaota ndoto isiyoweza kutimia, na haitatumika kukufanya uwe mtu usiye wa kawaida mbele ya Mungu mwenye haki. Kama unataka tu ndoto zitimie, basi usiote kamwe, lakini kabiliana na ukweli milele, kabiliana na mambo ya hakika. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuokoa. Je, kwa maneno thabiti, hatua za taratibu hizi ni zipi?

Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na kuchunguza mwenendo na mawazo yako yote ambayo hayafuati ukweli.

Hiki ni kipengee ambacho mnaweza kukifanya kwa urahisi, na Ninaamini kwamba watu wanaofikiri wanaweza kufanya hivi. Hata hivyo, wale watu ambao hawajui kamwe ni nini maana ya dhambi na ukweli ni tofauti, kwa sababu kimsingi wao si watu wa kufikiri. Mimi nazungumza na watu ambao wamethibitishwa na Mungu, ni waaminifu, hawajazikosea vibaya amri za utawala, na wanaweza kupata dhambi zao wenyewe kwa urahisi. Ingawa hiki ni kipengee ambacho Ninahitaji kwenu ambacho ni rahisi kwenu, sicho kipengee cha pekee Ninachohitaji kwenu. Lolote litokealo, Ninatumai kwamba hamtalicheka hitaji hili kwa siri, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kimzaha. Lichukulieni kwa umakini, na msilipuuze.

Pili, kwa kila moja ya dhambi na kutotii kwako tafuta ukweli unaoambatana na utumie ukweli huu kuzitatua, kisha badilisha vitendo vyako vya dhambi na mawazo yako na vitendo vya kutotii na kutenda ukweli.

Tatu, kuwa mtu mwaminifu, si mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, mwenye hila daima. (Hapa Ninakusihi tena uwe mtu mwaminifu.)

Kama unaweza kutimiza vipengee hivi vyote vitatu basi una bahati, wewe ni mtu ambaye ndoto zake zinatimia na ambaye hupata bahati nzuri. Labda mtayachukulia maombi haya matatu yasiyovutia kwa umakini, au labda mtayachukulia bila kuwajibika. Kwa vyovyote vile, azma Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka mawazo yenu katika matendo, si kuwadhihaki au kuwadanganya.

Madai Yangu yanaweza kuwa rahisi, lakini kile Ninachowaambia si rahisi hivyo kama kujumlisha moja na moja upate mbili. Kama mnazungumzia tu mambo haya bila kufikiria, mkiongea sana kwa kuparaganya kwa maneno matupu ya majivuno yanayopita kiasi, basi ramani zenu na matakwa yenu yatakuwa ukurasa mtupu milele. Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale kati yenu ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Kinyume cha hayo, Mimi Huwatendea wale ambao hawajatosheleza madai Yangu kwa adhabu, siyo zawadi, sembuse huruma yoyote. Labda mnawaza kwamba kwa kuwa wafuasi kwa miaka mingi mnaweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote hadi sasa mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na kutokuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa bora zaidi Niigeuze miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa utupu, kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo.

Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu. Kama kila mojawapo ya mazungumzo ambayo Nimekuwa nayo na nyinyi hayajatosha kuvuta nadhari yenu, basi huenda Sitasema mengine. Hata hivyo, nyinyi mnaelewa matokeo ya hayo. Sipumziki kamwe, kwa hiyo Nisiponena, Nitafanya kitu ili watu wakitazame. Ningeweza kuufanya ulimi wa mtu uoze, au mtu afe na viungo vyake kutolewa, au kumpa mtu kasoro za neva na kumfanya atende kama mwendawazimu. Au, basi tena, Ningeweza kufanya baadhi ya watu wavumilie maumivu makali Ninayowasababishia. Kwa njia hii Ningejihisi mwenye furaha, mwenye furaha sana na kufurahishwa sana. Imesemwa daima kwamba “Mema hulipizwa kwa mema, na maovu kwa maovu,” mbona isiwe hivyo sasa? Kama unataka kunipinga Mimi na unataka kutoa hukumu fulani kunihusu, basi Nitauozesha mdomo wako, na hilo litanipendeza Mimi sana. Hii ni kwa sababu mwishowe hujafanya lolote linalohusiana na ukweli, sembuse na maisha, ilhali kila kitu Ninachofanya ni ukweli, kila kitu kinahusiana na kanuni za kazi Yangu na amri za utawala Ninazoeleza rasmi. Kwa hiyo, Namsihi sana kila mmoja wenu kujilimbikiza wema kiasi, acha kufanya maovu mengi sana, na usikize madai Yangu katika wasaa wako. Kisha mimi Nitahisi furaha. Kama mngetoa (au kusaidia) kwa ukweli moja kwa elfu ya juhudi mnazoweka katika mwili, basi Nasema hungekuwa na dhambi mara kwa mara na midomo mbovu. Je, hili si dhahiri?

Kadri dhambi zako zilivyo nyingi, ndivyo nafasi zako za kupata hatima iliyo nzuri zilivyo chache. Kinyume chake, kadri dhambi zako zilivyo chache, ndivyo nafasi zako za kusifiwa na Mungu zilivyo nyingi. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi kiwango ambapo haiwezekani Mimi kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa jasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile kitakachokupata. Kama wewe ni mtu mwenye ari anayetenda ukweli basi kwa hakika una fursa ya kusamehewa dhambi zako, na kiwango cha kutotii kwako kitakuwa kidogo zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu asiye radhi kutenda ukweli basi hakika dhambi zako mbele ya Mungu zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitakua zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeangamia kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kufurahisha ya kupokea baraka itaharibiwa. Usizichukulie dhambi zako kama makosa ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu ubora wako wa tabia ulio duni ulifanya isiwezekane kuutenda, na hata zaidi, usizichukulie tu dhambi ulizofanya kama matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri zaidi. Kama unajua vizuri kujisamehe na unajua vizuri kujitendea kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hataupata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukusumbua, lakini zitakuzuia kuwahi kutosheleza madai ya ukweli na kukufanya milele kuwa mwenzi mwaminifu wa Shetani. Ushauri Wangu kwako bado ni: Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa makini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kuhusu hatima yako.

Iliyotangulia: Maonyo Matatu

Inayofuata: Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp