Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 21

Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa marejesho Yangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulukane waliko na gharika hii ya urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini mwandadamu hajawahi kunitabua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utarijiri uliofichika ndani Mwangu. Ingawa Mimi hutosheleza mahitaji ya mwanadamu kila siku, hajawa na uwezo wa kukubali kwa kweli, hana uwezo wa kupokea utajiri wote niliompa. Hakuna jambo lolote kuhusu upotovu wa mwanadamu ambalo huniepuka; Kwangu, ulimwengu wake wa ndani ni kama mwezi unaong’aa juu ya maji. Mimi Sifanyi mchezo na mwanadamu wala kufanya mambo kwake bila sababu; ni kwamba tu mwanadamu hawezi kuchukua jukumu kwa ajili yake mwenyewe, na hivyo uzao mzima wa mwanadamu daima umepotea, na hata wa leo bado hawana uwezo wa kujitoa wenyewe kutoka upotovu huo. Ole wao, maskini wanadamu! Kwa nini mwanadamu ananipenda lakini hawezi kufuata nia za Roho Wangu? Je, Mimi Sijajifichua kwa mwanadamu kwa kweli? Mwanadamu kwa kweli hajapata kuuona uso Wangu kamwe? Je, inawezekana kwamba Nimeonyesha huruma kiasi kidogo sana kwa wanadamu? Enyi waasi wa wanadamu wote! Lazima waharibiwe chini ya miguu Yangu, ni lazima watokomee kabisa katikati ya kuadibu Kwangu, na lazima, siku ambayo mpango Wangu mkubwa utakamilika, watatupiliwa mbali kutoka kati ya wanadamu, ili wanadamu wote wazijue nyuso zao mbaya. Sababu ya mwanadamu kuona uso Wangu na kusikia sauti Yangu mara chache ni kwamba dunia nzima imejawa na machafuko, na kelele zake ni kubwa mno, na hivyo wanadamu ni wavivu mno kutafuta uso Wangu na kujaribu kuelewa Moyo Wangu. Je, hii si sababu ya kupotoshwa kwa wanadaumu? Je, hii si ndiyo sababu mwanadamu ako na mahitaji? Wanadamu wote daima wamekuwa katika utoaji Wangu; kama isingekuwa hivyo, Nisingekuwa mwenye huruma, nani angenusuriwa mpaka leo? Utajiri Nilionao hauna kisawe, na bado maafa yote yamo mikononi Mwangu—ni nani awezaye kuepuka maafa wakati wowote apendapo? Je, maombi ya mwanadamu yanaweza kumruhusu afanye hivyo? Au machozi yaliyo moyoni mwa mwanadamu? Mwanadamu hajawahi Kuniomba Mimi kwa kweli, na hivyo miongoni mwa wanadamu hakuna mwanadamu aliyewahi kuishi maisha yake yote kwenye mwanga wa kweli, na watu wanaishi katikati ya mwanga unaoneka kwa kipindi pekee. Hii ndio imesababisha mahitaji ya mwanadamu leo.

Kila mwanadamu ana hamu kubwa, tayari kufanya jambo lolote kwa sababu Yangu ili wapate kitu kutoka Kwangu, na hivyo, nikizingatia saikolojia ya mwanadamu, Mimi humpa ahadi ya kuhamasisha upendo wa kweli ndani yake. Je, ni upendo wa kweli wa mwanadamu unaompa nguvu? Je, ni uaminifu wa mwanadamu Kwangu ndio umeigusa Roho Wangu mbinguni? Mbingu haijawahi kuathiriwa na matendo ya mwanadamu hata kidogo, na iwapo kumtendea Kwangu mwanadamu kungetegemea matendo yake yote, basi wanadamu wote wangeishi katikati ya kuadibu Kwangu. Nimewaona watu wengi wakitiririkwa na machozi, na Nimewaona watu wengi wakitoa nyoyo zao badala ya utajiri Wangu. Licha ya “uchaji Mungu” kama huu, Sijawahi kujitoa kwa mwanadamu kikamilifu kwa sababu ya hisia zake za ghafla, kwa sababu mwanadamu hajawahi kuwa radhi kujitoa kwa furaha mbele Yangu. Nimeng’oa barakoa ya watu wote na kutupa barakoa hizo katika ziwa la moto, na matokeo yake, uaminifu wa mwanadamu na maombi yake hayajawahi kuwa imara mbele Zangu. Mwanadamu ni kama wingu angani: Wakati upepo unapepea, anahofia uwezo mkubwa wa nguvu zake na hivyo huelea kwa haraka kufuata upepo, akiwa na woga sana kuwa atatupiliwa nje kwa sababu ya uasi wake. Je, huu sio uso mbaya wa mwanadamu? Je, hili silo linalojulikana kama kutii kwa mwanadamu? Je, hii siyo “hisia ya kweli” na nia njema bandia ya mwanadamu? Watu wengi hukataa kushawishiwa na maneno yote yatokayo kwenye kinywa Changu, na wengi hawakubali tathmini Yangu, na hivyo maneno na matendo yao husalitii nia zao za kuasi. Nisemacho ni kinyume cha asili ya zamani ya mwanadamu? Je, si Nimepeana ufafanuzi wa kufaa kwa binadamu kulingana na “sheria za asili”? Mwanadamu hanitii kwa kweli; angenitafuta kwa kweli, haingenibidi kusema mengi. Mwanadamu ni takataka isiyo na maana, na ni lazima Nitumie kuadibu Kwangu kumlazimisha kuendelea mbele; Nisingefanya hivyo, vipi—ingawa ahadi Ninazompa ni za kutosha starehe yake—moyo wake ungeweza kushawishiwa? Mwanadamu ameishi na mapambano machungu kwa miaka mingi; inaweza kusemekana, siku zote ameishi kwa kukata tamaa. Matokeo yake ni kuwa ameishi maisha ya kukata tamaa, na amechoka kimawazo na kimwili, na hivyo hapokei utajiri Ninaompa kwa furaha. Hata leo, hakuna mwanadamu aliye na uwezo wa kukubali utamu wote wa roho kutoka Kwangu. Watu wanaweza tu kubaki maskini, wakisubiri siku ya mwisho.

Watu wengi wangependa kunipenda kweli, lakini kwa sababu mioyo yao si yao wenyewe, hawana udhibiti wa wao wenyewe; watu wengi hunipenda kwa kweli katika majaribio Ninayotoa, lakini hawana uwezo wa kuelewa kwamba Mimi kwa kweli Nipo, na wananipenda tu katikati ya utupu; na si kwa sababu ya kuwepo Kwangu halisi; watu wengi, baada ya kuweka nyoyo zao mbele Zangu, hawazijali, na hivyo nyoyo zao zinanyakuliwa na Shetani wakati wowote anapopata nafasi, na baada yake Huniacha; watu wengi hunipenda kwa dhati Ninapotoa maneno Yangu, lakini hawathamini maneno Yangu katika roho zao, badala yake wakiyatumia kwa kawaida kama mali ya umma na kuyatupa yalipotoka wakati wowote wanapotaka. Mwanadamu hunitafuta akiwa na maumivu, na hunitazamia akiwa na majaribu. Wakati kuna amani yeye hunifurahia, wakati wa hatari yeye hunikana, wakati ana kazi nyingi yeye hunisahau, na asipokuwa na kitu cha kufanya yeye hujiweka kwenye hisia kwa ajili Yangu—lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amenipenda katika Maisha yake yote. Ningependa mwanadamu awe mwenye bidii mbele Zangu: Mimi Simuombi chochote, ila tu watu wote wanichukulie kwa umakini, kwamba, badala ya kunihadaa, waniruhusu kurudisha uwazi wa wanadamu. Kupata nuru Kwangu, mwangaza na gharama ya juhudi Zangu kupenya miongoni mwa watu wote, lakini pia ukweli halisi wa matendo yote ya mwanadamu hupenya miongoni mwa watu wote, ukipenyeza udanganyifu kunihusu kwao. Ni kama vile viungo vya udanganyifu wa mwanadamu vimekuwa naye tangu tumboni mwa mamake, kana kwamba amekuwa na mbinu hizi maalum za kuhadaa tangu kuzaliwa kwake. Kuzidisha, hajawacha mchezo huo; hakuna mwanadamu aliyewahi kutambua chanzo cha maarifa ya udanganyifu huu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu anaishi katika udanganyifu bila kujua, na ni kana kwamba yeye hujisamehe mwenyewe, kana kwamba ni mipango ya Mungu na sio udanganyifu wake wa makusudi Kwangu. Je, hiki sicho chanzo kamili cha udanganyifu wa mwanadamu Kwangu? Je, huu sio mpango wake wa ujanja? Sijawahi kuchanganywa na ushawishi na hila za mwanadamu, kwa maana Mimi Nilishatambua kiini chake muda mrefu uliopita. Nani anajua kiasi cha uchafu ulio katika damu yake, na kiasi gani cha sumu ya Shetani imo ndani ya mafupa yake? Mwanadamu anapata uzoefu wa sumu hii kila uchao, hata anakosa busara ya kufahamu maafa ya Shetani na hivyo hana nia ya kutambua “sanaa ya uwepo wa afya.”

Wakati mwanadamu yuko mbali nami, na wakati ananijaribu, Mimi hujificha kutoka kwake kati ya mawingu. Na hiyo, hawezi kunipata hata kidogo, na huishi tu mikononi mwa waovu, akifanya yote atakayo. Mwanadamu anaponikaribia, Mimi hujitokeza kwake na sifichi uso Wangu kutoka kwake, na kwa wakati huu, mwanadamu huona hisia ya ukarimu usoni Mwangu. Yeye ghafla hupata fahamu na ingawa hatambui, ndani yake kunazaliwa upendo Kwangu. Katika moyo wake, yeye ghafla huhisi utamu usio na kifani, na hustaajabu jinsi gani hakuweza kutambua kuwepo Kwangu ulimwenguni. Hivyo basi mwanadamu ana hisia kubwa ya uzuri Wangu, na zaidi, ya thamani kubwa Yangu. Matokeo yake, yeye hatamani kamwe kuniacha tena, Ananiona kama mwanga wa maisha yake, mwenye woga sana kuwa Naweza kumwacha, hunikumbatia kwa nguvu. Mimi siguswi na bidii ya mwanadamu, lakini ni mwenye rehema kwake kwa sababu ya upendo wake. Kwa wakati huu, mwanadamu mara moja huishi katika ya majaribio yangu. Uso Wangu hutoweka kutoka moyo wake, na yeye mara moja huona kuwa maisha yake ni tupu na anafikiria kukimbia. Wakati huu, moyo wa mwanadamu huwekwa wazi. Yeye hanikumbatii kwa sababu ya tabia Yangu, lakini ananiomba Nimlinde kwa sababu ya upendo Wangu. Hata hivyo, upendo Wangu unapomgeukia mwanadamu yeye mara moja hubadili mawazo yake na yeye hukiuka agano lake nami na hujiweka mbali na hukumu Yangu asiwe na nia ya kutafuta uso Wangu wa rehema tena, na hivyo hubadilisha mtazamo wake Kwangu na husema kuwa Sijawahi kumwokoa mwanadamu. Je, upendo wa kweli unahusiana na chochote ila huruma? Je, mwanadamu ananipenda tu anapoishi chini ya mwanga Wangu? Yeye anaangalia ya jana lakini anaishi katika wakati huu si hii ni hali ya mwanadamu? Je, kesho mtakuwa jinsi mlivyo leo? Ninachotaka ni mwanadamu awe na moyo unaonitamani kwa kina na sio moyo unaoridhishwa na vitu visivyo na thamani ya kimwili.

Machi 21, 1992

Iliyotangulia:Sura ya 20

Inayofuata:Sura ya 22

Unaweza Pia Kupenda